Serikali inavuna ilichopanda: Fundi Maiko Syndrome - Goba Collapse

Serikali inavuna ilichopanda: Fundi Maiko Syndrome - Goba Collapse

Nadhani unapotosha dhana ya force account

Force account haimaanishi kupunguza gharama kwa kupunguza material /ubora, bali kupunguza gharama kwa kutumia uwezo uliopo ndani ya Mifumo ya serikali na kwa wananchi pia.

Kwa mfano ujenzi wa madarasa unaofanyika sasa kwa Mtindo huo, Engineer wa halmashauri ndio msimamizi badala ya kumpa kandarasi mtu binafsi.

Wananchi nao wanachangia nguvu kazi hivyo gharama inapungua na urasimu pia.
Mtoa mada yupo sahihi nawe pia upo sahihi but yeye anaongelea quality.huu mtindo wa force account aliouanzisha Magufuli ni hovyo kabisa na hautakiwi kwa karne hii ya 21.
Watu wanaenda shule kusomea haya mambo kwa lengo la kuminimize risks zilizokuwa zinatokea kabla Nchi hatujawa na wataalamu hao.

Inachokifanya Serikali kuounguza gharama za ujenzi kwa njia ya kutumi local fundi kwa kisingizio cha supervision kutoka kwa engineer wa Halmashauri ni zaidi ya ujinga
 
Acha uongo force account haina maana hiyo. Force account maana yake unatumia ma engineer walioajiliwa na serikali badala ya kutumia makandarasi ambao wamekuwa na ukiritimba kibao na gharama kubwa. Miradi mingi local fundi ndio wanaotumika wakisimamiwa na qualified engineers kwa hiyo usiwadharau local fundi mkuu.
Chochote kinachohusisha utalaamu lazima kiwe na gharama,hakuna ujuzi ambao cheap sababu ya gharama za wakandarasi kuwa kubwa ni kutokana na ukirikimba wa serikali nyenyewe ikiwemo ucheleweshaji wa malipo.
 
False account na ubora wa hilo jengo binafsi unahusiana vipi?
Majengo yote yenye mfumo wa ghorofa kuna kanuni sake za ujenzi ikiwemo kutumia kandarasi kuanzia design,ujenzi wa mifumo na jengo lenyewe.Sasa kama wewe Serikali ambaye ndio msimamizi mkuu wa kila kitu katika Nchi unatumia local fundi katika majengo ya Umma vipi Mwananchi wa kawaida
 
Frame za hivi zipo nyingi Sana Dsm zinatakiwa kukaguliwa
 
Yaani foreman akisaidiwa na injinia mkuu uko serious kweli? Yaani una maanisha injinia amsaidie kazi foreman? Acha dharau asee!!
Soma sentensi nzima uone anachosaidiwa!! Kama huwezi kufanya kitu au kusoma mchoro si unasaidiwa na anaejua ama??
 
Kwa muda mrefu sasa Serikali imepigia debe ujenzi wa majengo kwa kutumia Force Account na kutumia Local Fundi , ambaye mitaani anajulikana kama fundi Maiko. Wananchi wameupokea mtindo huo kwa kuushangilia katika ujenzi wa majengo kwa nia ya kupunguza gharama. Jengo lililoanguka huko Goba lilititia na kuanguka kama mbuyu uliojaa maji.

Wanasiasa watajipiga jaramba huku wakiwalaumu wengine. Waziri wa Ujenzi Prof Mbarawa ni mmoja wa watu wamepigia sana upatu kujenga kwa Force Account na fundi Maiko. Serikali inavuna ilichopandikiza kwa wananchi wake.
Utaalamu unawekwa pembeni wakati watu wanataka kupanda chati za kisiasa
 
We jamaa huo sio mwandiko ni maandishi, insha au uandishi.

Unajifanya unajua wakati hujui.

Hakuna anae unda mwandiko kwenye simu, kumpyuta nk.

Mwandiko wa bunadamu huandikwa kwenye karatasi kwa kutimia peni au penseli.

Vile vile kuna pen za ectronic ambazo zinaweza onedha ubora wa mwandiko wa mtu.

Uwe unakosoa kwa kusema uandishi sasa.

Sio, mwandiko sasa.

Mi nakuchukulia unakosoa usichokijua. Mwehu humuona mwenzie kuwa mwehu kumbe yeye ndiye mwehu.

Katika compyuta kuna fonts style/ size ambazo mtu anaunganisha herufi kupata maandishi sio mwandiko, huna mamlaka ya mwandiko bali waliounda simu, kazi yako ni kuchagua mwandiko kutoka orodha maalumu ya mwandiko ambao ni; times new roman (ambao maarufu zaidi), aerial nk .

Sisi sote humu tunakosea uandishi mara kwa mara, hakuna alie bora.

Acha kujifanya unajua sana.
Emetumia nguvu nyingi mkuu, usichukulie kila kitu serious this is jf....nlipoandika mwandiko skumaanisha lazima wewe uelewe nlichoandika
 
Kwa muda mrefu sasa Serikali imepigia debe ujenzi wa majengo kwa kutumia Force Account na kutumia Local Fundi , ambaye mitaani anajulikana kama fundi Maiko. Wananchi wameupokea mtindo huo kwa kuushangilia katika ujenzi wa majengo kwa nia ya kupunguza gharama. Jengo lililoanguka huko Goba lilititia na kuanguka kama mbuyu uliojaa maji.

Wanasiasa watajipiga jaramba huku wakiwalaumu wengine. Waziri wa Ujenzi Prof Mbarawa ni mmoja wa watu wamepigia sana upatu kujenga kwa Force Account na fundi Maiko. Serikali inavuna ilichopandikiza kwa wananchi wake.
Kuna watu wanachekesha sana nchi hii,hata kama mi sio engineer lakini siwezi kufanya upuuzi kama uwo.juu umeweka tofari za kutosha alafu chini hamna tofari.unategemea uzito usizidi kweli
 
Kuna watu wanachekesha sana nchi hii,hata kama mi sio engineer lakini siwezi kufanya upuuzi kama uwo.juu umeweka tofari za kutosha alafu chini hamna tofari.unategemea uzito usizidi kweli
Tofali za kwako ni za kwako.
Jenga nyumba unayoitamani.
 
Kwa muda mrefu sasa Serikali imepigia debe ujenzi wa majengo kwa kutumia Force Account na kutumia Local Fundi , ambaye mitaani anajulikana kama fundi Maiko. Wananchi wameupokea mtindo huo kwa kuushangilia katika ujenzi wa majengo kwa nia ya kupunguza gharama. Jengo lililoanguka huko Goba lilititia na kuanguka kama mbuyu uliojaa maji.

Wanasiasa watajipiga jaramba huku wakiwalaumu wengine. Waziri wa Ujenzi Prof Mbarawa ni mmoja wa watu wamepigia sana upatu kujenga kwa Force Account na fundi Maiko. Serikali inavuna ilichopandikiza kwa wananchi wake.
Profession za watu CCM wanazifanyia mzaha kwa kufuata mawazo ya akina msukuma na kishimba. Watavuna kwa wakati wao.
 
Emetumia nguvu nyingi mkuu, usichukulie kila kitu serious this is jf....nlipoandika mwandiko skumaanisha lazima wewe uelewe nlichoandika
Huwa sipendi mtu mmoja kumdharau mwingine.
Haya bana.
 
Mtoa mada na baadhi ya wachangiaji hawaelewi kabisa dhana ya force account.

Lakini pia hajui taratibu za kifedha na manunuzi za Serikali kuwa ni tofauti na mtu binafsi

Pia haamini kuwa kuna watu wengi nchini wamejenga bila vibali
 
Back
Top Bottom