Serikali inayobadilisha maamuzi yake kwa kutegemea upepo ni Serikali dhaifu, haifai

Nadhani unapotosha watu, na unaipotosha hiyo serikali. Watu hawajakataa hiyo tozo au kodi - vyovyote vile itakavyoitwa. Ila watu wamelalamikia kiwango. Tatizo ni viwango vilivyowekwa, sio tozo au kodi. Nadhani kama ingekuwa imewekwa labda 10% au 20% kutoka zile gharama za kampuni ya simu, isingekuwa shida sana. Sasa kuwekwa 150% au 200% ya ile gharama ya muamala ya kampuni ya simu, ndio imekuwa tatizo...
Vyovyote vile, mimi msingi wangu wa hoja ni serikali kufanya maamuzi na kushindwa kuyatetea. Nina uhakika kabisa kwamba hiyo kodi ya muamala wa simu ingetetewa vizuri, ikiwemo na hayo unayoyasema watu wangeelewa. Mimi ni miongoni mwa watu wanaoamini kila mtanzania lazima alipe kodi. Haikufutwa kodi ya kichwa ili mzigo uwaelemee wafanyakazi na wafanyabiashara tena walioko mjini sehemu TRA wanaweza kufika. Kama ishu ni kiwango cha kodi ya muamala basi serikali yenye kujielewa inachokifanya ingeweza kutoa statement ya kuakisi hilo bila kuonekana haina msimamo.
 
Nimeshangazwa na hili hapa kama ni kweli: Mwigulu: Tumesikia malalamiko ya Watanzania kuhusu tozo za miamala na Rais ametoa maelekezo ya kuzitazama upya

Hivi inawezekanaje serikali (hapa serikali kwa maana ya watendaji wakuu wa serikali, mawaziri wakiwemo na vyombo vyao vinavyowasaidia katika maamuzi ya kisera) kuamua kitu na baadaye ikifikirie upya baada ya kusikilizia mwitikio wa watu?

Hebu imagine, hivi serikali ya aina hiyo itawezaje kweli kufikia malengo yake? Maana serikali ya aina hiyo itakuwa inaamua hili halafu sisi raia tukipiga kelele inaacha kulitekeleza.

Hii ni dalili kubwa kabisa kwamba tunaongozwa na watu dhaifu sijapata kuona. Hata JK hakuwa dhaifu hivi. Tulimpigia kelele kweli JK kuhusu safari zake but the man believed he was doing the right thing kwa masafari yake yasiyoisha. Na huyu mzee alisafiri hadi sekunde ya mwisho. Kiongozi wa aina yoyote ile anayestahili kuwa kiongozi lazima aamini katika maamuzi yake na kuyatetea ipasavyo.

Hivi mama ameshindwa kusimama na kujenga hoja ya kutushawishi watanzania kwa nini miamala ya simu ni muhimu kwa wakati huu?

Ameshindwa kusimama na kusema, kwa mfano, kwamba nchi yetu imehama kutoka kwenye uchumi wa kutegemea mataifa mengine, na ya kwambaa kuitwa nchi ya uchumi wa kati maana yake ni kwamba ni lazima kama wananchi tujitegemee kwa asilimia kubwa?

Ameshindwa kutetea ongezeko la kodi zake kwa kuutangazia umma wa watanzania kwamba miradi ya kimikakati iliyoachwa na JPM ni ya muhimu sana na ni lazima ikamilike kwa wakati, lakini zinahitaji pesa nyingi?

Ameshindwa kujenga hoja kwamba kwa mfumo wa zamani wa kukusanya kodi pesa ya kuendesha serikali na kutimiza miradi hiyo ya kimikakati ilitegemea kuwakamua watu wachache pesa nyingi, mfumo ambao haukuwa endeleve na ulileta malalamiko mengi na kukwamisha ukuaji wa sekta binafsi?

Ameshindwa kutushawishi watanzania kwamba ni kawaida kwa jambo jipya kama hilo la kukusanya kodi kwa njia ya miamala ni lazima lipokewe kwa mshtuko na watu na hilo linaeleweka, lakini uwaombe watu hao wawe na uvumilivu maana pesa yao inakwenda kufnaya mambo makubwa yatakoyogeuza sura ya nchi yao na kuwafanya wajivunie kuitwa watanzania?

Hakuna sababu ya kutikiswa iwapo unachokifanya unaamini ni sahihi. Sasa utafanya kitu gani ambacho hatutakupigia kelele -- baadhi yetu.

Aisee!
Rais ametumia busara sana kusikikiza raia kwakua ni msikivu, tuache kumfanya Mh. Mama awe dictator pasipo sababu...Tozo hii ni mzigo kwa watu wa chini kwahiyo ndiyo kuna makosa katika kufanya majaribio kwenye maisha ya watu wengi; lakini bora Mh. Rais ambaye yupo tayari kukubaliana na wananchi wake kuliko kukaza shingo na kuwaumiza hata wanapolalamika
 
Mkuu huna uzoefu na mambo ya serikali. Kuna serikali ziliondolewa katika uongozi kwa kukataa kushusha bei ya mkate tu, sembuse tozo!
Ni makoteo ya kufanya maamuzi hovyo in the first place. Serikali haitakiwi ifanye maamuzi hovyo halafu ijitoe baada ya kusikia malalamiko.
 
Vyovyote vile, mimi msingi wangu wa hoja ni serikali kufanya maamuzi na kushindwa kuyatetea. Nina uhakika kabisa kwamba hiyo kodi ya muamala wa simu ingetetewa vizuri, ikiwemo na hayo unayoyasema watu wangeelewa. Mimi ni miongoni mwa watu wanaoamini kila mtanzania lazima alipe kodi. Haikufutwa kodi ya kichwa ili mzigo uwaelemee wafanyakazi na wafanyabiashara tena walioko mjini sehemu TRA wanaweza kufika. Kama ishu ni kiwango cha kodi ya muamala basi serikali yenye kujielewa inachokifanya ingeweza kutoa statement ya kuakisi hilo bila kuonekana haina msimamo.
Kabla ya kuwatoza kodi, wape means za kuzalisha cash...Siyo kwamba kabla hata economy hajawa full cash unaleta vikwazo kwakuwabebesha kodi...Kuna namna nyingi sana ya kuongeza watu wengi kwenye wigo wa kodi...Hii hapa ni mzigo kwa watu wengi wasio na kipato.
 
Huyu hapA

IMG-20210718-WA0139.jpg
 
Jukumu namba moja la serikali ni kusimamia sheria. Baada ya Bunge kupitisha hiyo bajeti na kuifanya sheria, ni jukumu la serikali kuisimamia kwa udi na uvumba. Iwapo bajeti hiyo imekuwa ni vifungu vya hovyo ambavyo vilipitishwa na Bunge kuwa sheria lakini wananchi hawavipendi, basi njia pakee ya kuvishughulikia ni kuita kikao kingine cha bunge kuharamisha bajeti hiyo, na kuweka bajeti mpya. Ila katika kufanya hivyo, wabunge wasilipwe posho tena kwa sababu wanakuwa wamerudi bungeni kwa makosa yao, siyo kwa sababu ya ratiba ya bunge.

Serikali ikishaanza mchezo wa kusema kuwa sheria hii ni mbaya kwa wananchi tusiisimamie, basi wanatoa uhalali kwa raia kutotii sheria ambazo hawazipendi.

Serikali lazima isimamie sheria zilizoko vitabuni. Ndiyo maana kazi ya kuongoza serikali ni jambo linalohitaji ujasiri, kwani sheria nyingine zinaweza kuonekana kuwa ni ukatili lakini lazima zitekelezwe, kwa mfano jaji akimwona mtuhumiwa kuwa anastahili kunyongwa, hawezi kusema asamehewe bali atamhukumu anyongwe hadi afe kwa sababu sheria inasema hivyo, siyo kwa sababu jaji huyo hana huruma!!
 
Tulipompigia kelele JK kuhusu safari zake hadi tukamwita Vasco da Gama, serikali yake iliondolewa?

Mlipompigia kelele JPM kuhusu kile mlichokuwa mnakiita udkiteta serikali yake iliondolewa?

Ni kawaida ya raia kutoridhika, uongozi ni kujenga hoja na kuwashawishi watu kwamba maamuzi yako ni sahihi.

Urais ni mgumu, na usipokuwa na uthabiti wa maamuzi hiyo kazi haikufai.
Mimi siwalaumu kwa kutaka kupiga u-turn, nadhani ukweli ni kwamba hata wangekomaa wangeangukia pua. Wanasema ukigundua unazama kwenye shimo unaacha kuchimba.

Ninachoona kibaya ni kutokuwa makini na maamuzi kwenye mambo mazito yanayogusa mamilioni ya wananchi, walichemsha kwenye vifurushi, wakapiga u-turn; na hii nyingine wanaenda kupiga sasa hivi. Ni dalili ya kukosa umakini.
 
Vyovyote vile, mimi msingi wangu wa hoja ni serikali kufanya maamuzi na kushindwa kuyatetea. Nina uhakika kabisa kwamba hiyo kodi ya muamala wa simu ingetetewa vizuri, ikiwemo na hayo unayoyasema watu wangeelewa. Mimi ni miongoni mwa watu wanaoamini kila mtanzania lazima alipe kodi. Haikufutwa kodi ya kichwa ili mzigo uwaelemee wafanyakazi na wafanyabiashara tena walioko mjini sehemu TRA wanaweza kufika. Kama ishu ni kiwango cha kodi ya muamala basi serikali yenye kujielewa inachokifanya ingeweza kutoa statement ya kuakisi hilo bila kuonekana haina msimamo.
Kiwango lazima kirekebishwe... Haiwezekani ukatoza kiwango kikubwa ambacho kinawazidi hata kampunzi za simu, waliowekeza Human na Materials resources. Serikali haijawekeza chochote, na inataka ichukue 200% ya kile inachopata kampuni ya simu, kwa nini? Mbona VAT ni 18% ya base kwenye nchi nyingi, na Customs duty ni 25% ya base; corporate tax ni 30% ya base - hiyo 200% imetokea wapi?
 
Mwigulu Nchemba Mama Samia tuliwaambia sisi kanyaga twende tumechelewa sana , wangezoea hao wapiga kelele oneni sasa Leo binadamu wasivyo na jema

mnasemwa tena kwa kupiga reverse
 
Hajui huyu na madhara yake kiuchumi ya hyo tozo, vipi transcations za makampuni ya simu ka yameshuka, mawakala kukosa ajira na serikali kukosa kabisa hyo kodi
Weka data tuone yalivyoshuka na mawakala kukosa Kazi? Au mnapayuka hisia zenu tuu?

Haya kwamba miamala haifanyiki tena au ikoje? Mbona vibanda vya miamala viko busy au huko kwenu ndio havifanyi Kazi?

Hii mambo ya kubembeleza watu kulipa kodi matokeo yake ni watoto wa maskini kulundikana kwenye vyumba huku wanaojifanya kuwaonea huruma wakineemeka.
 
Hata picha hujui kusoma Hali halisi mie mwenyewe wakala Sasa why should I lie. Hafu Kodi ni muhimu Ila iendane na Hali halisi ya sisi Raia wa chini
 
Mbona hujaacha Kazi sasa kama haikulipi? Picha gani ya kuisoma? Huko mtaani unaishi peke yako au wakala ni wewe peke yako?

Kwamba nikitoa 130,000 nikakatwa 6180 nitakuwa nimeathirika Sana na hiyo unayoita Hali halisi ya maisha?

Mbona hao wanaowapa commission sijawahi kukusikia ukitetea wananchi kwamba mnakata wateja pesa nyingi? Kampuni inapata 3650 na Serikali 2530 ,hapo nani anafaidika Kati ya Serikali na Kampuni?

Kama serikali inakubali kusalimu amri basi na huo wizi wa kampuni za simu Ili kulipa mawakala wao ukome.
 
Nimeshangazwa na hili hapa kama ni kweli: Mwigulu: Tumesikia malalamiko ya Watanzania kuhusu tozo za miamala na Rais ametoa maelekezo ya kuzitazama upya

Hivi inawezekanaje serikali (hapa serikali kwa maana ya watendaji wakuu wa serikali, mawaziri wakiwemo na vyombo vyao vinavyowasaidia katika maamuzi ya kisera) kuamua kitu na baadaye ikifikirie upya baada ya kusikilizia mwitikio wa watu?

Hebu imagine, hivi serikali ya aina hiyo itawezaje kweli kufikia malengo yake? Maana serikali ya aina hiyo itakuwa inaamua hili halafu sisi raia tukipiga kelele inaacha kulitekeleza.

Hii ni dalili kubwa kabisa kwamba tunaongozwa na watu dhaifu sijapata kuona. Hata JK hakuwa dhaifu hivi. Tulimpigia kelele kweli JK kuhusu safari zake but the man believed he was doing the right thing kwa masafari yake yasiyoisha. Na huyu mzee alisafiri hadi sekunde ya mwisho. Kiongozi wa aina yoyote ile anayestahili kuwa kiongozi lazima aamini katika maamuzi yake na kuyatetea ipasavyo.

Hivi mama ameshindwa kusimama na kujenga hoja ya kutushawishi watanzania kwa nini miamala ya simu ni muhimu kwa wakati huu?

Ameshindwa kusimama na kusema, kwa mfano, kwamba nchi yetu imehama kutoka kwenye uchumi wa kutegemea mataifa mengine, na ya kwambaa kuitwa nchi ya uchumi wa kati maana yake ni kwamba ni lazima kama wananchi tujitegemee kwa asilimia kubwa?

Ameshindwa kutetea ongezeko la kodi zake kwa kuutangazia umma wa watanzania kwamba miradi ya kimikakati iliyoachwa na JPM ni ya muhimu sana na ni lazima ikamilike kwa wakati, lakini zinahitaji pesa nyingi?

Ameshindwa kujenga hoja kwamba kwa mfumo wa zamani wa kukusanya kodi pesa ya kuendesha serikali na kutimiza miradi hiyo ya kimikakati ilitegemea kuwakamua watu wachache pesa nyingi, mfumo ambao haukuwa endeleve na ulileta malalamiko mengi na kukwamisha ukuaji wa sekta binafsi?

Ameshindwa kutushawishi watanzania kwamba ni kawaida kwa jambo jipya kama hilo la kukusanya kodi kwa njia ya miamala ni lazima lipokewe kwa mshtuko na watu na hilo linaeleweka, lakini uwaombe watu hao wawe na uvumilivu maana pesa yao inakwenda kufnaya mambo makubwa yatakoyogeuza sura ya nchi yao na kuwafanya wajivunie kuitwa watanzania?

Hakuna sababu ya kutikiswa iwapo unachokifanya unaamini ni sahihi. Sasa utafanya kitu gani ambacho hatutakupigia kelele -- baadhi yetu.

Aisee!
Shida ni kwamba wanaopiga kelele ni wengi mno, wengi wape
 
Samia kama ni mkweli amfukuze mwigulu

Serikali ya JPM ilichukiwa na kupigwa zengwe kwa misimamo ya hayati. Ni pale aliposimama Ubungo na kuuambia umma kwamba hawezi kumfukuza kazi Makonda kwa kutegemea presha za mitandaoni.

Rais Samia amevaa sura ya kibinadamu na huo sio udhaifu bali ni hulka ya kistaarabu aliyonayo, anaweza kabisa kuamua kuwa mnyama na asiguswe na mtu yoyote kama ambavyo JPM alivyoamua kuendesha nchi kibabe.

Kuelezea nini serikali yake inasimamia pia ni kazi ya mawaziri wake na makatibu wakuu, demokrasia inawaruhusu kufanya hivyo na madaraka waliyonayo yanawaruhusu kufanya hivyo.

Pia Rais kusikiliza sauti nyingi za watu ni sifa ya ubinadamu, ni sifa ya uongozi. Kwani sauti ya wengi ni sauti ya Mungu hivyo hekima ya kweli ni kusikiliza kilio cha wengi.

Katiba yetu ndio imetupatia Rais huyu hivyo tujenge hoja zetu tukitambua juu ya ukweli huo.
Sio ilo tu misimamo ya JPM ilikuwa yakibabe! Hivi ingekuwaje Serikali kama ndiyo ya Samia ingejenga Bwawa la Umeme pale Rufiji na zengwe lote lile? Serikali ya Samia ndo ingekuwa madarakani kipindi corona inaingia umewahi kuwaza tungechezea lockdown mpaka tuishe wote!

Samia hana ubavu wa kukabiliana na pressure sio za nje tu ata ndani ya nchi
 
Nimeshangazwa na hili hapa kama ni kweli: Mwigulu: Tumesikia malalamiko ya Watanzania kuhusu tozo za miamala na Rais ametoa maelekezo ya kuzitazama upya

Hivi inawezekanaje serikali (hapa serikali kwa maana ya watendaji wakuu wa serikali, mawaziri wakiwemo na vyombo vyao vinavyowasaidia katika maamuzi ya kisera) kuamua kitu na baadaye ikifikirie upya baada ya kusikilizia mwitikio wa watu?

Hebu imagine, hivi serikali ya aina hiyo itawezaje kweli kufikia malengo yake? Maana serikali ya aina hiyo itakuwa inaamua hili halafu sisi raia tukipiga kelele inaacha kulitekeleza.

Hii ni dalili kubwa kabisa kwamba tunaongozwa na watu dhaifu sijapata kuona. Hata JK hakuwa dhaifu hivi. Tulimpigia kelele kweli JK kuhusu safari zake but the man believed he was doing the right thing kwa masafari yake yasiyoisha. Na huyu mzee alisafiri hadi sekunde ya mwisho. Kiongozi wa aina yoyote ile anayestahili kuwa kiongozi lazima aamini katika maamuzi yake na kuyatetea ipasavyo.

Hivi mama ameshindwa kusimama na kujenga hoja ya kutushawishi watanzania kwa nini miamala ya simu ni muhimu kwa wakati huu?

Ameshindwa kusimama na kusema, kwa mfano, kwamba nchi yetu imehama kutoka kwenye uchumi wa kutegemea mataifa mengine, na ya kwambaa kuitwa nchi ya uchumi wa kati maana yake ni kwamba ni lazima kama wananchi tujitegemee kwa asilimia kubwa?

Ameshindwa kutetea ongezeko la kodi zake kwa kuutangazia umma wa watanzania kwamba miradi ya kimikakati iliyoachwa na JPM ni ya muhimu sana na ni lazima ikamilike kwa wakati, lakini zinahitaji pesa nyingi?

Ameshindwa kujenga hoja kwamba kwa mfumo wa zamani wa kukusanya kodi pesa ya kuendesha serikali na kutimiza miradi hiyo ya kimikakati ilitegemea kuwakamua watu wachache pesa nyingi, mfumo ambao haukuwa endeleve na ulileta malalamiko mengi na kukwamisha ukuaji wa sekta binafsi?

Ameshindwa kutushawishi watanzania kwamba ni kawaida kwa jambo jipya kama hilo la kukusanya kodi kwa njia ya miamala ni lazima lipokewe kwa mshtuko na watu na hilo linaeleweka, lakini uwaombe watu hao wawe na uvumilivu maana pesa yao inakwenda kufnaya mambo makubwa yatakoyogeuza sura ya nchi yao na kuwafanya wajivunie kuitwa watanzania?

Hakuna sababu ya kutikiswa iwapo unachokifanya unaamini ni sahihi. Sasa utafanya kitu gani ambacho hatutakupigia kelele -- baadhi yetu.

Aisee!
Report ya cag imejaa ubadhitifu, na bado hakuna hatua inachukuliwa,

wamechota mihela BOT
alipofariki mwendazake ripoti imekaliwa mpaka leo

Samia anatumbua mihela ya hazina kwa misafara ya aghali Sana, dar - Dom kila siku

Bado matumizi ya serekali Yako juu mavieiti

Kwao muktadha huo wanawezaje kuwashawishi wananchi kuwa tozo ni kuwa manufaa ya maendeleo yao?
 
Back
Top Bottom