#COVID19 Serikali iongeze elimu dhidi ya chanjo ya COVID-19, imuombe Askofu Gwajima asiongelee chanjo

Watanzania tatizo letu ni kutopima mambo kwa undani. Sijui ni kwa sababu ya elimu yetu ya kukariri hivyo tunashindwa kutafakari. Hili la kusema Gwajima hana kosa na anatumia haki yake ya uhuru wa kuongea wamelikariri watu wengi. Ukilichukulia kwa haraka bila kutafakari utaona ni kweli hana kosa. Lakini ukiingia kwa undani unakuta Gwajima ana nyadhifa mbili. 1. Kiongozi wa ''kiroho'' 2. Kiongozi wa wananchi i.e. mbunge. Hapo ndipo linakuja tatizo. Na tatizo ni mgongano wa maslahi. Suala la chanjo limepishapishwa na serikali ya CCM kwa kutumia wataalam. Inakuwaje tena mbunge wa CCM anapinga? Kama anataka kupinga basi ajiuzulu! Kuna kosa lilifanywa la kuruhusu kiongozi wa dini kuwa mbunge bila kujiuzulu wadhifa wake wa kuongoza dini. Alipopata ubunge alitakiwa aambiwe ajivue wadhifa wa kuongoza kanisa ili kuepusha mgongano wa maslahi. Hili lipo duniani kote. Kwa mfano kama mtu ni mkurugenzi na mmiliki wa kampuni kubwa, na akitaka kugombea nyadhifa za kisiasa basi huwajibika kujiuzu ule ukurugenzi ili kuepusha mgongano wa maslahi. Hili la Gwajima kuhusu chanjo ni moja ya mambo mengi tu yanaweza kuleta mgongano kama ataendelea kuwa kiongozi wa kiroho. Hebu chukulia mfano wa condomu. Msimamo wa seriakli ni kuwahimiza wananchi kutumia kondomu. Gwajima kama mbunge, hawezi kuunga mkono kwa sababu za kidini. Kwa kifupi anatakiwa achague moja. Ama kubaki na ubunge lakini ajiuzulu uongozi wa kiroho na abaki kuwa muumini wa kawaida au ajiuzulu ubunge ili aendelee na kupinga chanjo
 
Ona hii ng'ombe inataka chanjo iwe lazima,kama umeshachanjwa kaa kimya usituonee huruma ambao hatutaki chanjo.hatutaki huruma yako.
 
Sitakujibu kwa sababu haihusiani na mada mezani. Anzisha mada nitakujibu huko!
Nikushauri tu uache kiherehere cha kujiona kama umeshafika mbinguni hivi. Bado upo duniani, na jifunze kuwa mnyenyekevu na persuasive badala ya kuwa dikteta!
 
Sitakujibu kwa sababu haihusiani na mada mezani. Anzisha mada nitakujibu huko!
Nikushauri tu uache kiherehere cha kujiona kama umeshafika mbinguni hivi. Bado upo duniani, na jifunze kuwa mnyenyekevu na persuasive badala ya kuwa dikteta!
nijibu
 
imuombe gwajiboy au imkamate na kumsweka ndani!
 
Wewe utukuwa ni mchawi siyo bure!! Una kiu na damu ya watu!!
 
Hivi kwa nini mnataka uhuru wa kuongea kuhusu chanjo ubinafisishwe na wachache? Hilo haliwezekaniki duniani pote!! Wala usidhani upinzani wa chanjo uko Tanzania tu!! Tena hapa kwetu chamtoto!! Angalia hapa!!
Your browser is not able to display this video.
 
Mashabiki hawalioni hilo....Akiwa upande wao wanafurahia akiwa kinyume chao wanagomba....huwezi kutumikia imani na siasa ukabaki salama
 
Itangaze chanjo kuwa lazima
Hapa ndipo tunaona watu mliokwisha chanjwa mmeshavurugwa.
Kwa nini mnapenda tusiochanjwa tulazimishwe? Kama mnaogopa kufa au kuwa mazombi na chanjo yenu,ni kwa nini mlienda wenyewe kuchanjwa?
Korona inaua kama njaa inavyoua,ni kwa nini hamjailazimisha serikali imgawie kila mwananchi kiloba cha mchele na mafuta ili kuepuka njaa?
Badala yake mnalazimisha watu wachanjwe.

Wapo watu wengi hawana mahitaji ya kuwapeleka watoto wao shule,mbona hamuonyeshi umoja wa kuwasaidia kupeleka watoto wao shule
lakini hili la chanjo mnataka wote masikini na matajiri wachanjwe,wakati kwenda shule mtoto wa masikini anakaa chini wa tajiri anasoma shule za kulipia na kupelekwa na magari.

Tumeishazoea kuishi kwa makundi, Hata katika hili matajiri nendeni mkachanjwe na watoto wenu,sisi wengine tuachie tukajichanje na limau na jua la mwenyezi Mungu.
 
Kwa sababu ipi unafikiri chanjo inatakiwa kuwa ya lazima kwa kila mmoja??
 
Serikali ingetoa tamko moja tu,kuwa Kama hujachanja na ikatokea ukaumwa Corona Basi hakuna hospitali itakayokupokea.Watu wangechagua wenyewe.Sema Gwajima Kuna sehemu anaisitiri serikali chanjo milioni moja Ni kidogo mno
Tehe Tehe.... Huu ndio mwisho wako wa kufikiri??
 
Wamevurugwa Hatari.... Embu watuache.... Na Hatuchanjwi. Period.
 
Hakuna haja ya kumnyamazisha Gwajima,huku kwetu watu wanachanja tu wala huyo Gwajima hawamjui.Kukaa kimya ndio jibu la mjinga
 
Wewe ukichanjwa, umepewa kinga inakuuma nini wengine wasipochanjwa?

Ninyi mnalalamika Magufuli alikuwa dictator, halafu hapa unamlazimisha rais avunje katiba na kuwa dictator, ino sane kweli?

Mnalalamika kwamba Maguflui aliminya uhuru wa watu kuzungumza, halafu leo eti Gwajima anyamaze ili usikie maneno ya upande mmoja.

Wewe unaaminije hayo unayotaka kuyasikia ndiyo ya kweli? Unajuaje hayo unayotaka kuyasikia ndiyo suluhisho la matatizo yako?

Corona ni janga, na unaimba hivyo kwa kuwa umeambiwa. Hivi unajua Malaria, HBP, Diabetes, ajali zinaua watu wangapi?

Ujajua tuberclosis inaua watu wangapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…