A
Anonymous
Guest
Fedha za OC (Other Charges) zinalenga kuwezesha uendeshaji wa shughuli za ofisi, ikiwemo kugharamia stahiki mbalimbali za watumishi zinazohusiana na utekelezaji wa majukumu yao.
Cha kusikitisha, watumishi wa kawaida wanapofanya kazi za ziada (Extra Duty) na kuwasilisha madokezo ya malipo, mara nyingi madokezo hayo hayalipwi hadi mwaka wa fedha unamalizika. Hata hivyo, kuna malalamiko kwamba madokezo yanayohusu baadhi ya wakuu wa idara hulipwa kwa wakati.
Hali hii imezua maswali miongoni mwa watumishi. Kila mwezi tunaelezwa kuwa Serikali inatoa fedha za OC kwa ajili ya uendeshaji wa shughuli za taasisi. Fedha hizo zinakwenda wapi, na kwa nini stahiki za watumishi wa kawaida hazilipwi kwa wakati?
Tunaomba Serikali na mamlaka husika zifanye uchunguzi na ukaguzi wa matumizi ya fedha za OC, ili kubaini namna fedha hizo zinavyotumika na kuhakikisha stahiki za watumishi zinalipwa kwa haki, uwazi na kwa wakati.
Tunaomba suala hili lifuatiliwe kwa kina na hatua zichukuliwe pale ambapo kutabainika matumizi yasiyo sahihi ya fedha za umma.