Serikali ipige marufuku utazamaji wa tamthlia hapa nchini

Serikali ipige marufuku utazamaji wa tamthlia hapa nchini

Niliichukia History kama somo, lakini cha kushangaza kuna channel ya,Tv inaitwa " History" very interesting. Lakini nikagundua ni jinsi wanavyosimulia sauti pamoja na videos ina capture mindset ya mtu. Sasa tukikremishana miaka ya waarab kuja Tz, miaka ya mazao, n.k bila kuweka iwe interesting tutabaki hivihivi.
Tamthilia ni wajibu wa mzazi kuweka " Parental control " na kudhibiti muda wa kuangalia TV kwa watoto , Ni wajibu wa Mzazi sio Serikali.
Mimi pia ni mmoja wao. Somo la historia nilikuwa naona umuhimu wake ila sikulipendi kwa sababu mfumo wa elimu na mitihani ulikuwa unasisitiza kukariri zaidi miaka na majina badala ya knowledge na critical analysis ya historia yenyewe. Nimekuja kupenda historia baadae kabisa nje ya shule.
 
Hili halikuwa swali linalohitaji kukariri bali ni swali lililokuwa linahusu uelewa mdogo wa mwanafunzi, hasa ukizingatia kwamba majina hayo yanatamkwa kila siku kwenye TV, redio na vyombo vingine vya habari. Lakini kwa kuwa watoto siku zote watazamishwa taarabu, bongofleva, singeli na vigodoro ndio maana wanashindwa kujibu maswali rahsi kama haya. Huu ndio ulikuwa msingi wa hoja yangu mkuu. Labda umeninukuu vibaya.
Ila hao wasanii wa singeli na bongo flava si ndiyo supporters wakubwa wa serikali na chama. Kwa nini msiwaambie kina Diamond waimbe nyimbo zenye kutaja majina ya viongozi kama enzi zile za TOT. Mbona mnawamudu wote hao.
 
ataje matunda ya muungano anataja maembe, maparachichi, machenza na machungwa!
Hata mimi ningetaja hayo hayo, maana siijui faida nyengine ya Muungano, vp hajauliza hasara za Muungano? Ningejibu Zanzibar kutawaliwa na Tanganyika.
 
Inasikitisha sana mtoto wa darasa la saba kutofahamu historia ya nchi yake. Juzi nilimsikia kiongozi mmoja wa serikali akiwahoji baadhi ya wanafunzi maswali mepesi kabisa lakini wakashindwa kujibu. Ni aibu kubwa sana mwanafunzi wa darasa la saba anayetarajia kufanya mtihani wa kitaifa miezi 8 ijayo kuulizwa ataje matunda ya muungano anataja maembe, maparachichi, machenza na machungwa!

Nimekuwa nikifuatilia malezi ya watoto hapa mjini kwa muda mrefu; nimegundua watoto wanatumia muda mwingi kutazama tamthlia za kichina, kihindi na kifilipino wawapo nyumbani na kwenye mabanda ya kutazamia video. Hata inapofika saa 2 jioni badala ya kutyuni taarifa ya habari, wazazi hubadilisha na kuanza kutazama sinema.

Matokeo yake watoto wanashindwa kujibu maswali rahisi kama vile kutaja majina ya viongozi wakubwa nchini wakimwemo Waziri Mkuu, Rais wa Zanzibar na Waziri Mkuu. Hili ni tatizo kubwa. Yaani nchi hii tunakoelekea Mungu tu atuonee huruma atufungue minyororo ya akili tuliyofungwa na shetani. Akina mama na beki 3 wanaharibu sana watoto kwa tamthlia hizi za kipuuzi. Na wakimaliza kutazama tamthlia wanahamia kusikiliza singeli, bongofleva, taarabu, vigodoro na nyimbo nyingine za kijinga kama hizo.

Inashangaza unamkuta mtoto anajua kusimulia tamthlia ya kichina mwanzo hadi mwisho lakini hajui historia ya nchi yake. Ifike wakati serikali itunge sheria kali ya kudhibiti ujinga huu ili kunusuru kizazi hiki na kizazi kijacho. Unadhani hawa watoto wanaotazamishwa tamthlia za kijinga wakiwa wazazi hili taifa litakuwa na watu wa aina gani? Nonsense!
Historia yenyewe imepindwapindwa kama barabara za Njombe Nani anaitaka? Yaani mapinduzi ya Zanzibar yanamsaidia nini Mtoto wa Nyashana Mara?
 
Hilo ni jukumu lako wewe mzazi au mlezi...

Leo watoto wako... wa mwenzio wakiwa vibaka waache ni mzigo wake...

Pambana na kibanzi ktk jicho lako na uachane na boliti ktk jicho la mwenzio...
Hao wa mwenzio wakishaharibika, ndio watakuja kukukaba wewe na wanao. Watakuwa panya road wa kutishia maisha yako.

Watoto walioharibika ni kitisho cha usalama kwa jamii nzima.
 
Mwisho wa siku hata mtoto akijua mpaka majina ya madiwani wa nchi nzima havimsaidii chochote.

Mambo mengine ni kumuonea tuu mtoto je wewe mpaka leo unaweza sema hayo matunda ya muungano ukiachana na uliyokaririshwa kwenye vitabu??
 
Inasikitisha sana...

Haswa huyo aliyejibu maembe...
Inasikitisha sana kwa kweli. Serikali isipoingilia kati tutakuwa na kizazi cha ovyo sana hapa nchini.
 
Nyingi hazina maadili mema ya jamii zetu!

Umalaya mtupuu[emoji108][emoji108]

Watoto wanaweza kujifunza uharibifu katika umri Mdogo sana.

Kwanini wasibuni
Na kufundisha watu kupenda kufanya kazi yoyote halali kujipatia kipato ?!
 
Nikikumbuka wale waliokuwa vilaza darasani leo hii ndio wenye pesa kuliko Mimi,, naogopa hata kuongea lolote kuhusu hao walioshindwa kutaja majina ya viongozi
 
Nyingi hazina maadili mema ya jamii zetu!

Umalaya mtupuu[emoji108][emoji108]

Watoto wanaweza kujifunza uharibifu katika umri Mdogo sana.

Kwanini wasibuni
Na kufundisha watu kupenda kufanya kazi yoyote halali kujipatia kipato ?!
Kweli kabisa mkuu. Mavipindi mengi yanahusu taarabu, singeli, vigodoro na ujinga mwingine kama huo. Huwezi kukuta televisheni yoyote, hata zile zenye maadili ya kidini kama Azam, wakionesha masomo au vipindi kwa wanafunzi na watoto zaidi ya makatuni ya ajabu ajabu. Inauma sana.
 
Matunda ya muungano maana yake nini? Tumieni lugha kulingana na umri wa mtoto.
Hata tamthilia zikiondolewa hakuna kitakachobadilika. Kama hafundishwi shuleni unadhani atajua wapi?
Wewe mzazi ni jukumu lako ku-monitor programs anazoangalia mtoto wako kwenye TV, serikali haijakununulia TV umejinunulia mwenyewe
 
Sio mtoto wangu tu mkuu. Watoto wengi wanaharibiwa na hizi tamthlia, singeli na bongofleva. Hata yule mtoto aliyeshindwa kujibu maswali mbona sio mwanangu mkuu? Sote tukishirikiana kuokoa kizazi chetu tutakuwa na taifa bora hapo baadaye. usipinge kila kitu mkuu; be positive, flexible and humble!
na sineli za kanisani nazo?

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom