MeruA
JF-Expert Member
- Aug 9, 2017
- 1,390
- 2,170
Mkuu huzuiliwi kujifungia ndani,jifungie tu na familia yako tuache tukatafute mkate wa watoto wetu, total lockdown bila chakula ni zaidi ya corona mkuu tafadhari sana usishabikie lockdown.Ajifunze kuandika vizuri!Ushauri wangu kwenye Corona ni huu mara zote kwa watu kama hawa,tuombe Mungu sana Corona isienee nchini maana tutaisha kama kuku!
Bado naona serikali inafanya mchezo na Corona,tunaona watu bado wanakusanyika vituo vya mabasi,tunaona Makonda bado anakusanya watu na kuwahutubia,level seat bado sio suluhisho maana distance kati ya mtu na mtu ni Zero distance nk!
Kwa mazingira kama hayo,ni kuomba muujiza tu ndio utuokoe!
Hao walioamua total lockdown wana sababu zao,huenda wamepiga hesabu wakaona ni heri wachache wafe wengi wapome,kupanga ni kuchagua!
Sent using Jamii Forums mobile app