tpaul
JF-Expert Member
- Feb 3, 2008
- 24,225
- 22,632
Inasikitisha sana mtoto wa darasa la saba kutofahamu historia ya nchi yake. Juzi nilimsikia kiongozi mmoja wa serikali akiwahoji baadhi ya wanafunzi maswali mepesi kabisa lakini wakashindwa kujibu. Ni aibu kubwa sana mwanafunzi wa darasa la saba anayetarajia kufanya mtihani wa kitaifa miezi 8 ijayo kuulizwa ataje matunda ya muungano anataja maembe, maparachichi, machenza na machungwa!
Nimekuwa nikifuatilia malezi ya watoto hapa mjini kwa muda mrefu; nimegundua watoto wanatumia muda mwingi kutazama tamthlia za kichina, kihindi na kifilipino wawapo nyumbani na kwenye mabanda ya kutazamia video. Hata inapofika saa 2 jioni badala ya kutyuni taarifa ya habari, wazazi hubadilisha chaneli na kuanza kutazama sinema.
Matokeo yake watoto wanashindwa kujibu maswali rahisi kama vile kutaja majina ya viongozi wakubwa nchini wakimwemo Waziri Mkuu, Rais wa Zanzibar na Waziri Mkuu. Hili ni tatizo kubwa. Yaani nchi hii tunakoelekea Mungu tu atuonee huruma atufungue minyororo ya akili tuliyofungwa na shetani. Akina mama na beki 3 wanaharibu sana watoto kwa tamthlia hizi za kipuuzi. Na wakimaliza kutazama tamthlia wanahamia kusikiliza singeli, bongofleva, taarabu, vigodoro na nyimbo nyingine za kijinga kama hizo.
Inashangaza unamkuta mtoto anajua kusimulia tamthlia ya kichina mwanzo hadi mwisho lakini hajui historia ya nchi yake. Ifike wakati serikali itunge sheria kali ya kudhibiti ujinga huu ili kunusuru kizazi hiki na kizazi kijacho. Unadhani hawa watoto wanaotazamishwa tamthlia za kijinga wakiwa wazazi hili taifa litakuwa na watu wa aina gani? Nonsense!