Serikali inapaswa ianzishe Kariakooo nyingine maeneo ya Mbezi Louis

Serikali inapaswa ianzishe Kariakooo nyingine maeneo ya Mbezi Louis

zandrano

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2017
Posts
7,893
Reaction score
8,816
Tatizo kubwa ni kuwa na soko kubwa eneo moja ndio maana wafanyabiashara wanapata jeuri ya kuivimbia Serikali, kuna haja sasa kwa Serikali kuanzisha soko kubwa la kimkakati katika maeneo ya Mbezi Mwisho karibu kabisa na stendi ya mabasi ya Magufuli.

Tumeona adha iliyo sababishwa na wafanyabiashara wa kkoo.

Mbezi mwisho ni eneo la kimkakati kwani ndipo lipo stendi ya mabasi kutoka mikoa mbalimbali pamoja na nchi mbalimbali, hivyo ni vyema Serikali ikaamua kujenga solo kubwa la kisasa ikawa ni kkoo nyingine badala ya kutegemea kkoo moja.
 
Why mbezi magufuli?
Kwasababu ndio lango kuu la kuingia katika Jiji la DSM.

Lakini stendi ya mabasi ya Magufuli inaingiza wageni wote kutoka mikoa yote na pia nchi jirani kama; Kenya, Uganda, Burundi, DRC, Malawi, msumbiji, n.k.

Pia Mbezi bado kuna nafasi ya kutosha, hakuna msongamano kama ilivyo kkoo.

Muda, wataokoa muda, mfanyaboashara atashuka kwenye basi Kisha atafanya manunuzi yake palepale bila kusumbuka kwenda kkoo.

Hivyo naishauri Serikali ijenge kkoo nyingine hapo Mbezi mwisho.
 
Mbezi Mwisho ipi hiyo isiyo na msongamano mkuu?
Huwezi kufananisha msongamano wa kkoo na Mbezi. Mbezi bado kuna nafasi ya kutosha.
Kkoo watu waneda kwajili ya mazoea tu lkn ni shida, msongamano mkubwa sana.
 
Tangu Mika ya 70 watu ni kariakooo tu! Hapana! Inabidi Serikali ya awamu ya 6 ifanye kitu tofauti, ianzishe soko kubwa la kimataifa maeneo ya Mbezi.
 
matozo yakiwa haya hata waanzishe masoko makuu kila kata, migomo haitakoma.
Wewe endelea kugoma ufe njaa, wenzako walio na maduka hapo kkoo Wana maduka maeneo mengine ikiwemo huko Mbezi wanaendelea kuuza kama kawaida.

Tatizo la kkoo kuna watu wamehodhi kila kitu!! hii ni hatari.
 
Kwasababu ndio lango kuu la kuingia katika Jiji la DSM.

Lakini stendi ya mabasi ya Magufuli inaingiza wageni wote kutoka mikoa yote na pia nchi jirani kama; Kenya, Uganda, Burundi, DRC, Malawi, msumbiji, n.k.

Pia Mbezi bado kuna nafasi ya kutosha, hakuna msongamano kama ilivyo kkoo.

Muda, wataokoa muda, mfanyaboashara atashuka kwenye basi Kisha atafanya manunuzi yake palepale bila kusumbuka kwenda kkoo.

Hivyo naishauri Serikali ijenge kkoo nyingine hapo Mbezi mwisho.
Bahati nzuri serikali imewaza hili kabla hata wewe hujaliwaza! Pale Ubungo ilipokuwa stendi kuu ya mabasi kunajengwa soko lenye hadhi ya kariakoo tena mkakati wake ni kwamba bidhaa kutoka China,UAE zitakuwa zinapatikana palepale kwa bei ile ile ya china.

After all eneo kariakoo huwezi kuita ni soko (ukiachana na lile soko la Mtaa wa Congo) ya kwamba serikali inaweza kujenga tu popote na kukawa kama kariakoo noo! Lile ni eneo tu la biashara(bussiness hub) halijajengwa na serikali kiuhalisia yale ni makazi ya watu walioamua kujiongeza kwa kujenga fremu kwenye nyumba zao matokeo yake mrundikano wa fremu ukazaa bussiness hub na sio kwamba serikali ndio imejenga,serikali kusema imejenga soko labda hapo inavyofanya ubungo sasa hivi,sijui umenipata hapa!
 
Wewe endelea kugoma ufe njaa, wenzako walio na maduka hapo kkoo Wana maduka maeneo mengine ikiwemo huko Mbezi wanaendelea kuuza kama kawaida.

Tatizo la kkoo kuna watu wamehodhi kila kitu!! hii ni hatari.
hata masoko mengine yakianza yatahodhiwa.
 
Bahati nzuri serikali imewaza hili kabla hata wewe hujaliwaza! Pale Ubungo ilipokuwa stendi kuu ya mabasi kunajengwa soko lenye hadhi ya kariakoo tena mkakati wake ni kwamba bidhaa kutoka China,UAE zitakuwa zinapatikana palepale kwa bei ile ile ya china...

After all eneo kariakoo huwezi kuita ni soko (ukiachana na lile soko la Mtaa wa Congo) ya kwamba serikali inaweza kujenga tu popote na kukawa kama kariakoo noo! Lile ni eneo tu la biashara(bussiness hub) halijajengwa na serikali kiuhalisia yale ni makazi ya watu walioamua kujiongeza kwa kujenga fremu kwenye nyumba zao matokeo yake mrundikano wa fremu ukazaa bussiness hub na sio kwamba serikali ndio imejenga,serikali kusema imejenga soko labda hapo inavyofanya ubungo sasa hivi,sijui umenipata hapa!!
Bado Ubungo hapatoshi ni pa finyu, Mbezi ni eneo zuri zaidi kibiashara na linaweza kuwa zaidi ya kkoo.

Tunqchotaka kusiqchiwe kuwe holela kama ilivyo kuwa congo/kkoo, kuwe na utaratibu wa kisasa .

Mbezi ni businesses hub nzuri zaidi kama Serikali itaweka miundombinu sahihi na mpangilio
 
Kwasababu ndio lango kuu la kuingia katika Jiji la DSM.

Lakini stendi ya mabasi ya Magufuli inaingiza wageni wote kutoka mikoa yote na pia nchi jirani kama; Kenya, Uganda, Burundi, DRC, Malawi, msumbiji, n.k.

Pia Mbezi bado kuna nafasi ya kutosha, hakuna msongamano kama ilivyo kkoo.

Muda, wataokoa muda, mfanyaboashara atashuka kwenye basi Kisha atafanya manunuzi yake palepale bila kusumbuka kwenda kkoo.

Hivyo naishauri Serikali ijenge kkoo nyingine hapo Mbezi mwisho.
Mbez bado kando ya mji. Hilo ni rahis kuzungumzika lkin ni ngum kutekelezeka. Kkoo Iko karib sna n city center... N pale ilipo ni karibu n bandari. Unalifham n Hilo?
 
Mbez bado kando ya mji. Hilo ni rahis kuzungumzika lkin ni ngum kutekelezeka. Kkoo Iko karib sna n city center... N pale ilipo ni karibu n bandari. Unalifham n Hilo?
Stendi ya kimataifa ipo Mbezi, inaingiza wageni kwa maelfu usiku na mchana.

Mbezi watu hawalali.

Kama soko kubwa la kisasa litaanzishwa basi biashara zitafanyika usiku na mchana.

Kwa sasa Mbezi ni centre.
 
Back
Top Bottom