#COVID19 Serikali iongeze elimu dhidi ya chanjo ya COVID-19, imuombe Askofu Gwajima asiongelee chanjo

#COVID19 Serikali iongeze elimu dhidi ya chanjo ya COVID-19, imuombe Askofu Gwajima asiongelee chanjo

Mama samia amethibitisha bayana kwamba mwanamke hawezi kuongoza hii nchi, taifa linapiga kampeni ya chanjo, halafu anasimama mtu mmoja kwa dharau na kiburi cha kupitiliza nae anapiga kampeni ya kupinga chanjo tena anatamka hadharani kwamba viongozi wanaopigia debe chanjo akili wameziweka likizo,

yeye Rais na Amiri jeahi mkuu ametulia tu sijui ni uoga sijui ni kutokujitambua , yani simuelewi kabisa
Nashindwa kuelewa wanashindwa kumzima huyu mpuuzi ambae anapingana na serikali, Gwajima Ni muhaini, ana lengo la kupindua nchi na kikundi Cha sukuma gang wenzie wachache, inatakiwa muda huu awe jela au apandishwe cheo haraka
 
Watanzania tatizo letu ni kutopima mambo kwa undani. Sijui ni kwa sababu ya elimu yetu ya kukariri hivyo tunashindwa kutafakari. Hili la kusema Gwajima hana kosa na anatumia haki yake ya uhuru wa kuongea wamelikariri watu wengi. Ukilichukulia kwa haraka bila kutafakari utaona ni kweli hana kosa. Lakini ukiingia kwa undani unakuta Gwajima ana nyadhifa mbili. 1. Kiongozi wa ''kiroho'' 2. Kiongozi wa wananchi i.e. mbunge. Hapo ndipo linakuja tatizo. Na tatizo ni mgongano wa maslahi. Suala la chanjo limepishapishwa na serikali ya CCM kwa kutumia wataalam. Inakuwaje tena mbunge wa CCM anapinga? Kama anataka kupinga basi ajiuzulu! Kuna kosa lilifanywa la kuruhusu kiongozi wa dini kuwa mbunge bila kujiuzulu wadhifa wake wa kuongoza dini. Alipopata ubunge alitakiwa aambiwe ajivue wadhifa wa kuongoza kanisa ili kuepusha mgongano wa maslahi. Hili lipo duniani kote. Kwa mfano kama mtu ni mkurugenzi na mmiliki wa kampuni kubwa, na akitaka kugombea nyadhifa za kisiasa basi huwajibika kujiuzu ule ukurugenzi ili kuepusha mgongano wa maslahi. Hili la Gwajima kuhusu chanjo ni moja ya mambo mengi tu yanaweza kuleta mgongano kama ataendelea kuwa kiongozi wa kiroho. Hebu chukulia mfano wa condomu. Msimamo wa seriakli ni kuwahimiza wananchi kutumia kondomu. Gwajima kama mbunge, hawezi kuunga mkono kwa sababu za kidini. Kwa kifupi anatakiwa achague moja. Ama kubaki na ubunge lakini ajiuzulu uongozi wa kiroho na abaki kuwa muumini wa kawaida au ajiuzulu ubunge ili aendelee na kupinga chanjo
Gwajima ni mbunge wa bunge la JMT.Na kazi ya mbunge sio kusimamia Maamuzi ya Serikali kisa chama chake ndio kinaunda serikali. Huwa mnasema wabunge wa ccm ni kasuku na wao kila kitu ni NDIYO. Leo anatokea mtu anapinga,mnaanza kumshambulia. HIVI NYIE WATU MNASIMAMIA NINI?
 
Kanisani ni bungeni? Umesoma ukaelewa nilichomaanisha?
 
We jamaa ungekuwa hata tu Waziri mkuu ungekuwa dikteta zaidi ya Hitler au Mussolini.
Mama Samia yuko sahihi kuwaacha watu waongelee mambo haya ikiwemo chanjo. Amiri Jeshi mkuu anapaswa kuwa na ngozi ngumu maana maamuzi yake yanaweza leta madhara makubwa. Kiufupi hufai hata kuongoza kijiji, sijui hata ubavu wa kumshauri mtu mzito kama CiC unaupata wapi?

Rais sio muoga wala sio kwamba hajitambui. Watu wasiojitambua kama wewe ndio mnamuona hivyo.

By the way kama wanaokataa chanjo wana sababu za kijinga na zisizo na mashiko, mbona sasa unataka kuwanyamazisha? Si uwaache watu wachambue mchele na pumba? Au una maana Watanzania ni vilaza plus na hawana akili hata chembe ya kujua mpaka wapate handlers kama wewe?

Shame on you dictator!
Mwendazake mwenyewe pamoja na kuimba chanjo hazifai,bado wengine walienda kuchanjwa kwenye nchi nyingine.Akabaki kulalamika waliochanjwa wametuletea Corona ya ajabuajabu ila hakupiga marufuku.

Mama naye asilazimishe abaki tu na msimamo wake kuwa chanjo zinafaa.
Wananchi tumeshajua mchele ni upi na pumba ni zipi.
 
1. Badala ya kumwomba asiongelee chanjo, serikali inatakiwa ijibu hoja zake (mf. Madhara ya muda mrefu ya hizo chanjo ni nini?) Kisayansi. Kumfumba mtu mdomo kwa vitisho siyo solution nzuri ya tatizo.
2. Nchi zote zinazotambua uhuru na haki za binadamu hakuna hata moja ambayo imefanya chanjo kuwa ya lazima.
Hilo ndo la msingi Sana.Tena wakianza kumjibu hoja zake wapite Mashuleni ili wanafunzi waache kukimbia madarasani kuogopa chanjo,maana imefikia sehemu zingine mtu akionekana ni mgeni Ana kibox mkononi watoto wanatimua mbio.

Kama hawana majibu ya kisayansi Basi wamuache Gwajima aendelee kutamba madhabahuni.
 
Tumeshindwa kuelewa kwamba COVID ipo tunaishi maisha yetu ya miaka yote,unazan tutaelewa kuhusu chanjo....?
 
Mwendazake mwenyewe pamoja na kuimba chanjo hazifai,bado wengine walienda kuchanjwa kwenye nchi nyingine.Akabaki kulalamika waliochanjwa wametuletea Corona ya ajabuajabu ila hakupiga marufuku.

Mama naye asilazimishe abaki tu na msimamo wake kuwa chanjo zinafaa.
Wananchi tumeshajua mchele ni upi na pumba ni zipi.
Ikibakia kuwa hiyari ni tukaacha kulazimishana, kila mtu atatumia akili yake na utashi wake na tutabakia salama na wamoja kama taifa. Kila mtu aseme msimamo wake kwa uhuru bila kumlazimisha mwingine. Kila mtu aamue na abebe msalaba utakaotokana na maamuzi yake. Hapo ndipo usalama upo. Akitokea wa kulazimisha, iwe kuchanja au kuzuia kuchanja, taifa litapata shida sana na litagawanyika.

Kila mtu ajiamulie. Watu wameshapata elimu, imetosha. tujikite kukuza uchumi maana tatizo la umaskini ni kubwa kuliko hizi mambo za Korona!
 
Up dates; waziri wa afya aagiza gwajima kukamatwa kwa kosa LA kupotosha umma juu ya chanjo ya corona!
 
Heading ya uzi huu ni 'very confusing'! Yaani heading inapiga teke uzi kisha inajikata ngwala.

Msomaji, ebu rudia kusoma heading ya uzi huu utaelewa ninachomaanisha.
 
Jana nilimskiliza tena askofu Gwajima! Matamshi yake yanaungwa mkono na watu wengi sana kuliko hata watu waliopewa ubalozi wa Corona. Nashauri yafuatayo:

1. Serikali iongeze elimu juu ya chanjo
2. SerikaLi imuombe Gwajima abaki na msimamo wake lakini asiongelee chanjo
3. Itangaze chanjo kuwa lazima
4. Vyama vya upinzani vishirikishe hatua kwa hatua ilikuleta umoja katika kupambana na hili janga.

ÑB: Clip za Gwajima zinauzwa na warusha movie tsh 300 na unaambiwa mauzo ni makubwa. Jana kwenye kijiwe cha chai tuliwekewa hiyo video mpaka watu wakasahau kuangalia movie.
Imuombe...??????
 
Mama samia amethibitisha bayana kwamba mwanamke hawezi kuongoza hii nchi, taifa linapiga kampeni ya chanjo, halafu anasimama mtu mmoja kwa dharau na kiburi cha kupitiliza nae anapiga kampeni ya kupinga chanjo tena anatamka hadharani kwamba viongozi wanaopigia debe chanjo akili wameziweka likizo,

yeye Rais na Amiri jeahi mkuu ametulia tu sijui ni uoga sijui ni kutokujitambua , yani simuelewi kabisa
Kwa hiyo wewe ulitakaje??.
 
Hilo ndo la msingi Sana.Tena wakianza kumjibu hoja zake wapite Mashuleni ili wanafunzi waache kukimbia madarasani kuogopa chanjo,maana imefikia sehemu zingine mtu akionekana ni mgeni Ana kibox mkononi watoto wanatimua mbio.

Kama hawana majibu ya kisayansi Basi wamuache Gwajima aendelee kutamba madhabahuni.
Nimecheka kwa sauti...Jamani hakuna kitu kibaya kama fear of unknown!
Tuwaelewe tu raia wetu na tuwaache muda uwasaidie wafanye maamuzi ya binafsi bila mashinikizo....Kama ni kupiga chanjo kimya kimya na kuacha iwe kimya kimya, kama ni kupiga kwa campaign basi na wale ambao wanahitaji maelezo waeleze doubts zao...Tusigawanywe pasipo msingi wowote
 
Naomba kuuliza, side effects za hiyo chanjo baada ya miaka mi5 au 10 ni yapi? Na side effects kwa watoto atakaowazaa baada ya miaka mi5 au 10 ni yapi?
 
Naomba kuuliza, side effects za hiyo chanjo baada ya miaka mi5 au 10 ni yapi? Na side effects kwa watoto atakaowazaa baada ya miaka mi5 au 10 ni yapi?
Watashambuliwa na virusi vya Corona ila hawtapata madhara makubwa
 
Watashambuliwa na virusi vya Corona ila hawtapata madhara makubwa
Hayo ni madhara au ni faida za kuchoma chanjo? Na hayo majaribio mliyafanya kuanzia mwaka gani hadi mwaka gani kwa majaribio ya miaka 5 na 10?
 
Naomba kuuliza, side effects za hiyo chanjo baada ya miaka mi5 au 10 ni yapi? Na side effects kwa watoto atakaowazaa baada ya miaka mi5 au 10 ni yapi?
Mpaka sasa hakujawahi kutokea chanjo yenye kuleta side effects baada ya siku ya 40 baada ya kuchoma chanjo. Hivyo hivyo kwa chanjo ya uviko na kwa kuangalia viambata vilivyomo ndani ya chanjo za uviko, wataalamu hawategemei kama kutakua na side effects zitazoweza kutokea zaidi ya siku ya 40 baada ya kuchoma chanjo ya uviko.
 
Back
Top Bottom