#COVID19 Serikali iongeze elimu dhidi ya chanjo ya COVID-19, imuombe Askofu Gwajima asiongelee chanjo

Nashindwa kuelewa wanashindwa kumzima huyu mpuuzi ambae anapingana na serikali, Gwajima Ni muhaini, ana lengo la kupindua nchi na kikundi Cha sukuma gang wenzie wachache, inatakiwa muda huu awe jela au apandishwe cheo haraka
 
Gwajima ni mbunge wa bunge la JMT.Na kazi ya mbunge sio kusimamia Maamuzi ya Serikali kisa chama chake ndio kinaunda serikali. Huwa mnasema wabunge wa ccm ni kasuku na wao kila kitu ni NDIYO. Leo anatokea mtu anapinga,mnaanza kumshambulia. HIVI NYIE WATU MNASIMAMIA NINI?
 
Kanisani ni bungeni? Umesoma ukaelewa nilichomaanisha?
 
Mwendazake mwenyewe pamoja na kuimba chanjo hazifai,bado wengine walienda kuchanjwa kwenye nchi nyingine.Akabaki kulalamika waliochanjwa wametuletea Corona ya ajabuajabu ila hakupiga marufuku.

Mama naye asilazimishe abaki tu na msimamo wake kuwa chanjo zinafaa.
Wananchi tumeshajua mchele ni upi na pumba ni zipi.
 
Hilo ndo la msingi Sana.Tena wakianza kumjibu hoja zake wapite Mashuleni ili wanafunzi waache kukimbia madarasani kuogopa chanjo,maana imefikia sehemu zingine mtu akionekana ni mgeni Ana kibox mkononi watoto wanatimua mbio.

Kama hawana majibu ya kisayansi Basi wamuache Gwajima aendelee kutamba madhabahuni.
 
Tumeshindwa kuelewa kwamba COVID ipo tunaishi maisha yetu ya miaka yote,unazan tutaelewa kuhusu chanjo....?
 
Ikibakia kuwa hiyari ni tukaacha kulazimishana, kila mtu atatumia akili yake na utashi wake na tutabakia salama na wamoja kama taifa. Kila mtu aseme msimamo wake kwa uhuru bila kumlazimisha mwingine. Kila mtu aamue na abebe msalaba utakaotokana na maamuzi yake. Hapo ndipo usalama upo. Akitokea wa kulazimisha, iwe kuchanja au kuzuia kuchanja, taifa litapata shida sana na litagawanyika.

Kila mtu ajiamulie. Watu wameshapata elimu, imetosha. tujikite kukuza uchumi maana tatizo la umaskini ni kubwa kuliko hizi mambo za Korona!
 
Up dates; waziri wa afya aagiza gwajima kukamatwa kwa kosa LA kupotosha umma juu ya chanjo ya corona!
 
Heading ya uzi huu ni 'very confusing'! Yaani heading inapiga teke uzi kisha inajikata ngwala.

Msomaji, ebu rudia kusoma heading ya uzi huu utaelewa ninachomaanisha.
 
Imuombe...??????
 
Kwa hiyo wewe ulitakaje??.
 
Nimecheka kwa sauti...Jamani hakuna kitu kibaya kama fear of unknown!
Tuwaelewe tu raia wetu na tuwaache muda uwasaidie wafanye maamuzi ya binafsi bila mashinikizo....Kama ni kupiga chanjo kimya kimya na kuacha iwe kimya kimya, kama ni kupiga kwa campaign basi na wale ambao wanahitaji maelezo waeleze doubts zao...Tusigawanywe pasipo msingi wowote
 
Naomba kuuliza, side effects za hiyo chanjo baada ya miaka mi5 au 10 ni yapi? Na side effects kwa watoto atakaowazaa baada ya miaka mi5 au 10 ni yapi?
 
Naomba kuuliza, side effects za hiyo chanjo baada ya miaka mi5 au 10 ni yapi? Na side effects kwa watoto atakaowazaa baada ya miaka mi5 au 10 ni yapi?
Watashambuliwa na virusi vya Corona ila hawtapata madhara makubwa
 
Watashambuliwa na virusi vya Corona ila hawtapata madhara makubwa
Hayo ni madhara au ni faida za kuchoma chanjo? Na hayo majaribio mliyafanya kuanzia mwaka gani hadi mwaka gani kwa majaribio ya miaka 5 na 10?
 
Naomba kuuliza, side effects za hiyo chanjo baada ya miaka mi5 au 10 ni yapi? Na side effects kwa watoto atakaowazaa baada ya miaka mi5 au 10 ni yapi?
Mpaka sasa hakujawahi kutokea chanjo yenye kuleta side effects baada ya siku ya 40 baada ya kuchoma chanjo. Hivyo hivyo kwa chanjo ya uviko na kwa kuangalia viambata vilivyomo ndani ya chanjo za uviko, wataalamu hawategemei kama kutakua na side effects zitazoweza kutokea zaidi ya siku ya 40 baada ya kuchoma chanjo ya uviko.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…