Serikali irudishe Tsh 20,000/= Ada ya sekondari kwa mwaka

Kipindi wananchi wanatozwa kodi ya kichwa na baiskeli waliacha kufyatuana? Hizi kodi zilikuwa zinamgusa kila mwananchi moja kwa moja je ni mabadiliko gani ya maana yalitokea?
 
Pumzi imekata.

Mapato yamepungua mno.

Serikali haiwezi tena kutoa elimu bure na kufanya miradi ya maendeleo.
 
Bure inasababisha watu wasiwe responsible na maisha yao
 
Wazo lako hovyo kabisa kuwahi kulileta humu.

IHivi kama tunatozwa tozo kwa Mambo mengineyo kusaidia taifa,
Basi iongezwe tozo nyingine kwa ajiili ya elimu.

Ili mzigo huu wa elimu ubebwe na kila mtanzania..

20000 si kitu chochote kitakacho izidishia serikali.

Kama kila mwanainchi anakatwa tozo zaidi ya 500,000 kwa mwaka mzima,
Na hakuna cha maana kinachofanyika kwa tozo hizo.
Huo mchango wa 20000 itasaidia nn?

Sasa ni Bora tuongezewe tozo,,
Ili Maisha yawe magumu zaidi..
 
Hivi hapa hoja ni bure ama umuhimu wa huduma husika?.

Ni kweli bure ni aghali...lakini tuangalie lengo kuu la kufanya hivyo kabla ya hayo mengine...nadhani msingi hapa ni kwanza kwa serikali kutimiza wajibu wake, na pili ni kuhakikisha Mwananchi hapati kisingizio cha kutokumpeleka Mtoto shule.

Na wakati unatamani kuwe na ada ujue tu kuwa bado wapo wanaoshindwa kupeleka Mtoto shule kwa visingizio vingine kama kukosa unifomu n.k.

Kutokuweka ada kuwe kama njia mbadala ya kuwalazimisha Wazazi kuwapeleka Watoto shule...wakielimika wengi nadhani hata hiki unachokiandika watakuelewa kwa urahisi.
 
Wewe ndiyo hujamuelewa!
Taikoni anamaanisha kwamba tusubiri tutajirike ndipo tutoe elimu ya bure..
Maana bado tu maskini mno.
Nami namuunga mkono.
 
yet unakula na kulala.... chini ya huyo asiefaa
 
Ili uipate hiyo nafasi hata kama kweli ni yatima ni shughuli pevu.
Speaking from my experience, uyatima mbaya sana usiombe mkuu

Ni kutokana na watu kukosa uadilifu.

Pia kupewa burebure ni Dalili ya mtu asiye muadilifu
 
watu ni masikini, simple! niko wa kabila fulani, wao ni madarasa, hiyo mtoto atapigwa mpaka afe kama hakwenda, lakini hizi formal classes ni hiari ya mtoto kwenda. Ukiweka na ada umewamaliza!

😀😀

Waache kusoma waendelee kuwa Watumwa wa wengine huo ndio uchaguzi wao
 
Anaeshauri kuwa elimu iwe na ada yeye mwenyewe chuo kikuu kadoma kwa mkopo na hajalipa deni Sasa sijui akili za wapi hizi anatumia.
Elimu bure iliwekwa kwa Sababu ya umasikini wa Wananchi ili watoto waweze kusoma kwa Sababu elimu ni haki na Kila mwenye sifa ya kuipata anatakiwa aipate .
Kwenye swala la uzazi wa mpango nakuunga mkono
 
watu ni masikini, simple! niko wa kabila fulani, wao ni madarasa, hiyo mtoto atapigwa mpaka afe kama hakwenda, lakini hizi formal classes ni hiari ya mtoto kwenda. Ukiweka na ada umewamaliza!

Umasikini WA watu unatokana na Mtazamo mbaya na ujinga ulioletwa na Uvivu.

Mtu anawatoto wakubwa wa miaka 15 wapo sekondari anashindwaje kuwafanya wapate 20,000 Kwa mwaka wapate Ada ya shule?

Ni vile serikali nayo bado inazembeazembea makusudi ili nchi uendelee kuwa Masikini.

Burebure haijawahi kumsaidia masikini tangu dunia ianze mpaka itakapoisha

Watu walipie Kwa kila watakacho hiyo ndio namna ya kuisaidia nchi

Sema gharama ndio iangaliwe kulingana na Hali za watu wa nchi.
 

Sijasoma makala yako, lkn nilivyo nilivyoona heading nimeunga mkono hoja yako. Wazazi lazima wawajibike na kuipa thamani elimu ya watoto wao. Labda kwa wale wenye hali ngumu ndiyo wapate elimu bila malipo.
 

Kusoma Kwa mkopo tangu lini ikawa bure Sheikhe?
Au hujui maana ya mkopo?

Sijawahi kusoma bure, sijafundishwa kupewa mambo ya burebure.

Na ndio maana nalitumikia taifa kuielimisha jamii bila kulipwa na yoyote Yule nikijua nchi yangu inanidai na mambo mengi, achilia mbali kusoma Chuo kikuu.
 
Sijasoma makala yako, lkn nilivyo nilivyoona heading nimeunga mkono hoja yako. Wazazi lazima wawajibike na kuipa thamani elimu ya watoto wao. Labda kwa wale wenye hali ngumu ndiyo wapate elimu bila malipo.

Wenye Hali ngumu watoto wao wanaweza kuchangia Matofali Kwa kuyafyatua yanayolingana na gharama za Ada. Mbona rahisi tuu.

Wala usingesikia habari za uhaba WA madarasa.

Mtaji wa masikini ni nguvu zake mwenyewe, Kama sio mzazi basi mtoto awajibike.

Ndio maana nikasema watoto wa shule ya Msingi wao Kwa vile ni wadogo wasilipe Ada, Ila hawa wa sekondari walipe Ada, Kama hawawezi Kwa ufukara WA pesa basi serikali kupitia kila shule iandae Miradi ambayo watoto hao kupitia likizo wawe wanafanya kazi kujilipia Ada.
 

Tumefyatua sana matofali kwenye kazi au elimu ya kujitegemea (ek) almaarufu kama self reliance activities.
 
Naunga mkono hoja,Ada itafanya wazazi wafuatilie mwenendo na maendeleo ya mtoto wao..

Saizi kwenye bure wanawasukumizia walimu na Serikali afu wanaanza kulaumu.
 
Nasema ukiweka ada hiyo kuna watu haya mambo ya western education is not an issue to them, wataacha na nchi itakuwa na lundo la wajinga, I guess you see my point! Let them at least have primary and if possible secondary education
 
Ujinga wa kiwango cha marumaru.

Unamlipia mzazi ada ya mwanae tshs 70000/- kwa mwaka wakati huo huo mzazi mwenyewe ana uwezo wa kunywa bia 6 kwa siku
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…