Course Coordinator
JF-Expert Member
- Jul 27, 2019
- 1,738
- 3,236
Kenya lockdown inaanza saa 11 jioniKawaulize Kenya kwa nini hakuna total lockdown mpaka sasa ilhali cases zimehit 100+ sababu unaongea mambo ya aibu tu

Mtoa mada kakwambia yeye ni muathirika wa total lockdown, hivyo yupo nchi inayofanya hivyo...Wewe unaanza kuleta mambo ya uandishi wake;yana uhusiano gani na content yake?Kuna mtu mwenye experience na madhara ya Corona hapa nchini?
Ni total lockdown hiyo?Kenya lockdown inaanza saa 11 jioni
Acha mambo hayo wafunge tuMUHTASARI:
Nchi nyingi duniani, hasa za Magharibi, zimetangaza karantini au “lockdown” inayowazuia wanachi kutoka ndani muda wote isipokua kutafuta mahitaji ya lazima tu (dawa na chakula). Hatua hii imechukuliwa na nchi ambazo maambukizi ya Covid-19 yamekua makubwa, sio kwa lengo la kuzuia watu wasipate maambuziki, bali zinalenga kupunguza kasi ya maambukizi kwa wakti mmoja ili mfumo wa utoaji huduma za afya usilemewe zaidi. Hali hiyo haina muda maalum na itaendelea hadi mlipuko wa Covid-19 utakapoonekana umepungua au kwisha. Hivyo watu wengi hapa kwetu nao wanaishauri serikali kufanya hivyo wakiamini ni hatua ya lazima kwa sasa na wanachukulia kutotangaza karantini mapema ni uzembe au ni kutokujali.
Katika makala hii, nimeeleza kwa nini sio sahihi kwa nchi yetu na nyingi za kiafrika kufanya hivyo. Pia ninashauri kwa kusisitiza serikali isiwaze kabisa kuchukua hatua hii sababu haifai na haitekelezeki kwenye mazingira yetu. Iwapo njia hii itatutumika, madhara yake kwa wananchi yanaweza kuwa makubwa kuliko tatizo linaloepukwa. Nimeeleza hoja yangu kwa kutumia uzoefu binafsi wa kuwa kwenye karantini na kufananisha mazingira ya utekelezaji wa amri hii kwenye nchi za Magharibi unapolinganisha na nchi zetu. Kwa undani zaidi soma makala nzima hapa chini.
View attachment 1406728
Utangulizi
Nianze ujumbe wangu kwa kutangaza maslahi binafsi. Hapa nilipo, hii ni wiki ya pili tunamaliza tukiwa chini ya “total lockdown”. Nchi nzima tunalazimika kukaa ndani tu na hatujui tutatoka lini. Sina hakika na watu wengine waliowahi kuishi mazingira ya aina hii, ila niseme kwa ujasiri kabisa kwamba mazingira haya ni mabaya, ni magumu, na yanaumiza sana kisaikolojia. Muda mwingi huwezi kufanya lolote la maana kwa kuwa unakua kama umepoteza "network". Mtu asiombe kabisa kukosa uhuru wa kutoka ndani.
Kwa nini nashauri hili?
Kwa sababu hizi na kwa hoja nitakazozieleza hapa, ninapingana kwa 100% na kila ambaye anaishawishi, anaishauri, au anailazimisha serikali kutangaza karantine kama nchi nyingine au anailaumu kwa kutokufanya hivyo. Labda nieleze kwa kifupi nini maana ya kuwa kwenye karantini katika uhalisia ili kuweka ninachoongea kwenye muktadha:
Unajua kwa nini wanaweza kufanya haya?
- Wazazi, watoto na munaoishi nao munashinda mukiwa mumejifungia ndani: usiku unakuja, asubuhi inafika, munaaendelea na zoezi kam ajana. Mbaya zaidi hamujui zoezi hili litakwisha lini. Wakati mwingine munasahau siku au tarehe maana hakuna matukio yanayowakumbusha. Serikali inasema inaweza kuwa hivi hadi miezi 6.
- Haijalishi mukakokuita nyumbani au ndani kukoje kwa maana ya ukubwa/udogo, ubaya/uzuri na kuna nini cha kufurahisha au kufanya: munazunguka humohumo mchana na usiku.
- Munatoka ndani mara moja au mbili kwa wiki kwenda kutafuta mahitaji ya lazima. Na mahitaji ya lazima ni chakula na mdawa pekee maana maduka mengine yote yasiyo ya chakula na madawa yamefungwa. Munashauriwa kufanya hivyo inapokua ni lazima lakini kama inawezekana muagize online.
- Wakati mwingine vitu vya lazima hakuna madukani au supermarkets maana watu wananunua kwa wingi kwa hofu hivyo vinakwisha.
- Ukifika supermarket mupanga foleni ndefu ya kuingia ndani kwa vile munatakiwa muwe umbali wa mita 2 kati ya mtu na mtu na hamutakiwi kuingia wengi kwa wakati mmoja ili musisongamane. Na unaweza kufiuka ndani unakosa unachotaka.
- Kwa anayeweza, munaruhusiwa kutoka nje mara moja kwa siku kufanya zoezi moja (kutembea au kukimbia) na uwe mwenyewe au na mtu wa familia yako maana hakuna kukutana zaidi ya watu wawili.
- Makazi mengi hayana viwanja vya nje kama kwetu Afrika maana nyumba zimejengwa kwa mipango na kubana nafasi. Mara nyingi, nje ya mlango ni bararaba ya mtaa.
- Sheria imepitishwa na bunge kwamba ukikamatwa kwenye mkusanyiko au unazurura unaweza kutozwa faini na polisi ya hadi milioni tatu za Tanzania (zile faini za papo kwa hapo kama za makosa ya barabarani)
Wenzetu wanapochukua hatua hizi za kukaa ndani ni kwa sababu mazingira yao yanaruhusu ya yameandaliwa hivyo. Kwa mfano:
Haya ndio mazingira ya wenzetu yanayowaruhusu kutangaza TOTAL LOCKDOWN au KARANTINI kirahisi kama vile wanatangaza mshahara kupanda. Wanaposema watu wakae ndani wasitoke, wana hakika kwa zaidi ya 95% mazingira ya kila mtu yanamruhusu kukaa ndani na akaishi bila matatizo makubwa. Pia, kwa kuwa wana mifumo inayofanya kazi na makazi yamepangika, kwa sehemu kubwa wanajua kila mtu anayefanya kazi (binafsi au kijiajiri), kipato chake, na anaishi wapi. Hivyo serikali wanaweza kutangaza kutoa ruzuku za kuishi kwa kiwango fulani kwa kila raia au mfanyakazi huu muda wa mlipuko na wakazipata bila mizengwe.
- Wao kukaa ndani sio jambo geni. Maisha yao kwa sehemu kubwa ni ya kibinafsi. Watu wanakaa ndani muda mwingi maana yale maisha ya kijamaa/kijamii wameyaacha. Munaweza kuiishi milango imetazamana na jirani zako lakini musisalimiane hata munapogongana mukitoka au kuingia ndani. Unaweza usimjue jirani yako munayetazamana au kutengwa na ukuta ni nani, anafanya nini, nk. Huku ndiko tumeiga msemo wa “mind your own business” na “I don’t care what yu think of me” na tunadhani ni maendeleo.
- Nchi za Ulaya zina msimu wa baridi kuanzia mwezi wa 10 na wa 11 hadi mwishoni mwa mwezi wa tatu. Kipindi hiki hali ya hewa inaweza kua mbaya muda mwingi na baridi ni kali sana. Giza linakua muda mrefu kuliko mchana. Kuna kipindi linaanza kuingia saa tisa jioni na linaendelea hadi saa mbili asubuhi Kesho yake. Hivyo mchana kwa maana ya mwanga unaweza kuwa kama masaa 6 hadi 8 tu. Mvua na barafu huweza kuwepo kwa wingi pia. Kwa jumla, mazingira hayaruhusu kukaa nje wala kutembea hivyo kama mtu hana anapolazimika kwenda basi muda mwingi ni kukaa ndani.
- Nyumba za wenzetu hazijengwi kienyeji kama sisi ambapo kila mtu anajijengea atakavyo na atakapo. Nyumba zinajengwa na makampuni na serikali kwa mipango na viwango maalumu. Kutokana na hali ya hewa ya baridi na majanga kama vimbunga, zinajengwa zikiwa na uwezo wa kustahimili baridi na upepo mkali. Madirisha yana vioo viwili; ukuta wa nyumba una leya mbuli na katikati unajazwa vitu vya kupunguza hewa ya baridi; paa linadhibitiwa kiasi kwamba mvu akinyesha unaweza usijue kama hujatazama nje.
- Kila nyumba ina maji yasiyokatika; ina bomba la gesi linaloingia ndani kama maji isiyokatika; ina umeme wa uhakika usiokatika. Nyumba zisizo na mabomba ya gesi basi umeme ndio unatumika kupikia na kwenye mifumo ya kupasha maji na nyumba joto.
- Kila nyumba inaijengwa, inaingiziwa waya (connection) ya TV, simu ya landline na internet. Huduma hizi ni za uhakika kwa kila nyumba labda uwe tu huwezi kulipia bills. Internet ni rahisi sana hivyo kwa gharama ambayo hapa kwetu mtu anatumia kununua bando la GB kama ya 20, kwao unapata internet ya kutumia vifaa zaidi ya kumi kwa wakati mmoja (simu, computers, smart tv, tablets) usiku na mchana mwezi mzima mukifanya kila munachotaka kwenye internet bila kupimiwa.
- Huduma za maji, umeme, internet, gesi, simu, tv hazikatiki na hazikatwi kienyeji hata ukishindwa kulipa bills. Tarehe ya kulipia ikifika huna pesa kwenye kwenye akaunti utafutatiliwa na kukumbushwa kwanza kwa muda ingawa ukichelewa sana utapigwa faini ya kukuumiza.
- Unaweza kuagiza KITU CHOCHOTE online (kwa kupiga simu au internet) na kikaletwa hadi mlangoni iwe dawa, chakula, nguo, viatu, mashuka, vinywaji, nk.
- Ukiiumwa unawasiliana na daktari kituo cha afya uliposajiliwa kabla ya uamuzi wakwenda hospitali kama sio matatizo ya dharura. Matatizo yote ya dharura ukipiga simu ndani ya dakika chache ambulance iko mlangoni na ukichelewa kufungua wanaweza kuvunja mlango wakaingia wakidhani umezidiwa.
- Ukipata tatizo kama kupigwa na mwenza, kuingiliwa na wezi, au mtoto kupigwa na mzazi; ukipiga simu ndani ya dakika chache polisi wako mlangoni.
Sasa linganisha mazingira haya yao nay a kwetu.
Sasa niambie, serikali ikitangaza karantini ya kumtaka kila mtu akae ndani na asichangamane hata na jirani yake tutaishije kwenye mazingira haya? Tutaweza kuishi hivyo hata kwa wiki moja? Na kama tukilazimika kwa kiboko kama kule Kenya, unadhani ni madhara kiasi gani tutapata?
- Sisi wananchi wengi hawana uwezo wa kununua chakula cha kesho. Inamlazimu mtu kutoka ndani kila siku ili angalau aweze kuweka mlo mezani.
- Sisi tumezoea kwenda duknai/sokoni kila siku au mara kadhaa kwa wiki kununua kila kitu kidogokigogo. tubamia, kaunga, tudagaa, tunyanya, tuvitunguu, tumchicha, nk.
- Sisi tuna familia nyingi hazijui umeme ni nini. Hata walionao, hauna uhakika wa kuwaka kila siku. Kwa wenzetu umeme kukatika kwenye nyumba kwa nusu dakika tu ni moja ya miujiza kwa mwaka labda kuwe na majanga kama vimbunga, mafuriko, nk.
- Sisi watu wengi hawana maji ya bomba ndani. Wengi inawalazimu kila siku kwenda kuteka maji mtoni, bombani, kisimani, chemchem, bwawani au hata kuomba kwa jirani mwenye uwezo. Wengi inawalazimu kutembea umbali mrefu kupata maji.
- Makazi yetu hayana anuani za kueleweka hivyo hatuwezi kuwa na huduma za kununua vitu online na kushushiwa nyumbani hata kama tukitaka.
- Wengi wetu tunaishi kwenye nyumba mbovu, mbaya, hazina mvuto, na wengine ni ndogo sana ukilinganisha na ukubwa wa familia. Pia wote nchi nzima tunaishi na mifugo kadhaa ndani ya nyumba. Kama sio mbuzi, kuku, kondoo au ng’ombe, basi tunaishi na mende, panya, viroboto, nzi na mbu.
- Hatuna maduka makubwa (supermarkets) kila mahali karibu na watu ambapo utasema mahitaji ya lazima unapokua kwenye karantini utayapata kwa karibu kirahisi. Wengi hutembea au kusafiri mbali kwenda madukani au sokoni kupata chakula.
- Wananchi wengi wanatumia mkaa, kuni au mafuta ya taaa kupikia. Wengine wakitaka kuwasha moto lazima wakaombe kiberiti au kaa la moto kwa jirani.
- Wengi wetu hatuna vyoo vya ndani na vya nje havitamaniki.
Mwisho
Msukumo wa kuishauri serikali kutangaza lock-down, kama ilivyo kwa misukumo mingi, inatoka kwa kundo dogo la watu wenye uwezo (middle class). Duniani kote kundi hili hujisahau na kudhani kila mtu ana maisha kama yao. Lina kiwango kikubwa sana cha ubinafsi na wakati mwingine wanasahau kabisa kwamba hata ndugu zao wa karibu kabisa hawana uwezo walionao wa. Lakini ukweli ni kwamba kwa watanzania walio wengi karantini ya kututaka kukaa ndani ni hata kubwa mara nyingi kuliko Covid-19. Wanashawishi hatua hii wakumbuke kwanza kijijini kwao walikotoka wao au wazazi wao kabla hawajashauri lockdown.
Serikali ichukue kila tahadhari na hatua wanazoshauriwa na wataalamu kuhusu kuzuia au kupunguza maambukizi ya Covid-19. Tusikilize wataalamu ni kwa jinsi gani tunaweza kuwakinga watu ambao wakipata maambukizi watadhuruka zaidi (wazee, wenye magonjwa ya kupua, na wenye chronic diseases). Ila isikubali wala kusikiliza ushawishi wa mtu, watu, taasisi, au nchi yoyote kwamba inalazimika kutangaza karantini. Njia hii ni mbaya na haifai kwa wananchi wetu. Itakua na madhara makubwa sana kiafya, kijamii, na kimaisha iwapo itachukuliwa. Kufanya hivyo itakua ni sawa na kukimbia kuumbwa na mbwa ukakimbilia kwenye zoo walipo simba na chui huku ukidhani unatafuta kinga kwa kuogopa kumwa na mbwa.
MM Togolani ([email protected])
Mwathirika wa "Total Lockdown"
Sawa....lakin shule zifunguliwe bora..Taadhari iwepo kubwa wanafunzi angalau wasome kwa shift siku 3 kwa wiki
Wewe unaonaje
Mimi nimwalimu primary seeikalin lakin nimepata taarifa za wanafunz kupewa mimba
MUHTASARI:

Ajifunze kuandika vizuri!Ushauri wangu kwenye Corona ni huu mara zote kwa watu kama hawa,tuombe Mungu sana Corona isienee nchini maana tutaisha kama kuku!Mtoa mada kakwambia yeye ni muathirika wa total lockdown, hivyo yupo nchi inayofanya hivyo...Wewe unaanza kuleta mambo ya uandishi wake;yana uhusiano gani na content yake?
Kawaulize Kenya kwa nini hakuna total lockdown mpaka sasa ilhali cases zimehit 100+ sababu unaongea mambo ya aibu tu
Sielewi pointi yako ni niniKenya wako njia moja kwenda total lockdown. Watakapokwenda total lockdown utakuja hapa kufuta bandiko lako?
South Africa na Rwanda wako on total lockdown. Rwanda kaongoza siku 15 baada ya 14 za kwanza kwisha. Je hawa ndiyo wajinga sana na hawajui walitendalo.
Nadhani tatizo ni kushindwa kuelewa nature ya mlipuko kwenye huu ugonjwa. Ukiielewa vyema utatambua ugonjwa ukishaingia only way out for now ni total lockdown (pekee).
Tokea waathirika 200,000 jana, leo waathirika ni zaidi ya 1,000,000. Endeleeni kujidanganya kuwa nyie mna ufumbuzi usio na maumivu.
Wakuu hamna haja ya kuchukiana huo ndiyo ukweli mchungu.
Anasema Angel Merkel na pia Trump, changamoto za corona hazijawahi onekana tangu world war 2. Hali kadhalika kuutokomeza kwake hakuta kosa maumivu kweli kweli.
Ni rahisi zaidi kusalimu amri na kutoweka kwa huu ugonjwa au kupambana na ku survive. Uchaguzi ni wetu kama taifa.
Ina fahamika kwa nini hauwezi kuwa wa mtu mmoja mmoja.
'Fools die'.
Nakuunga mkono mkuu. Serikali haijazuia 'personal or family lock down', anayeweza kujifungia ajifungie sisi wengine tuendele na mambo yetu.
Sent using Jamii Forums mobile app
Sielewi pointi yako ni nini
Tena hapo Kahama ikitangazwa Lockdown cha moto mtapata.Na wenzetu wana supermarket kila mtaa. huku sasa, mmh mie nipo kahama supermarket zipo tano 5, na idadi ya wananchi wa hapa kahama mji ni 1.5+million.
Na katika hizo supermarket yenye akili ni ROYAL Supermarket na royal food tu.
Karibu bidhaa zote zinapatikani masokoni
when a slave dies he loses nothing but his pain!! ni kweli maskini hana cha kupoteza!! matajiri wasiojua njaa ndio wanaoshinikiza lockdown ili wajaze misosi ndani na kufurahia mateso ya maskini watakaopigwa mabuti na virungu kwa kutapatapa barabarani kutafuta msosi,Hapa sio inshu ya mwana ccm!! Huo ndio ukweli maisha yetu ya ndege tunduni hatuwezi!! Nyie wachache wenye uwezo ndio mnaona sawa, kwani una uhakika wa kutunza familia hata kwa miezi mitatu, bila kufanya kazi, akiba au mshahara unao!! Na ndio waoga sana, lakini masikini siku zote huwa hana cha kupoteza, na sio muoga.