Serikali ipige marufuku biashara ya minofu ya samaki kwenda Ulaya

Serikali ipige marufuku biashara ya minofu ya samaki kwenda Ulaya

una uhakika gogogo na hao samaki wengine wapo masoko yote Tanzania ? mimi nimeishi zaidi ya mikoa 5 wananchi wengi wanaoenda sokoni huenda kununua mboga za majani na dagaa tu,na hata wachache wanaonunua nyama na samaki hulia bei ni kubwa

Kama unazungumzia suala la nutrition, dagaa ni bora kuliko sangala au samaki wengine wakubwa katika ziwa Victoria
ingawaje radha ya mdomoni ni vise versa. Hivyo siyo vibaya kufanya biashara ya kigeni ya sangala.
 
kama kweli tunawajali wanyonge hizo samaki ziende masoko ya watanzania zikauzwe bei ndogo
hivi lile agizo la kuwauzia nyama ya kifimbo watanzania lilitekelezwa ?
Unafikili samaki anauzwa kwa bei kama mchicha? Zidhani hata bei ya samaki unaijua.
 
Kama unazungumzia suala la nutrition, dagaa ni bora kuliko sangala au samaki wengine wakubwa katika ziwa Victoria
ingawaje radha ya mdomoni ni vise versa. Hivyo siyo vibaya kufanya biashara ya kigeni ya sangala.
Hapana mkuu nilikuwa nazungumzia kubadilisha chakula yani watu wa kipato cha chini wawe na uwezo wa kubadili mboga na wa kipato cha kati waweze kumudu gharama za mboga bila kulia,ila ahsante kwa mchango wako maana sikufahamu kuhusu Nutrition
 
Unafikili samaki anauzwa kwa bei kama mchicha? Zidhani hata bei ya samaki unaijua.
Mkuu bila shaka hujanielewa maana umeongea kitu tofauti na nilichoandika,naomba unisome tena utanielewa
 
The only,
Mkuu matusi yametoka wapi? Nakushauri usiwe unacomment bila kuelewa kilichoandikwa, nani amekwambia wewe au mtu yeyote awekeze kuvua? Anyway ngoja nikueleweshe nilichoandika

Ninasema hivi, hao samaki wanaouzwa nje ya nchi kutokea hapa Tanzania hata mtanzania mwenye kipato cha kati hawezi kumudu kuwanunua mara kwa mara kutokana na bei yake kuwa juu, nikashauri Serikali iwavue na iwauze kwa bei ya chini ambayo Mtanzania ataweza ku Afford yaani wapelekwe katika Masoko ya Tanzania kutokana na Kwamba ninayafahamu Masoko Mengi ya hapa nchini kwetu asilimia kubwa ya wananchi wanaoenda huko hununua.

Dagaa na mboga za majani kila siku kwa sababu hawamudu gharama za nyama na samaki, hao samaki ambao mleta mada anawazungumzia wanapelekwa nje ni kazi ngumu sana kwa hawa wavuvi wetu kuwavua kutokana na kwamba inahitajika vifaa vya kisasa kwa mfano kuna samaki ana urefu sawa na Binadamu huwezi kumvua kwa nyavu

Nimesikitika sana kuona nimeandika kitu cha maana umejibu kwa tusi na mbaya zaidi hujanielewa kabisa, ungeuliza, humu JF tupo kwa ajili ya kujadiliana kwa hoja
 
Usijali mku ili mradi sato zetu zipo. Acha wachukue hizo sangara
 
The only,
Kwa kifupi wewe umedhani mimi nazungumzia mfanya biashara kupangiwa bei, ukisoma kwa makini comment yangu utaona nimesema samaki wavuliwe na serikali halafu auziwe mfanya biashara kwa bei ya chini ambapo na yeye atauzia wananchi kwa bei nafuu, hapo mfanya biashara hapangiwi bei ataipanga yeye mwenyewe baada ya kuona amepata bidhaa kwa bei nafuu
 
Tanzania makabila magapi hula Samaki hadi samaki iwe issue? Masai huwa Hali samaki ulishawahi muona mtoto wa kimasai mwenye utapiamlo? Mleta maada una agenda ya kishetani tu kuua uchumi waua uchumi Kama nyie ndio mnataka mpewe nchi Mungu hawezi kubali atatupa hata nguvu ya kuwaibia kura

wewe ni economic hitman shetani wewe
Kwa akili za kiwango cha chini namna hii, inahitaji uvumulivu wa hali ya juu kuweza kukuelewesha jambo lolote
 
Sorry wanajamvi Tueleweshane kwanza jamani
Hii biashara ya samaki toka mwanza inafanyikaje!

Wateja toka nje ya Tz wanakuja mwanza kununua na hayo mashirika ya ndege yanakodiwa na hao wafanyabiashara?

Au wafanyabiashara waTz (companies) wanakodi hizo ndege kwenda kuuza huko ulaya?

Au serikali ndo inahusika na hii biashara
 
Ziwa victoria haikuwahi kuwa na sangara, sangara ilipakdikizwa toka ulaya nadhan ni Norway, hivyo wanachukua kilicho chao
Viwanda vya sangara vilianzia kenya na wengi toka mara waliuza huko kupitia maji na nchi ilikuwa hainufaiki zaidi ya vibali vya wauzaji yaan pasport hiyo ni miaka ya 90 then ikajengwa Mazara pale Musoma daima wahindi wanapeleka kwa magari hadi kenya kisha husafirisha hivyo tz hatujawahi kuexport hii ndiyo mara ya kwanza hivyo lazima tufurahie kwani tunawaza kununua ndege ya mizigo


Tanzania fileti zipo chache nakumbuka mm nilikula 2007 kwenye warsha ya wazungu mjini Musoma
Ebu zirafuteni kwenye malls kubwa
 
Tanzania makabila magapi hula Samaki hadi samaki iwe issue? Masai huwa Hali samaki ulishawahi muona mtoto wa kimasai mwenye utapiamlo? Mleta maada una agenda ya kishetani tu kuua uchumi waua uchumi Kama nyie ndio mnataka mpewe nchi Mungu hawezi kubali atatupa hata nguvu ya kuwaibia kura

wewe ni economic hitman shetani wewe
Wamejaa mahospitalin nenda muhimbil
 
Samaki mbona wengi tu mtaani. Kuna perege, kitoga, changu, mbarata, kibua, kambale. Acha wivu mtoa mada
Dah!

Umekumbusha mbali sana ulivyotaja samaki MBARATA mkuu. Wewe umewaona wapi?
 
Back
Top Bottom