Serikali irudishe Tsh 20,000/= Ada ya sekondari kwa mwaka

Mtoa mada ni zero brain yeye ana amini kulipia ndiyo huduma bora! Kweli tanzania tunasafari ndefu
 
Kuna mambo kadha wa kadha inaonekana wanaJF hawaelewi, kujua au siyo wafuatiliaji wa issues.

Mfano TANAPA, NCAA miaka ya nyuma mapato yote ya watalii, wawindaji nk yalikuwa yanalipiwa dirishani au kwenye maofisi yao mpaka huko polini.

Ndivyo ilivyokuwa kwa skuli zote nchini, baadae mfumo uulabadirika ukaja wa kulipia kwa control number, pesa yote inaingia hazina ndiposa huko juu wanatoa fungu uliloomba.

Sasa basi hizo 20kl mnazosema zirudishwe kisa shule zijiendeshe, ni lini government skuli zilishindwa kujiendesha kwa kukosa pesa?.

Na kutokana na mfumo wa control number mnadhani pesa inajaa kwenye account ya skuli na kutumika kesho yake?.

Muwaulize waliopo kwenye sector zilizokuwa zinakusanya mapato na kutumia wenyewe but now wanaomba hazina ndipo muwe mnaandika mada pasi kukurupuka!.
 
Hata hiyo 20,000 si bure tuu, ada irudishwe tuu lakini mtoto akifaulu hata kama hana ada asome tuu atalipa baadaye
 
Naunga mkono hoja hakuna elimu ya bure duniani - tena hiyo 20,000 si ada bali uitwe ni mchango wa Elimu
 
Elimu bure ni mzigo kwa serikali
Lets say tuna watoto form I hadi IV nchi nzima ni 5,000,000 kwa mchango wa 20,000 kwa kila mtoto

inakuwa Bil 100 kwa mwaka, hii inaweza kusaidia walau kuboreshe mfumo wa elimu nchini.

wazo zuri, tena isije 20,000 iwe walau 40,000 kwa mwaka.
 
Ukiona hivi ujue kuwa mfumo wetu wa elimu ni Mzuri (ina Capacity)na sasa mabeberu wanataka fungu linalaoelekezwa kwa Wananchi lielekezwe kwao.

Siungi mkono uhuni huo.
 
Magufuri alitegewa ndoano na ukawa akameza na haya ndo madhara ya kudandia sera ambayo hujui utaitekeleza vp.
 
Tanzania ni Tajiri, tembeeni kifua mbele; CCM imeshasema Elimu ni bure toka Msingi hadi vyuo vikuu - watanzania msijichoshe na ada, serikali yenu ipo makini.

Achaneni na matapeli.
 
Tanzania ni Tajiri, tembeeni kifua mbele; CCM imeshasema Elimu ni bure toka Msingi hadi vyuo vikuu - watanzania msijichoshe na ada, serikali yenu ipo makini.

Achaneni na matapeli.

πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

Mambo ya Bure huondoa uwajibikaji.
 
Unadhani hio elfu 20,000/= au laki ndio inaweza kusomesha watoto shule ? Ni kwamba kuna ruzuku na kodi zako mimi, wewe na yeye ndio zinasomesha hao watoto....

Ni Faida kwa Taifa kuwa na watu wenye Elimu kuliko otherwise........

Na Ifike wakati tujiulize hata hio elimu ni worth hizo pesa mtu anazotoa (mamilioni kadhaa) Je bado ni value for money kama mtu anatoka huko unamwambie akawe machinga ?

Ndio maana hapo zamani baada ya grey matter yangu kuamka ikiwa charged nilitoa bandiko hili....

 
Aisee
Idadi kubwa hswatasoma
 
Elimu bure inasababisha kutowajibika kwa wazazi
 
Elimu bure inasababisha kutowajibika kwa wazazi
20k ndogo sana kulinganisha na wanachochanga sasa. Wanawajibika vizuri tu
Ni sawa na kuambiwa hakuna nauli utapanda daladala bure Ila utachangia mafuta. Hapo kwenye kuchangia mafuta ndio unajikuta unachangia zaidi ya ile 500 ya nauli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…