Serikali iongeze umri wa kustaafu Kwa baadhi ya kada kutoka miaka 60 ya Sasa mpaka 65

Kwa jinsi hali zilivyo ngumu kitaa na ukosefu wa ajira hakuna anayekataa kwenda vijijini miaka hii

Hata masista duu, mabraza duu ajira za TAMISEMI wako wengi tu vijijini maji ya kisima wanakunywa na ng'ombe nenda TikTok ukaone video zao maGen Z wameshapauka life la kijiji

Wewe staafu tu mzee, ukiwa kazini epuka sana kusema eti bila mimi hapa mambo hayaendi kuna watu wanajua kukuzidi kwa mbali
 

NIKUKUMBUSHE TU KUWA, TANZANIA INATATIZO KUBWA SANA LA UKOSEFU WA WAALIMU WA HESABU HASA KWA SHULE ZA MSINGI IKIFUATIWA NA SEKONDARI. KWA HIYO, UNGESEMA WAALIMU WA HESABU (WALE WENYE PASS YA HESABU YA KUELEWEKA) NDIO WAONGEZEWE MUDA; UNGE PATA WAUNGAJI MKONO.....
 
Shule Gani hiyo,Mimi shuleni kwangu Kuna walimu 7 wa hesabu na wanafundisha kwa kugawana topiki wakati walimu wa kingereza wapo wawili tu.

Tuache kukariri
 
Mwanangu huko Serikalini hakuna mtu muhimu! Ukifa Leo anakuja mtu Bora zaidi Yako. Kaa kijanja
 
Labda Kama ingekuwa mTu akistaaafu hakuna kiktoo, anapewa mzgo wake woTe.
ila kwa hal ya sasa 60 yenyew mingi
 
Shule Gani hiyo,Mimi shuleni kwangu Kuna walimu 7 wa hesabu na wanafundisha kwa kugawana topiki wakati walimu wa kingereza wapo wawili tu.

Tuache kukariri
Waalimu wa hesabu shule za msingi waliopo ni takriban 20% ya mahitaji; huku masomo ya Arts wakiwa 90%+
na ndio sababu kila mwaka takribani 75 to 80% ya wanafunzi hupata alama sifuri kwenye Hesabu.
Nafikiri hiyo shule yako itakuwa ipo Iran au China ambapo Hesabu ni kipaumbele namba moja....
Kumbuka, mwalimu wa Hesabu anayetambulika ni yule mwenye pass ya Hesabu kidato cha nne.
 
Solution; serikaL kuboresha mazingira ya vijijini & pawepo na posho za watumish wa vijijini Na Kuajiri watumishi wengi zaidi..
 
Solution; serikaL kuboresha mazingira ya vijijini & pawepo na posho za watumish wa vijijini Na Kuajiri watumishi wengi zaidi..

Hizi Sifuri za Hesabu za kila mwaka, zikiwekewa mkakati wa kuajiri Waalimu wenye pass za Hesabu, kwa ajili ya kufundisha Hesabu; ndani ya miaka 3, zinafutika
 
Hizi Sifuri za Hesabu za kila mwaka, zikiwekewa mkakati wa kuajiri Waalimu wenye pass za Hesabu, kwa ajili ya kufundisha Hesabu; ndani ya miaka 3, zinafutika
Pasipo kuboresha mazingira ya vijijini kazi bure, wataajiriwa kisha watakaa kwa muda na kuhama_
 
Pasipo kuboresha mazingira ya vijijini kazi bure, wataajiriwa kisha watakaa kwa muda na kuhama_

Kwa sasa kila wilaya ina vijana waliosoma kidato cha nne na kupata ufaulu wa kawaida.
Wanaweza kuajiri waalimu wa Hesabu wanaotokea maeneo yenye upungufu, mfano kwa huku kwetu Sumbawanga, watokee maeneo ya kwetu; wala hakuna atakayehama...aende wapi?
Mfano; waseme Vijana 40 kutoka sumbawanga vijijini wenye pass za hesabu...mbona wapo?
 
Wakiajiri kwa mtindo huo itasaidia pakubwa, _ sasa mfumo wa sasa mtu toka sumbawanga anapangiwa musoma, ni ngumu kudumu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…