Serikali inaogopa nini kufanya lugha ya kufundishia iwe kingereza kuanzia shule ya msingi hadi chuo kikuu?

Umesema private school na sio za serikali ama
Sasa kwani hakuna somo la kiingereza mashuleni?
Mbona kijana wa form 4 hawezi kuongea
Hapo tatizo ni nini wakati wapo waalimu wa masomo.hayo
Hakutaka kujibidiisha. Ukienda shule za kanisa (RC) kama mtoto hajitumi Wana kwambia mzazi mtafutie shule nyingine. Sijajua shule za dini nyingine na shule za serikali
 
Tuma walimu ambao ni akina mwanasesele na mwanambilimbi kiingereza sifuri unaanzaje, labda waalike experts from foreign neighbouring countries
 
Wenye teknolojia woooote huko duniani, mashule yao hufundisha kwa lugha za kwao, lugha inayotakiwa kufundishia hapa Tz ni kiswahili .
 
Umeshawahi kusikia Inglishi ya wale vipanga wa hisabati na fizikia? Unaweza kucheka hadi upasuke.

Lakini shughuli yao kwenye masomo si ya kitoto. Same applies kwenye masomo mengine.

Lugha is very important, but should never be overrated.
Ushasema ni vipanga. Lugha ndio inayotumika kufundishia hivyo huwezi kuichukulia poa namna hiyo. Matokeo yake tunakuwa na vipanga waliokariri vitu ambavyo hawavielewi.
 
Hakutaka kujibidiisha. Ukienda shule za kanisa (RC) kama mtoto hajitumi Wana kwambia mzazi mtafutie shule nyingine. Sijajua shule za dini nyingine na shule za serikali
Sasa kwanini wasimsaidie mpaka aelewe badala ya kumvunja moyo mzazi
Kuna watoto wasioelewa Autistic ila kama yuko sawa mbona anafundishwa vizuri tu
Au wanataka the finest
 
Watakubaliaje kiinglish wakati wenyewe hakipandi mwanangu? Watakubalije wakati wakishasomesha watoto wao kiinglish wanakitumia kunyonyea wengine?
Watatumiaje kiinglish wakati wanataka kuzalisha wajinga wengi ambao ni rahisi kuwaibia na kuwatawala kama ilivyo?
Kiinglish chanini wakati kitawawezesha wabongo kujua mambo wasiyopaswa kujua na kuasi?
Napendekeza tutumie kimakonde mashuleni lau tujue kitu.
 
.Fact.
 
Ndiyo maana kwenye mikataba nchi yetu inapigwa! Wanasheria wetu hawajui Kiingereza!
Kupigwa sio kutokujua kingereza, shida ni rushwa na umimi ndio maana tunapigwa mikataba mibovu.
JPM tulikua tukimsema hajui kingereza lakini haikutaka mikataba mibovu kwake na hata iliyokua imeingiwa baadhi alianza kuivunja.
Kwahiyo ishu sio kingeresa
 
Kila taasisi na taratibu zake

Leo feza ukiwa top 3 au 10 kitaifa katika mitihani ya kitaifa ya kidato cha pili, nne

vile vile mitihani ya darasa la nne na la saba wanakupa ufadhili wa kusoma bure shuleni kwao kama sikosei

NB
ilikuwa ni muda kidogo kipindi cha top top za kitaifa, sasa hivi hawatangazi tena hayo ma top top

kwanin wachukue top kwanini wasitengeneze top??

kila taasisi na taratibu zake, ukiwauliza watakujibu vizuri

Sasa kwanini wasimsaidie mpaka aelewe badala ya kumvunja moyo mzazi
Kuna watoto wasioelewa Autistic ila kama yuko sawa mbona anafundishwa vizuri tu
Au wanataka the finest
 
Hata huko vyuoni msipoelewa Lecturer anabidi amwage kisakwinga kingi sana.

Lugha muhimu ni kichina ikiwa Taifa litaangalia miaka 50 au 100 ijayo.

Nje ya hapo, mkazo uongezwe kwenye kiswahili kwa ngazi zote na kiingereza kibakie somo tu.
 
Ajira za lugha ya kiswahili zinahitajika sehemu mbalimbali duniani

Leo wazungu wanajifunza kiswahili wakiwa kwao, wanakuja huku wakiwa wanafahamu angalau kidogo na zaidi

Balozi zetu zinafanya vizuri mfano ubalozi wa Tanzania Korea kusini, taasisi binafsi na vyuo kadhaa vina toa elimu ya lugha ya kiswahili huko ulaya na marekani (ujerumani, uingereza, marekani nk)

Hivyo kiswahili kina songa mbele kwa mwenye kukithamini, wapo ambao kingereza cha nini na wapo ambao wanakithamini kama unavyofanya
 
Jambo hilo lilishafanyiwa utafiti matokeo yakaonekana haiwezekani . Sasa sijui wewe unalenga nini mdau
 
Hata huko vyuoni msipoelewa Lecturer anabidi amwage kisakwinga kingi sana.

Lugha muhimu ni kichina ikiwa Taifa litaangalia miaka 50 au 100 ijayo.

Nje ya hapo, mkazo uongezwe kwenye kiswahili kwa ngazi zote na kiingereza kibakie somo tu.
Bado una uhuru wa kujifunza lugha zaidi ya moja

Kihindi, Kichina, kifaransa, Spanish, kireno na hata kiarabu. Sio Vibaya kujifunza lugha zaidi na lugha ikumbukwe ni kwa ajili ya kurahisisha mawasiliano

Unaweza kwenda sehemu ukajikita unatakiwa uanze kujinoa na lugha mpya. Mfano unaenda SA ukijua utapiga kizungu tu lakini utaongeza kishona au kizulu nk

Utaenda ulaya (sweden) utajikuta unajifunza kiswedesh, maisha yatakufundisha vitu vingi kama utaruhusu kufanya hivyo
 
Wanataka tofauti ya watoto wa kishua na wa Uswazi iwe dhahiri, kwenye nafasi za kazi hasa za mashirika ya kimataifa na opportunities za kazi nje ya nchi.
 
Tatizo la elimu yetu siyo lugha ya Kiswahili wala Kiingereza. Shida kubwa iko hasa kwenye miundombinu, vifaa/nyenzo za kufundishia na walimu mahiri na mazingira bora na wezeshi kwa walimu na wanafunzi.
Lugha ni tatizo kubwa sana
 
Inasikitisha sana
 
ACHA UJINGA

hutaki wenzio nao wajue kiingereza et eee,PIMBI
 
Kwa hiyo wakitumia kiingereza ndo watoto watakuwa na uelewa mkubwa?...
Kiingereza ni lugha tu mkuu mataifa yaliyoendelea yoote yanatumia lugha zao kufundishia acheni kushobokea lugha za watu! Kiingereza ukitaka kukijua unakijuq tu hata kama hujaenda shule hakihusiani na akili wala maarifa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…