Serikali inavuna ilichopanda: Fundi Maiko Syndrome - Goba Collapse

Ndugu,
Nimesikitishwa na kilichotokea huko Goba, lakini tuweke sawa hapa....
Sijui unajua nini kuhusiana na hiyo ''force account'' uliyoitaja kwenye bandiko lako lakini ni wazi kuwa unataka kupotosha umma kwa makusudi ama kwa kutokujua.

Kwa lugha ya malkia maana ya ''force account'' - the part of the expense account of a public body (as a municipality) resulting from the employment of a labor force (as for garbage collection and the maintenance of streets) usually distinguished from the part resulting from contracting similar services with commercial agencies.

Hiyo ''force account'' inayotumika hasa kwenye manispaa na halmashauri mbalimbali nchini wala haina mahusiano na ujenzi holela au ujenzi wa kutokufuata taratibu na kanuni za ujenzi.

Hakuna mahali popote ambapo wizara ya ujenzi inatambua wataalamu wa ujenzi ama mafundi ambao hawajapata mafunzo.

Wizara kupitia taasisi zake kama ERB - Engineer's Registration Board na AQRB - Architect's and Quantity Surveryors Registration Board imekuwa ikisisitiza weredi katika ujenzi.

Hali kadhalika wananchi wanasisitizwa kila mara kutumia wataalamu wa ujenzi wanapotaka kujenga ikiwemo kusajili na kupeleka ramani ili zikaguliwe kwenye ofisi za manispaa zetu.

Swali, wananchi wangapi huwa wanaona umuhimu wa ramani za majengo kukaguliwa kabla ya ujenzi kuanza?.

Kwa kuwa JF ni home of Great Thinkers, tujitahidi kuleta habari zenye maana na zilizo za kweli.

Mungu azilaze mahali pema roho za marehemu. Amina.
 
Kwa muda mrefu sasa Serikali imepigia debe ujenzi wa majengo kwa kutumia Force Account na kutumia Local Fundi , ambaye mitaani anajulikana kama fundi Maiko.

Wananchi wameupokea mtindo huo kwa kuushangilia katika ujenzi wa majengo kwa nia ya kupunguza gharama.

Jengo lililoanguka huko Goba lilititia na kuanguka kama mbuyu uliojaa maji.

Wanasiasa watajipiga jaramba huku wakiwalaumu wengine.

Waziri wa Ujenzi Prof Mbarawa ni mmoja wa watu wamepigia sana upatu kujenga kwa Force Account na fundi Maiko.

Serikali inavuna ilichopandikiza kwa wananchi wake.
Force account ina taratibu zake ambazo zikifatwa ipasavyo jengo linakua imara tu km ambalo limejengwa na mkandarasi.
Si vizuri kupotoshana kwa sasa.
 
Ndugu,
Nimesikitishwa na kilichotokea huko Goba, lakini tuweke sawa hapa....
Sijui unajua nini kuhusiana na hiyo ''force account'' uliyoitaja kwenye bandiko lako lakini ni wazi kuwa unataka kupotosha umma kwa makusudi ama kwa kutokujua.

Kwa lugha ya malkia maana ya ''force account'' - the part of the expense account of a public body (as a municipality) resulting from the employment of a labor force (as for garbage collection and the maintenance of streets) usually distinguished from the part resulting from contracting similar services with commercial agencies.

Hiyo ''force account'' inayotumika hasa kwenye manispaa na halmashauri mbalimbali nchini wala haina mahusiano na ujenzi holela au ujenzi wa kutokufuata taratibu na kanuni za ujenzi.

Hakuna mahali popote ambapo wizara ya ujenzi inatambua wataalamu wa ujenzi ama mafundi ambao hawajapata mafunzo.

Wizara kupitia taasisi zake kama ERB - Engineer's Registration Board na AQRB - Architect's and Quantity Surveryors Registration Board imekuwa ikisisitiza weredi katika ujenzi.

Hali kadhalika wananchi wanasisitizwa kila mara kutumia wataalamu wa ujenzi wanapotaka kujenga ikiwemo kusajili na kupeleka ramani ili zikaguliwe kwenye ofisi za manispaa zetu.

Swali, wananchi wangapi huwa wanaona umuhimu wa ramani za majengo kukaguliwa kabla ya ujenzi kuanza?.

Kwa kuwa JF ni home of Great Thinkers, tujitahidi kuleta habari zenye maana na zilizo za kweli.

Mungu azilaze mahali pema roho za marehemu. Amina.
Hii elimu ungeielekeza kwa walioanzisha huo mtindo wa Force Account na kutumia kuhamasisha upigaji wa pesa na matumizi ya local fundi, au fundi Maiko, basi utakuwa unatekelezwa wajibu wako kisawasawa.

Lakini tumeona wakuu wa shule kuchukuliwa hatua kwa kutosimamia ujenzi, wakati si wajibu wao.
Madarasa mengi sakafu kutoboka toboka kutokana na ujenzi usio na viwango, wakuu wa idara mikoani, hata Takukuru, kutumika kusimamia ujenzi.

Mnajidai hamuoni haya yakitendeka kila siku.
Wananchi wasio na elimu wameanza kuiga, wanafikiri ndio mtindo mpya wa Ujenzi na kwa kasi.
Mnavuna mlichopandikiza kielimu katika sekta ya ujenzi na hili mnapashwa kulielewa na kurekebisha.
 
Back
Top Bottom