Serikali irudishe Tsh 20,000/= Ada ya sekondari kwa mwaka

Serikali irudishe Tsh 20,000/= Ada ya sekondari kwa mwaka

Mtoa mada ni zero brain yeye ana amini kulipia ndiyo huduma bora! Kweli tanzania tunasafari ndefu
 
Kuna mambo kadha wa kadha inaonekana wanaJF hawaelewi, kujua au siyo wafuatiliaji wa issues.

Mfano TANAPA, NCAA miaka ya nyuma mapato yote ya watalii, wawindaji nk yalikuwa yanalipiwa dirishani au kwenye maofisi yao mpaka huko polini.

Ndivyo ilivyokuwa kwa skuli zote nchini, baadae mfumo uulabadirika ukaja wa kulipia kwa control number, pesa yote inaingia hazina ndiposa huko juu wanatoa fungu uliloomba.

Sasa basi hizo 20kl mnazosema zirudishwe kisa shule zijiendeshe, ni lini government skuli zilishindwa kujiendesha kwa kukosa pesa?.

Na kutokana na mfumo wa control number mnadhani pesa inajaa kwenye account ya skuli na kutumika kesho yake?.

Muwaulize waliopo kwenye sector zilizokuwa zinakusanya mapato na kutumia wenyewe but now wanaomba hazina ndipo muwe mnaandika mada pasi kukurupuka!.
 
Hata hiyo 20,000 si bure tuu, ada irudishwe tuu lakini mtoto akifaulu hata kama hana ada asome tuu atalipa baadaye
 
Naunga mkono hoja hakuna elimu ya bure duniani - tena hiyo 20,000 si ada bali uitwe ni mchango wa Elimu
 
Elimu bure ni mzigo kwa serikali
Lets say tuna watoto form I hadi IV nchi nzima ni 5,000,000 kwa mchango wa 20,000 kwa kila mtoto

inakuwa Bil 100 kwa mwaka, hii inaweza kusaidia walau kuboreshe mfumo wa elimu nchini.

wazo zuri, tena isije 20,000 iwe walau 40,000 kwa mwaka.
 
Ukiona hivi ujue kuwa mfumo wetu wa elimu ni Mzuri (ina Capacity)na sasa mabeberu wanataka fungu linalaoelekezwa kwa Wananchi lielekezwe kwao.

Siungi mkono uhuni huo.
 
Magufuri alitegewa ndoano na ukawa akameza na haya ndo madhara ya kudandia sera ambayo hujui utaitekeleza vp.
 
Tanzania ni Tajiri, tembeeni kifua mbele; CCM imeshasema Elimu ni bure toka Msingi hadi vyuo vikuu - watanzania msijichoshe na ada, serikali yenu ipo makini.

Achaneni na matapeli.
 
Tanzania ni Tajiri, tembeeni kifua mbele; CCM imeshasema Elimu ni bure toka Msingi hadi vyuo vikuu - watanzania msijichoshe na ada, serikali yenu ipo makini.

Achaneni na matapeli.

😂😂😂

Mambo ya Bure huondoa uwajibikaji.
 
Unadhani hio elfu 20,000/= au laki ndio inaweza kusomesha watoto shule ? Ni kwamba kuna ruzuku na kodi zako mimi, wewe na yeye ndio zinasomesha hao watoto....

Ni Faida kwa Taifa kuwa na watu wenye Elimu kuliko otherwise........

Na Ifike wakati tujiulize hata hio elimu ni worth hizo pesa mtu anazotoa (mamilioni kadhaa) Je bado ni value for money kama mtu anatoka huko unamwambie akawe machinga ?

Ndio maana hapo zamani baada ya grey matter yangu kuamka ikiwa charged nilitoa bandiko hili....

 
Kwema Wakuu!

Serikali inapaswa iirejeshe Ada kwa wanafunzi wanaosoma shule, nchi yetu bado hatujafikia nyakati za kutoa vitu bure,

Shule ya Msingi ndio iwe Bure lakini sekondari, wanafunzi watoe pesa,
Isiwe pesa kubwa Sana, iwe Tsh 20,000/= Kwa familia yenye watoto watano ni 100,000/= Kwa mwaka, nusu mhula 10,000/=

Raia wasipende Dezodezo, wasipende burebure Kwa kisingizio nchi ni Tajiri, hakunaga Utajiri Kwa watu wanapenda Dezo, wanaopenda vyabure.

Mimi sikubalianagi na Wanasiasa wanaohubiri kutoa vitu vya bure, unatoa vitu vya bure kwa misingi ipi, bure inafaa Kwa makundi maalumu ya watu Kama Walemavu lakini tofauti na hapo hakuna bure.

Watoto wanatoka shuleni mapema Kwa vile hawana kazi wanaishia mitaani vijiweni Kupiga Umbeya, kujadili vitu vya kipuuzi, wengine wanajiingiza kwenye madawa ya kulevya huku wasichana wakijitafutia mabwana Kwa sababu ya kukosa kazi watokaoo shuleni.

Wakati tunasoma wengine tumeshalima Sana vibarua, tumebeba Kago, tumeosha magari, tumeuza miwa na sambusa ili kupata pesa za kujikimu kuwasaidia wazazi ambao ni masikini.

Ndio wazazi wetu Sisi Kama watoto ilikuwa wajibu wetu kuwasaidia na sio kwenda vijiweni bila ya kazi alafu ukikosa Ada shuleni mnailaumu serikali.

Serikali lipisheni Ada na iwe ni lazima watoto waende shule,
Ada itasaidia mambo mengi, itawarahisishia mambo katika sekta ya elimu,

Masuala ya mishahara ya waalimu unaweza kusaidia, kuajiri waalimu wapya itasaidia, na miundombiny mingine katik sekta ya elimu.
Kila sekta inatakiwa iwe na uwezo wa kujitegemea ili Kupunguza utegemezi Kati ya sekta moja na nyingine.

Faida zingine za kurejesha Ada
1. Uzazi wa mpango utazingatiwa.
Tabia ya watu kuzaa bila mipango itapungua.
Maana kuna watu wanazaa bila mpango alafu watoto wanawatupia shuleni Kwa waalimu Asubuhi mtoto anaondoka hanywi hata chai anarudi jioni. Wanaichukulia shule Kama sehemu ya Kupunguza bajeti ya familia. Elimu sinibure bhana!

Moja ya mbinu ya kudhibiti ongezeko kubwa la watu lenye athari Hasi ni kupandisha gharama za maisha, ukiachia mbinu zingine Kama Elimu, propaganda, Maradhi n.k.

2. Kuondoa kasumba ya Kupenda burebure na utegemezi!
Kasumba ya uburebure ipo Kwa jamii masikini, mtoto tangu akiwa mdogo anasoma lazima aone wazazi wake na Yeye mwenyewe akiwajibika, hii itamfanya ayaelewe maisha Kwa upesi zaidi kuwa Maisha sio burebure.

Vile mtoto anavyosumbuliwa Ada au kufukuzwa Ada inamjengea fikra za majukumu, nyakati za jioni akirudi lazima ashiriki kazi za nyumbani za uzalishaji kama kilimo, ufugaji, au biashara ndogondogo kuwasaidia wazazi wake kwani anajua Kwa kufanya hivyo ni ili apate Ada asome.

Wazazi nao wawaambie watoto kuwa kazi wazifanyazo ndizo zinazolisha familia na kuwasomesha watoto, hii itafanya watoto waheshimu kazi kwani watakuwa wanashiriki kazi hizo.

Siku hizi ni nadra Sana kumkuta mtoto akimsaidia mzazi wake kazi za uzalishaji Mali awapo likizo au akitoka jioni shuleni Ile saa tisa, hasa huku mjini.

Mambo ya burebure yametengeneza Matoto ya burebure, kupenda vitu bila kutoa jasho, sio Kwa mabinti sio Kwa Vijana.
Mabinti yanapenda pesa za burebure Kwa vile yamelelewa hivyo, yaani kisa ni mwanamke ndio upewe bure hiyo ni Akili za jamii fukara.

Taikon mara zote nawaambiaga ukiona Msichana anapenda burebure kuomba pesa hata hajafanya kazi yeyote huyo ni Shetani chumaulete, ni aibu Kwa mtu mwenye akili timamu zenye kufanya kazi kuomba pesa au kukubali pesa ya burebure.
Halikadhalika na vijana.

Mambo haya yalisababishwa na ujamaa, mambo ya ujamaa tuachane nayo Kwanza.

3. Kizazi chenye kuwajibika na wachapakazi.
Huwezi ukazaa watoto ukitegemea serikali ikusomeshee watoto hao, huo ni uhuni. Ukizaa watoto wajibika Kwa watoto wako, wazazi wanachopaswa kuiomba serikali ni Kupunguza gharama na sio kuiondoa kabisa, huko ni kuipa serikali mizigo alafu baadaye unailaumu serikali Kwa nini inakopa.

Wazazi waelewe kuwa kadiri unavyozaa ndivyo unatakiwa kuzidi kuchapa Kazi zaidi na zaidi Kwa ajili ya familia yako. Sio uzae Matoto mengi alafu Ada utake bure alafu uanze kuilaumu serikali haijajenga madarasa, sijui haijaajiri waalimu WA kufundisha watoto wako, sijui shule haina vifaa huo ni ukichaa.

Wingi unamaana Kwa watu wenye akili, unaweza kuzaa watoto hata Mia moja lakini kama ni wazembe hawana maana yoyote zaidi ya kuleta mabalaa katika Dunia.

4. Watoto kuwa na uchungu wa shule.
Siku zote kitu cha Bure kamwe hakijawahi kuwa na thamani. Mtoto vile anavyoona wazazi wake wanahenyeka kumsomesha anapata hamasa ya kusoma zaidi ili kuwafurahisha wazazi wake.


5. Kuongeza Upendo wa mtoto Kwa wazazi.
Alafu jinsi ilivyo kadiri mzazi anavyohangaika kumsomesha mtoto Kwa nguvu kubwa ndivyo mtoto anavyoongeza mapenzi Kwa mzazi wake.

Wazazi wanaopenda mambo ya burebure husababisha watoto wao wasiwachukulie Sirius Sana ukilinganisha na wazazi waliomenyeka kuwalea watoto wao(shule ikiwemo).

Ndio maana watoto wa Matajiri wanaupendo mara mbili Kwa wazazi wao tofauti na watoto wa masikini, kanuni inasema ukitoa kidogo utapendwa kidogo, ukitoa kikubwa utapendwa pakubwa.

Mzazi aliyemenyeka kuuza mitumba au pombe za kienyeji au vitumbua kisa kumsomesha mtoto, anapendwa zaidi na mtoto wake kuliko mzazi ambaye hakufanya jitihada yoyote zaidi ya kuitupia serikali asome mtoto bure Kwa kisingizio cha umasikini. Upendo hauna kisingizio.

Serikali inachopaswa kufanya ni kuweka gharama ndogo zinazoendana na Watanzania waliowengi na sio kuondoa kabisa Ada katika shule za sekondari.

Tuache kulipia Ada za Shule ikifika mwaka 2200 huko Nchi ikiwa imeendelea,
Sio sasa Waalimu hawatoshi, hakuna vifaa, hakuna miundombinu.

Hao wanaotoa elimu bure walimenyeka miaka iliyopita,
Vinginevyo tuvamie mataifa mengine Kama nilivyowahi kusema.

Nawatakia maandalizi Mema ya SABATO
Aisee
Idadi kubwa hswatasoma
 
Elimu bure inasababisha kutowajibika kwa wazazi
 
Elimu bure inasababisha kutowajibika kwa wazazi
20k ndogo sana kulinganisha na wanachochanga sasa. Wanawajibika vizuri tu
Ni sawa na kuambiwa hakuna nauli utapanda daladala bure Ila utachangia mafuta. Hapo kwenye kuchangia mafuta ndio unajikuta unachangia zaidi ya ile 500 ya nauli
 
Back
Top Bottom