Serikali ipige marufuku utazamaji wa tamthlia hapa nchini

Serikali ipige marufuku utazamaji wa tamthlia hapa nchini

Hilo ni jukumu la wazazi kumlea mtoto wao kwa mujibu wa maadili waiojiwekea wenyewe.

Serikali itapiga marufuku mangapi hapa nchini? Yalimshinda Nyerere hayo alikuwa hataki watu wamiliki TV, friji kwa kuwa ni anasa, matokeo yake ilikuwaje?
raha sio raha bila shaka hii ni raha

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Wewe historia imekusaidia nini?
Hebu muulize historia ya kujua Ziwa Viktoria lilivumbuliwa na mzungu inamsaidia nini?

Au kujua Kenya ipo Afrika mashariki inamsaidia nini?

Mwambie pia, Cha msingi tafuta pesa kisha fasta utayajua matunda ya Muungano bila hata kuwa na mwalimu wa kukufundisha. Hata Kenya utaijua tu iko wapi maana utaenda kutembea
 
ACHA NIANDIKE KWA HERUFI KUBWA!!

MBONA XVDS ILIPIGWA STOP NA HAMKUSEMA ETI MTAKOSESHWA RAHA?
KWANINI BANGI INAZUILIWA NA HAMSEMI?
KWANINI UPUUZI(TIGO) INAZUILIWA NA HAMSEMI?

UKWELI JAMBO BAYA LOLOTE LINATAKIWA KUPINGWA TENA KWA NGUVU.. LEO HII TUNAMPINGA MTOA MADA LAKINI WATOTO WAKIFELI MASHULENI MNASINGIZIA WALIMU!

UKWELI KUNA VITU VINAINGIA HADI UBONGONI NA KWA MTOTO HUACHA DAMAGE KUBWA!!

NIMEISHI NA JAMAII ZA TAMTHLIA NA UOVYO MWINGINE NA JAMII ZILIZOKUWA BUSY NA ELIMU UKWELI TOFAUTI IPO!
 
Na mimi nakuuliza wewe maswali haya : Nitajie changamoto/kero 10 za huu Muungano, pili ni changamoto/kero ngapi tayari zimeshapatiwa ufumbuzi? Kwa mujibu wa rasimu ya katiba ya mzee Warioba ni yepi yalikuwa ni mapendekezo yao kuhusiana na mfumo wa huu Muungano? Asente.
 
Hii ni hoja mpya kabisa mkuu. Haihusiani na hii iliyopo mezani.
 
ACHA NIANDIKE KWA HERUFI KUBWA!!

MBONA XVDS ILIPIGWA STOP NA HAMKUSEMA ETI MTAKOSESHWA RAHA?
KWANINI BANGI INAZUILIWA NA HAMSEMI?
KWANINI UPUUZI(TIGO) INAZUILIWA NA HAMSEMI?

UKWELI JAMBO BAYA LOLOTE LINATAKIWA KUPINGWA TENA KWA NGUVU.. LEO HII TUNAMPINGA MTOA MADA LAKINI WATOTO WAKIFELI MASHULENI MNASINGIZIA WALIMU!

UKWELI KUNA VITU VINAINGIA HADI UBONGONI NA KWA MTOTO HUACHA DAMAGE KUBWA!!

NIMEISHI NA JAMAII ZA TAMTHLIA NA UOVYO MWINGINE NA JAMII ZILIZOKUWA BUSY NA ELIMU UKWELI TOFAUTI IPO!
Kweli kabisa mkuu. Watanzania wengi wanaonipinga ni zao la tamthlia, kwa hiyo, hawawezi kunikubali hata kidogo. Hawajui kuwa nazi mbovu ni harabu ya nzima. Utadhani huko shuleni walienda kusomea ujinga badala ya kusoma elimu.
 
Imekuuma Sana we jamaa watoto kushindwa kutaja Rais na makamu wa Zanzibar eeenh?

Hata wakiyajua haya yanawasaidia nini mwishowe?

Maisha Ni magumu Sana sasa hivi, acheni watu wa refresh asee hata na tamthilia, we kwa ugumu huu wa maisha unataka mtoto wa Urambo au Kitumbikwela Lindi akariri jina la waziri mdogo wa maji na nishati wa Zanzibar!
Hahahaha,,kitumbikwela napajua sana
 
Inasikitisha sana mtoto wa darasa la saba kutofahamu historia ya nchi yake. Juzi nilimsikia kiongozi mmoja wa serikali akiwahoji baadhi ya wanafunzi maswali mepesi kabisa lakini wakashindwa kujibu. Ni aibu kubwa sana mwanafunzi wa darasa la saba anayetarajia kufanya mtihani wa kitaifa miezi 8 ijayo kuulizwa ataje matunda ya muungano anataja maembe, maparachichi, machenza na machungwa!

Nimekuwa nikifuatilia malezi ya watoto hapa mjini kwa muda mrefu; nimegundua watoto wanatumia muda mwingi kutazama tamthlia za kichina, kihindi na kifilipino wawapo nyumbani na kwenye mabanda ya kutazamia video. Hata inapofika saa 2 jioni badala ya kutyuni taarifa ya habari, wazazi hubadilisha chaneli na kuanza kutazama sinema.

Matokeo yake watoto wanashindwa kujibu maswali rahisi kama vile kutaja majina ya viongozi wakubwa nchini wakimwemo Waziri Mkuu, Rais wa Zanzibar na Waziri Mkuu. Hili ni tatizo kubwa. Yaani nchi hii tunakoelekea Mungu tu atuonee huruma atufungue minyororo ya akili tuliyofungwa na shetani. Akina mama na beki 3 wanaharibu sana watoto kwa tamthlia hizi za kipuuzi. Na wakimaliza kutazama tamthlia wanahamia kusikiliza singeli, bongofleva, taarabu, vigodoro na nyimbo nyingine za kijinga kama hizo.

Inashangaza unamkuta mtoto anajua kusimulia tamthlia ya kichina mwanzo hadi mwisho lakini hajui historia ya nchi yake. Ifike wakati serikali itunge sheria kali ya kudhibiti ujinga huu ili kunusuru kizazi hiki na kizazi kijacho. Unadhani hawa watoto wanaotazamishwa tamthlia za kijinga wakiwa wazazi hili taifa litakuwa na watu wa aina gani? Nonsense!

View attachment 2641042
Hivi kwenye hizi shule za kata wanafunzi wanafundishwa elimu au ujinga?
 
Back
Top Bottom