Serikali inashindwa nini kuboresha maeneo ya kitalii kama haya kujiongezea pesa kuliko kuendelea kukamua walalahoi kwa vitu vidogo?

Serikali inashindwa nini kuboresha maeneo ya kitalii kama haya kujiongezea pesa kuliko kuendelea kukamua walalahoi kwa vitu vidogo?

Kibosho1

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2017
Posts
2,621
Reaction score
4,293
Kwa sasa kilo moja ya ngano imefika 1500 na inakwenda juu, vivyo hivyo kwa sembe. Kuna jamaa mmoja kanipigia simu anadai bandarini huko wanakamuliwa sana ndio maana mitaani mambo yamebadilika.

Tuna maeneo mengi sana ya kitalii yanaweza kuingizia serikali pesa nyingi tu,shida inakuja je haya maeneo yanatangazwa?.

Asilimia kubwa ya maeneo yametangazwa na mabeberu pamoja na watalii wa ndani. Lakini tatizo limekuja kwenye miundombinu ya kufika huko. Barabara nyingi sana za kwenda maeneo hayo ni mbovu mno kiasi hata mtalii akifanikiwa kufika hawezi kufikiria kurudi tena.

Ushauri kwa serikali: serikali ya Tanzania inabidi sasa iige mfano kwa nchi ambazo zina maendeleo kwenye utalii kama Brazil, China nk. Wameboresha njia zao kuhakikisha mtalii hapati usumbufu.

Barabara,reli (metro train) hata cable car. Naamini tukiboresha sekta hiyo hata makodi ya madjs,mamc,kodi ya vitanda haitakuwa muhimu tena.
 
Bei ya chakula ikipanda, it means wakulima wetu wanafaidika sana. Mlizoea kuwanyonya wakulima wanaoshinda kutwa kuchwa shambani, juani, mvuani, tena wakifa njaa na kiu, ili tu kuwatafutieni chakula nyie mshindao kwenye viyoyozi ofisini na garini na majumbani mwenu. Unakuta ndizi moja kubwa tu -- saizi almost 30 cm ruler -- kutoka Moshi inauzwa 250 Tsh Dar. Unajiuliza hivi mkulima yeye mwanzoni huko migombani ameuza kwa shilingi ngapi hiyo? Sasa huyo mkulima ni wazi hapati tija yoyote kutokana na kilimo chake. It is not fair! Tuacheni tabia ya ulafi ya kuwaelemea wakulima wetu ilhali wao ndio wanatulisha. Nao wana haki ya kuwa mazilionea. Ukinunua ndizi moja kwa shilingi 500, mia saba ama elfu, basi unakuwa umemchangia kwa kiasi fulani mkulima huyo, tofauti na sasa ambapo mnazidi kumwibia na kummaskinisha. Halafu mnasema kilimo ni uti wa mgongo!??? Labda mngesema tu kwamba kilimo ni ^mauti ya mnyonge^ tungewaelewa.
 
Lafudhi chafu,mbwembe nyingi za kipuuzi lotion na lipstick zinauhusiano gani!
 
Mawazo mazuri sana haya! I wish hiyo serikali itafanyia kazi.
 
Lafudhi chafu,mbwembe nyingi za kipuuzi lotion na lipstick zinauhusiano gani!
Hii video sio mambo yote yana maana angalia tu jinsi watalii walivyofika kwa shida
 
Tatizo watanzania tulizoea kuishi kiujanja ujanja Ndio maana tunaumia
Ukitaka kufaidi awamu hii ya Rais mwema mwenye Moyo wa huruma na upendo kwa RAIA wake
Tii sheria bila shuruti
Lipa kodi
LA sivyo utaumia sana maana mianya ya wapiga dili imeziba kabisa
 
Wangepunguza Kodi ya magari yanayohusiana na mambo ya utalii na kupunguza gharama za wageni kuingia Tanzania na pia kupunguza Kodi ya uwanja wa KIA kwa ndege zinazotua pale ili ndege nyingi zifike kumwaga wageni ili waache kutua Nairobi kwenye Kodi kidogo huku coaster shuttle zikiwafata huko sijaelewa hilo nalo hawalioni Tanzania ni moja ya Nchi chache duniani yenye vivutio vingi sana sema hatujapata wasimamizi wanaojua thamani ya utalii.

Punguzeni Kodi ya macruiser hayo ili watu walete ya miaka ya karibuni 2020 na si ya 2006 harafu anaacha Dollar za kutosha ninyi mnaona sawa wakati hawezi kumshawishi mgeni mwingine aje au yeye mwenyewe arudi kwa kitu kingine..huo mlima Kilimanjaro kuupanda tuu ni hatari
 
Nimempenda dada mtoa video ni mtu wa kweeetu kule kanyigo eee !!
 
Hii video sio mambo yote yana maana angalia tu jinsi watalii walivyofika kwa shida
Huyo dada amenikera anavyoongea hata ladha ya hiyo video pia imenitoka,alafu hana msambwanda wala big boobs angalau tuzugwe na hivyo,Anashindwa na dada mmoja UTV nimemuona leo asubui amekaa lakini kitu kwenye kochi kimemwagika.Kipindi cha morning Trumpet leo.
 
Tatizo watanzania tulizoea kuishi kiujanja ujanja Ndio maana tunaumia
Ukitaka kufaidi awamu hii ya Rais mwema mwenye Moyo wa huruma na upendo kwa RAIA wake
Tii sheria bila shuruti
Lipa kodi
LA sivyo utaumia sana maana mianya ya wapiga dili imeziba kabisa
Sijaelewa kabisa malalamiko yako na hii mada vinausianaje
 
Bei ya chakula ikipanda, it means wakulima wetu wanafaidika sana. Mlizoea kuwanyonya wakulima wanaoshinda kutwa kuchwa shambani, juani, mvuani, tena wakifa njaa na kiu, ili tu kuwatafutieni chakula nyie mshindao kwenye viyoyozi ofisini na garini na majumbani mwenu. Unakuta ndizi moja kubwa tu -- saizi almost 30 cm ruler -- kutoka Moshi inauzwa 250 Tsh Dar. Unajiuliza hivi mkulima yeye mwanzoni huko migombani ameuza kwa shilingi ngapi hiyo? Sasa huyo mkulima ni wazi hapati tija yoyote kutokana na kilimo chake. It is not fair! Tuacheni tabia ya ulafi ya kuwaelemea wakulima wetu ilhali wao ndio wanatulisha. Nao wana haki ya kuwa mazilionea. Ukinunua ndizi moja kwa shilingi 500, mia saba ama elfu, basi unakuwa umemchangia kwa kiasi fulani mkulima huyo, tofauti na sasa ambapo mnazidi kumwibia na kummaskinisha. Halafu mnasema kilimo ni uti wa mgongo!??? Labda mngesema tu kwamba kilimo ni ^mauti ya mnyonge^ tungewaelewa.
Mangi wanaopata faida ni wanunuzi wa jumla na wauzaji wa rejareja sio mlaji wa mwisho
Unadhani mtu akinunua ndizi moja shs 50 Machame na baada ya gharama za usafiri na tozo mbalimbali atauza ile ile 50 Dar es salaam?
 
Back
Top Bottom