uko sahihi kabisa binafsi niliamua kuanza biashara nikaenda tra nikakadiriwa kodi kubwa nikawa tayari kuilipa cha kushangaza nikaambiwa siwezi kulipa mtandao umekatika hadi leo miezi miwili eti mtandao hamna, ukienda ofisi za mwanza kahama geita watu wanahangaishwa kupata tax clearence wakati kodi washalipa mtandao umekuwa shida, mara mzuiliwe kuingia ofisini kuna korona, siwaweke sanitizer. Kahama watu wanazuiliwa kuingia tra eti hawana barakoa, jpm mwenyewe katwambia zingine zina madhara
zipo wilaya kama mbogwe msalala busega hazina huduma ya tra, kuna shida gani pale ofisi ya biashara akawepo ofisa mmoja wa tra badala ya kulundikana kahama na bariadi? Umetoka karumwa unaenda kahama unaambiwa mtandao hakuna njoo jumatatu, unatoka masanza ngasamo zaidi ya km200 unaenda tra bariadi unaambiwa hakuna mtandao mara hauna barakoa mji mzima wa bariadi kahuna wanapouza barakoa uitoe wapi? naona kuna juhudi za makusudi za kumkwamisha Rais JPM