Serikali irudishe Tsh 20,000/= Ada ya sekondari kwa mwaka

Serikali irudishe Tsh 20,000/= Ada ya sekondari kwa mwaka

Nchi za ulaya wangekuwa wamelemaa na uchumi umeanguka kabisa. Maana wao huduma za kijamii ni bure
Yani unalinganisha upotolo wa uongozi wa nchi za kiafrika na nchi za ulaya..tuanzie tu kwenye GDP.

Ndio uje ulete hoja zako hapa..hao jama wana uchumi mkubwa sana..sio.sisi uchumi wa mikopo.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Swali langu linarudi palepale, hatuwezi kuendesha shule kwa ruzuku Ila hapo hapo kila mwaka mabilioni ya pesa yanaibwa. Kipi ni rahisi hapo kufanya? Kudhibiti hayo mabilioni yasiibiwe au kutoa hiyo ruzuku ya elimu bure?
Huduma zikiwa bure wizi au rushwa vitakoma?
 
Swali langu linarudi palepale, hatuwezi kuendesha shule kwa ruzuku Ila hapo hapo kila mwaka mabilioni ya pesa yanaibwa. Kipi ni rahisi hapo kufanya? Kudhibiti hayo mabilioni yasiibiwe au kutoa hiyo ruzuku ya elimu bure?

Elimu Tanzania haiwezi kuwa bure Mkuu, bado hatujafika huko
 
My balance Mambo iyo ada irudishwe tu
 
Kwa nini usiilipe wewe kwa niaba ya Wanafunzi kama inakuuma hivyo ? Unaonea wivu hata watoto yatima wanaojitahidi kujikomboa ? Hata hicho kidogo unataka wanyang‘anywe pia ? Hiyo Ni psyochopathy!

Yatima wanautaratibu wao wakusoma hiyo ni mpaka Chuo kikuu, mbona unakuwa Kama huishi Tanzania
 
Huenda hujakisoma ulichoandika. Umesema kasumba burebure ipo kwa maskini, nikakuambia mbkna nchi tajiri ndio zinaongoza kwa kutoa hizo huduma burebure?

Unasema Watoto wakisoma bure wanakosa uwaajibikaji na uchapakazi, huko wanaposoma bure hakuna uwajibikaji na uchapakazi?
Tulikuwa tunalipia elimu, je tuliwahi kuwa na huo uwajibikaji na uchapakazi??

Elewa kuwa huko wanakosoma bure kuna watu walilipia mbona huelewi Kiswahili?

Au unafikiri nchi hizo zilianza Jana Kama nchi yetu
 
Nchi za ulaya wangekuwa wamelemaa na uchumi umeanguka kabisa. Maana wao huduma za kijamii ni bure

Nchi za Ulaya mifumo Yao unalinganisha na mifumo ya nchi zetu?

Wenzanu walivamia na bado wanaendelea kutuvamia ndio maana wanawastarehesha watu wao.

Mimi nikishauri hapa nasi tutumie Sera na mifumo Yao kuna watu hawaelewi nazungumzia nini
 
Kwema Wakuu!

Serikali inapaswa iirejeshe Ada kwa wanafunzi wanaosoma shule, nchi yetu bado hatujafikia nyakati za kutoa vitu bure,

Shule ya Msingi ndio iwe Bure lakini sekondari, wanafunzi watoe pesa,
Isiwe pesa kubwa Sana, iwe Tsh 20,000/= Kwa familia yenye watoto watano ni 100,000/= Kwa mwaka, nusu mhula 10,000/=

Raia wasipende Dezodezo, wasipende burebure Kwa kisingizio nchi ni Tajiri, hakunaga Utajiri Kwa watu wanapenda Dezo, wanaopenda vyabure.

Mimi sikubalianagi na Wanasiasa wanaohubiri kutoa vitu vya bure, unatoa vitu vya bure kwa misingi ipi, bure inafaa Kwa makundi maalumu ya watu Kama Walemavu lakini tofauti na hapo hakuna bure.

Watoto wanatoka shuleni mapema Kwa vile hawana kazi wanaishia mitaani vijiweni Kupiga Umbeya, kujadili vitu vya kipuuzi, wengine wanajiingiza kwenye madawa ya kulevya huku wasichana wakijitafutia mabwana Kwa sababu ya kukosa kazi watokaoo shuleni.

Wakati tunasoma wengine tumeshalima Sana vibarua, tumebeba Kago, tumeosha magari, tumeuza miwa na sambusa ili kupata pesa za kujikimu kuwasaidia wazazi ambao ni masikini.

Ndio wazazi wetu Sisi Kama watoto ilikuwa wajibu wetu kuwasaidia na sio kwenda vijiweni bila ya kazi alafu ukikosa Ada shuleni mnailaumu serikali.

Serikali lipisheni Ada na iwe ni lazima watoto waende shule,
Ada itasaidia mambo mengi, itawarahisishia mambo katika sekta ya elimu,

Masuala ya mishahara ya waalimu unaweza kusaidia, kuajiri waalimu wapya itasaidia, na miundombiny mingine katik sekta ya elimu.
Kila sekta inatakiwa iwe na uwezo wa kujitegemea ili Kupunguza utegemezi Kati ya sekta moja na nyingine.

Faida zingine za kurejesha Ada
1. Uzazi wa mpango utazingatiwa.
Tabia ya watu kuzaa bila mipango itapungua.
Maana kuna watu wanazaa bila mpango alafu watoto wanawatupia shuleni Kwa waalimu Asubuhi mtoto anaondoka hanywi hata chai anarudi jioni. Wanaichukulia shule Kama sehemu ya Kupunguza bajeti ya familia. Elimu sinibure bhana!

Moja ya mbinu ya kudhibiti ongezeko kubwa la watu lenye athari Hasi ni kupandisha gharama za maisha, ukiachia mbinu zingine Kama Elimu, propaganda, Maradhi n.k.

2. Kuondoa kasumba ya Kupenda burebure na utegemezi!
Kasumba ya uburebure ipo Kwa jamii masikini, mtoto tangu akiwa mdogo anasoma lazima aone wazazi wake na Yeye mwenyewe akiwajibika, hii itamfanya ayaelewe maisha Kwa upesi zaidi kuwa Maisha sio burebure.

Vile mtoto anavyosumbuliwa Ada au kufukuzwa Ada inamjengea fikra za majukumu, nyakati za jioni akirudi lazima ashiriki kazi za nyumbani za uzalishaji kama kilimo, ufugaji, au biashara ndogondogo kuwasaidia wazazi wake kwani anajua Kwa kufanya hivyo ni ili apate Ada asome.

Wazazi nao wawaambie watoto kuwa kazi wazifanyazo ndizo zinazolisha familia na kuwasomesha watoto, hii itafanya watoto waheshimu kazi kwani watakuwa wanashiriki kazi hizo.

Siku hizi ni nadra Sana kumkuta mtoto akimsaidia mzazi wake kazi za uzalishaji Mali awapo likizo au akitoka jioni shuleni Ile saa tisa, hasa huku mjini.

Mambo ya burebure yametengeneza Matoto ya burebure, kupenda vitu bila kutoa jasho, sio Kwa mabinti sio Kwa Vijana.
Mabinti yanapenda pesa za burebure Kwa vile yamelelewa hivyo, yaani kisa ni mwanamke ndio upewe bure hiyo ni Akili za jamii fukara.

Taikon mara zote nawaambiaga ukiona Msichana anapenda burebure kuomba pesa hata hajafanya kazi yeyote huyo ni Shetani chumaulete, ni aibu Kwa mtu mwenye akili timamu zenye kufanya kazi kuomba pesa au kukubali pesa ya burebure.
Halikadhalika na vijana.

Mambo haya yalisababishwa na ujamaa, mambo ya ujamaa tuachane nayo Kwanza.

3. Kizazi chenye kuwajibika na wachapakazi.
Huwezi ukazaa watoto ukitegemea serikali ikusomeshee watoto hao, huo ni uhuni. Ukizaa watoto wajibika Kwa watoto wako, wazazi wanachopaswa kuiomba serikali ni Kupunguza gharama na sio kuiondoa kabisa, huko ni kuipa serikali mizigo alafu baadaye unailaumu serikali Kwa nini inakopa.

Wazazi waelewe kuwa kadiri unavyozaa ndivyo unatakiwa kuzidi kuchapa Kazi zaidi na zaidi Kwa ajili ya familia yako. Sio uzae Matoto mengi alafu Ada utake bure alafu uanze kuilaumu serikali haijajenga madarasa, sijui haijaajiri waalimu WA kufundisha watoto wako, sijui shule haina vifaa huo ni ukichaa.

Wingi unamaana Kwa watu wenye akili, unaweza kuzaa watoto hata Mia moja lakini kama ni wazembe hawana maana yoyote zaidi ya kuleta mabalaa katika Dunia.

4. Watoto kuwa na uchungu wa shule.
Siku zote kitu cha Bure kamwe hakijawahi kuwa na thamani. Mtoto vile anavyoona wazazi wake wanahenyeka kumsomesha anapata hamasa ya kusoma zaidi ili kuwafurahisha wazazi wake.


5. Kuongeza Upendo wa mtoto Kwa wazazi.
Alafu jinsi ilivyo kadiri mzazi anavyohangaika kumsomesha mtoto Kwa nguvu kubwa ndivyo mtoto anavyoongeza mapenzi Kwa mzazi wake.

Wazazi wanaopenda mambo ya burebure husababisha watoto wao wasiwachukulie Sirius Sana ukilinganisha na wazazi waliomenyeka kuwalea watoto wao(shule ikiwemo).

Ndio maana watoto wa Matajiri wanaupendo mara mbili Kwa wazazi wao tofauti na watoto wa masikini, kanuni inasema ukitoa kidogo utapendwa kidogo, ukitoa kikubwa utapendwa pakubwa.

Mzazi aliyemenyeka kuuza mitumba au pombe za kienyeji au vitumbua kisa kumsomesha mtoto, anapendwa zaidi na mtoto wake kuliko mzazi ambaye hakufanya jitihada yoyote zaidi ya kuitupia serikali asome mtoto bure Kwa kisingizio cha umasikini. Upendo hauna kisingizio.

Serikali inachopaswa kufanya ni kuweka gharama ndogo zinazoendana na Watanzania waliowengi na sio kuondoa kabisa Ada katika shule za sekondari.

Tuache kulipia Ada za Shule ikifika mwaka 2200 huko Nchi ikiwa imeendelea,
Sio sasa Waalimu hawatoshi, hakuna vifaa, hakuna miundombinu.

Hao wanaotoa elimu bure walimenyeka miaka iliyopita,
Vinginevyo tuvamie mataifa mengine Kama nilivyowahi kusema.

Nawatakia maandalizi Mema ya SABATO
Rubbish from a rabid mind!
 
Sawa!

Embu niambie sasa ni Kwa nini unataka Elimu ya sekondari itolewe bure?
watu ni masikini, simple! niko wa kabila fulani, wao ni madarasa, hiyo mtoto atapigwa mpaka afe kama hakwenda, lakini hizi formal classes ni hiari ya mtoto kwenda. Ukiweka na ada umewamaliza!
 
ILI KUWEZA KUPATA KURA ZA WANAWAKE UCHAGUZI WA MWAKA 2015 IKABIDI WATEUE MGOMBEA MWENZA MWANAMKE ILI KUZIPATA KURA HIZO KWA URAHISI.

WAKASAHAU KUWA KUNA KESHO NA YULE WALIEMTEUA HAWAKUJUA AU KWA KUJUA KUWA HATOSHI KABISA KUWA RAISI LIKITOKEA LA KUTOKEA.

WOTE WALIOSHIRIKI MCHAKATO ULE WALAANIWE WAO NA KIZAZI CHAO HADI CHA NNE.
Wewe unaishi Nchi gani ambayo uko peke yako? Unatumia kigezo gani kusema Rais Samia hatoshi?

Vitu pekee ambavyo Magufuli anamzidi Samia ni; Kuua wakosoaji, UDIKTETA, kudhibiti bunge, kuitisha Mahakama, kubana vyombo vya habari na kukurupuka kwenye maamuzi kama alivyoharibu bei ya sukari na biashara ya korosho.
 
Sijui Kama ulichoandika unakielewa vizuri. Nchi zenye uchumi imara karibu zote hutoa huduma za kijamii bure, Sasa tuseme na wao wanaupenda umaskini?

Mara kadhaa humu watu wanasifi nchi za ulaya kuwa elimu kuanzia kindergarten hadi chuo kikuu ni bure. Sasa sijui na wao tusemaje
Huko wameenda mbali wana hadi package kwa wale ambao ni unemployed.
Nchi gani elimu kuanzia kindagate hadi chuo kikuu ni bure!?habu Tutajie moja tu.
 
Back
Top Bottom