Serikali inavuna ilichopanda: Fundi Maiko Syndrome - Goba Collapse

Serikali inavuna ilichopanda: Fundi Maiko Syndrome - Goba Collapse

Kwa muda mrefu sasa Serikali imepigia debe ujenzi wa majengo kwa kutumia Force Account na kutumia Local Fundi , ambaye mitaani anajulikana kama fundi Maiko. Wananchi wameupokea mtindo huo kwa kuushangilia katika ujenzi wa majengo kwa nia ya kupunguza gharama. Jengo lililoanguka huko Goba lilititia na kuanguka kama mbuyu uliojaa maji.

Wanasiasa watajipiga jaramba huku wakiwalaumu wengine. Waziri wa Ujenzi Prof Mbarawa ni mmoja wa watu wamepigia sana upatu kujenga kwa Force Account na fundi Maiko. Serikali inavuna ilichopandikiza kwa wananchi wake.
Majengo ya serikali ndio hujengwa Kwa force account. Mbona majengo mengi tuu wakandarasi wameyajenga yapo chini ya kiwango kabisa
 
Nadhani unapotosha dhana ya force account

Force account haimaanishi kupunguza gharama kwa kupunguza material /ubora, bali kupunguza gharama kwa kutumia uwezo uliopo ndani ya Mifumo ya serikali na kwa wananchi pia.

Kwa mfano ujenzi wa madarasa unaofanyika sasa kwa Mtindo huo, Engineer wa halmashauri ndio msimamizi badala ya kumpa kandarasi mtu binafsi.

Wananchi nao wanachangia nguvu kazi hivyo gharama inapungua na urasimu pia.
Kuna bweni lilijengwa kwa usimamizi wa engineer ambae baadae ilikuja kugundulika ni engineer wa mitaro ya maji ya kumwagilia hiyo usijidanganye kuna tatizo mbele ya safari tuendako. Maengineer wengi wa halmashauri hatusemi sana. Nisaidieni wenzangu
 
Mimi situmii ma engineer, wana uwezo mdogo sana. Nimejenga ghorofa mbili kwa kumtumia fundi Maiko, hadi sasa sijaona tatizo.
 
Mimi situmii ma engineer, wana uwezo mdogo sana. Nimejenga ghorofa mbili kwa kumtumia fundi Maiko, hadi sasa sijaona tatizo.
Mwenzio mwenye akili kama yako yuko lupango sasa hivi kwa kuua watu wanne na kujeruhi 17.
 
Kwa muda mrefu sasa Serikali imepigia debe ujenzi wa majengo kwa kutumia Force Account na kutumia Local Fundi , ambaye mitaani anajulikana kama fundi Maiko.

Wananchi wameupokea mtindo huo kwa kuushangilia katika ujenzi wa majengo kwa nia ya kupunguza gharama.

Jengo lililoanguka huko Goba lilititia na kuanguka kama mbuyu uliojaa maji.

Wanasiasa watajipiga jaramba huku wakiwalaumu wengine.

Waziri wa Ujenzi Prof Mbarawa ni mmoja wa watu wamepigia sana upatu kujenga kwa Force Account na fundi Maiko.

Serikali inavuna ilichopandikiza kwa wananchi wake.
Na hapo alikuwa anajipanga kuongeza ghorofo moja hapo juu
 
Fuatilia sifa za kutumia force account kwanza. Hii inatumika katika taasisi na panapaswa kuwa na wataalam watakaosimamia huo ujenzi, sio kujijengea tu.
 
Kuna bweni lilijengwa kwa usimamizi wa engineer ambae baadae ilikuja kugundulika ni engineer wa mitaro ya maji ya kumwagilia hiyo usijidanganye kuna tatizo mbele ya safari tuendako. Maengineer wengi wa halmashauri hatusemi sana. Nisaidieni wenzangu
Kumweka Mhandisi wa mitambo ya ujenzi akasimamie ujenzi wa madarasa hivi unategemea nini?
 
Shida Nini ? Engineers hawapo au
Force account nilikuwa ni mfumo wa kujenga nyumba nyingi kwa kutumia gharama kidogo,
Matokeo yake ni majengo mabovu yanayowapa watu political milage
 
Force account nilikuwa ni mfumo wa kujenga nyumba nyingi kwa kutumia gharama kidogo,
Matokeo yake ni majengo mabovu yanayowapa watu political milage
Hiyo ni staili ya pendwa wetu, self centered, selfish, me first, liar, know all, know everything, uncultivated phase 5 presidaa!
 
Hiyo ni staili ya pendwa wetu, self centered, selfish, me first, liar, uncultivated phase 5 presidaa!
Mkuu kwa wanaojielewa tu, walipitia njia ngumu sana awamu hiyo

I hate with passion mtu muongo pamoja na uwongo wenyewe ,uongo ni zaidi ya kuuq

For strange reasons though Watanzania tunapenda kuishi maisha ya uongo uongo.
 
Huku mbwinde majengo ya serikali yanajengwa na fundi Ally na yapo poa tu

Maengeneer mjipange hawa watoto watawapoteza

Hawa watoto huku kitaa wanajenga na hawana gharama za contingency, supervision, mara 15% and 10% na nyingine nyingi

Watu wanataka impact sio DEGREE zenu
 
Back
Top Bottom