Serikali isikubali kutangaza “total lockdown” au Karantini. Wanaoishawishi ama hawajui wanachokishauri au ni wabinafsi

Serikali isikubali kutangaza “total lockdown” au Karantini. Wanaoishawishi ama hawajui wanachokishauri au ni wabinafsi

Si kwamba bongo hatuna maambukizi sema mfumo wetu wa afya ni hoe hae,Jana Kuna familia moja imebebwa huko mbezi msakuzi baada ya baba kuugua corona aliyoambukizwa huko Kongo,je safari nzima na roli lake toka tunduma mpaka amewashushia wangapi hilo zigo.Kama Tanzania haina Mungu wa pekee yake just wait you will see
Nilikuwa nazungumzia lockdown mm
 
wakaambukizane kwa wingi eti kisa wanajitafutia riziki .sasa ninyi kwa ujinga wenu singizieni umasikini wa mtanzania,
Kwahiyo unataka watu wafe njaa kwa sababu ya ujinga wako wa corona! Hebu kwendeni huko na hiyo corona yenu!

Ukishajaza vimayai viwili kwenye friji unadhani watanzania wote wanaweza kumudu mahitaji yao bila kutoka nje!

Mamantilie, bodaboda, machinga, wauza magenge... wote hao wanategemea kubangaiza wapate chochote cha siku!

Umeshavimbiwa maharage unadhani watu wote wanaishi kwenye huo ulimwengu wako wa corona!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ungekuwa serious ungeishauri serikali wafanye kitu kuliko kuwambia watu wakafe au wakaambukizane kwa wingi eti kisa wanajitafutia riziki while ukijua mfumo wetu wa afya hauwezi ukawahandle Wala kuwatibu pale hali itakapokuwa imekuwa mbaya.Siku zote kwa watu wenye akili kinga ni bora kuliko tiba.sasa ninyi kwa ujinga wenu singizieni umasikini wa mtanzania,sasa wakishaambukizana kwa maelfu ndo umasikini wao utakuwa umeisha mkuu
Asante ndugu Sijijui . Mimi ujinga kwangu ni hazina maana ndio unanifanya kila siku nijitahidii kujifunza na kujua mengi zaidi. Hivyo hakuna shida kabisa ukiniita mjinga.Usipokubali ujinga, huwezi kujifunza.

Kuhusu ushauri, nadhani kila mtu ana nafasi ya kushauri anachojua, anachoweza, anachoona ni sawa; na akasema kwa nini; ama kwa akili/elimu yake au kwa ujinga kama wangu. Mimi nimeshauri hili kwa hoja na wewe unaweza kushauri vinginevyo kwa hoja. Huo ndio msingi wa uhuru wa mawazo na kufikiri. Na ushauri ukitolewa wa aina nyingi unamsaidia zaidi anayeshauriwa kufanya maamuzi bora zaidi.

Nasubiri kusoma hoja za ushauri wako.

MM Togolani
 
Kenya wako njia moja kwenda total lockdown. Watakapokwenda total lockdown utakuja hapa kufuta bandiko lako?

South Africa na Rwanda wako on total lockdown. Rwanda kaongeza siku 15 baada ya 14 za kwanza kwisha. Je hawa ndiyo wajinga sana na hawajui walitendalo.

Nadhani tatizo ni kushindwa kuelewa nature ya mlipuko kwenye huu ugonjwa. Ukiielewa vyema utatambua ugonjwa ukishaingia only way out for now ni total lockdown (pekee).

Tokea waathirika 200,000 jana, leo waathirika ni zaidi ya 1,000,000. Endeleeni kujidanganya kuwa nyie mna ufumbuzi usio na maumivu.

Wakuu hamna haja ya kuchukiana huo ndiyo ukweli mchungu.

Anasema Angel Merkel na pia Trump, changamoto za corona hazijawahi onekana tangu world war 2. Hali kadhalika kuutokomeza kwake hakuta kosa maumivu kweli kweli.

Ni rahisi zaidi kusalimu amri na kutoweka kwa huu ugonjwa au kupambana na ku survive. Uchaguzi ni wetu kama taifa.

Ina fahamika kwa nini ufumbuzi hauwezi kuwa wa mtu mmoja mmoja.

'Fools die'.
Tanzania tuna rais wenye uwezo wa kupambana na Chadema na kutoa maneno anayoyajua mwenyewe na si kuongoza nchi hasa kwenye majanga,sometimes najiuliza katika hali ya taharuki ya namna hii ujasri wa kwenda likizo unaupata wapi?
 
Kwahiyo unataka watu wafe njaa kwa sababu ya ujinga wako wa corona! Hebu kwendeni huko na hiyo corona yenu!

Ukishajaza vimayai viwili kwenye friji unadhani watanzania wote wanaweza kumudu mahitaji yao bila kutoka nje!

Mamantilie, bodaboda, machinga, wauza magenge... wote hao wanategemea kubangaiza wapate chochote cha siku!

Umeshavimbiwa maharage unadhani watu wote wanaishi kwenye huo ulimwengu wako wa corona!

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu siku umelazwa pale kwa mkapa bila nesi wala daktari wa kukuhudumia ndo utajua lockdown ilikuwa kwa ajiri yako
 
Muslim minority doctors first to die on front line of UK pandemic
Families and patients remember the four doctors who contracted coronavirus while fighting for others with the disease.
by Aina Khan
1 Apr 2020

[IMG alt="From left: Adil El Tayar, Alfa Sa'adu, Habib Zaidi and Amged el-Hawrani were the first named doctors to die while fighting on the front lines of the coronavirus pandemic in the UK [Images courtesy of doctors' families]
"]https://www.aljazeera.com/mritems/i...60df6135cede4d19be4416daa49f15a3_18.jpg[/IMG]
From left: Adil El Tayar, Alfa Sa'adu, Habib Zaidi and Amged el-Hawrani were the first named doctors to die while fighting on the front lines of the coronavirus pandemic in the UK [Images courtesy of doctors' families]
MORE ON HEALTH
London, United Kingdom - The United Kingdom is paying tribute to the first doctors on the front lines of the coronavirus pandemic who have died after contracting COVID-19.
All four men - Alfa Sa'adu; Amged el-Hawrani; Adil El Tayar and Habib Zaidi - were Muslim and had ancestry in regions including Africa, Asia and the Middle East.
More:
Dr Salman Waqar, the general secretary of the British Islamic Medical Association, said the contribution of these doctors was "immeasurable".
"They were devoted family men, committed senior doctors, and dedicated decades of service to their communities and patients," he said.
"They gave the ultimate sacrifice while fighting this disease. We urge everyone to do their part and stop further deaths from happening - stay at home, protect the NHS, save lives."
As the country fears a shortage of medical staff amid the pandemic, which has so far killed 2,352 people and infected 29,474 according to government figures, the loss of the doctors has highlighted the vital contribution of medics from minority backgrounds to the UK's National Health Service (NHS).
The NHS is the largest employer of Black and Minority Ethnic (BME) staff in the UK with 40.1 percent of medical workers from BME backgrounds.
Priti Patel, the home secretary, announced on Tuesday that about 2,800 medical staff whose visas expire before October 1, will have their visas extended for a year "free of charge".
Here, we profile the four doctors who have sadly passed away:
Amged el-Hawrani - A father figure who fought for people
Born in Sudan, the second of six brothers, Amged el-Hawrani was an ear, nose, and throat consultant at university hospitals in the north of England.
Despite having no underlying health issues, el-Hawrani died in hospital on Saturday aged 55.
His youngest brother Amal paid tribute to his sibling who selflessly "took on the burdens of others" and became a "father figure" following the deaths of their eldest brother and father.
"Amged was someone who was very strong in character, both mentally and physically, but in a calm and gentle way," he said. "His strength was one that was always used as a force for good. He was a protector, a shielder, fighting for people, fighting for his brothers."
Weeks before his death, el-Hawrani was concerned for his elderly mother who was ill again after having recovered from pneumonia. El-Hawrani finished his night shift and drove a long distance to see her in Bristol, in southwest England. At the time, he had mild flu symptoms which he put down to being overworked.
His funeral went ahead on Tuesday, with only immediate family in attendance. He was buried in Bristol.
El-Hawrani's colleagues held a minute's silence for the doctor at Queen's Hospital in Burton on Monday.
Habib Zaidi - A kind, caring GP whose dedication cost him his life
A general practitioner with Pakistani origins, Habib Zaidi moved to the UK almost 50 years ago and worked in Leigh-on-Sea in Essex, southeast England.
On Wednesday, at 76 years old, he died of COVID-19.
He had been self-isolating for a week when he was taken to hospital and died 24 hours later in the intensive care unit.
His family said they were "heartbroken" by his death, in a statement.
Christine Playle, 73, one of Zaidi's former patients on whom he performed minor surgery less than three weeks before his death, said she was "shocked and saddened".
"Dr Zaidi was a very well-liked and respected doctor and was the embodiment of what everyone looks for in their GP - kind, caring, friendly and jolly," she told Al Jazeera.
"He was a dedicated GP, and that dedication cost him his life."
In accordance with distancing restrictions, only his immediate family attended his funeral. His widow has now gone into self-isolation.
Adil El Tayar - A consultant who gave his life volunteering in emergency
Adil El Tayar, an NHS surgeon, died on March 25, aged 64.
An organ transplant consultant, he graduated from the University of Khartoum in 1982.
El Tayar had been working at Hereford County Hospital in the west of England as a volunteer in the emergency department amid the pandemic, where his family believes he caught the virus.
He began to self-isolate when he displayed symptoms but was eventually hospitalised and placed on a ventilator.
The British ambassador to Sudan, Irfan Siddiq, paid tribute to the father of four on Twitter and thanked healthcare workers everywhere for showing "extraordinary courage".

346 people are talking about this



BBC journalist Zeinab Badawi, his cousin, said: "He wanted to be deployed where he would be most useful in the crisis.
"It had taken just 12 days for Adil to go from a seemingly fit and capable doctor working in a busy hospital to lying in a hospital morgue."
His funeral is being arranged this week.
Alfa Sa'adu - A veteran doctor whose face lit up talking about medicine
Alfa Sa'adu, who was born in Nigeria, worked with the NHS for nearly 40 years. He died on Tuesday aged 68 after a two-week battle with the virus.
Having retired, he was volunteering at the time of his passing.
Born in Nigeria, Sa'adu began his medical career as a consultant physician in geriatric medicine when he came to London and graduated from the University College Hospital Medical School in 1976.

Dr. Abubakar Bukola Saraki

✔@bukolasaraki

· Mar 31, 2020

Inalilahi Wa Ina Ilaehi rajiun. My condolences go to the family of late Dr. Alfa Sa'adu, the people of Pategi and Kwara State on the death of the foremost medical practitioner who passed away in London this morning.

Dr. Abubakar Bukola Saraki

✔@bukolasaraki


Late Dr. Sa'adu provided leadership for our people in the diaspora as he served for many years as Chiarman, Kwara State Association of Nigeria (Kwasang UK). Back at home, he was a community leader and traditional office holder as Galadima of Pategi. He will be sorely missed.

263

3:45 PM - Mar 31, 2020
Twitter Ads info and privacy

88 people are talking about this



He went on to become a medical director.
Sa'adu's son Dani told Al Jazeera: "He was a very passionate man, who cared about saving people. As soon you spoke to him about medicine his face would light up. He worked for the NHS for nearly 40 years in different hospitals across London.
"He loved to lecture people in the world of medicine, he did so in the UK and Africa. My dad retired and was working part time at the Queen Victoria Memorial Hospital in Welwyn, Hertfordshire until his passing. He was a massive family man and we did everything together, family came first. He left two sons and a wife, who is a retired doctor herself."
The former president of the Nigerian Senate, Bukola Saraki, paid tribute to Sa'adu on Twitter, saying he provided "leadership for our people in the diaspora".
SOURCE: AL JAZEERA NEWS
 
Tanzania tuna rais wenye uwezo wa kupambana na Chadema na kutoa maneno anayoyajua mwenye na si kuongoza nchi hasa kwenye majanga,sometime najiuliza katika hali ya namna hii ujasri wa kwenda likizo unaupata wapi?

Mkuu unasomeka vyema. Tatizo jingine elimu ya msingi tu kwa watu ni shida. Utamaduni wa kusoma hamna.

Hata wasionauelewa nao ni wajuzi.
 
Ukiacha supermarket umejiuliza hapo kahama mna hospital ngapi na manesi wangapi na zinaweza kuhudumia watu wangapi kwa mpigo? Kama US wanachemsha na wanamlaumu Trump kwa kufanya uzembe sisi tutaisha na hii lugha ya umasikini sijui itatoweka na kila mtu atajiweka mwenyewe kwenye lockdown same way mipaka yetu ilivyojifunga

Sijijui kwa kuwa wewe huoni dhana ya mazingira yetu ina mashiko, hebu piga moja zaidi ya kusaidia. Tuambie data zako kuhusu uwezo wa watanzania kujifungia ndani zainasemaje? Wangapi wanaweza kujifungia angalau wiki moja bila kazi na wakaishi wakiwa na chakula? Tuambie watanzania wangapi wanalazimika kutafuta maji, kuni, mkaa, au mafuta ya taa kila siku mbali na wanapoishi angalau wapike na itakuwaje wakifungiwa ndani kwa muda usiojulikana? Tuambie wananchi wenye mifugo watailisha vipi ukiwafungia ndani angalau kwa wiki moja tu? Tuambie mazingira ya nyumba za watanzania walio wengi yanawawezeshaje kujifungia ndani familia nzima usiku na mchana bila kutoka ndani kwa wiki kadhaa?

Usituteshe tu kufa na kukosa tiba. Tupe soluhisho. Halafu utuambie nchi gani unayoijuailiyopona maambukizi kwa sababu waliweka watu karantini?

Tusaidiene kutoa suluhisho badala ya kupambana kushambulia wanaotoa maoni yao.
 
Mkuu siku umelazwa pale kwa mkapa bila nesi wala daktari wa kukuhudumia ndo utajua lockdown ilikuwa kwa ajiri yako

Mkuu kwa yale ya TWAWEZA kimsingi walisema:

Wana macho hawawezi kuona na wana masikio hawawezi kusikia.
 
Mkuu siku umelazwa pale kwa mkapa bila nesi wala daktari wa kukuhudumia ndo utajua lockdown ilikuwa kwa ajiri yako
Wacha vitisho. Haiwezekani watu wajifungie ndani wafe njaa kwa ajili ya huo ugonjwa wa kipuuzi.

Watu wachukue tahadhari binafsi inatosha. Zaidi ya hapo ni kutaka kutengeneza matatizo makubwa zaidi ya hiyo corona yenu!


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Muslim minority doctors first to die on front line of UK pandemic
Families and patients remember the four doctors who contracted coronavirus while fighting for others with the disease.
by Aina Khan
1 Apr 2020

[IMG alt="From left: Adil El Tayar, Alfa Sa'adu, Habib Zaidi and Amged el-Hawrani were the first named doctors to die while fighting on the front lines of the coronavirus pandemic in the UK [Images courtesy of doctors' families]
"]https://www.aljazeera.com/mritems/i...60df6135cede4d19be4416daa49f15a3_18.jpg[/IMG]
From left: Adil El Tayar, Alfa Sa'adu, Habib Zaidi and Amged el-Hawrani were the first named doctors to die while fighting on the front lines of the coronavirus pandemic in the UK [Images courtesy of doctors' families]
MORE ON HEALTH
London, United Kingdom - The United Kingdom is paying tribute to the first doctors on the front lines of the coronavirus pandemic who have died after contracting COVID-19.
All four men - Alfa Sa'adu; Amged el-Hawrani; Adil El Tayar and Habib Zaidi - were Muslim and had ancestry in regions including Africa, Asia and the Middle East.
More:
Dr Salman Waqar, the general secretary of the British Islamic Medical Association, said the contribution of these doctors was "immeasurable".
"They were devoted family men, committed senior doctors, and dedicated decades of service to their communities and patients," he said.
"They gave the ultimate sacrifice while fighting this disease. We urge everyone to do their part and stop further deaths from happening - stay at home, protect the NHS, save lives."
As the country fears a shortage of medical staff amid the pandemic, which has so far killed 2,352 people and infected 29,474 according to government figures, the loss of the doctors has highlighted the vital contribution of medics from minority backgrounds to the UK's National Health Service (NHS).
The NHS is the largest employer of Black and Minority Ethnic (BME) staff in the UK with 40.1 percent of medical workers from BME backgrounds.
Priti Patel, the home secretary, announced on Tuesday that about 2,800 medical staff whose visas expire before October 1, will have their visas extended for a year "free of charge".
Here, we profile the four doctors who have sadly passed away:
Amged el-Hawrani - A father figure who fought for people
Born in Sudan, the second of six brothers, Amged el-Hawrani was an ear, nose, and throat consultant at university hospitals in the north of England.
Despite having no underlying health issues, el-Hawrani died in hospital on Saturday aged 55.
His youngest brother Amal paid tribute to his sibling who selflessly "took on the burdens of others" and became a "father figure" following the deaths of their eldest brother and father.
"Amged was someone who was very strong in character, both mentally and physically, but in a calm and gentle way," he said. "His strength was one that was always used as a force for good. He was a protector, a shielder, fighting for people, fighting for his brothers."
Weeks before his death, el-Hawrani was concerned for his elderly mother who was ill again after having recovered from pneumonia. El-Hawrani finished his night shift and drove a long distance to see her in Bristol, in southwest England. At the time, he had mild flu symptoms which he put down to being overworked.
His funeral went ahead on Tuesday, with only immediate family in attendance. He was buried in Bristol.
El-Hawrani's colleagues held a minute's silence for the doctor at Queen's Hospital in Burton on Monday.
Habib Zaidi - A kind, caring GP whose dedication cost him his life
A general practitioner with Pakistani origins, Habib Zaidi moved to the UK almost 50 years ago and worked in Leigh-on-Sea in Essex, southeast England.
On Wednesday, at 76 years old, he died of COVID-19.
He had been self-isolating for a week when he was taken to hospital and died 24 hours later in the intensive care unit.
His family said they were "heartbroken" by his death, in a statement.
Christine Playle, 73, one of Zaidi's former patients on whom he performed minor surgery less than three weeks before his death, said she was "shocked and saddened".
"Dr Zaidi was a very well-liked and respected doctor and was the embodiment of what everyone looks for in their GP - kind, caring, friendly and jolly," she told Al Jazeera.
"He was a dedicated GP, and that dedication cost him his life."
In accordance with distancing restrictions, only his immediate family attended his funeral. His widow has now gone into self-isolation.
Adil El Tayar - A consultant who gave his life volunteering in emergency
Adil El Tayar, an NHS surgeon, died on March 25, aged 64.
An organ transplant consultant, he graduated from the University of Khartoum in 1982.
El Tayar had been working at Hereford County Hospital in the west of England as a volunteer in the emergency department amid the pandemic, where his family believes he caught the virus.
He began to self-isolate when he displayed symptoms but was eventually hospitalised and placed on a ventilator.
The British ambassador to Sudan, Irfan Siddiq, paid tribute to the father of four on Twitter and thanked healthcare workers everywhere for showing "extraordinary courage".

346 people are talking about this


BBC journalist Zeinab Badawi, his cousin, said: "He wanted to be deployed where he would be most useful in the crisis.
"It had taken just 12 days for Adil to go from a seemingly fit and capable doctor working in a busy hospital to lying in a hospital morgue."
His funeral is being arranged this week.
Alfa Sa'adu - A veteran doctor whose face lit up talking about medicine
Alfa Sa'adu, who was born in Nigeria, worked with the NHS for nearly 40 years. He died on Tuesday aged 68 after a two-week battle with the virus.
Having retired, he was volunteering at the time of his passing.
Born in Nigeria, Sa'adu began his medical career as a consultant physician in geriatric medicine when he came to London and graduated from the University College Hospital Medical School in 1976.


88 people are talking about this


He went on to become a medical director.
Sa'adu's son Dani told Al Jazeera: "He was a very passionate man, who cared about saving people. As soon you spoke to him about medicine his face would light up. He worked for the NHS for nearly 40 years in different hospitals across London.
"He loved to lecture people in the world of medicine, he did so in the UK and Africa. My dad retired and was working part time at the Queen Victoria Memorial Hospital in Welwyn, Hertfordshire until his passing. He was a massive family man and we did everything together, family came first. He left two sons and a wife, who is a retired doctor herself."
The former president of the Nigerian Senate, Bukola Saraki, paid tribute to Sa'adu on Twitter, saying he provided "leadership for our people in the diaspora".
SOURCE: AL JAZEERA NEWS
New York wametangaza ujira wa USD 10,000 a week kwa manesi huku usafiri na hotel ukipewa bure bado wahudumu wamekosekana,I think sisi hatujui tunachokifanya
 
Wacha vitisho. Haiwezekani watu wajifungie ndani wafe njaa kwa ajili ya huo ugonjwa wa kipuuzi.

Watu wachukue tahadhari binafsi inatosha. Zaidi ya hapo ni kutaka kutengeneza matatizo makubwa zaidi ya hiyo corona yenu!


Sent using Jamii Forums mobile app
Sawa mkuu Kama unadhani vile vifo vinavyotangazwa kwa wenzetu ni maigizo au Kama unadhani mshauri wetu kagame hana akili au Uhuru Kenyatta amekuwa mwehu basi endelea kupiga kazi mkuu ili watu wengine wakicoronwa huko wewe wapige pesa
 
Huyu unayesema hajui kuandika alikuwa Mwandishi wa Hotuba wa Rais Kikwete, akiachiwa kazi hiyo na January Makamba...


So fikiri kabla ya kusema, yawezekana aliyoyaandika yanazidi upeo wa akili zako, Pole sana!

Finally, Linganisha muda MM Togolani aliojiunga JF(2010) na muda wako Wewe, Then uweke hoja zako chini tujadili
Hujaona makosa lukuki ya kiuandishi?Halafu kujiunga JF mapema sio sifa ya kunieleza hapa,wengine tulikuwa wasomaji tu na hatukuona haja ya kujisajili!Niko hapa jukwaani kitambo sana zaidi ya unavyofikiri!
 
Hapana kaka yangu...

Mimi naona Lockdown ni muhimu kuzuia maambukizi....

Kasi ya hichi kirusi ni kubwa...

Kinaua maelfu per day...

Hio lockdown itazuia kidogo mortality rate...

Issue hapa wangapi wataokolewa..

hata kama ni mmoja..poa tu...

Kuliko kutochukua tahadhari muhimu juu ya maambukizi,..only on the basis of 'what if'...what if tukifa na njaa..what if tukose mahitaji muhimu, tunahitaji evidence ndio tuseme kweli tutakufa na njaa..lol

Kusema ule ukweli,umelinganisha Tanzania na huko nje ila umesahau mazingira yetu Tanzania yana differ kwa sana na wa huko nje..embu fikiria scenario ya kupanda daladala jioni na asubuhi, jinsi watu wanavyobanana..changamoto hii ulaya haipo..well kama ipo ni kidogo sana...sasa utawezaje kuformulate formular ya kuzuia maambukizi kwa watanzania kwa kutumia measurements za ki ulaya?..infection control between these countries obviously differ..this is what you have to put in mind...

Kwa kweli hatujajiandaa kupigana na Corona,Mungu atunusuru tu..tushazoea njaa na typhoid na kula mlo mmoja kwa siku.hizo changamoto ni daily life ya watanzania..umefikiria jinsi wagonjwa wa corona wanavyoongezeka,hospitali zetu zimejiandaaje..................tuna ambiwa tunawe na maji safi na sabuni,wakati maji bado ni changamoto kwa watu..again, Mungu tunusuru waja wako..maana yajayo yanatisha eti....
 
Sijijui kwa kuwa wewe huoni dhana ya mazingira yetu ina mashiko, hebu piga moja zaidi ya kusaidia. Tuambie data zako kuhusu uwezo wa watanzania kujifungia ndani zainasemaje? Wangapi wanaweza kujifungia angalau wiki moja bila kazi na wakaishi wakiwa na chakula? Tuambie watanzania wangapi wanalazimika kutafuta maji, kuni, mkaa, au mafuta ya taa kila siku mbali na wanapoishi angalau wapike na itakuwaje wakifungiwa ndani kwa muda usiojulikana? Tuambie wananchi wenye mifugo watailisha vipi ukiwafungia ndani angalau kwa wiki moja tu? Tuambie mazingira ya nyumba za watanzania walio wengi yanawawezeshaje kujifungia ndani familia nzima usiku na mchana bila kutoka ndani kwa wiki kadhaa?

Usituteshe tu kufa na kukosa tiba. Tupe soluhisho. Halafu utuambie nchi gani unayoijuailiyopona maambukizi kwa sababu waliweka watu karantini?

Tusaidiene kutoa suluhisho badala ya kupambana kushambulia wanaotoa maoni yao.
Covid 19 ni janga la kimataifa na suluhisho la kupunguza mambukizi kwa sasa ni ku ji distance angalau mita mbili jambo ambalo kulifikia ni lock down.....

wataalamu wa wingereza wamesema lock down waliofanya 2wks back wamenusuru vifo vya watu zaid ya 24,000, Uganda ambayo ni mfano mzuri wa Africa mashariki wako kwenye total lock-down wameweza vizuri kudhibiti ugonjwa kwa mambukizi mapya na ni nchi ambayo haina tofouti sana na Tz isipo waganda wengi ni waelewa na wame elimika kuliko sisi, impact ya covid wameiona mapema wa meshirikiana na serikali yao kudhibiti ugonjwa hu, suala la Tz to lockdown, time will tell you like it or not...... emergency 'does not know poverty' masikini wa singe ugua

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Social distance, imesaidia kupunguza maambukizi UK, watu wakwepe kuwa karibu/msongamano
 
Nadhani hapa kuna point ya msingi anayojenga Sijijui. Ni vyema MM Togolani na wengine tujadili kwa mtizamo hasi(na sio chanya peke yake). Mfano, pale ambapo tutaendelea kuacha watu wajitafutia riziki halafu hapo hapo waambukizane wengi, hapo serikali itamudu kuwahudumia kwa hali hiyo hiyo uliyoelezea ya mazingira yetu ya kitanzania? Ni dhahiri kuwa kama maambukizi yakiongezeka na kubidi total lockdown, maana yake kutakua na maambukizi mengi yatakayoendelea kwa kiwango kikubwa na kuambatana na vifo kutokana na serikali kushindwa kabisa kumudu kutoa huduma za afya zinazohitajika kwa wagonjwa.

Ni kweli ugonjwa hauna dawa, ila magonjwa yanayoambatana kama kisukari , pressure, n.k yana dawa hata za kupunguza makali tu. Sasa kama tu kwa haliya kawaida dawa zinakua changamoto, je wakati wa total lockdown tunategemea serikali kuweza kuwatibu? Na je mifumo yetu ya afya inaweza kumudu tofauti tu kidogo tu ya idadi kubwa ya wagonjwa itakayoongezeka?

Mimi nafikiri tukiangalia kwa mtazamo chanya ni vyema kuona total lockdown ikizaa matunda. Ila kwa hali yetu ya kitanzania, lockdown iwe ya muda mfupi. Ikionekana kuna kupungua kwa maambukizi unafungua tena halafu unawaweka watu lockdown tena hali ikibadilika mpaka hali itakapokua shwari.

Pia, serikali kuanza kujiandaa na kuimarisha mifumo ya afya. Ifanye taratibu za vyakula kwa kipindi cha hatari. Kama mpango wa TASAF ungekua effective tungeweza kujua priority ilipo. Hata hivyo, ni mahali pa kuanzia kutambua familia duni hasa zilizoko maeneo ya karibu na miji. Pia sio lazima kufanya total lockdown. Kama kijijini rate ya maambukizi ikiwa ndogo then hakuna haja ya lockdwon huko. Ila kwa sehemu kama Dsm na zenye mikusanyiko ni vyema hili likawepo. Hata kama haliko kama wafanyavyo wenzetu basi kuwa na control mfano za social distancing n.k. Kingine tunaweza customize namna tutakavyoita hali hii hatari. Wale wasio na umuhimu wa kwenda nje wabaki majumbani - na hii itawezekana pale tu serikali itakapotamka hali ya hatari. Ila kama haijatamka maana yake hata wale wanaotaka kufanya kazi majumbani hawana justification ya kufanya hivyo na hili ni kwa taasisi za umma zaidi. Kwa private wanaweza kuwa na utaratibu binafsi ila kwa taasisi za umma haziwezi jiwekea utaratibu wa kufanya kazi majumbani wakati serikali haijatangaza hali ya hatari.

Mwisho, mjadala huu bado ni mzuri kwa kuangalia mantiki ya pande zote. Ila namalizia kwa kusema kuna umuhimu wa customized total lockdown kwa baadhi ya sehemu yenye hatari zaidi. Kijijini wanaweza kuendelea kwenda shamba kama kawaida. Ila mjini kama jiji la dsm aisee tunahitaji kufanya kitu zaidi. MM Togolani nakusubiri hapa.
Ungekuwa serious ungeishauri serikali wafanye kitu kuliko kuwambia watu wakafe au wakaambukizane kwa wingi eti kisa wanajitafutia riziki while ukijua mfumo wetu wa afya hauwezi ukawahandle Wala kuwatibu pale hali itakapokuwa imekuwa mbaya.Siku zote kwa watu wenye akili kinga ni bora kuliko tiba.sasa ninyi kwa ujinga wenu singizieni umasikini wa mtanzania,sasa wakishaambukizana kwa maelfu ndo umasikini wao utakuwa umeisha mkuu
 
MUHTASARI:
Nchi nyingi duniani, hasa za Magharibi, zimetangaza karantini au “lockdown” inayowazuia wanachi kutoka ndani muda wote isipokua kutafuta mahitaji ya lazima tu (dawa na chakula). Hatua hii imechukuliwa na nchi ambazo maambukizi ya Covid-19 yamekua makubwa, sio kwa lengo la kuzuia watu wasipate maambuziki, bali zinalenga kupunguza kasi ya maambukizi kwa wakti mmoja ili mfumo wa utoaji huduma za afya usilemewe zaidi. Hali hiyo haina muda maalum na itaendelea hadi mlipuko wa Covid-19 utakapoonekana umepungua au kwisha. Hivyo watu wengi hapa kwetu nao wanaishauri serikali kufanya hivyo wakiamini ni hatua ya lazima kwa sasa na wanachukulia kutotangaza karantini mapema ni uzembe au ni kutokujali.

Katika makala hii, nimeeleza kwa nini sio sahihi kwa nchi yetu na nyingi za kiafrika kufanya hivyo. Pia ninashauri kwa kusisitiza serikali isiwaze kabisa kuchukua hatua hii sababu haifai na haitekelezeki kwenye mazingira yetu. Iwapo njia hii itatutumika, madhara yake kwa wananchi yanaweza kuwa makubwa kuliko tatizo linaloepukwa. Nimeeleza hoja yangu kwa kutumia uzoefu binafsi wa kuwa kwenye karantini na kufananisha mazingira ya utekelezaji wa amri hii kwenye nchi za Magharibi unapolinganisha na nchi zetu. Kwa undani zaidi soma makala nzima hapa chini.

View attachment 1406728

Utangulizi
Nianze ujumbe wangu kwa kutangaza maslahi binafsi. Hapa nilipo, hii ni wiki ya pili tunamaliza tukiwa chini ya “total lockdown”. Nchi nzima tunalazimika kukaa ndani tu na hatujui tutatoka lini. Sina hakika na watu wengine waliowahi kuishi mazingira ya aina hii, ila niseme kwa ujasiri kabisa kwamba mazingira haya ni mabaya, ni magumu, na yanaumiza sana kisaikolojia. Muda mwingi huwezi kufanya lolote la maana kwa kuwa unakua kama umepoteza "network". Mtu asiombe kabisa kukosa uhuru wa kutoka ndani.

Kwa nini nashauri hili?
Kwa sababu hizi na kwa hoja nitakazozieleza hapa, ninapingana kwa 100% na kila ambaye anaishawishi, anaishauri, au anailazimisha serikali kutangaza karantine kama nchi nyingine au anailaumu kwa kutokufanya hivyo. Labda nieleze kwa kifupi nini maana ya kuwa kwenye karantini katika uhalisia ili kuweka ninachoongea kwenye muktadha:
  1. Wazazi, watoto na munaoishi nao munashinda mukiwa mumejifungia ndani: usiku unakuja, asubuhi inafika, munaaendelea na zoezi kam ajana. Mbaya zaidi hamujui zoezi hili litakwisha lini. Wakati mwingine munasahau siku au tarehe maana hakuna matukio yanayowakumbusha. Serikali inasema inaweza kuwa hivi hadi miezi 6.

  2. Haijalishi mukakokuita nyumbani au ndani kukoje kwa maana ya ukubwa/udogo, ubaya/uzuri na kuna nini cha kufurahisha au kufanya: munazunguka humohumo mchana na usiku.

  3. Munatoka ndani mara moja au mbili kwa wiki kwenda kutafuta mahitaji ya lazima. Na mahitaji ya lazima ni chakula na mdawa pekee maana maduka mengine yote yasiyo ya chakula na madawa yamefungwa. Munashauriwa kufanya hivyo inapokua ni lazima lakini kama inawezekana muagize online.

  4. Wakati mwingine vitu vya lazima hakuna madukani au supermarkets maana watu wananunua kwa wingi kwa hofu hivyo vinakwisha.

  5. Ukifika supermarket mupanga foleni ndefu ya kuingia ndani kwa vile munatakiwa muwe umbali wa mita 2 kati ya mtu na mtu na hamutakiwi kuingia wengi kwa wakati mmoja ili musisongamane. Na unaweza kufiuka ndani unakosa unachotaka.

  6. Kwa anayeweza, munaruhusiwa kutoka nje mara moja kwa siku kufanya zoezi moja (kutembea au kukimbia) na uwe mwenyewe au na mtu wa familia yako maana hakuna kukutana zaidi ya watu wawili.

  7. Makazi mengi hayana viwanja vya nje kama kwetu Afrika maana nyumba zimejengwa kwa mipango na kubana nafasi. Mara nyingi, nje ya mlango ni bararaba ya mtaa.

  8. Sheria imepitishwa na bunge kwamba ukikamatwa kwenye mkusanyiko au unazurura unaweza kutozwa faini na polisi ya hadi milioni tatu za Tanzania (zile faini za papo kwa hapo kama za makosa ya barabarani)
Unajua kwa nini wanaweza kufanya haya?
Wenzetu wanapochukua hatua hizi za kukaa ndani ni kwa sababu mazingira yao yanaruhusu ya yameandaliwa hivyo. Kwa mfano:
  1. Wao kukaa ndani sio jambo geni. Maisha yao kwa sehemu kubwa ni ya kibinafsi. Watu wanakaa ndani muda mwingi maana yale maisha ya kijamaa/kijamii wameyaacha. Munaweza kuiishi milango imetazamana na jirani zako lakini musisalimiane hata munapogongana mukitoka au kuingia ndani. Unaweza usimjue jirani yako munayetazamana au kutengwa na ukuta ni nani, anafanya nini, nk. Huku ndiko tumeiga msemo wa “mind your own business” na “I don’t care what yu think of me” na tunadhani ni maendeleo.

  2. Nchi za Ulaya zina msimu wa baridi kuanzia mwezi wa 10 na wa 11 hadi mwishoni mwa mwezi wa tatu. Kipindi hiki hali ya hewa inaweza kua mbaya muda mwingi na baridi ni kali sana. Giza linakua muda mrefu kuliko mchana. Kuna kipindi linaanza kuingia saa tisa jioni na linaendelea hadi saa mbili asubuhi Kesho yake. Hivyo mchana kwa maana ya mwanga unaweza kuwa kama masaa 6 hadi 8 tu. Mvua na barafu huweza kuwepo kwa wingi pia. Kwa jumla, mazingira hayaruhusu kukaa nje wala kutembea hivyo kama mtu hana anapolazimika kwenda basi muda mwingi ni kukaa ndani.

  3. Nyumba za wenzetu hazijengwi kienyeji kama sisi ambapo kila mtu anajijengea atakavyo na atakapo. Nyumba zinajengwa na makampuni na serikali kwa mipango na viwango maalumu. Kutokana na hali ya hewa ya baridi na majanga kama vimbunga, zinajengwa zikiwa na uwezo wa kustahimili baridi na upepo mkali. Madirisha yana vioo viwili; ukuta wa nyumba una leya mbuli na katikati unajazwa vitu vya kupunguza hewa ya baridi; paa linadhibitiwa kiasi kwamba mvu akinyesha unaweza usijue kama hujatazama nje.

  4. Kila nyumba ina maji yasiyokatika; ina bomba la gesi linaloingia ndani kama maji isiyokatika; ina umeme wa uhakika usiokatika. Nyumba zisizo na mabomba ya gesi basi umeme ndio unatumika kupikia na kwenye mifumo ya kupasha maji na nyumba joto.

  5. Kila nyumba inaijengwa, inaingiziwa waya (connection) ya TV, simu ya landline na internet. Huduma hizi ni za uhakika kwa kila nyumba labda uwe tu huwezi kulipia bills. Internet ni rahisi sana hivyo kwa gharama ambayo hapa kwetu mtu anatumia kununua bando la GB kama ya 20, kwao unapata internet ya kutumia vifaa zaidi ya kumi kwa wakati mmoja (simu, computers, smart tv, tablets) usiku na mchana mwezi mzima mukifanya kila munachotaka kwenye internet bila kupimiwa.

  6. Huduma za maji, umeme, internet, gesi, simu, tv hazikatiki na hazikatwi kienyeji hata ukishindwa kulipa bills. Tarehe ya kulipia ikifika huna pesa kwenye kwenye akaunti utafutatiliwa na kukumbushwa kwanza kwa muda ingawa ukichelewa sana utapigwa faini ya kukuumiza.

  7. Unaweza kuagiza KITU CHOCHOTE online (kwa kupiga simu au internet) na kikaletwa hadi mlangoni iwe dawa, chakula, nguo, viatu, mashuka, vinywaji, nk.

  8. Ukiiumwa unawasiliana na daktari kituo cha afya uliposajiliwa kabla ya uamuzi wakwenda hospitali kama sio matatizo ya dharura. Matatizo yote ya dharura ukipiga simu ndani ya dakika chache ambulance iko mlangoni na ukichelewa kufungua wanaweza kuvunja mlango wakaingia wakidhani umezidiwa.

  9. Ukipata tatizo kama kupigwa na mwenza, kuingiliwa na wezi, au mtoto kupigwa na mzazi; ukipiga simu ndani ya dakika chache polisi wako mlangoni.
Haya ndio mazingira ya wenzetu yanayowaruhusu kutangaza TOTAL LOCKDOWN au KARANTINI kirahisi kama vile wanatangaza mshahara kupanda. Wanaposema watu wakae ndani wasitoke, wana hakika kwa zaidi ya 95% mazingira ya kila mtu yanamruhusu kukaa ndani na akaishi bila matatizo makubwa. Pia, kwa kuwa wana mifumo inayofanya kazi na makazi yamepangika, kwa sehemu kubwa wanajua kila mtu anayefanya kazi (binafsi au kijiajiri), kipato chake, na anaishi wapi. Hivyo serikali wanaweza kutangaza kutoa ruzuku za kuishi kwa kiwango fulani kwa kila raia au mfanyakazi huu muda wa mlipuko na wakazipata bila mizengwe.

Sasa linganisha mazingira haya yao nay a kwetu.
  1. Sisi wananchi wengi hawana uwezo wa kununua chakula cha kesho. Inamlazimu mtu kutoka ndani kila siku ili angalau aweze kuweka mlo mezani.

  2. Sisi tumezoea kwenda duknai/sokoni kila siku au mara kadhaa kwa wiki kununua kila kitu kidogokigogo. tubamia, kaunga, tudagaa, tunyanya, tuvitunguu, tumchicha, nk.

  3. Sisi tuna familia nyingi hazijui umeme ni nini. Hata walionao, hauna uhakika wa kuwaka kila siku. Kwa wenzetu umeme kukatika kwenye nyumba kwa nusu dakika tu ni moja ya miujiza kwa mwaka labda kuwe na majanga kama vimbunga, mafuriko, nk.

  4. Sisi watu wengi hawana maji ya bomba ndani. Wengi inawalazimu kila siku kwenda kuteka maji mtoni, bombani, kisimani, chemchem, bwawani au hata kuomba kwa jirani mwenye uwezo. Wengi inawalazimu kutembea umbali mrefu kupata maji.

  5. Makazi yetu hayana anuani za kueleweka hivyo hatuwezi kuwa na huduma za kununua vitu online na kushushiwa nyumbani hata kama tukitaka.
  6. Wengi wetu tunaishi kwenye nyumba mbovu, mbaya, hazina mvuto, na wengine ni ndogo sana ukilinganisha na ukubwa wa familia. Pia wote nchi nzima tunaishi na mifugo kadhaa ndani ya nyumba. Kama sio mbuzi, kuku, kondoo au ng’ombe, basi tunaishi na mende, panya, viroboto, nzi na mbu.

  7. Hatuna maduka makubwa (supermarkets) kila mahali karibu na watu ambapo utasema mahitaji ya lazima unapokua kwenye karantini utayapata kwa karibu kirahisi. Wengi hutembea au kusafiri mbali kwenda madukani au sokoni kupata chakula.

  8. Wananchi wengi wanatumia mkaa, kuni au mafuta ya taaa kupikia. Wengine wakitaka kuwasha moto lazima wakaombe kiberiti au kaa la moto kwa jirani.

  9. Wengi wetu hatuna vyoo vya ndani na vya nje havitamaniki.
Sasa niambie, serikali ikitangaza karantini ya kumtaka kila mtu akae ndani na asichangamane hata na jirani yake tutaishije kwenye mazingira haya? Tutaweza kuishi hivyo hata kwa wiki moja? Na kama tukilazimika kwa kiboko kama kule Kenya, unadhani ni madhara kiasi gani tutapata?

Mwisho
Msukumo wa kuishauri serikali kutangaza lock-down, kama ilivyo kwa misukumo mingi, inatoka kwa kundo dogo la watu wenye uwezo (middle class). Duniani kote kundi hili hujisahau na kudhani kila mtu ana maisha kama yao. Lina kiwango kikubwa sana cha ubinafsi na wakati mwingine wanasahau kabisa kwamba hata ndugu zao wa karibu kabisa hawana uwezo walionao wa. Lakini ukweli ni kwamba kwa watanzania walio wengi karantini ya kututaka kukaa ndani ni hata kubwa mara nyingi kuliko Covid-19. Wanashawishi hatua hii wakumbuke kwanza kijijini kwao walikotoka wao au wazazi wao kabla hawajashauri lockdown.

Serikali ichukue kila tahadhari na hatua wanazoshauriwa na wataalamu kuhusu kuzuia au kupunguza maambukizi ya Covid-19. Tusikilize wataalamu ni kwa jinsi gani tunaweza kuwakinga watu ambao wakipata maambukizi watadhuruka zaidi (wazee, wenye magonjwa ya kupua, na wenye chronic diseases). Ila isikubali wala kusikiliza ushawishi wa mtu, watu, taasisi, au nchi yoyote kwamba inalazimika kutangaza karantini katika hatua ya sasa.

Karantini ya kuwataka watu kukaa nyumbani (tena kwa muda usiojulikana) ni njia isiyofaa kwa wananchi wetu. Itakua na madhara makubwa sana kiafya, kijamii, na kimaisha iwapo itachukuliwa katika hatua hii. Kufanya hivyo itakua ni sawa na kukimbia kuumwa na mbwa kwa kuingia kwenye zoo walipo simba na chui huku ukidhani unatafuta kinga.

Kwa ngazi ya maambukizi tuliyopo sisi (ukilinganisha na nchi zilizoathirika sana), bado tunaweza kuwa na maambukizi hadi miezi 5 au 6 kuanzia sasa. Njia hii inaweza kusaidia kama suluhisho la mwisho kabisa wakati maambukizi yamezidi uwezo wa kukabiliana nayo, kwa maana ya kwamba watu wengi walioambukizwa watakua na hali mbaya kiafya (critical conditions). Ikifika hatua hiyo, mlipuko utakua umefika kileleni na kukaribia kushuka hivyo muda wa watu kukaa ndani utakua ni mfupi na madhara yatakua kidogo. Kitu cha kushauri serikali kwa sasa ni namna ya kuandaa mikakati ya nini cha kufanya iwapo tutalazimika kufikia hatua hiyo (worse case scenario). Ukiweka watu ndani sasa wakati hujui utawaweka kwa muda gani, madhara yake ni makubwa sana.

Pia tukumbuke sio lazima kila nchi ifikie hatua ya kua na vifo vingi kama tunavyoona Italy, Spain na kwingine. Ni makosa kuchukulia kinachotokea kwenye nchi hizo kama kielelezo.

MM Togolani ([email protected])
Mwathirika wa "Total Lockdown"
Leo hii nilikuwa nazungumza na kijana mmoja, mengi ya niliyomuambia ndio uliyoyafafanua wewe. Asante sana kwa ujumbe nzuri kwa Taifa letu la Tanzania.
Mimi ni kati ya wanaopinga hii "Lockdown" kwa 100% Ningeikubali tu, iwapo kama janga hili lingekuwa la muda, au dawa ipo mbioni kupatikana, ila kwa hali ilivyo tunaweza kujipiga lockdown ya maisha. Tuache mihemko, tuangalie uhalisia wa mambo yanavyotokea.
Niliwaza sana leo juu ya huu ugonjwa na kujisemea moyoni kuwa, yawezekana wanamlazimisha hii "Lockdown" ili baadae waje wamcheke kwa madhara yatakayotokea.
Uzi wako umenigusa sana, na ninakiri kuwa kumbe mawazo ya mtu yanaweza kuwasilishwa na mtu mwingine kama vile yeye angewasilisha.
Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom