Serikali inayobadilisha maamuzi yake kwa kutegemea upepo ni Serikali dhaifu, haifai

Vyovyote vile, mimi msingi wangu wa hoja ni serikali kufanya maamuzi na kushindwa kuyatetea. Nina uhakika kabisa kwamba hiyo kodi ya muamala wa simu ingetetewa vizuri, ikiwemo na hayo unayoyasema watu wangeelewa. Mimi ni miongoni mwa watu wanaoamini kila mtanzania lazima alipe kodi. Haikufutwa kodi ya kichwa ili mzigo uwaelemee wafanyakazi na wafanyabiashara tena walioko mjini sehemu TRA wanaweza kufika. Kama ishu ni kiwango cha kodi ya muamala basi serikali yenye kujielewa inachokifanya ingeweza kutoa statement ya kuakisi hilo bila kuonekana haina msimamo.
 
Rais ametumia busara sana kusikikiza raia kwakua ni msikivu, tuache kumfanya Mh. Mama awe dictator pasipo sababu...Tozo hii ni mzigo kwa watu wa chini kwahiyo ndiyo kuna makosa katika kufanya majaribio kwenye maisha ya watu wengi; lakini bora Mh. Rais ambaye yupo tayari kukubaliana na wananchi wake kuliko kukaza shingo na kuwaumiza hata wanapolalamika
 
Mkuu huna uzoefu na mambo ya serikali. Kuna serikali ziliondolewa katika uongozi kwa kukataa kushusha bei ya mkate tu, sembuse tozo!
Ni makoteo ya kufanya maamuzi hovyo in the first place. Serikali haitakiwi ifanye maamuzi hovyo halafu ijitoe baada ya kusikia malalamiko.
 
Kabla ya kuwatoza kodi, wape means za kuzalisha cash...Siyo kwamba kabla hata economy hajawa full cash unaleta vikwazo kwakuwabebesha kodi...Kuna namna nyingi sana ya kuongeza watu wengi kwenye wigo wa kodi...Hii hapa ni mzigo kwa watu wengi wasio na kipato.
 
Jukumu namba moja la serikali ni kusimamia sheria. Baada ya Bunge kupitisha hiyo bajeti na kuifanya sheria, ni jukumu la serikali kuisimamia kwa udi na uvumba. Iwapo bajeti hiyo imekuwa ni vifungu vya hovyo ambavyo vilipitishwa na Bunge kuwa sheria lakini wananchi hawavipendi, basi njia pakee ya kuvishughulikia ni kuita kikao kingine cha bunge kuharamisha bajeti hiyo, na kuweka bajeti mpya. Ila katika kufanya hivyo, wabunge wasilipwe posho tena kwa sababu wanakuwa wamerudi bungeni kwa makosa yao, siyo kwa sababu ya ratiba ya bunge.

Serikali ikishaanza mchezo wa kusema kuwa sheria hii ni mbaya kwa wananchi tusiisimamie, basi wanatoa uhalali kwa raia kutotii sheria ambazo hawazipendi.

Serikali lazima isimamie sheria zilizoko vitabuni. Ndiyo maana kazi ya kuongoza serikali ni jambo linalohitaji ujasiri, kwani sheria nyingine zinaweza kuonekana kuwa ni ukatili lakini lazima zitekelezwe, kwa mfano jaji akimwona mtuhumiwa kuwa anastahili kunyongwa, hawezi kusema asamehewe bali atamhukumu anyongwe hadi afe kwa sababu sheria inasema hivyo, siyo kwa sababu jaji huyo hana huruma!!
 
Mimi siwalaumu kwa kutaka kupiga u-turn, nadhani ukweli ni kwamba hata wangekomaa wangeangukia pua. Wanasema ukigundua unazama kwenye shimo unaacha kuchimba.

Ninachoona kibaya ni kutokuwa makini na maamuzi kwenye mambo mazito yanayogusa mamilioni ya wananchi, walichemsha kwenye vifurushi, wakapiga u-turn; na hii nyingine wanaenda kupiga sasa hivi. Ni dalili ya kukosa umakini.
 
Kiwango lazima kirekebishwe... Haiwezekani ukatoza kiwango kikubwa ambacho kinawazidi hata kampunzi za simu, waliowekeza Human na Materials resources. Serikali haijawekeza chochote, na inataka ichukue 200% ya kile inachopata kampuni ya simu, kwa nini? Mbona VAT ni 18% ya base kwenye nchi nyingi, na Customs duty ni 25% ya base; corporate tax ni 30% ya base - hiyo 200% imetokea wapi?
 
Mwigulu Nchemba Mama Samia tuliwaambia sisi kanyaga twende tumechelewa sana , wangezoea hao wapiga kelele oneni sasa Leo binadamu wasivyo na jema

mnasemwa tena kwa kupiga reverse
 
Hajui huyu na madhara yake kiuchumi ya hyo tozo, vipi transcations za makampuni ya simu ka yameshuka, mawakala kukosa ajira na serikali kukosa kabisa hyo kodi
Weka data tuone yalivyoshuka na mawakala kukosa Kazi? Au mnapayuka hisia zenu tuu?

Haya kwamba miamala haifanyiki tena au ikoje? Mbona vibanda vya miamala viko busy au huko kwenu ndio havifanyi Kazi?

Hii mambo ya kubembeleza watu kulipa kodi matokeo yake ni watoto wa maskini kulundikana kwenye vyumba huku wanaojifanya kuwaonea huruma wakineemeka.
 
Hata picha hujui kusoma Hali halisi mie mwenyewe wakala Sasa why should I lie. Hafu Kodi ni muhimu Ila iendane na Hali halisi ya sisi Raia wa chini
 
Hata picha hujui kusoma Hali halisi mie mwenyewe wakala Sasa why should I lie. Hafu Kodi ni muhimu Ila iendane na Hali halisi ya sisi Raia wa chini
Mbona hujaacha Kazi sasa kama haikulipi? Picha gani ya kuisoma? Huko mtaani unaishi peke yako au wakala ni wewe peke yako?

Kwamba nikitoa 130,000 nikakatwa 6180 nitakuwa nimeathirika Sana na hiyo unayoita Hali halisi ya maisha?

Mbona hao wanaowapa commission sijawahi kukusikia ukitetea wananchi kwamba mnakata wateja pesa nyingi? Kampuni inapata 3650 na Serikali 2530 ,hapo nani anafaidika Kati ya Serikali na Kampuni?

Kama serikali inakubali kusalimu amri basi na huo wizi wa kampuni za simu Ili kulipa mawakala wao ukome.
 
Shida ni kwamba wanaopiga kelele ni wengi mno, wengi wape
 
Samia kama ni mkweli amfukuze mwigulu
 
Sio ilo tu misimamo ya JPM ilikuwa yakibabe! Hivi ingekuwaje Serikali kama ndiyo ya Samia ingejenga Bwawa la Umeme pale Rufiji na zengwe lote lile? Serikali ya Samia ndo ingekuwa madarakani kipindi corona inaingia umewahi kuwaza tungechezea lockdown mpaka tuishe wote!

Samia hana ubavu wa kukabiliana na pressure sio za nje tu ata ndani ya nchi
 
Report ya cag imejaa ubadhitifu, na bado hakuna hatua inachukuliwa,

wamechota mihela BOT
alipofariki mwendazake ripoti imekaliwa mpaka leo

Samia anatumbua mihela ya hazina kwa misafara ya aghali Sana, dar - Dom kila siku

Bado matumizi ya serekali Yako juu mavieiti

Kwao muktadha huo wanawezaje kuwashawishi wananchi kuwa tozo ni kuwa manufaa ya maendeleo yao?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…