Serikali ipige marufuku utazamaji wa tamthlia hapa nchini

Hilo ni jukumu lako wewe mzazi au mlezi...

Leo watoto wako... wa mwenzio wakiwa vibaka waache ni mzigo wake...

Pambana na kibanzi ktk jicho lako na uachane na boliti ktk jicho la mwenzio...
Wewe watoto wa wenzio wakiwa vibaka au watu wa ovyo utanufaika nini mkuu? Acha kuetetea uharibifu wa taifa. Mtoto wa mwenzio ni mtoto wako pia. Na ukumbuke nazi mbovu ni harabu ya nzima.
 
Hapo ni sawa na useme serikali ipige marufuku uuzwaji wa pombe which is totally impossible.
 
Hapo ni sawa na useme serikali ipige marufuku uuzwaji wa pombe which is totally impossible.
Basi kama ni hivyo iruhusi pia uuzaji wa bangi na madawa ya kulevya ili taifa liangamie kabisa.
 
Wazazi wamewaachia waalimu wawalelee watoto.
 
IZI NDIO zinasababisha umasikini na uvivu. kwa mtu mwerevu, amua kutupa mbali tv, fanya mambo ya maana badala yake, maendeleo lazima utayapata tu.
 
Huo ulikuwa mfano tu.My point was hilo swala kutaka serikali ipige ban tamthilia haliwezekani. Labda ungeishauri jamii na hasa wazazi.
Basi kama ni hivyo iruhusi pia uuzaji wa bangi na madawa ya kulevya ili taifa liangamie kabisa.
 
Historia hii ya CCM na uzalendo uchwara wa viongozi kutumia fedha za kodi kwa uchoyo kwa kujinunulia ma toyota V8 kila moja millions zaidi ya 400 badala ya kutumia fedha hizo kuboresha elimu na afya ili waTanzania waweze kujiajiri kwa kutumia elimu inayostahiki siyo elimu hii iliyowekewa historia ruhani ya kiCCM!

Pia waTanzania wanastahili kuwa na afya bora kabisa ya kufanya kazi huku wameshiba milo mitatu kama serikali itaacha matumizi ya anasa kama magari V8 na kuelekeza fedha ktk rasilimali vifaa bora, dawa bora, matibabu bora huku sekta ya Afya na elimu ikiajiri watumishi wengi waliopikwa vizuri katika vyuo vyao vya elimu ili isaidie kufungua bongo za watoto wawe kizazi cha mabadiliko chanya cha baadaye.
 
Harafu Kwa vichekesho kama hivyo unatarajia Mwalimu atazeeka mapema kweli?
 
Niliichukia History kama somo, lakini cha kushangaza kuna channel ya,Tv inaitwa " History" very interesting. Lakini nikagundua ni jinsi wanavyosimulia sauti pamoja na videos ina capture mindset ya mtu. Sasa tukikremishana miaka ya waarab kuja Tz, miaka ya mazao, n.k bila kuweka iwe interesting tutabaki hivihivi.
Tamthilia ni wajibu wa mzazi kuweka " Parental control " na kudhibiti muda wa kuangalia TV kwa watoto , Ni wajibu wa Mzazi sio Serikali.
 
Swali aliloulizwa lilikuwa na utata wa lugha (ambiguity); neno tunda laweza kuwa mafanikio au zao la mmea lenye mbegu ndani yake. Kwahiyo mwanafunzi alikuwa sahihi kwa muktadha mwingine
 
Utakariri majina ya mawaziri wangapi? ili iweje?
Hili halikuwa swali linalohitaji kukariri bali ni swali lililokuwa linahusu uelewa mdogo wa mwanafunzi, hasa ukizingatia kwamba majina hayo yanatamkwa kila siku kwenye TV, redio na vyombo vingine vya habari. Lakini kwa kuwa watoto siku zote watazamishwa taarabu, bongofleva, singeli na vigodoro ndio maana wanashindwa kujibu maswali rahsi kama haya. Huu ndio ulikuwa msingi wa hoja yangu mkuu. Labda umeninukuu vibaya.
 
Elimu ya uraia siyo ya kuwakaririsha majina ya viongozi wa nchi, ambao kwanza wanaweza kubadilishwa muda wowote lakini muhimu ni kuwafundisha haki na wajibu wa raia na kuwapa elimu za demokrasia na haki za binadamu, hayo ndiyo muhimu.

Mkitaka wawajue viongozi wa serikali, mna wajibu pia wajue muundo wa vyama vingi vya siasa ulivyo na viongozi wa vyama vikuu vya upinzani.
 
Na kuhusu historia yetu, historia hiyo imehojiwa na wadau mbalimbali kwamba haiko kamili au haisemi uhalisia wa nini kilifanyika ila Serikali imekuwa na uzito katika kuifanyia marekebisho. Tuirekebishe kwanza kabla hatujaifundisha.
 
Kutojua historia na kujua tamthilia vina mahusiano Kweli!?

Mbona kuna wasiojua vyote tamthilia wala historia na wapo wasiojua tamthilia wanajua historia na wale wasiojua historia wanajua tamthilia
Ila kukariri na kuimba miziki ya bongo fleva wako makini,tena wanakata mpaka mauno

Ova
 
Tamthilia sasa hivi zimewakamata watoto vibaya mno:hasa zile za kicking,kituruki kihindi yaani ni hatari sana kwa taifa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…