Serikali inapaswa ianzishe Kariakooo nyingine maeneo ya Mbezi Louis

Labda Mpigi Magoe na Makabe
Mbezi bado kuna nafasi kubwa ilimradi tu maafisa wa mipango miji wafanye sketching,

tuodokane na mazoea ya kila kitu kkoo, kila mtu kkoo..

sasa Dar imekuwa na wakazi wameongezeka sana, kuna haja sasa ya kuepusha msongamano kkoo na kuanzisha soko kubwa la kisasa Mbezi.
 
Haswaa
Unajua sisi ujuaji mwingi ila viongozi huwa hawawazi na kutatua matatizo
Yote haya wanayaona ila kuyafanya ndio mzigo

Mambo mengi sana tuko nyuma ukikinganisha na mataifa mengine ila tunajifanya wajuaji lakini ndio washamba wakubwa na masikini wa kutupwa kuanzia akili

Imagine soko tangu miaka na miaka bado lipo moja tu wakati tungeweza kuwa na masoko hata matatu ya kimataifa

Enzi hizo mpaka leo yaani miaka 100 bado mpo tu pale pale
 
Wafanyabiashara wanadengua kwasabu Hakuna ushindani toka kenya ipate Uhuru sijawahi ona wafanyabiashara wamegoma...wabongo uswahili na siasa ushwara vinawaponza
 
Mzilankende Alivyoanzisha Bandari Kavu Maeneo Ya Kwara Lengo Ilikuwa Kuleta Wepesi Kwa Mizigo Na Endapo Inakwenda Nchi Jirani Iwe Kwa Haraka Na Wepesi
Kariakoo Nyingine Inatakiwa Iwekwe Mkoa Wa Morogoro Hapo Itasaidia Udhibiti Wa Endapo
Kinachoendelea Sasa Dar Es Salaam. Hakitawauza Watu Wa Nchi Jirani Na Nchi Kwa Ujumla



Maana Nchi Jirani Malawi, Zambia, Congo, Rwanda, Burundi
Watapata Wepesi Tofauti Na Sasa Ambavyo Serikali Inasema Maduka Yafunguliwe, Wamiliki Wanataka Kuongea Na Rais




Jambo La Kariakoo Ni Kubwa Mno Linaweza Kuleta Kuzorota Kwa Uchumi Nchi Nzima
Kutakapokuwa Na Masoko Makubwa Mikoani Mambo Yatakwenda Vizuri Sana
 
Tatizo ni kodi mkuu, kodi zimekuwa nyingi sana hata wakijenga kibaha kodi si bado zipo tu
 
Kwani wamegoma kwasababu tu soko ni moja?

Uhuni wanaofanya hao TRA hapo Kariakoo wasingeweza kuufanya kwenye hilo soko jingine unalopendekeza liwe Mbezi?
 
Mbezi tayari imeshakuwa mji mkubwa. Unless ungesema hata Kibamba ama Kibaha ndo kuna maeneo makubwa.
 
Wewe endelea kugoma ufe njaa, wenzako walio na maduka hapo kkoo Wana maduka maeneo mengine ikiwemo huko Mbezi wanaendelea kuuza kama kawaida.

Tatizo la kkoo kuna watu wamehodhi kila kitu!! hii ni hatari.
Sasa kama wana maduka mengine Mbezi kwanini watu/wafanyabiashara wanalialia kufungwa kwa maduka Kariakoo wakilalamika kwamba hawapati mahitaji muhimu?
 
Kulikua na tetesi soko kubwa litajengwa baada ya kupita kinyerezi kama unaelekea mbezi kuna sehemu inaitwa msitu wa nyuki,kijiografia pale palifaa sana maana ni katikati ya maeneo kwa dar,sijui ile idea iliishia wapi maana hata ile stendi ya kinyerezi mwisho ilisemekana itajengwa hapo
 
Hapana kkoo iliachiliwa sana, Serikali imekuja kushituka late!!
sasa hakuna budi kujipanga, ianzishe soko kubwa Mbezi tuache kungqngania kkoo
kwa kuwa wewe unakaa Mbezi; doko kuu lianzishwe katika kona kuu zote za Barabara inayoingia jijini, namaanisha Kilwa rd, Moro rd,. na bagamoyo rd. Pia pale gongolamboto, yani mtu anashuka airport ansingia shopping gongolamboto na kulala hukohuko mpaka anaondoka.
jiji la kibiashara ndio lipo hivyo sio kuvutia maslahi
 
you took it wrong. hili ni suala la kitaifa maana ni sheria kuu kwa nchi nzima. wafanyabiashara wa kariakoo hawagombani na mamlaka ya soko au eneo la kariakoo. anagombana na serikali kwa sababu ya sheria mpya ya bajeti/kodi
 
you took it wrong. hili ni suala la kitaifa maana ni sheria kuu kwa nchi nzima. wafanyabiashara wa kariakoo hawagombani na mamlaka ya soko au eneo la kariakoo. anagombana na serikali kwa sababu ya sheria mpya ya bajeti/kodi

Tatizo baadhi ya wafanyabiashara wa hapo kkoo wanaifanyia ubabe Serikali!!!

Waziri Mkuu alikuja hapo na akawaonyesha uungwana wa Hali ya juu sana lakini baadhi Yao waliendelea kukaidi ombi la waziri Mkuu, huko ni kukosa adabu.

Sasa Leo j.tano trh 17/5 mtaenda kuongea nae nn wakati mlimpuuza.
Kwa tabia kama hii walio ionyesha baadhi ya wafanyabiashara kwa kukaidi ombi la PM ndio maana Hayati JPM alikuwa mbabe. Maana wabongo ukiwabembeleza watakukujolea kichwani.

Serikali isiyumbishwe, wakomae tuone watakula Nini....Serikali ikomae tuone nani zaidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…