Serikali inapaswa kujitathmini kwenye matokeo ya Kidato cha Nne ya mwaka 2019 kwa kutafuta sababu chanzi "root cause"

Serikali inapaswa kujitathmini kwenye matokeo ya Kidato cha Nne ya mwaka 2019 kwa kutafuta sababu chanzi "root cause"

Victor Mlaki

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2016
Posts
5,628
Reaction score
6,411
Mara kadhaa sasa tunashuhudia uradidi wa kutafuta chanzo cha tatizo na kimbilio likiwa kwenye sababu zile zile "Walimu hawafundishi vizuri"na tunashuhudia adhabu zikitolewa ikiwemo ile ya kushushwa vyeo.

Ni kama tunaamini ukiumwa kichwa tu ni malaria na inatakiwa kumeza dawa ya kutuliza maumivu. Matokeo ya Kidato cha Nne (CSEE) ya mwaka 2019 yaliyofanyiwa uchambuzi na gazeti la Mwananchi yanaonesha kati ya shule za Serikali zilizoingia 100 bora ni shule saba (07) tu na mikoa iliyofanya vizuri ambayo ni Mwanza na Kilimanjaro inaonekana kuingiza shule kumi na mbili 12 kila mmoja.

Serikali inajitahidi kutenga fedha kwa ajili ya uendeshaji wa shule kila mwezi lakini pia inapaswa pia kutenga muda kwa ajili ya kusikiliza kilio cha shule zake kila wakati kwa sababu bado maadui watatu tunapambana nao na ujinga bado upo.

Afya na usalama wa Walimu mahali pa kazi "Teacher's Occupational health and safety"ni changamoto kubwa inayohitaji majadiliano ya pamoja "Collective bargaining "na nia thabiti ya kutafuta ufumbuzi kama tunatamani kwa dhati kabisa kuhakikisha shule zetu zinafanya vizuri kitaifa.

Mwalimu mwenye afya bora na anayefanya kazi kwenye mazingira safi na salama ni raslimali bora kabisa ya kuweka kusababisha ufanisi mkubwa kwenye sekta ya elimu.

Tafiti zinaonesha kuwa Nchi zilizoendelea zinatoa huduma za Afya na Usalama Maeneo ya kazi kati ya asilimia asilimia 10-20 huku Nchi zinazoendelea zikitoa kati ya asilimia 5-10 na Tanzania inaonekana kutoa huduma hizo chini ya asilimia 5. Jambo hili linakwamisha kwa kiasi kikubwa siyo elimu tu bali hata maeneo mengine ya kazi.

Pamoja na Wakala wa Afya na Usalama Mahali pa kazi Nchini "Occupational Health and Safety Agency (OSHA)kujitahidi katika kutanua wigo kwa kuondoa urasimu kwenye usajili, kuongezeka maradufu kwa usajili mwaka 2019.Bado maeneo mengi yaliyopo vijijini ambako shule zetu zipo hayajafikiwa (kuna tafiti zilizowahi kuonesha kuwa ni asilimia 24%tu ya maeneo ndiyo yaliyotembelewa huku asilimia 76% yakiwa bado hayajafikiwa kabisa.

Afya na Usalama ni Mtaji bora kabisa wa kufikia Muono wa Taifa wa mwaka 2025 na Malengo ya Maendeleo endelevu ya Dunia 2030.
 
Aina ya watoto wanaoingia shule za sekondari za Serikali naonni pasua kichwa kulaumu Serikali au walimu Mara ingine Ni kuwaonea
 
Aina ya watoto wanaoingia shule za sekondari za Serikali naonni pasua kichwa kulaumu Serikali au walimu Mara ingine Ni kuwaonea
Mwalimu ameandaliwa kuwatengeneza watoto hata kama ni wabovu ila ili aweze kufanya kazi yake kwa ufanisi anapaswa kuwa mzima na salama.
 
Tuanzie hapa wewe ni mwalimu kama sio mwalimu usiongee hitu usivyo vijue hivi unafahamu kuna watoto wanatoka shule za msingi hawajui kusoma na kuandika pili wengine hata kuongea kiswahili ni shida anakuja anakuja is secondary anakutana na lugha geni kwake hebu fikilia kimbembe kilichopo hapo mpo mjini ndio maana hamjui aza ya vijijini
Mwalimu ameandaliwa kuwatengeneza watoto hata kama ni wabovu ila ili aweze kufanya kazi yake kwa ufanisi anapaswa kuwa mzima na salama.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tuanzie hapa wewe ni mwalimu kama sio mwalimu usiongee hitu usivyo vijue hivi unafahamu kuna watoto wanatoka shule za msingi hawajui kusoma na kuandika pili wengine hata kuongea kiswahili ni shida anakuja anakuja is secondary anakutana na lugha geni kwake hebu fikilia kimbembe kilichopo hapo mpo mjini ndio maana hamjui aza ya vijijini

Sent using Jamii Forums mobile app
Professionally Mimi ni Mwalimu haswaa.. na nimeandika nikiwa naelewa ni kwa nini nimeandika kila neno hapo.
Ipo hivi Kaka Mwalimu haandaliwi kufundisha wanaoelewa tu ila Wanafunzi wa aina zote na ninachoamini ili Waalimu tufanye vizuri sharti shule zetu ziwe katika mazingira yanayoruhusu ufundishaji wa Wanafunzi wa aina zote.
 
Ulichoandika kinaonyesha wazi Kama ulisomea ualimu hukuelewa ulichofundishwa.Kusoma na kuandika mtoto hufundishwa shule ya msingi.Sekondari sio sehemu ya mtu kufungishwa kusoma na kuandika.Mwenzio kasema vijijini mtoto anakuja sekondari hajui kusoma na kuandika unamfundishaje masomo ya sekondari ?
 
Ulichoandika kinaonyesha wazi Kama ulisomea ualimu hukuelewa ulichofundishwa.Kusoma na kuandika mtoto hufundishwa shule ya msingi.Sekondari sio sehemu ya my kufungishwa kusoma na kuandika.Mwenzio kasema vijijini mtoto anakuja sekondari uakuja kusoma na kuandika unamfundishaje masomo ya sekondari ?
Nakuja na jibu lako jioni Mkuu
 
Nakuja na jibu lako jioni Mkuu
Sawa ila ujue Wengine huenda sekondari bila kujua kusoma na kuandika sababu mitihani Ni multiple choice anajaza tu kwa kupiga ramli unakuta mwingine huyo kaibuka lakini kichwani mweupe.Ndio maana sgukebza sekondari private hutaka wafanye upya mitihani hawategemei necta tu
 
Pamoja na ukweli kuwa watoto wengi wanaanza elimu ya sekondari wakiwa hawajui kusoma na kuandika, serikali haithamini walimu. Iache kuwabagua walimu, itoe posho kwa walimu wote.
Sio wakuu wa shule pekee wanaostahili posho na nyumba ya kuishi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom