Serikali inafahamu kuwa kwa kuwapatia watu wake passport kunaweza kuwahamasisha kutafuta fursa nchi zingine?

Siyo kwamba alikuwa hana tamaa ya kwenda nje, alikuwa, "mjinga"

"Ideology" ya ZIDUMU FIKRA ZA MWENYEKITI zilimlewesha!
Hawa wazee wengine walikuwa watu wa mfumo ambao kwa Tanzania walikuwa na majina makubwa sana, walikuwa wanaweza kustawi kwa majina yao, waliona wakitoka nje nyota zao hazitang'ara, watakuwa just onother bloody African, wakaona bora wabaki ndani tu watambe kwa mfumo wa "unanijua mimi ni nani wewe?".

Waliona wakienda Ulaya hawawezi kutumia mfumo wa "unanijua mimi ni nani wewe?".

Rais Rutto wa Kenya alikwenda South Korea, akawa anawaambia Wakenya walio South Korea kwamba anataka kuongeza idadi ya Wakenya South Korea, waende kufanya kazi huko na kuongeza hela wanazotuma Kenya.

Siasa za Kenya zina mengi sana, na mimi si Rutto supporter, ila, katka hili, namkubali sana William Rutto, anajua anataka nini, anajua nchi yake ina nini cha ku offer, na anaonekana ku support hilo. Huku Tanzania hatuna political will hapo juu. Kuachia uraia pacha tu ni mgogoro.

Msikilize Rutto kuanzia dakika ya pili kwenye hii video.

 
Nimeisikiliza yote. Na siwashangai, Wakenya na Viongozi wao ni watu wanaojitambua.

Wakati viongozi wetu wakiwaonea wivu watu wao kwenda "duniani", Ruto anajisikia fahahari Wakenya kutapakaa ulimwenguni kote.

"...as Kenyans we have the best human capital all over the global...speaking good English, creative, innovative, hard working, self driven, friendly, educated...you rarely get those many qualities in one...of human beings, but you get in Kenya. And is because of that spirit that Kenyans are different everywhere they go" - William S. Rutto.
 
Watu wenye mentality za kishamba hivyo wafukuzwe haraka hapo uhamiaji....

Hao ndo wale wamekuja Dar tayari watu wazima...ushamba haujawatoka bado
Ni ulimbukeni tu. Ndiyo maana Wahenga walisema, "Maskini akipata...hulia mbatwa"
 
Sijui Wabunge wenyewe wanalionaje hilo!

Au siyo tatizo kwa kuwa wao wakishaitwa tu "MHESHIMIWA" na passport anapewa hata kama hajaomba.
 
Kwa hali hiyo rushwa itakaa ipungue?
Hawezi kuisha, fata process uone shughuli yake.
Barua katibu kata, serikali za mitaa, balozi nyumba 10.
Mashahidi 3
Nilipeleka vyote document
Nikawa napigwa kalenda tu
siku ofisa wao mwenyewe kasema lainisha kidogo shauri lako liende fasta
nikajua hela hapo
Na bado ukifika pale utapigishwa kwata sana tu.
Mwisho utaishia kuhonga tu
 
"
"... lainisha kidogo..."

Mbona kwa NIDA hawafanyi hivyo?
 
Usitegemee akili mgando ya kikoloni ikaleta mabadiliko chanya katika hili. Wao wanaamini kufanya hivyo ni katika kutulinda wakati kiuhalisia ndio inakandamiza, kukosesha watu fursa na kutengeneza mazingira ya rushwa katika kupata hizo passport.

Kimsingi kwa dunia ya sasa maendeleo yanakwenda kasi na wenye dhamana ya kukalia ofisi bado wapo karne ya 20 na mbaya zaidi hawataki kubadilika kwenda na usasa na nini dunia inataka.
 
Tanzania viongozi wengi na watu wengi wenye mamlaka ni malimbukeni waliojawa roho mbaya.

Yani ukiomba tu passport wanaona kama vile utatoboa kimaisha kuliko wao.

Huu ujinga unatakiwa ukemewe kwa nguvu zote.

Mtu akitaka passport vigezo vikuu viwe kitambulisho chake cha NIDA na malipo ya passport tu.

Longolongo nyingine zikomeshwe.
 
Kama tumeshindwa kubuni namna ambayo ni bora kwetu, tuige basi hata ya wenye "akili" kama Kenya, Uganda au Rwanda.

Haina maana kutumia mbinu za enzi za Ukoloni katika karne hii.
 
Ukomunist ni upuuzi kabisa
 
,[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Me kupata passport imekua changamoto kidogo coz cheti changu cha kuzaliwa kilikosewa tarehe ya kuzaliwa
Nkaenda Rita kubadili cheti cha kuzaliwa nkafanikiwa nkapeleka Kule uhamiaji lakini cha ajabu Passport ikatoka ikiwa imeandikwa Ile tarehe ya mwanzo ya kuzaliwa yenye makosa (cheti cha mwanzo)
Nimeirudisha ile passport uhamiaji ili waanze upya mchakato

Wameniambia kuwa passport kukosewa tarehe ya kuzaliwa sio big issue lakini mimi sijaridhika kabisa nimekubali kuingia hasara ya kujaza form upya
 
Mm pia imenikuta hii mpaka sasa nimenyimwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…