Serikali ipige marufuku utazamaji wa tamthlia hapa nchini

Mimi pia ni mmoja wao. Somo la historia nilikuwa naona umuhimu wake ila sikulipendi kwa sababu mfumo wa elimu na mitihani ulikuwa unasisitiza kukariri zaidi miaka na majina badala ya knowledge na critical analysis ya historia yenyewe. Nimekuja kupenda historia baadae kabisa nje ya shule.
 
Ila hao wasanii wa singeli na bongo flava si ndiyo supporters wakubwa wa serikali na chama. Kwa nini msiwaambie kina Diamond waimbe nyimbo zenye kutaja majina ya viongozi kama enzi zile za TOT. Mbona mnawamudu wote hao.
 
ataje matunda ya muungano anataja maembe, maparachichi, machenza na machungwa!
Hata mimi ningetaja hayo hayo, maana siijui faida nyengine ya Muungano, vp hajauliza hasara za Muungano? Ningejibu Zanzibar kutawaliwa na Tanganyika.
 
Historia yenyewe imepindwapindwa kama barabara za Njombe Nani anaitaka? Yaani mapinduzi ya Zanzibar yanamsaidia nini Mtoto wa Nyashana Mara?
 
Hilo ni jukumu lako wewe mzazi au mlezi...

Leo watoto wako... wa mwenzio wakiwa vibaka waache ni mzigo wake...

Pambana na kibanzi ktk jicho lako na uachane na boliti ktk jicho la mwenzio...
Hao wa mwenzio wakishaharibika, ndio watakuja kukukaba wewe na wanao. Watakuwa panya road wa kutishia maisha yako.

Watoto walioharibika ni kitisho cha usalama kwa jamii nzima.
 
Mwisho wa siku hata mtoto akijua mpaka majina ya madiwani wa nchi nzima havimsaidii chochote.

Mambo mengine ni kumuonea tuu mtoto je wewe mpaka leo unaweza sema hayo matunda ya muungano ukiachana na uliyokaririshwa kwenye vitabu??
 
Inasikitisha sana...

Haswa huyo aliyejibu maembe...
 
wakijua majina ya viongozi ndo itapunguza ugumu wa maisha yao!!!?????
 
Inasikitisha sana...

Haswa huyo aliyejibu maembe...
Inasikitisha sana kwa kweli. Serikali isipoingilia kati tutakuwa na kizazi cha ovyo sana hapa nchini.
 
Nyingi hazina maadili mema ya jamii zetu!

Umalaya mtupuu[emoji108][emoji108]

Watoto wanaweza kujifunza uharibifu katika umri Mdogo sana.

Kwanini wasibuni
Na kufundisha watu kupenda kufanya kazi yoyote halali kujipatia kipato ?!
 
Nikikumbuka wale waliokuwa vilaza darasani leo hii ndio wenye pesa kuliko Mimi,, naogopa hata kuongea lolote kuhusu hao walioshindwa kutaja majina ya viongozi
 
Nyingi hazina maadili mema ya jamii zetu!

Umalaya mtupuu[emoji108][emoji108]

Watoto wanaweza kujifunza uharibifu katika umri Mdogo sana.

Kwanini wasibuni
Na kufundisha watu kupenda kufanya kazi yoyote halali kujipatia kipato ?!
Kweli kabisa mkuu. Mavipindi mengi yanahusu taarabu, singeli, vigodoro na ujinga mwingine kama huo. Huwezi kukuta televisheni yoyote, hata zile zenye maadili ya kidini kama Azam, wakionesha masomo au vipindi kwa wanafunzi na watoto zaidi ya makatuni ya ajabu ajabu. Inauma sana.
 
Matunda ya muungano maana yake nini? Tumieni lugha kulingana na umri wa mtoto.
Hata tamthilia zikiondolewa hakuna kitakachobadilika. Kama hafundishwi shuleni unadhani atajua wapi?
Wewe mzazi ni jukumu lako ku-monitor programs anazoangalia mtoto wako kwenye TV, serikali haijakununulia TV umejinunulia mwenyewe
 
na sineli za kanisani nazo?

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…