Serikali inafahamu kuwa kwa kuwapatia watu wake passport kunaweza kuwahamasisha kutafuta fursa nchi zingine?

Serikali inafahamu kuwa kwa kuwapatia watu wake passport kunaweza kuwahamasisha kutafuta fursa nchi zingine?

Siyo kwamba alikuwa hana tamaa ya kwenda nje, alikuwa, "mjinga"

"Ideology" ya ZIDUMU FIKRA ZA MWENYEKITI zilimlewesha!
Hawa wazee wengine walikuwa watu wa mfumo ambao kwa Tanzania walikuwa na majina makubwa sana, walikuwa wanaweza kustawi kwa majina yao, waliona wakitoka nje nyota zao hazitang'ara, watakuwa just onother bloody African, wakaona bora wabaki ndani tu watambe kwa mfumo wa "unanijua mimi ni nani wewe?".

Waliona wakienda Ulaya hawawezi kutumia mfumo wa "unanijua mimi ni nani wewe?".

Rais Rutto wa Kenya alikwenda South Korea, akawa anawaambia Wakenya walio South Korea kwamba anataka kuongeza idadi ya Wakenya South Korea, waende kufanya kazi huko na kuongeza hela wanazotuma Kenya.

Siasa za Kenya zina mengi sana, na mimi si Rutto supporter, ila, katka hili, namkubali sana William Rutto, anajua anataka nini, anajua nchi yake ina nini cha ku offer, na anaonekana ku support hilo. Huku Tanzania hatuna political will hapo juu. Kuachia uraia pacha tu ni mgogoro.

Msikilize Rutto kuanzia dakika ya pili kwenye hii video.

 
Hawa wazee wengine walikuwa watu wa mfumo ambao kwa Tanzania walikuwa na majina makubwa sana, walikuwa wanaweza kustawi kwa majina yao, waliona wakitoka nje nyota zao hazitang'ara, watakuwa just onother bloody African, wakaona bora wabaki ndani tu watambe kwa mfumo wa "unanijua mimi ni nani wewe?".

Waliona wakienda Ulaya hawawezi kutumia mfumo wa "unanijua mimi ni nani wewe?".

Rais Rutto wa Kenya alikwenda South Korea, akawa anawaambia Wakenya walio South Korea kwamba anataka kuongeza idadi ya Wakenya South Korea, waende kufanya kazi huko na kuongeza hela wanazotuma Kenya.

Siasa za Kenya zina mengi sana, na mimi si Rutto supporter, ila, katka hili, namkubali sana William Rutto, anajua anataka nini, anajua nchi yake ina nini cha ku offer, na anaonekana ku support hilo. Huku Tanzania hatuna political will hapo juu. Kuachia uraia pacha tu ni mgogoro.

Msikilize Rutto kuanzia dakika ya pili kwenye hii video.


Nimeisikiliza yote. Na siwashangai, Wakenya na Viongozi wao ni watu wanaojitambua.

Wakati viongozi wetu wakiwaonea wivu watu wao kwenda "duniani", Ruto anajisikia fahahari Wakenya kutapakaa ulimwenguni kote.

"...as Kenyans we have the best human capital all over the global...speaking good English, creative, innovative, hard working, self driven, friendly, educated...you rarely get those many qualities in one...of human beings, but you get in Kenya. And is because of that spirit that Kenyans are different everywhere they go" - William S. Rutto.
 
Watu wenye mentality za kishamba hivyo wafukuzwe haraka hapo uhamiaji....

Hao ndo wale wamekuja Dar tayari watu wazima...ushamba haujawatoka bado
Ni ulimbukeni tu. Ndiyo maana Wahenga walisema, "Maskini akipata...hulia mbatwa"
 
Pole mno mkuu,na tuendelee kulalama humu, Passport ni HAKI YAKO KIKATIBA, ila tatizo ni la middle class kulalama bila ya push back, NIDA ilitakuwa iwe ndio documents pekee ya kuombea Passport, tatizo systems za nchi yetu haziongei!ni za Kachina,ndio maana ukiwa immigrations ni vichekesho vitupu,counter 1 anakukatalia kukupa exit stamp, unaenda nje unapata fresh air, then unarudi tena unaenda counter 4 unagongewa exit stamps!,systems ya counter 1 haiongei na ya counter 4!!,it's craze
Sijui Wabunge wenyewe wanalionaje hilo!

Au siyo tatizo kwa kuwa wao wakishaitwa tu "MHESHIMIWA" na passport anapewa hata kama hajaomba.
 
Kwa hali hiyo rushwa itakaa ipungue?
Hawezi kuisha, fata process uone shughuli yake.
Barua katibu kata, serikali za mitaa, balozi nyumba 10.
Mashahidi 3
Nilipeleka vyote document
Nikawa napigwa kalenda tu
siku ofisa wao mwenyewe kasema lainisha kidogo shauri lako liende fasta
nikajua hela hapo
Na bado ukifika pale utapigishwa kwata sana tu.
Mwisho utaishia kuhonga tu
 
"
Hawezi kuisha, fata process uone shughuli yake.
Barua katibu kata, serikali za mitaa, balozi nyumba 10.
Mashahidi 3
Nilipeleka vyote document
Nikawa napigwa kalenda tu
siku ofisa wao mwenyewe kasema lainisha kidogo shauri lako liende fasta
nikajua hela hapo
Na bado ukifika pale utapigishwa kwata sana tu.
Mwisho utaishia kuhonga tu
"... lainisha kidogo..."

Mbona kwa NIDA hawafanyi hivyo?
 
Mwanzoni mwa mwaka huu, nilienda Mutukula kufanya manunuzi ya vitu fulani. Niliamua kuvifuata huko kwa sababu niliamini bei ni nafuu zaidi kuliko nilikokuwa. Kuna wafanyabiashara wanaofuata mizigo yao huko. Ikiwa wao wanafuata huko na kuja kutuuzia tuliko, nilijua, kwa vyo vyote, bei ingekuwa ni ya chini kuliko wanayouzia.

Nilipofika Mutukula, nilipata wazo jingine. Kweli mzigo niliouhitaji ulikuwepo hapo kwa bei nafuu kama nilivyodhania, lakini nilibaini na wenyewe wanaufuata Kampala. Nilipopiga hesabu ya kwenda Kampala na kurudi na mzigo, niligundua ningeokoa kiasi kikubwa cha fedha. Nikaona bora niende Kampala.

Kwa sababu sikuwa na pasi ya kusafiria, nilienda ofisi za Uhamiaji kuomba usaidizi wa kupatiwa TRAVEL DOCUMENT, alau niweze kufika Kampala. Ilishindikana. Mlolongo niliopaswa kuufuata ungeishia kuniongezea gharama zaidi, na ingenichukua muda mrefu kidogo kuukamilisha. Nilifikiri kitambulisho cha Taifa(NIDA), kingeweza kuwa mbadala wa nyaraka zilizohitajika, lakini sivyo.

NIDA haikutosha. Nilihitajika kuwa na cheti changu cha kuzaliwa na cha wazazi, pamoja na barua ya Afisa Mtendaji wa Kata yangu. Sikuwa na hizo, sikutembea nazo. Na kuvifuata, ingenigharimu zaidi.

Kama ningekuwa na PASSPORT, nisingekwama kwenda kuchukua mzigo Kampala, kwa bei nzuri zaidi.

Lakini kwa nini yote hayo? Kwa nini Serikali isiondoe kipengele cha mpaka mtu awe na Safari ndipo apewe PASSPORT? Akipewa akakaa nayo kusubiria fursa ya safari itaipotezea Serikali kitu gani?

Miaka ya nyuma, nilijaribu kutafuta PASSPOT lakini vipengele viwili vilinikwamisha.

Cha kwanza, waraka unaothibitisha kuwa nina Safari.

Cha pili, tiketi ya ndege.

Unajua vitu vingine vinachekesha ee! Kukata tu tiketi ya basi kwenda Nairobi, watahitaji Namba ya passport, na ndege, tena za masafa marefu itakuwaje?

Unakataje tiketi ya ndege kabla ya kupata passport? Hiyo haiwezi kuwa ni namna mojawapo ya kutengeneza mianya ya rushwa?

Fikiri ofisa anayekuhudumia akafahamu kuwa umeshakata tiketi, kama siyo mwadilifu si anaweza akakusudia kukusumbua ili tu uzungumze kwa ile staili wengine wanayoiita, "kikubwa?"

Uganda, kwenye fomu yao ya maombi ya pasi ya kusafiria, wamewatahadharisha watu wao wasikate wala kufanya booking ya tiketi kabla ya kupata passport! Unaona utofauti wa viongozi wenye "exposure" na wasiokuwa nao?

Kuna wakati fulani nilienda Nairobi - Kenya, ilikuwa 2018. Nilipomweleza rafiki yangu masikitiko niliyokuwa nayo kwa sababu ya vikwazo visivyo na "umuhimu" kwenye upewaji wa passport, alinishauri nifanye application ya kusoma kwenye moja ya Vyuo Vikuu Nairobi, siyo kwamba ili kweli nisome, bali nitumie barau ya kuitwa Masomoni Nairobi kuombea Passport nyumbani TANZANIA. Sikufanya hivyo.

Rafiki yangu mwingine aliyekuwa akifanya kazi Dubai alitaka kuniandikia barua ya mwaliko "fake", ili niiutumie kuombea Passport. Hilo nalo pia sikulifanyia kazi.

Sijui kama wote waliopewa passport, walitaka kusafiri kwa wakati huo au walilazimika kudanganya, kwa kutengeneza, labda mialiko ya michongo.

Serikali haijui kuwa Watanzania wengi wa sasa si wajinga, wanafahamu umuhimu wa kuwa na passport? Kwa mwingine, ukimbania kupata kihalali, atapitia mlango wa nyuma. Atadanganya na ataipata. Halafu bado Serikali inataka raia wawe wakweli wakati ni yenyewe inayowatengenezea mazingira ya kudanganya. Afanyeje Sasa!

Hiyo itakuwa ni ajabu kuwa Wafanyabiashara wengine wanakwepa kulipa kodi? Ni kwa sababu hizo hizo, anapobanwa isivyostahiki, anatafuta pa kutokea. Atadanganya.

Mpaka sasa bado sina passport, ingawa naamini nitapata tu. Sababu ya kuipata ninayo, na kwa sababu ninaamini ni haki yangu kuwa nayo, haitanipiga chenga.

Lakini kwa nini Serikali inajitahidi kuweka ugumu wa watu wake kupata passport? Nitakosea nikisema kuwa baadhi ya Viongozi wetu wana mawazo mgando?

Fikiria, kwa mfano, inaweza ikatokea fursa, labda ya kikazi nchini Sudan, inayohitaji kujazwa haraka na mtu kutoka ndani ya EAC, unafikiri ni raia wa nchi ipi watakaokuwa tayari kuidaka?

Watanzania wengi wanaweza wakawa na sifa kwa hiyo nafasi, lakini mpaka watakapomaliza kushghulikia "TRAVEL DOCUMENT", itakuwa imeshakuwa "too late" kwake. Yule ambaye nchi yake inafahamu kuwa kuwa na passport ni kuwa tayari kwa fursa zitakazotokea nje ya mipaka yake, atakuwa ameshainyakua. Sana sana hiyo nafasi inaweza ikaenda kwa Mkenya au Mganda au Mnyarwanda, nchi ambazo viongozi wao Wana "exposure" kubwa.

Nilishasoma mahala fulani kipindi cha nyuma, nafikiri ni humu Jamii Forum, makala yaliyoandokwa na Mtanzania mwenzetu akihoji sababu iliyomfanya Rais wa Kenya wa enzi hizo, Mwai Kibaki, kuwaambia Watanzania waende wakatembee Kenya kwa sababu anajua kuwa Watanzania huwa hawasafiri.

Lakini pia na mwingine alishawahi kusema kuwa hayati Jomo Kenyatta, ambaye alikuwa Rais wa kwanza wa Kenya, alishamkejeli baba wa Taifa kuwa anawaongoza maiti. Sijui kama ni kweli alisema hayo, na kama alisema, ... acha niishie hapo.

Eti bila uthibitisho wa safari hupewi Passport! Hongera nchi yangu Tanzania, lakini hututendei haki kujitahidi kutufungia ndani mithili ya mbuzi wasumbufu.

Tarehe 16 March, 2021, mwana Jamii Forum, Erythrocyte, alipandisha bandiko humu jukwaani lenye kichwa kisemacho, UHAMIAJI TANZANIA: BILA DHUMUNI LA SAFARI HAKUNA KUPEWA PASI YA KUSAFIRIA.

Alielezea msimamo wa Serikali kupitia kwa kiongozi wa Uhamiaji, ambaye alisisitiza, pamoja na mambo mengine, ni lazima mtu athibitishe kuwa na safari ndiyo atapewa passport.

Nilisikitishwa sana, na kushangazwa pia na huo msimamo.

Kwa nini wasiangalie vinavyofanywa na nchi zingine? Hawaoni jinsi Kenya, Uganda na Rwanda walivyowarahishia watu wao mchakato wa pasi ya kusafiria? Au Serikali haipendi watu wake wasafiri?

Inashangaza, na inasikitisha. Ni mtazamo na msimamo wa kijima kabisa. Aiseei!!! Sera ya UJAMAA ingali inaitesa Tanzania, kabisa.

Rafiki yangu mmoja kutoka moja ya makabila yanayosifika kwa biashara hapa Tanzania alishawahi kunisimulia jinsi baadhi ya wazee wa huko kwao walivyokuwa wakifurahia watoto wao kusafiri. Walijua ni njia mojawapo ya kuwafungua akili, na kujua jinsi ulimwengu unavyoenda. Ilikuwa kama ukatili fulani hivi, lakini baadhi waliweza "kutoka" kimaisha kwa njia hiyo.

Ilikuwa kwamba, mtoto anapomaliza shule, madhalani shule ya Msingi, kama hajafaulu kwenda Sekondari, alikuwa haachwi akae tu nyumbani. Alikuwa anafanyiwa mpango wa kusafiri kwenda ama Dar Es Salaam au miji mingine mikubwa ndani na nje ya Tanzania.

Kama hana ndugu maeneo hayo, kijana(wa kiume tu) alikuwa akipewa nauli na kuambiwa aende kwa ndugu yake anayeishi sehemu fulani katika jiji fulani, labda Nairobi. Walikuwa wakipendelea "kuwatuma" kwenye miji mikubwa ya mbali ambayo haikuwa rahisi kurejea nyumbani bila nauli. Na alikuwa akipewa nauli ya kwenda tu na hela ya kula njiani, huku mzee akifahamu fika kuwa huko anakomtuma mtoto hakuna cha ndugu wala jamaa.

Alikuwa anajua kuwa akifika huko, akiteseke kidogo, atajiongeza kutafuta namna ya kusurvive, na akimudu, anaweza akaishia kuanzisha biashara itakayokuwa na mafanikio. Kwa maelezo ya rafiki yangu, kuna waliotumwa kwa staili hiyo na wakaishia kuwa wanyabishara wenye mafanikio makubwa sana.

Hao wazee hawakuwa wamesoma, lakini walikuwa na uelewa kiasi cha kujua umuhimu wa kuwatafutia watoto wao exposure. Walionekana kama ni wakatili, lakini walikuwa wakiona mbali.

Ingekuwaje kama viongozi wetu na wenyewe wangekuwa wanawaza kijasiriamali kama hao wazee? Bila shaka, kungekuwa na kiasi kikubwa zaidi cha pesa kinachoingia nchini kila mwaka, kutoka kwa Watanzania watakaokuwa wametapakaa mataifa mbali mbali.

Kwa nini viongozi wetu wanatubania passport? Wanataka wao tu na familia zao ndiyo wawe nazo, ili tusibanane nao Airport?

Wameweka sharti kwamba lazima mtu athibitishe safari ndipo apate passport, lakini inawezekana wengi wao walishawakatia wenza wao na watoto wao nyakati ambazo hawakuwa na mpango wa kusafiri. Ndiyo, inawezekana wamewakatia, ili ikitokea siku "akafurahi" na kuamua kuruka chap hadi Dubai na familia yake kula ICE CREAM, passport isiwatie kiwingu.

Ni vyema Serikali ikaliangalia hilo upya.

Passport haitolewi bure, zikitolewa kwa wingi, Serikali nayo inapata mapato.

Passport inaweza kumhamasisha mtu kusafiri, na kusafiri kutamsaidia mtu kuongezeka na kupanuka uelewa. Kusafiri ni "shule" mojawapo maishani. Kutachochea ubunifu wa kuona, kutengeneza na kubaini fursa za mafanikio.

Passport inamuweka mtu tayari kwa fursa itakayojitokeza itakayohitaji mtu kusafiri.

Inasemekana Wakenya na Waganda wanaofanya kazi Dubai ni wengi kuliko Watanzania. Kwa nini hivyo?

Inawezekana ni kwa sababu Wana viongozi wanaojitambua. Serikali zao zinawajali sana, ndiyo maana haziwabani katika suala la kupata passport. Zimefanya kila linalowezekana, ili kila raia anayehitaji apate.

Kuna mtu anaweza akaniambia Watanzania hawazipendi hizo fursa zinazofurahiwa na Wakenya, Waganda, Wanyarwanda, Wanaigeria n.k.?

Ujamaa! Ujamaa!!! Ujamaa, kwa kiasi fulani, uliathiri kufikiri kwa Viongozi wetu. Mpaka sasa, bado kuna wenye "hangover' ya fikra za kijamaa. Ndilo tatizo, nafikiri!!!

Lakini kwa wenzetu, Wakenya na Waganda, viongozi wao walifahamu mapema kuwa fursa si za kusubiria. Ni ama kuzitengeneza au kuzifuata zinakopatikana. Wanawaza kifursa kwa sababu hawakulogwa na ujamaa.

Serikali isiwafungie watu wake ndani. Watanzania siyo kondoo wa kufugwa. Ni watu wenye akili, na ni watu wanaojiheshimu.

Siyo wahalifu, ni watu wema.

Serikali isiwafungie watu wake ndani ya mipaka. Iwahamashishe "watoke", itakuwa faida kwao na kwa Serikali.

Iwarahishie kwa kuwaondolea vikwazo visivyo na umuhimu katika ufuatiliaji wa passport.

Nimeangalia taratibu za Kenya, Uganda na Rwanda kwenye utoaji wa PASSPORT. Wako very "smart". Hawana longo longo kama za Tanzania.

Hatupaswi kupitwa na hizo nchi, zenyewe ndizo zinapaswa kuja kujifunza kwetu. Sisi ni Taifa kubwa.

Please Tanzania, amka! Zama za UJAMAA zilishapita.

Tanzania, Tanzania, usitubanie kupata passport.

Asante.
Usitegemee akili mgando ya kikoloni ikaleta mabadiliko chanya katika hili. Wao wanaamini kufanya hivyo ni katika kutulinda wakati kiuhalisia ndio inakandamiza, kukosesha watu fursa na kutengeneza mazingira ya rushwa katika kupata hizo passport.

Kimsingi kwa dunia ya sasa maendeleo yanakwenda kasi na wenye dhamana ya kukalia ofisi bado wapo karne ya 20 na mbaya zaidi hawataki kubadilika kwenda na usasa na nini dunia inataka.
 
Tanzania viongozi wengi na watu wengi wenye mamlaka ni malimbukeni waliojawa roho mbaya.

Yani ukiomba tu passport wanaona kama vile utatoboa kimaisha kuliko wao.

Huu ujinga unatakiwa ukemewe kwa nguvu zote.

Mtu akitaka passport vigezo vikuu viwe kitambulisho chake cha NIDA na malipo ya passport tu.

Longolongo nyingine zikomeshwe.
 
Tanzania viongozi wengi na watu wengi wenye mamlaka ni malimbukeni waliojawa roho mbaya.

Yani ukiomba tu passport wanaona kama vile utatoboa kimaisha kuliko wao.

Huu ujinga unatakiwa ukemewe kwa nguvu zote.

Mtu akitaka passport vigezo vikuu viwe kitambulisho chake cha NIDA na malipo ya passport tu.

Longolongo nyingine zikomeshwe.
Kama tumeshindwa kubuni namna ambayo ni bora kwetu, tuige basi hata ya wenye "akili" kama Kenya, Uganda au Rwanda.

Haina maana kutumia mbinu za enzi za Ukoloni katika karne hii.
 
Hizi ni tabia za serikali za kikomunisti na mabaki ya ujamaa.

Serikali inawafungia watu ndani wasione dunia inaendaje, wakiona watafunguka macho na kudai maendeleo nyumbani.

Kuna mzee mmoja alikuwa anafanya kazi East African Community ile original ya miaka ya 1970s, alikuwa anasema wenzao Waganda na Wakenya walikuwa wanachangamkia fursa za kwenda Ughaibuni kusoma na kufanya kazi, ila Watanzania mtu akichangamkia hizo fursa alikuwa anaonekana msaliti.

Kuna Mama mmoja alikuwa anafanya kazi serikalini, alikuwa anajisifia kabisa kwamba yeye hana tamaa ya kwenda nje, aliina hiyo ni sifa nzuri.

Ni tabia za nchi za kikomunisti.
Ukomunist ni upuuzi kabisa
 
Pole mno mkuu,na tuendelee kulalama humu, Passport ni HAKI YAKO KIKATIBA, ila tatizo ni la middle class kulalama bila ya push back, NIDA ilitakuwa iwe ndio documents pekee ya kuombea Passport, tatizo systems za nchi yetu haziongei!ni za Kachina,ndio maana ukiwa immigrations ni vichekesho vitupu,counter 1 anakukatalia kukupa exit stamp, unaenda nje unapata fresh air, then unarudi tena unaenda counter 4 unagongewa exit stamps!,systems ya counter 1 haiongei na ya counter 4!!,it's craze
,[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Me kupata passport imekua changamoto kidogo coz cheti changu cha kuzaliwa kilikosewa tarehe ya kuzaliwa
Nkaenda Rita kubadili cheti cha kuzaliwa nkafanikiwa nkapeleka Kule uhamiaji lakini cha ajabu Passport ikatoka ikiwa imeandikwa Ile tarehe ya mwanzo ya kuzaliwa yenye makosa (cheti cha mwanzo)
Nimeirudisha ile passport uhamiaji ili waanze upya mchakato

Wameniambia kuwa passport kukosewa tarehe ya kuzaliwa sio big issue lakini mimi sijaridhika kabisa nimekubali kuingia hasara ya kujaza form upya
 
Hawezi kuisha, fata process uone shughuli yake.
Barua katibu kata, serikali za mitaa, balozi nyumba 10.
Mashahidi 3
Nilipeleka vyote document
Nikawa napigwa kalenda tu
siku ofisa wao mwenyewe kasema lainisha kidogo shauri lako liende fasta
nikajua hela hapo
Na bado ukifika pale utapigishwa kwata sana tu.
Mwisho utaishia kuhonga tu
Mm pia imenikuta hii mpaka sasa nimenyimwa
 
Back
Top Bottom