zimmerman
JF-Expert Member
- Feb 17, 2011
- 1,644
- 3,176
Nimeshangazwa na hili hapa kama ni kweli: Mwigulu: Tumesikia malalamiko ya Watanzania kuhusu tozo za miamala na Rais ametoa maelekezo ya kuzitazama upya
Hivi inawezekanaje serikali (hapa serikali kwa maana ya watendaji wakuu wa serikali, mawaziri wakiwemo na vyombo vyao vinavyowasaidia katika maamuzi ya kisera) kuamua kitu na baadaye ikifikirie upya baada ya kusikilizia mwitikio wa watu?
Hebu imagine, hivi serikali ya aina hiyo itawezaje kweli kufikia malengo yake? Maana serikali ya aina hiyo itakuwa inaamua hili halafu sisi raia tukipiga kelele inaacha kulitekeleza.
Hii ni dalili kubwa kabisa kwamba tunaongozwa na watu dhaifu sijapata kuona. Hata JK hakuwa dhaifu hivi. Tulimpigia kelele kweli JK kuhusu safari zake but the man believed he was doing the right thing kwa masafari yake yasiyoisha. Na huyu mzee alisafiri hadi sekunde ya mwisho. Kiongozi wa aina yoyote ile anayestahili kuwa kiongozi lazima aamini katika maamuzi yake na kuyatetea ipasavyo.
Hivi mama ameshindwa kusimama na kujenga hoja ya kutushawishi watanzania kwa nini miamala ya simu ni muhimu kwa wakati huu?
Ameshindwa kusimama na kusema, kwa mfano, kwamba nchi yetu imehama kutoka kwenye uchumi wa kutegemea mataifa mengine, na ya kwambaa kuitwa nchi ya uchumi wa kati maana yake ni kwamba ni lazima kama wananchi tujitegemee kwa asilimia kubwa?
Ameshindwa kutetea ongezeko la kodi zake kwa kuutangazia umma wa watanzania kwamba miradi ya kimikakati iliyoachwa na JPM ni ya muhimu sana na ni lazima ikamilike kwa wakati, lakini zinahitaji pesa nyingi?
Ameshindwa kujenga hoja kwamba kwa mfumo wa zamani wa kukusanya kodi pesa ya kuendesha serikali na kutimiza miradi hiyo ya kimikakati ilitegemea kuwakamua watu wachache pesa nyingi, mfumo ambao haukuwa endeleve na ulileta malalamiko mengi na kukwamisha ukuaji wa sekta binafsi?
Ameshindwa kutushawishi watanzania kwamba ni kawaida kwa jambo jipya kama hilo la kukusanya kodi kwa njia ya miamala ni lazima lipokewe kwa mshtuko na watu na hilo linaeleweka, lakini uwaombe watu hao wawe na uvumilivu maana pesa yao inakwenda kufnaya mambo makubwa yatakoyogeuza sura ya nchi yao na kuwafanya wajivunie kuitwa watanzania?
Hakuna sababu ya kutikiswa iwapo unachokifanya unaamini ni sahihi. Sasa utafanya kitu gani ambacho hatutakupigia kelele -- baadhi yetu.
Aisee!