Serikali irudishe Tsh 20,000/= Ada ya sekondari kwa mwaka

20k ndogo sana kulinganisha na wanachochanga sasa. Wanawajibika vizuri tu
Ni sawa na kuambiwa hakuna nauli utapanda daladala bure Ila utachangia mafuta. Hapo kwenye kuchangia mafuta ndio unajikuta unachangia zaidi ya ile 500 ya nauli
Hii michango miaka yote ipo, yaani unalipa ADA na michango inakuwepo pia.
 
Waswahili wanajaribu kujitofautisha Kwa Kila alichofanya Magu bila kujali ni kizuri au kibaya.

Tatizo ndo linapoanzia.
 
Naunga mkono hoja! Ada irudishwe shuleni hata kama ni kwa kiwango kidogo kama alivyopendekeza mtoa hoja! Pesa inayotumika kugharamia elimu bure ifanye miundombinu mingine. Kadharika ubadhirifu wa mali ya umma udhibitiwe na serikali, hapo Nchi itasonga mbele.Kitu kingine serikali inachotakiwa kukifanya ni kuchukua wanafunzi cream tu ndo waweze kujiunga na elimu ya secondary, wanafunzi wengine wanaweza kwenda vyuo vya ufundi
 
Ada irudishwe igharamie malipo ya walimu, kununua vifaa vya maabara
 
Uchumi wetu unaweza kuhimili huduma za kijamii bure? Hata hiyo elf 20 ni mchango tu sio kwamba ni ada toshelevu!
Nchi inauwezo wakusomesha watoto bure.
Ivi mnajua pesa kiasigani zinatumika katika matumizi ya kawaida kama kununua magari ya kifahari kwa watumishi wa uma NK.
Niki kuambia kunawatu wanashindwa hata kuwapa watotowao nauli ya kwenda shule utaelewa? Then hiyo ada ndio wataiweza?.

Pesa zipo nyingi lakini zonavujia kwa watu wabinafsi wasio na uzalendo.
 
We jamaa some time umeme mdogo.

Kuna mida unaandika fact lakini Saazingine unakuja na upuuzi kama huu.

Hii nchi nitajiri sana na tunauwezo wakusomeshana bure, ikiwa tutaamua kubana matumizi yasiyo ya lazima nakusimamia uwajibikaji ipasavyo.

Siku tutakapo amua kuacha ubinafsi,tukiacha ufisadi na tamaa za viongozi kujilimbikizia mali kwa ulafi, then tukafanya kazi kwa maslahi ya taifa kilakitu kitawezekana.
 

Aiseeh πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ mkuu hivi unajua kwamba mpaka Sasa kuna watu Wana tumia chumvi za mawe,?
Wali wanakula skukuu tuu?,

nguo mpya Wana nunua ikikaribia skukuu na akii vaa anaitunza mpaka skukuu nyingine?,

vipi kuhusu vibatari,?

au we born town hujaishi bushi nin?

nikukumbushe mkuu Mishe zetu za mjini zisitufanye tusahau maumivu, mateso, na magumu,waliyo yapitia wale walio tufanya tuwe hivi leo ?

Lakini hata hivyo mkuu

hata tukianza kulipia pesa zitaishia mifukoni mwa watu

Acha nasisi japo tufaidi hizi punje punje za keki ya taifaπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Mambo ni yale yale tu mkuu, ukipendekeza hivi au vile, bado ni mzigo kwa mlipa kodi na anaongezewa mzigo mwingine! Hizo ni kodi tu zinazoendesha hizi shule na sio zinatoka Ikulu boss

Embu zihesabu kodi anazozilipa mwananchi

Anza na tozo, n.k
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…