Serikali ipitie upya masuala ya kodi kwa makampuni ya kibiashara

Serikali ipitie upya masuala ya kodi kwa makampuni ya kibiashara

Kinacho zungumzwa na kinacho tendeka field ni vitu 2 tofauti sana mkuu. Uliza hayo makampuni vizuri, hivi ina maana hata kina Msukuma, Nape na yule mbunge wa Mafinga wote waliongea uongo? Yule wa Mafinga alitolea mifano ya makampuni ya mbao, tena akataja hadi idadi ya makampuni yalifunga biashara zao kabisa, remember hiyo ilizungumzwa bungeni, sio kijiweni au sosho midia
Unatakiwa ujue story za pande zote mbili ili uweze ku take side , sio kusikiliza hadithi ya upande moja, sasa unatakiwa kuwa na taarifa za mlipa kodi kwa upande moja na taarifa za wakadiria kodi kwa upande mwingine, ndio ujieleweshe, kuhusu wabunge kuongelea hilo jambo ni kawaida yao kupewa taarifa na wapiga kura wao lakini kama nilivyosema hapo awali, taarifa zinakuwa za upande moja wakati mbunge anapo ongelea hilo jambo
 
Hili suala tumelijadili sana humu mtandaoni, wengine wakifikiri ni mfanya biashara wanamkomoa, hadi wakadiriki kusema ,kama hulipi kodi, hata zikiwa za kubambikwa, funga biashara.

Kweli wengi wanafunga biashara na wanaoathirika kikubwa zaidi si mfanyabiashara bali wananchi wanyonge.
Serikali kwa ajiria hawezi basi Sekta binafsi inayobeba maisha ya watanzania wengi isaidini basi
 
Kuna swali la msingi hapa, sina hakika kama huwa tunaogopa kujiuliza ama tu huwa hatulioni. Hivi haya wanayofanya TRA ni kinyume na sheria zilizopitishwa na Bunge letu au wanafuata sheria?

Maana kama wanafuata sheria, kosa la TRA ni nini hasa? Najaribu kufikirisha akili yako msomaji. Usikute tunahangaika na dawa ya Malaria ilhali mgonjwa ana Typhoid!
Kuna lawama kwa TRA kwa kukiuka maadili wakibambika kodi na ukosefu wa ubunifu wa kikodi. Hili ni la kwao lakini pia kuna tatizo la sheria zisizo rafiki za kodi. Hili ni la mfumo. Yote mawili yanahitaji suluhisho
 
Mchawi mkuu wa hayo ma kodi na TOZO ni jamaa mwenyewe anaboronga mahusiano kati ya TZ na nchi marafiki wa TANZANIA(ambao wakina KIKWETE na MKAPA walihangaika kuwapata) anajitanabaisha kuwa TANZANIA ni nchi tajiri(vihela alivyowapiga faini makapuni kwa kureview miaka mingi iliyopita akajiona DONOR kantri akafika mbali na kuanza kuwakebehi wazungu na kuwaita jina la MABEBERU) Mbaya zaid kiburi chake kikazua chuki akatamani hiyo chuki tuibebe waTZ wote kwa kutuaminisha TZ imekuwa kiuchumi mpka kuingia vita ya kiuchumi na nchi za MABEBERU uongo wa kijinga huu.

Pili kumekuwepo ujinga wa kukusanya kodi kwa kutumia TASK FORCE yenye askari wenye bunduki ambapo kodi imekuwa kama uporaji wa hela kwa wafanyabiashara kupitia vitisho.

Tatu ni kwamba jamaa kaweka malengo yamakusanyo makubwa kwa kila idara ya serikali ambayo yameambatana na vitisho kwa wakuu wa vitendo au idara na hii imepelekea idara na vitengo vingi vya serikali vijione vina power ya kucheza rafu ya aina yoyote kwa makampuni na business entities za humu nchini ili kutimiza malengo.

NAWASILISHA KWA MAPITIO ZAIDI
 
Kwa maelezo yako juu ya kodi ya makampuni , hao watakuwa wameshindwa biashara kwa sababu nyingine. Sababu kodi ya makampuni inatozwa kwenye faida.
Corporate tax . Na kama umezungumzia kodi ya mauzo hiyo ni kitu ingine yenyewe inatozwa kama VAT na kama ni bidhaa za kutoka nje kunaweza kuwepo kwa import duty, hivyo kusababisha bidhaa kuwa bei juu, na labda uongeze pia watu kipato kimeshuka, hivyo mauzo yamekuwa hafifu
Acha kubwabwaja, wengi wa watu type yako hawajihusishi na business kabisa, wewe unafanya biashara gani? kama huna biashara yoyote plz better ukae kimya
 
Kwa maelezo yako juu ya kodi ya makampuni , hao watakuwa wameshindwa biashara kwa sababu nyingine. Sababu kodi ya makampuni inatozwa kwenye faida.

Corporate tax . Na kama umezungumzia kodi ya mauzo hiyo ni kitu ingine yenyewe inatozwa kama VAT na kama ni bidhaa za kutoka nje kunaweza kuwepo kwa import duty, hivyo kusababisha bidhaa kuwa bei juu, na labda uongeze pia watu kipato kimeshuka, hivyo mauzo yamekuwa hafifu.
Umeeleza vizuri ila kuna kitu una miss, shida kubwa ya kodi zetu ni kwenye ku define hiyo Faida .

Mara nyingi formula inayotumika haiangalii gharama kiuhalisia. Matokeo yake kampuni zinaonekana zimetengeneza Faida kubwa kuliko uhalisia .Faida kubwa maana yake ni kodi kubwa pia , matokeo yake makampuni yanaamua kufunga biashara .

Ubaya ni kuwa huwezi kulazimisha kampuni ifanye biashara , na wakifunga pato la taifa direct linapungua . Mbaya zaidi ni kuwa makampuni makubwa yanafunga biashara kwetu na kwenda kuazisha biashara hiyo hiyo nchi za jirani zetu.
 
Kabisa mi mwenyewe nilikua siamini lakini baada ya kunikuta nimeamini.
Pole mkuu naona umelazimishwa kuamini baada ya wewe kuguswa, kiukweli hali ni mbaya kibiashara kutokana na kodi pamoja na adhabu zake, ni swala la muda tu kila mtu ataguswa kwa namna yake
 
Kuna swali la msingi hapa, sina hakika kama huwa tunaogopa kujiuliza ama tu huwa hatulioni. Hivi haya wanayofanya TRA ni kinyume na sheria zilizopitishwa na Bunge letu au wanafuata sheria?

Maana kama wanafuata sheria, kosa la TRA ni nini hasa? Najaribu kufikirisha akili yako msomaji. Usikute tunahangaika na dawa ya Malaria ilhali mgonjwa ana Typhoid!
Gentlemen , you nailed it
TRA ni kama watchdog , kwa kiasi fulani tunakosea kuwalaumu kwa hali inayoendelea , shida ya sheria za Kodi kama zilivyo sheria zingine , hutungwa na bunge ,sheria mbovu zote za Kodi zina mkono wa bunge . Lakini pia TRA kama taasisi iliyopewa jukumu la kusimamia sheria hizi walitakiwa watoe feedback ya matokeo ya sheria zote wanazosimamia , zinazotekelezeka na ngumu kutekelezeka , hii ingetufanya tuwe na sheria zinazofanya kazi bila uonevu. Lakini kuna mambo kadhaa hapa , sheria ngumu hu attract rushwa kubwa kubwa na mtego upo hapo. Hakuna Officer wa TRA anayeweza kupaza sauti juu ya hilo maana ndo zinawapa jeuri mjini hapa.
 
Lipo tatizo kubwa serikali ichukue hatua na bunge letu la ndio lisione aibu kufanya maamuzi magumu kuishauri serikali pamoja na biashara holela machinga pia.
Bunge la ndiyo huwa halishauri bali hushauriwa.
 
Umeeleza vizuri ila kuna kitu una miss, shida kubwa ya kodi zetu ni kwenye ku define hiyo Faida .
Mara nyingi formula inayotumika haiangalii gharama kiuhalisia. Matokeo yake kampuni zinaonekana zimetengeneza Faida kubwa kuliko uhalisia .Faida kubwa maana yake ni kodi kubwa pia , matokeo yake makampuni yanaamua kufunga biashara .
Ubaya ni kuwa huwezi kulazimisha kampuni ifanye biashara , na wakifunga pato la taifa direct linapungua . Mbaya zaidi ni kuwa makampuni makubwa yanafunga biashara kwetu na kwenda kuazisha biashara hiyo hiyo nchi za jirani zetu.
Hapana , formula ni standard, sema bongo suala la kuweka kumbukumbu za mauzo na za kuweka kumbukumbu za matumizi ndio inayoleta shida na mvutano.

Hivyo kuleteleza wafanya biashara kuto kuweka mauzo mengine kwa near ya kukwepa kodi, kupunguza faida, jingine ni kuongeza matumizi ambayo hayakuwepo ili kupunguza faida.

Leo hii nenda kwa wauza mbao karibu wote utanunua mbao za 1m , wasikupe receipt au receipt wakupe ya 600,000.00
Hata maduka mengine ya vifaa vya ujenzi
 
Acha kubwabwaja,wengi wa watu type yako hawajihusishi na business kabisa,wewe unafanya biashara gani?kama hunabiashara yoyote plz better ukae kimya
Wewe una biashara gani inayo shindwa kulipa provisional tax, au corporate tax .
Kama huwezi funga biashara , ukahubiri dini au piga mishe mishe zingine
 
Unatakiwa ujue story za pande zote mbili ili uweze ku take side , sio kusikiliza hadithi ya upande moja, sasa unatakiwa kuwa na taarifa za mlipa kodi kwa upande moja na taarifa za wakadiria kodi kwa upande mwingine, ndio ujieleweshe, kuhusu wabunge kuongelea hilo jambo ni kawaida yao kupewa taarifa na wapiga kura wao lakini kama nilivyosema hapo awali, taarifa zinakuwa za upande moja wakati mbunge anapo ongelea hilo jambo
Kwani baada ya hayo madai ya wabunge, wizara ya fedha au TRA walijibu nini?
 
Mimi sio ongelei majibu ya kisiasa, bali naongelea masuala ya kodi , yanayo lalamikiwa na kuzungumziwa na wanasiasa .
Wizara na TRA walitakiwa kujibu kitaalamu, na ndio nauliza, kwani wao walijibu nini kuhusu madai ya wale wabunge? Umeniambia nitafute na habari kwa upande mwingine, ndio huo sasa, TRA walitakiwa ku respond haraka kama yale madai ya wabunge yalikua ni ya uongo
 
Wote mnaotetea humu kwa vinotisi vya kugoogle ni wapumbavu.

Mwaka jana nililetewa kodi ya 153 milioni. Tukakaa pamoja ikawa 17 milioni. Yaani almost ten times less.

Kuna matumizi mabaya ya sheria za kodi. TRA ni kama traffic yaani kosa linategenezwa kwa namna yoyote. August na wenzio jinga sana.
 
Wizara na TRA walitakiwa kujibu kitaalamu, na ndio nauliza, kwani wao walijibu nini kuhusu madai ya wale wabunge? Umeniambia nitafute na habari kwa upande mwingine, ndio huo sasa, TRA walitakiwa ku respond haraka kama yale madai ya wabunge yalikua ni ya uongo
Suala linaongelewa Bungeni, na mara nyingi linakuwa sio specific, na linapokuwa specific lazima taasisi husika zipeane muda wa kuleta majibu. Na Majibu yenyewe ili kulinda nafsi za wahusika zinakuwa kimya kimya
 
Back
Top Bottom