Serikali irudishe pesa za IMF trilioni 2.4, ni nyingi sana - zote hizi za nini?

Haiwezekani la sivyo tutakuwa na taifa lisilo project future, kuna miradi inafanyika kwa mikopo ambapo hiyo miradi pia inakuwa ni source of capital formation na repayments ya hizo loans unakuta ni ya more than 20 years sasa hapo itakuaje?

Nukta muhimu hapa ni kuwa viongozi wawe na hili swali kichwani "tunakopa ili tufanye nini?" , bila kusahau report za CAG ziwe zina wa hold accountable wafujaji na ikiwezekana CAG apewe mandate ya ku prosecute pengine italeta heshima na fedha za Umma.
 
void and void ab initio. Point yako ilikuwa hiyo "void and void ab initio" ili tujue kuwa na we unajua
 
hivi wewe hujaona matokeo?
 
OBC na Loliondo ni tangulizi tu,iko siku maneno ya Job yatadhihiri.
 
Serikali ina akili mukichwa, wanajua wanafanya nini. Natumaini kiasi cha fedha zitatumika kuongeza kasi ya ujenzi wa bwawa la Nyerere na SGR. Lakini tukumbuke hao jamaa wa IMF hawapendelei kutoa mikopo inayosaidia taifa kugharamia miradi mikubwa ya ujenzi/viwanda mikakati inayopunguza utegemezi. Hili ni angalizo tu.
 
Hizo pesa ni kuziwinda ili na wewe zikija uzichote,kama zinaenda kwenye ujenzi basi hakikisha na wewe unakua angalau fundi ujenzi,duka la vifaa vya ujenzi,muuza kokote au mchanga ndio utaona faida ya hiyo mikopo, hasara ya hii mikopo inapandisha gharama za maisha inflation
 
sijui tunakoelekea, badala ya msisitizo kuwa kuzalisha mali kwa kazi na kujenga nchi, tunakopa na kuweka miguu juu mikopo itujengee nchi? Tunaendelea kufanywa wategemezi wa kudumu.
 
Tangu UHURU wanakopa tu hadi mwisho wa dunia, anaeweza afrika itaendelea inatakiwa akapimwe akili. Waligombania UHURU kwa maslai yao binafsi na sio kwa maslai ya waafrika
 
Alaa kwa sababu Tzn Sasa ni Nchi ya ahadi au sio?
 
Tangu UHURU wanakopa tu hadi mwisho wa dunia, anaeweza afrika itaendelea inatakiwa akapimwe akili. Waligombania UHURU kwa maslai yao binafsi na sio kwa maslai ya waafrika
Wewe kama hukopi utaishia kuwa fukara..

Taja Nchi hata moja ambayo haikopi..

Isikope Ili iwaje?
 
Wangekuwa na akili wangemtumia raslimali tele kuendesha nchi na sio kuwatia watu umasikini kwa kukopa
Tangu lini mkopo ukakutia kwenye umaskini?

Hata kwenye saccos yenu huko kamahamkopi mtaishia kuwamafukara hivyo hivyo hadinafukiwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…