Serikali iongeze umri wa kustaafu Kwa baadhi ya kada kutoka miaka 60 ya Sasa mpaka 65

Hoja yako ni nzuri ila kwamba nafasi zao zinakuwa vigumu kuzibwa si sawa. Sasa hivi kada hizo mbili zina vijana wengi tu wanaozurura mjini kwa kukosa ajira. Ili hawa vijana wapate ajira ni vyema hao waliofikisha umri wa kustaafu wafanye hivyo ili wapate muda wa kupumzika na kuwalea vyema wajukuu wao. Nawashauri kufanya hivyo kwani si vyema kuendelea kuwa kazini ilhali umri umekwenda na hivyo kutokuwa na uwezo mzuri wa utendaji kazi. Hoja nyingine hutolewa kwamba vijana hawana ujuzi na uzoefu wa kazi husika. Uzoefu hupatikana wakati ukiwa kazini. Sasa wewe unataka wawe na uzoefu huku unawazibia ajira. Yote hii ni kutaka kuatamia nafasi na kuwazibia vijana ambayo ni stahili yao sasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…