Hivi karibuni hii biashara ya kusafirisha minofu kutoka kanda ya ziwa kwa kutumia mashirika kama Rwanda Air na leo tena nimesikia Ethiopian airways imerudi kwa kasi na kimekuwa kama kitu cha kujivunia hadi waziri anaenda kushuhudia.
Wengi humu tunajua watoto wetu wamedumaa kwa zaidi ya asilimia 35 na tunaelewa samaki wana protini nyingi na madini muhimu kwa ajili ya mama wajawazito na ukuaji wa ubongo wa watoto.
Kwa nini kama watu wameona soko la minofu Ulaya wasifuge hao samaki kibiashara kwenye mabwawa kuliko kushindania hawa samaki wachache wanaovuliwa kwenye maziwa na mito yetu?
Yaani wananchi wetu washindane na wanunuaji wa Ulaya, kweli? naamini Rais ataliona hili kwa manufaa mapana ya vizazi vya watanzania.