Serikali iongeze umri wa kustaafu Kwa baadhi ya kada kutoka miaka 60 ya Sasa mpaka 65

Serikali iongeze umri wa kustaafu Kwa baadhi ya kada kutoka miaka 60 ya Sasa mpaka 65

Kutokana na uzoefu nilionao nimgundua kuwa Kuna watumishi ambao ni muhimu na wakistafu kupatikana mwingine wakuziba pengo ni ngumu, mfano watumishi wakada ya ualimu na afya. Naleta maelezo na ufafanuzi kama ifuatavyo

1. Huko vijijini ambako mazingiria ni magumu utamkuta nesi na tabibu ambao wamejitolea kufanya kazi hapo, wananchi wanafaidika na wanaridhika na utendaji kazi wao ,Sasa kimbembe kinakuja muda wakustaafu umefika anastaafu tabibu au nesi kuja kuletwa mwingine inachukua muda mrefu wakati huyo anaye staafu Bado ana nguvu.
Hali hii inawaumiza sana wananchi kwakukosa mtaalamu WA kuwahudumia waongezewe umri wa kustaafu ili waendelee kutoa huduma, Kuna sehemu zingine watumishi wakipangiwa hawataki kwenda wapo tayari hata kuacha kazi.

2. Walimu nao ni kada muhimu yakuangaliwa kwenye umri wa kustaafu, tunaenda shule huko vijijini ina wanafunzi mianne au miatano LAKINI walimu waloajiliwa na serikali wapo watatatu harafu Kuna walimu wanne wakujitolea, inafika wakati mwalimu anastaafu , kumbuka hayo maeneo hakuna watumishi wako tayari kwenda kufanya kazi Sasa kama hao waliopo wana nguvu na wamejitolea kufanya kazi hapo kwenye mazingiria magumu unamtafishaje wakati uwezekano wakum nileta mwalimu mwingine ni mgumu.

Mapendekezo yangu Kwa serikali yangu tukufu ni kuwa Kuna kada ni muhimu sana na wapo karibu nchi nzima katika maeneo mbalimbali ambayo mengine Yana mazingiria magumu ya kuishi na kufanya kazi kama wapo tayari kuendelea kufanya kazi waongezewe umri wa kustaafu kwasababu wakistafu kumpata mbadala inachukua muda mrefu wakati huo wananchi wanakuwa wanaumia Kwa kukosa huduma za elimu na afya.

Ingawa baadhi ya wadau watasema Kwa nini serikali isiajili LAKINI ukweli ni kwamba hata ikiajiri Bado Kuna watumishi hawako tayari kwenda kufanya kazi baadhi ya maeneo. Naomba tuwashikilie waliopo wakati tunatafuta mbadala
Hoja yako ni nzuri ila kwamba nafasi zao zinakuwa vigumu kuzibwa si sawa. Sasa hivi kada hizo mbili zina vijana wengi tu wanaozurura mjini kwa kukosa ajira. Ili hawa vijana wapate ajira ni vyema hao waliofikisha umri wa kustaafu wafanye hivyo ili wapate muda wa kupumzika na kuwalea vyema wajukuu wao. Nawashauri kufanya hivyo kwani si vyema kuendelea kuwa kazini ilhali umri umekwenda na hivyo kutokuwa na uwezo mzuri wa utendaji kazi. Hoja nyingine hutolewa kwamba vijana hawana ujuzi na uzoefu wa kazi husika. Uzoefu hupatikana wakati ukiwa kazini. Sasa wewe unataka wawe na uzoefu huku unawazibia ajira. Yote hii ni kutaka kuatamia nafasi na kuwazibia vijana ambayo ni stahili yao sasa.
 
Back
Top Bottom