Serikali isikubali kutangaza “total lockdown” au Karantini. Wanaoishawishi ama hawajui wanachokishauri au ni wabinafsi

Nimekupa like mkuu!
Huyu unayesema hajui kuandika alikuwa Mwandishi wa Hotuba wa Rais Kikwete, akiachiwa kazi hiyo na January Makamba...

So fikiri kabla ya kusema, yawezekana aliyoyaandika yanazidi upeo wa akili zako, Pole sana!

Finally, Linganisha muda MM Togolani aliojiunga JF(2010) na muda wako Wewe, Then uweke hoja zako chini tujadili
 
Nikurudishe palepale unapokwepa. Zaidi ya haya maelezo yako ya jumla, ni sayansi au theory gani unayotumia inayokuambia lockdown inazuia watu kufa au itazuia watu wengi kuambukizwa? Na itakua kwa muda gani?

Mbili, hii hoja ya watu kufa wote wakiambukizwa unaitoa kwenye data au utafiti gani? Unaweza kutupa data zinazoonesha watu wote wanaopata corono wanakufa? Crude Mortality Rate and Mortality Rate ya Covid-19 ni kiasi gani na tafsiri yake ikoje? Unaitafsije kwa conetxt ya kila nchi?

Inarahisisha sana ukijibu CLAIMS za kisayansi au kitafiti kwa data.

Sent using Jamii Forums mobile app

vitu vingine ni common sense tu hauhitaji kufikiria mara mbili au kwenda maaabara!?? ? ….my dear kisayansi inawezekana kabisaa ku control ama kumonitor rate of infection ya coronavirus and statistics hazidanganyi na ndio sayansi ilipo….and yes lockdown itazuia wengi kuambukizwa au kufa...hili nalo hata sio la kufikiria mara mbili...ni kitu ambacho kinaweza kuwa proved kwa nyie wanasayansi!

Hilo la kufa, sijui mwenzetu umeamua kuwa tu blind,hivi huoni ulimwengu watu wanavyokufa kwa siku??..ngoja tusichukue measure za kujikinga and then tuone jinsi tulivyo na low resources kupambana na huu ugonjwa itakuwaje...kama infection ikisambaa?

MAJORITY vifo nilikua namaanisha..ukiruhusu free movements of people katika kipindi hiki,inamaanisha unawa expose wengi kwenye hii contagious disease, a lot will catch the virus and knowing how we have under resourced health care system, A LOT will die at one given time..kuacha wale FEW waliobaki nyumbani..conversley tukiweka lockdown Majority watabaki nyumbani na kupunguza kasi ya maambukizi,But this means wachache watakufa serving the larger population..ni hayo mkuu
 
Kuna kitu watu wengi mnajidanganya. Mnasema ni bora kufa kwa corona kuliko kufa kwa njaa.

Wewe na wenzako wenye mindset kama yako mkae mkijua kwamba moja ya masharti ya mtu anayeumwa Covid 19 ni kurest.

Ukishaumwa hiyo corona kuendelea kufanya kazi zako itakuwa ni kukitafuta kifo chako kwa kasi.

Hapo ndipo tutakapopukutika kama kuku wenye kideli.
MUHTASARI:
Nchi nyingi duniani, hasa za Magharibi, zimetangaza karantini au “lockdown” inayowazuia wananchi kutoka ndani muda wote isipokua kutafuta mahitaji ya lazima tu (dawa na chakula). Hatua hii imechukuliwa na nchi ambazo maambukizi ya Covid-19 yamekua makubwa, sio kwa lengo la kuzuia watu wasipate maambuziki, bali zinalenga kupunguza kasi ya maambukizi kwa wakati mmoja ili mfumo wa utoaji huduma za afya usilemewe na kushindwa kuwahudumia wanaozidiwa. Lockdown haina muda maalum na itaendelea hadi mlipuko wa Covid-19 utakapoonekana umepungua au kwisha. Hivyo watu wengi hapa Tanzania nao wanaishauri serikali kufanya hivyo wakiamini ni hatua ya lazima kwa sasa na wanachukulia kutotangaza karantini mapema ni uzembe au ni kutokujali.

Katika makala hii, nimeeleza kwa nini sio sahihi kwa nchi yetu na nyingi za kiafrika kutangaza Lockdown. Pia nimeshauri kwa kusisitiza serikali isiwaze kabisa kuchukua hatua hii katika hatua hii hasa kwa sababu haitekelezeki kwenye mazingira yetu na hatujui mlipuko utachukua muda gani. Iwapo njia hii itatutumika, madhara yake kwa wananchi yanaweza kuwa makubwa kuliko yatokanayo na Covid-19. Nimeeleza hoja yangu kwa kutumia uzoefu binafsi wa kuwa kwenye karantini. Pia nimefananisha mazingira ya utekelezaji wa amri hii kwenye nchi za Magharibi na nchi zetu ili kuweka hoja yangu katika muktadha.Kwa undani zaidi soma makala nzima hapa chini.

View attachment 1406728

Utangulizi
Nianze ujumbe wangu kwa kutangaza maslahi binafsi. Hapa nilipo, hii ni wiki ya pili tunamaliza tukiwa chini ya “total lockdown”. Nchi nzima tunalazimika kukaa ndani muda na hatujui tutatoka lini. Sina hakika na watu wengine waliowahi kuishi mazingira ya aina hii, ila niseme kwa ujasiri kabisa kwamba mazingira haya ni mabaya, ni magumu, na yanaumiza sana kisaikolojia. Muda mwingi huwezi kufanya lolote la maana kwa kuwa unakua kama umepoteza "network". Mtu asiombe kabisa kukosa uhuru wa kutoka ndani. Ninapingana kwa 100% na kila ambaye anaishawishi, anaishauri, au anailazimisha serikali kutangaza karantine kama nchi nyingine au anailaumu kwa kutokufanya hivyo.

Nini msingi wa hoja yangu?
Labda nieleze kwa kifupi nini maana ya kuwa kwenye karantini katika uhalisia ili kuweka ninachoongea kwenye muktadha:
  1. Wazazi, watoto na munaoishi nao munashinda mukiwa mumejifungia ndani: usiku unakuja, asubuhi inafika, munaaendelea na zoezi kama jana. Mbaya zaidi hamujui zoezi hili litakwisha lini. Wakati mwingine munasahau siku au tarehe maana hakuna matukio yanayowakumbusha. Serikali inasema inaweza kuwa hivi hadi miezi 6.

  2. Haijalishi munakokuita nyumbani au ndani kukoje kwa maana ya ukubwa/udogo, ubaya/uzuri na kuna nini cha kufurahisha au kufanya: munazunguka humohumo mchana na usiku.

  3. Munatoka ndani mara moja au mbili kwa wiki kwenda kutafuta mahitaji ya lazima. Na mahitaji ya lazima ni chakula na madawa maana maduka ya mahitaji mengine yamefungwa. Munashauriwa kama inawezekana muagize vyakula online.

  4. Wakati mwingine vitu vya lazima hakuna madukani/supermarkets maana kutokana na hofu, watu wananunua kwa wingi hivyo vinakwisha.

  5. Ukifika supermarket mupanga foleni ndefu ya kuingia ndani kwa vile munatakiwa muwe umbali wa mita 2 kati ya mtu na mtu na hamutakiwi kuingia wengi kwa wakati mmoja ili musisongamane. Unaweza kufika ndani unakosa unachotaka.

  6. Kwa anayeweza, munaruhusiwa kutoka nje mara moja kwa siku kufanya zoezi moja (kutembea au kukimbia) na uwe mwenyewe au na mtu wa familia yako maana hakuna kukutana zaidi ya watu wawili.

  7. Makazi mengi hayana viwanja vya nje kama kwetu Afrika maana nyumba zimejengwa kwa mipango na kubana nafasi. Mara nyingi, nje ya mlango ni bararaba ya mtaa.

  8. Sheria imepitishwa na bunge kwamba ukikamatwa kwenye mkusanyiko au unazurura unaweza kutozwa faini na polisi ya hadi milioni tatu za Tanzania (zile faini za papo kwa hapo kama za makosa ya barabarani)
Unajua kwa nini wanaweza kufanya haya?
Wenzetu wanapochukua hatua hizi za kukaa ndani ni kwa sababu mazingira yao yanaruhusu ya yameandaliwa hivyo. Kwa mfano:
  1. Wao kukaa ndani sio jambo geni. Maisha yao kwa sehemu kubwa ni ya kibinafsi. Watu wanakaa ndani muda mwingi maana yale maisha ya kijamaa/kijamii wameyaacha. Munaweza kuiishi milango imetazamana na jirani zako lakini musisalimiane hata munapogongana mukitoka au kuingia ndani. Unaweza usimjue jirani yako munayetazamana au kutengwa na ukuta kua ni nani, anafanya nini, nk. Huku ndiko tumeiga msemo wa “mind your own business” na “I don’t care what yu think about me” na tunadhani ni maendeleo.

  2. Nchi za Ulaya zina msimu wa baridi kuanzia mwezi wa 10 na wa 11 hadi mwishoni mwa mwezi wa tatu. Kipindi hiki hali ya hewa inaweza kua mbaya muda mwingi sababu ya upepo mkali, mvua nyingi, baridi ni kali, na kunaweza kuwa na barafu. Giza linakua muda mrefu kuliko mchana. Kuna kipindi linaanza kuingia saa tisa jioni na linaendelea hadi kesho yake saa mbili asubuhi. Hivyo mchana kwa maana ya mwanga unaweza kuwa kama masaa 6 hadi 8 tu. Kwa jumla, mazingira hayaruhusu kukaa nje wala kutembea hivyo kama mtu hana anapolazimika kwenda basi muda mwingi ni kukaa ndani.

  3. Nyumba za wenzetu hazijengwi kienyeji kama sisi ambapo kila mtu anajijengea atakavyo na atakapo. Nyumba zinajengwa na makampuni au na serikali kwa mipango na viwango maalumu. Kutokana na hali ya hewa ya baridi na majanga kama vimbunga, nyumba zinajengwa zikiwa na uwezo wa kustahimili baridi na upepo mkali. Madirisha yana vioo viwili; ukuta wa nyumba una kuta mbili na katikati unajazwa vitu vya kupunguza hewa ya baridi; paa linadhibitiwa kiasi kwamba mvu akinyesha unaweza usijue iwapo hujatazama nje.

  4. Kila nyumba ina maji yasiyokatika; ina bomba la gesi linaloingia ndani kama maji; ina umeme wa uhakika usiokatika. Nyumba zisizo na mabomba ya gesi basi umeme ndio unatumika kupikia na kwenye mifumo ya kupasha maji na nyumba joto.

  5. Kila nyumba inapojengwa, inaingiziwa waya (connection) ya TV, simu ya landline na internet. Huduma hizi ni za uhakika kwa kila nyumba labda uwe tu huwezi kulipia bills. Internet ni rahisi sana hivyo kwa gharama ambayo hapa kwetu mtu anatumia kununua bando la GB kama ya 20, kwao unapata internet ya kutumia vifaa zaidi ya kumi kwa wakati mmoja (simu, computers, smart tv, tablets) usiku na mchana mwezi mzima mukifanya kila munachotaka kwenye internet bila kupimiwa.

  6. Huduma za maji, umeme, internet, gesi, simu, tv hazikatiki na hazikatwi kienyeji hata ukishindwa kulipa bills. Tarehe ya kulipia ikifika huna pesa kwenye akaunti utafutatiliwa na kukumbushwa kwanza kwa muda ingawa ukichelewa sana utapigwa faini ya kukuumiza.

  7. Unaweza kuagiza KITU CHOCHOTE online (kwa kupiga simu au internet) na kikaletwa hadi mlangoni iwe dawa, chakula, nguo, viatu, mashuka, vinywaji, nk.

  8. Ukiiumwa unawasiliana na daktari kituo cha afya uliposajiliwa kabla ya uamuzi wa kwenda iwapo sio matatizo ya dharura. Matatizo yote ya dharura ukipiga simu ndani ya dakika chache ambulance iko mlangoni na ukichelewa kufungua wanaweza kuvunja mlango wakaingia wakidhani umezidiwa.

  9. Ukipata tatizo kama kupigwa na mke au mume, kuingiliwa na wezi, au mtoto kupigwa na mzazi; ukipiga simu ndani ya dakika chache polisi wako mlangoni.
Haya ndio mazingira ya wenzetu yanayowaruhusu kutangaza TOTAL LOCKDOWN au KARANTINI kirahisi kama vile wanatangaza mshahara kupanda. Wanaposema watu wakae ndani wasitoke, wana hakika kwa zaidi ya 95% mazingira ya kila mtu yanamruhusu kukaa ndani na akaishi bila matatizo makubwa. Pia, kwa kuwa wana mifumo inayofanya kazi na makazi yamepangika, kwa sehemu kubwa wanajua kila mtu anayefanya kazi (binafsi au kijiajiri), kipato chake, na anaishi wapi. Hivyo serikali wanaweza kutangaza kutoa ruzuku za kuishi kwa kiwango fulani kwa kila raia au mfanyakazi kipindi hiki cha mlipuko na watu wakazipata bila mizengwe.

Sasa linganisha mazingira haya yao nay a kwetu.
  1. Sisi wananchi wengi hawana uwezo wa kununua chakula cha kesho. Inamlazimu mtu kutoka ndani kila siku ili angalau aweze kuweka mlo mezani.

  2. Sisi tumezoea kwenda dukani/sokoni kila siku au mara kadhaa kwa wiki kununua kila kitu kidogokigogo: tubamia, kaunga, tudagaa, tunyanya, tuvitunguu, tumchicha, nk.

  3. Sisi tuna familia nyingi hazijui umeme ni nini. Hata walionao, hauna uhakika wa kuwaka kila siku. Kwa wenzetu umeme kukatika kwenye nyumba kwa nusu dakika tu ni moja ya miujiza kwa mwaka labda kuwe na majanga kama vimbunga, mafuriko, nk.

  4. Sisi watu wengi hawana maji ya bomba ndani. Wengi inawalazimu kila siku kwenda kuteka maji mtoni, bombani, kisimani, chemchem, bwawani au hata kuomba kwa jirani mwenye uwezo. Wengi inawalazimu kutembea umbali mrefu kupata maji.

  5. Makazi yetu hayana anuani za kueleweka hivyo hatuwezi kuwa na huduma za kununua vitu online na kushushiwa nyumbani hata kama tukitaka.

  6. Wengi wetu tunaishi kwenye nyumba mbovu, mbaya, hazina mvuto, na wengine ni ndogo sana ukilinganisha na ukubwa wa familia. Pia wote nchi nzima tunaishi na mifugo kadhaa ndani ya nyumba. Kama sio mbuzi, kuku, kondoo au ng’ombe, basi tunaishi na mende, panya, viroboto, nzi na mbu.

  7. Hatuna maduka makubwa (supermarkets) kila mahali karibu na watu ambapo utasema watapata mahitaji ya lazima kwa urahisi wakiwa kwenye karantini. Wengi hutembea au kusafiri mbali kununua chakula madukani au sokoni

  8. Wananchi wengi wanatumia mkaa, kuni au mafuta ya taa kupikia. Wengine wakitaka kuwasha moto lazima wakaombe kiberiti au kaa la moto kwa jirani.

  9. Wengi wetu hatuna vyoo vya ndani na vya nje havitamaniki.
Sasa niambie, serikali ikitangaza karantini ya kumtaka kila mtu akae ndani na asichangamane hata na jirani yake tutaishije kwenye mazingira haya? Tutaweza kuishi hivyo hata kwa wiki moja? Na kama tukilazimika kwa kiboko kama kule Kenya, unadhani ni madhara kiasi gani tutapata?

Mwisho
Msukumo wa kuishauri serikali kutangaza total lockdown, kama ilivyo kwa misukumo mingine kwenye janga hili, inatoka kwa kundi dogo la watu wenye uwezo (middle class). Duniani kote kundi hili hujisahau na kudhani kila mtu ana maisha kama yao. Lina kiwango kikubwa sana cha ubinafsi na wakati mwingine wanasahau kabisa kwamba hata ndugu zao wa karibu hawana uwezo walionao wao. Lakini ukweli ni kwamba kwa watanzania walio wengi karantini ya kututaka kukaa ndani ni janga kubwa mara nyingi kuliko Covid-19. Wanaoshawishi hatua hii wakumbuke kwanza kijijini kwao walikotoka wao au wazazi wao kukoje kabla hawajashauri total lockdown.

Serikali ichukue kila tahadhari na hatua wanazoshauriwa na wataalamu kuhusu kuzuia au kupunguza maambukizi ya Covid-19. Tusikilize wataalamu ni kwa jinsi gani tunaweza kuwakinga watu ambao wakipata maambukizi watadhuruka zaidi (wazee, wenye magonjwa ya kupua, na wenye chronic diseases). Ila isikubali wala kusikiliza ushawishi wa mtu, watu, taasisi, au nchi yoyote kuilazimisha kutangaza karantini katika hatua ya sasa.

Karantini ya kuwataka watu kukaa nyumbani (tena kwa muda usiojulikana) ni njia isiyofaa kwa wananchi wetu. Itakua na madhara makubwa sana kiafya, kijamii, na kimaisha iwapo itachukuliwa katika hatua hii. ndio tuko mwanzoni kabisa mwa maambukizi na hatuna hata mgonjwa mmoja aliye na hali mbaya. Kutangaza lockdown itakua ni sawa na kumkimbia mbwa kwa kuingia kwenye zoo walipo simba na chui huku ukidhani unatafuta kinga.

Kwa ngazi ya maambukizi tuliyopo sisi (ukilinganisha na nchi zilizoathirika sana na tabia ya mlipuko), bado tunaweza kuwa na maambukizi hadi miezi 5 au 6 kuanzia sasa. Njia ya lockdown naweza kusaidia kama suluhisho la mwisho kabisa wakati maambukizi yamezidi uwezo wa kukabiliana nayo: kwa maana ya kwamba watu wengi walioambukizwa watakua na hali mbaya kiafya (critical conditions). Ikifika hatua hiyo, mlipuko utakua umefika kileleni na kukaribia kushuka hivyo muda wa watu kukaa ndani utakua ni mfupi na madhara yatakua kidogo. Kitu cha kushauri serikali kwa sasa ni namna ya kuandaa mikakati ya nini cha kufanya iwapo tutalazimika kufikia hatua hiyo (worse case scenario). Ukiweka watu ndani sasa wakati hujui utawaweka kwa muda gani na huna uwezo wa kuwahudumia, madhara yake ni makubwa sana.

Pia tukumbuke sio lazima kila nchi ifikie hatua ya kua na vifo vingi kama tunavyoona Italy, Spain na kwingine. Ni makosa kuchukulia kinachotokea kwenye nchi hizo kama kielelezo na sababu ya kujengea hofu na taharuki katika kufanya maamuzi.

MM Togolani ([email protected])
Mwathirika wa "Total Lockdown"

------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
Ziada na hitimisho
Kwenye uzi huu nimefafanua na nimejibu hoja kinzani na maswali ya wachangiaji kadiri nilivyoweza. Kwa kufanya hivyo nimefafanua mambo mengine ambayo sikuyataja kwenye makala yangu. Kwa ujumla ninaweza kuhitimisha hoja namaswali yao kama ifuatavyo:

Nikisoma maoni, matusi, maonyo, hofu na taahadhari ya waotamani serikali itangaze total lockdown, hakuna hata mmoja anayetoa suluhisho au mbinu ya utekelezaje wake. Hakuna anayetoa data yoyote kiuchumi, kijamii, afya, nk. Hawatuambii watanzania wasio na maji, ajira, umeme, nk ambao wataathirika kuanzia siku ya kwanza ni asilimia ngapi na watasidikaje. Hoja yao ni moja tu, HOFU na watu wengi watakufa tusipotangaza Lockdown sasa. Hakuna scientific argument yoyote wanayotoa yenye ushawishi au theory and practices za crisis management or outbreaks control/response.

Kauli zao zinaonesha kifo kinachotisha ni cha Corona pekee. Vifo vitokanavyo na njaa, malaria, kipindupindu, kuhara, na utapiamlo (baadhi ya maradhi ambayo yatakumba wengi kukiwa na lockdown ya muda mrefu) havitishi wala sio tatizo. Tatizo ni Corona tu kwa madai kwamba tutakufa kama Italy na Spain. Wakati hofu hizi ni za msingi ila hazitakiwi kuwa msingi wa maamuzi na kufikiria kwetu.

Watu hawa hawaelevi bado inamaanisha nini hasa kuwa kwenye total lockdown. Hawatazami multiplying effect ya lockdown. Hawaelewi makampuni mengi yatafungwa na wafanyakazi watapoteza kazi. Hakuna mwajiri ataendelea kulipa mshahara watu wasiofanya kazi na yeye hazalishi. Hata makampuni yatakayooperate yatapunguza wafanyakazi kwa sehemu kubwa maana hakuna biashara. Nimeongea na wafanyakazi kadhaa wa sekta ya utalii wako majumbani hawana kazi na hawajui kazi itarejea lini. Waliobahatika kubaki na ajira wengine wameahidiwa wanalipwa nusu ya mshahara kwa miezi 3 au 5 wakati kisha maamuzi mengine yatafuata.

Kinachotokea na kitakachotokea zaidi, uwezo wa serikali kukusanya kodi utakua mdogo maana hakuna biashara; uzalishaji unapungua; PAYE itapungua maana watu wamepoteza kazi. Nchi yetu bado inategemea makusanyo ya kila mwezi kugharamia mahitaji muhim ya nchi kama kulipa wafanyakazi, kununua madawa, ulinzi na usalama, na kazi za utawala wa nchi.

Hivyo unapoishauri serikali kukimbilia total lockdown sasa na kwa muda usiojulikana (maana ndio tuko asubuhi mwa mlipuko), tuiambie pia itaendeshaje nchi. Kama hatuelewi complexity ya lockdown basi tuendelee tu kuisilikiliza kwenye vyombo vya habari kuliko kujiona sisi ni wataalamu wa utekelezahi wa total lockdown. Nirudie tena, huwezi kukimbia kung'atwa na mbwa (Corona) kwa kukimbilia walipo chui na simba (madhara ya total lockdown).

Namishukuruni waliosoma, waliochangia, waliokosoa, waliosahihisha, walioniita mjinga, na hata walionitukana. Wote wametumia uhuru weo kadiri ilivyowapendeza. Bado kuna mambo mengi ya muhim ya kuchambua na kujadili kuhusu Covid-19.

Mubarikiwe.

MM Togolani.
 
Ungejibu maswali niliyokuuliza ungekua umesaidia sana.

Halafu nimewakumbusha munaposisitiza lockdown, muishauri pia serikali itakavyoitekeleza. Hili halihitajo kaulizi za jumlajumla kwamba tutakufa au ni uzembe. Kunahitajika solutions. Tuambie wale wamama kule kijijini wanaotembea km2 au 3 kufuata ndoo ya maji na kaunga sokoni wataishije? Nyie munaosema lockdown huenda ndani muna umeme na gesi na akiba ya mafuta. Tuambieni wale wanaosafiri kutafuta mkaa wa siku au kuni au mafutaa ya taa kwenye chupa, huko lockdown watapika na nini hata kama wakiwa na chakula?

Sent using Jamii Forums mobile app
Hakutaweza kuwa na majibu hapo mkuu hata siku moja! Kuna kufuata mkumbo na siyo uhalisia wa Jambo.

Nakupongeza saaana kwa ufafanuzi makini na mada yenye tija mkuu.
 
My kaka naona hatuelewani, na moja ya sababu ni kwamba huelewi kwamba lockdown inasaidia ni ku protect MAJORITY ya watu katika jamii..na kufanya hivi kutacost lives za WACHACHE .sasa wewe unapigania tofauti ; watu WACHACHE wawe protected Majority wafe...mfano wako wa huyo mama wa kijijini..unge quantify jinsi ambavyo anaenda sokoni na kuambukiza ama kuambukizwa na kuiletea familia yake maafa, ungeona kwamba asingeenda sokoni ama akapunguza safari za sokoni kuna ka cheni hapo angekua amekakata, Hii ni scenario inaonyesha jinsi hili swala lisiangalie upande mmoja tu wa mtu mmoja mmoja,bali angalia jamii kwa ujumla….

Kujibu mliosema hamuogopi Corona sababu kukaa ndani, sijui mahitaji yenu nini..na pengine hili haliwashtui...mna matatizo kibao ya kudeal nayo,malaria,typhoid mmeshazizoea..na hamtakaa nyumbani..naomba tu kuwaambia jamani. NDIO TUNA MATATIZO MENGI,ila KUJA KWA CORONA , hakupunguzi ama kureplace matatizo tuliyonayo!!!...ni kwamba unaweza kuwa na malaria, kipindu pindu..na corona inakuja ku complicate mambo EVEN MORE!!!..hamtakua na ugonjwa mmoja wa ku deal nao….choices zinabaki kwenu!!!!!

Lastly tutakua wajinga kama tunaona yanayoendelea duniani halafu hatuchukui hatua….Coronavirus: UK should have gone into lockdown 10 days ago, Italy's scientific adviser warns

Ni kweli niliona mahali infection rate ya corona Virus inapungua UK, nimeshindwa ku locate hio article.japokuwa vifo vimeongezekaThe lockdown looks to be reducing the number of people infected

UK coronavirus infection rate slowing due to lockdown, scientists say

'Confinement is working' – New analysis shows Spain's coronavirus lockdown having effect as long-term infection rates fall - Olive Press News Spain

Coronavirus measures may have already averted up to 120,000 deaths across Europe | Imperial News | Imperial College London

Rebeca 83 Hizi links ulizotoa sio ngeni kwangu. Kuna mambo ya msingi ungetakiwa kuzingatia kabla ya kuzitumia kama references.

Moja, unazitumia out of context. Hawa wote wanajadili faida ya lockdown at a stage when the epidemic is gaining momentum toward the peak, not at its onset. Sisi tuko mwanzoni mwa mlipuko hii njia katili haifa. Jaribu kuwaza UK ingekuwaje leo iwapo ingetangaza lockdown tarehe moja February walipokua na wagonjwa chini ya 20? Ukisoma scientific predictions and analysis jaribu kutozisoma kama news. Kama serikali yao itatumia zaidi ya paundi trillion moja (zaidi ya trilioni 3,000 za Tanzania) kusaidia wafanyakazi na biashara zisife ndani ya kama miezi 2 tu, ingekuwaje sasa mwezi wa nne huku kukiwa ndio bado ni saa nne asubuhi?

Pili, hata kama kwao imefanya kazi, bado rudia hoja ya makala uchambuzi wangu. Kwamba context ya utekelezaji wa lockdown haifanani na kwetu. Ni mbali kama Mashariki ilivyo kwa Magharibi. Nilishaeleza sababu.

Tatu, hizi ni scientific predictions and suggestions sio empirical or clinical data. Zinaweza kutofautiana kabisa na ukweli. Yes, modelling zanapredict RATE ya maambukizi imepunguzwa na lockdown, ila sio kupungua kwa IDADI ya maambukizi. Kama lockdown ingepunguza maambukizi Italy wasingekua na cases mpya hadi leo maana wana zaidi ya mwezi wakiwa ndani ya lockdown. Kwa tafsiri yako ya Lockdown, leo wangetakiwa wasiwe na hata mgonjwa mmoja mpya wawe wanamalizia kutibu wale tu ambao walishalazwa hospital. Ila data hazioneshi hilo. hadi sasa wanareport wastani wa wagonjwa waya10,000 na vifo 800 kwa siku. Kwa nini wakati wako kwenye strict lockdown zaidi ya mwezi?

Nne, unaposoma habari kisayansi kama hizi ulizoweka hapa (ambazo sio machapisho ya utafiti), jaribu kujiongeza kwa kutazama real data zinasemaje (kama zipo) kisha changanya na za kwako kupata maana. Pia nirudie kukukumbusha kwamba outbreaks/epidemics surveillance, control and response ni sayansi ngumu kweli kuliko unavyoitafsiri kwa lockdown.

Naomba nisikujibu tena kwenye hii hoja.

MM Togolani
 
vitu vingine ni common sense tu hauhitaji kufikiria mara mbili au kwenda maaabara!?? ? ….my dear kisayansi inawezekana kabisaa ku control ama kumonitor rate of infection ya coronavirus and statistics hazidanganyi na ndio sayansi ilipo….and yes lockdown itazuia wengi kuambukizwa au kufa...hili nalo hata sio la kufikiria mara mbili...ni kitu ambacho kinaweza kuwa proved kwa nyie wanasayansi!

Hilo la kufa, sijui mwenzetu umeamua kuwa tu blind,hivi huoni ulimwengu watu wanavyokufa kwa siku??..ngoja tusichukue measure za kujikinga and then tuone jinsi tulivyo na low resources kupambana na huu ugonjwa itakuwaje...kama infection ikisambaa?

MAJORITY vifo nilikua namaanisha..ukiruhusu free movements of people katika kipindi hiki,inamaanisha unawa expose wengi kwenye hii contagious disease, a lot will catch the virus and knowing how we have under resourced health care system, A LOT will die at one given time..kuacha wale FEW waliobaki nyumbani..conversley tukiweka lockdown Majority watabaki nyumbani na kupunguza kasi ya maambukizi,But this means wachache watakufa serving the larger population..ni hayo mkuu
Hao majority unaowasema wewe kila siku wanafundishwa juu ya sanitizers na masks, juu ya kuosha mikono kwa sekundi ishirini. Nadhani wanakifanyia kazi kivitendo kila wanachoelezwa na wataalam wa afya.

Total lockdown ni ngumu sana kwa mazingira ya afrika ambapo watu wanaishi maisha ya kutafuta riziki leo hii kesho ni vita nyingine mpya kabisa.

Marekani kuna watu milioni sita na laki sita wameshasema kwamba hawana kazi na hawana pato lolote sababu ya lockdown, watu wenye ajira zenye mshahara mdogo kama waosha mashuka wa mahotelini, wafagiaji na wapangaji wa bidhaa madukani ndio hao wanaolalamika umasikini kwa sasa.

Nchi za wenzetu wanazo akiba zenye kuwawezesha kuzitumia wakati wa majanga kama corona, afrika ukashinda nyumbani umelala njaa.
 
Hujaona makosa lukuki ya kiuandishi?Halafu kujiunga JF mapema sio sifa ya kunieleza hapa,wengine tulikuwa wasomaji tu na hatukuona haja ya kujisajili!Niko hapa jukwaani kitambo sana zaidi ya unavyofikiri!
Sasa mbona unawavamia watu tu hata pasipo kuwajua, ukifikiri wana ufahamu wa chini kama wewe...huyo ni Mwandishi wa Hotuba za Rais mstaafu mind you, ni Mtu ana akili kuliko wewe😀
 
My kaka, Italy haikuchukua hatua mwanzo..wengi wakawa infected , na sisi tusipochukua hatua ugonjwa ndio ushaingia hivyo ...tusisubiri wale wote walioambukizwa waambukize wengine..maambukizi yakishakua makubwa.ndio tuweke lockdown...hata pamoja na virus kuua wengi , hali ya Italy ime improve baada ya kuweka lockdown,hata Spain nao hali ni hivyo hivyo..yanayotokea duniani lazima yatu guide katika kufanya maamuzi..au ulikua unataka mpaka na sisi tusibiri coronavirus ku 'gain momentum' ??...ndio tuchukue hatua????lockdown haiepukiki..ku accept this is better than living in denial......Again Italy nadhani sababu hawakuchukua hatua mapema, wengi wakawa infected ,I believe hivi vifo tunavyoviona sasa hivivinatokana na hao walioambukizwa KABLA ya lockdown na sio NEW PATIENTS ….(what I believe). baada ya hawa watu walioambukizwa kabla ya lockdown kuisha,then tutaona improvement...kama wataendelea na lockdown though..kuzuia maambukizi mapya...

Halafu hizo 'news' zinatoka kwenye credible sources..lol..CORONA VIRUS being a novel subject..sidhani kuna RESEARCH nyingi..LOL..we do rely on 'news'..nisamehe kama nimekukwaza mahali bro...
 
True..... Dada umejitahidi kumueleza ukweli..... we don't need to have scientific research au data kujua kama lock down inasaidia kupunguza mambukizi mapya, ni logic tu naona kaka amengangania scientifical proof na data za ugonjwa ku support lock-down..........which is wrong hu ungonjwa inahitaji common sense na little medical knowledge kupambana nao, sio academic papers au research, hamna namna Tz will lock down with in this month no other alternative au tupate the worse

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Marais wastaafu wameshaiomba AU,WHO,World Bank kwa msaada ngoja tusubiri.Hata hivyo to me kumuomba tiba aliyekuchawia ni ajabu kidogo.

World Health Organization nao wameiandikia serikali kushauri what should be done.Hii nayo ni case ya mchawi kumshauri aliyemloga!Ni ajabu,but true.

Anyway,tusuburi response ya serikali.Hata hivyo haya mambo,sijui lockdown,social distancing,kufunga biashara etc.,yaana maana beyond what our eyes can see and apparently what we are able to comrehend.This is part of an agenda with long term goals. I wish we new.
 
Sasa mbona unawavamia watu tu hata pasipo kuwajua, ukifikiri wana ufahamu wa chini kama wewe...huyo ni Mwandishi wa Hotuba za Rais mstaafu mind you, ni Mtu ana akili kuliko wewe😀
Nashangaa mwandishi wa Rais hawezi kuandika kiswahili fasaha!
Inakuwaje anaandika kwa kurudiarudia "muna" badala ya "mna"?
 
Ndugu Tigershark.

Moja, nashukuru sana kwa kunikosoa. Ni kweli nasumbuka sana kuandika Kiswahili fasaha. Lengo la kuandika hapa ni kufikia watu walio wengi na kufikisha ujumbe kuliko usahihi/ufasaha wa lugha. Hivyo nitatumia Kiswahili hivyohivyo ninavyoweza. Hata hivyo nitajitahidi kujifunza na kusahihisha ninapokosea. Uandishi wa kutumia lugha fasaha unahitaji muda mrefu ambao kwa sasa sina kabisa. Unisaheme bure. Sisi tuliosoma namba muda mwingi tuliacha kujifunza Kiswahili tulipofanya mtihani wa mwisho wa kidato cha nne.

Pili, mimi sijawahi kuwa mwandishi wa Rais. Mimi sio Togolani Mavura aliyekua msaidizi wa Mh Kikwete hivyo musimuhusishe na makosa yangu ya uandishi. Mimi ni Mathew Togolani Mndeme. Sijawahi kufanya kazi ya uandishi. Kazi yangu ni kufundisha (ila sio soma la Kiswahili na Kiswahili sio lugha ya kufundishia).

Ubarikiwe.

MM togolani
 
Tigershark .. Ila rafiki yangu kuna uwezekano mkubwa ukawa na tatizo kubwa la ukosoaji usio na tija au una matatizo (reservations) binafsi na mwandishi. Dunia iko busy inajadili janga la Corona na namna ya kukabiliana nalo, ila kwako cha maana unachokiona (na kuona kinafaa kujadiliwa kwenye huu uzi) ni makosa ya uandishi pekee!!! Seriously!!!. Naona haujadili mada umeng'ang'ana na uandishi.

Naomba niwe nakutumia maandishi yangu unisahihishe kabla sijayaweka hapa maana inaonekana you are a qualified proofreader. Please.

MM Togolani
 
MUHTASARI:
Nchi nyingi duniani, hasa za Magharibi, zimetangaza karantini au “lockdown” inayowazuia wananchi kutoka ndani muda wote isipokua kutafuta mahitaji ya lazima tu (dawa na chakula). Hatua hii imechukuliwa na nchi ambazo maambukizi ya Covid-19 yamekua makubwa, sio kwa lengo la kuzuia watu wasipate maambuziki, bali zinalenga kupunguza kasi ya maambukizi kwa wakati mmoja ili mfumo wa utoaji huduma za afya usilemewe na kushindwa kuwahudumia wanaozidiwa. Lockdown haina muda maalum na itaendelea hadi mlipuko wa Covid-19 utakapoonekana umepungua au kwisha. Hivyo watu wengi hapa Tanzania nao wanaishauri serikali kufanya hivyo wakiamini ni hatua ya lazima kwa sasa na wanachukulia kutotangaza karantini mapema ni uzembe au ni kutokujali.

Katika makala hii, nimeeleza kwa nini sio sahihi kwa nchi yetu na nyingi za kiafrika kutangaza Lockdown. Pia nimeshauri kwa kusisitiza serikali isiwaze kabisa kuchukua hatua hii katika hatua hii hasa kwa sababu haitekelezeki kwenye mazingira yetu na hatujui mlipuko utachukua muda gani. Iwapo njia hii itatutumika, madhara yake kwa wananchi yanaweza kuwa makubwa kuliko yatokanayo na Covid-19. Nimeeleza hoja yangu kwa kutumia uzoefu binafsi wa kuwa kwenye karantini. Pia nimefananisha mazingira ya utekelezaji wa amri hii kwenye nchi za Magharibi na nchi zetu ili kuweka hoja yangu katika muktadha.Kwa undani zaidi soma makala nzima hapa chini.

View attachment 1406728

Utangulizi
Nianze ujumbe wangu kwa kutangaza maslahi binafsi. Hapa nilipo, hii ni wiki ya pili tunamaliza tukiwa chini ya “total lockdown”. Nchi nzima tunalazimika kukaa ndani muda na hatujui tutatoka lini. Sina hakika na watu wengine waliowahi kuishi mazingira ya aina hii, ila niseme kwa ujasiri kabisa kwamba mazingira haya ni mabaya, ni magumu, na yanaumiza sana kisaikolojia. Muda mwingi huwezi kufanya lolote la maana kwa kuwa unakua kama umepoteza "network". Mtu asiombe kabisa kukosa uhuru wa kutoka ndani. Ninapingana kwa 100% na kila ambaye anaishawishi, anaishauri, au anailazimisha serikali kutangaza karantine kama nchi nyingine au anailaumu kwa kutokufanya hivyo.

Nini msingi wa hoja yangu?
Labda nieleze kwa kifupi nini maana ya kuwa kwenye karantini katika uhalisia ili kuweka ninachoongea kwenye muktadha:
  1. Wazazi, watoto na munaoishi nao munashinda mukiwa mumejifungia ndani: usiku unakuja, asubuhi inafika, munaaendelea na zoezi kama jana. Mbaya zaidi hamujui zoezi hili litakwisha lini. Wakati mwingine munasahau siku au tarehe maana hakuna matukio yanayowakumbusha. Serikali inasema inaweza kuwa hivi hadi miezi 6.

  2. Haijalishi munakokuita nyumbani au ndani kukoje kwa maana ya ukubwa/udogo, ubaya/uzuri na kuna nini cha kufurahisha au kufanya: munazunguka humohumo mchana na usiku.

  3. Munatoka ndani mara moja au mbili kwa wiki kwenda kutafuta mahitaji ya lazima. Na mahitaji ya lazima ni chakula na madawa maana maduka ya mahitaji mengine yamefungwa. Munashauriwa kama inawezekana muagize vyakula online.

  4. Wakati mwingine vitu vya lazima hakuna madukani/supermarkets maana kutokana na hofu, watu wananunua kwa wingi hivyo vinakwisha.

  5. Ukifika supermarket mupanga foleni ndefu ya kuingia ndani kwa vile munatakiwa muwe umbali wa mita 2 kati ya mtu na mtu na hamutakiwi kuingia wengi kwa wakati mmoja ili musisongamane. Unaweza kufika ndani unakosa unachotaka.

  6. Kwa anayeweza, munaruhusiwa kutoka nje mara moja kwa siku kufanya zoezi moja (kutembea au kukimbia) na uwe mwenyewe au na mtu wa familia yako maana hakuna kukutana zaidi ya watu wawili.

  7. Makazi mengi hayana viwanja vya nje kama kwetu Afrika maana nyumba zimejengwa kwa mipango na kubana nafasi. Mara nyingi, nje ya mlango ni bararaba ya mtaa.

  8. Sheria imepitishwa na bunge kwamba ukikamatwa kwenye mkusanyiko au unazurura unaweza kutozwa faini na polisi ya hadi milioni tatu za Tanzania (zile faini za papo kwa hapo kama za makosa ya barabarani)
Unajua kwa nini wanaweza kufanya haya?
Wenzetu wanapochukua hatua hizi za kukaa ndani ni kwa sababu mazingira yao yanaruhusu ya yameandaliwa hivyo. Kwa mfano:
  1. Wao kukaa ndani sio jambo geni. Maisha yao kwa sehemu kubwa ni ya kibinafsi. Watu wanakaa ndani muda mwingi maana yale maisha ya kijamaa/kijamii wameyaacha. Munaweza kuiishi milango imetazamana na jirani zako lakini musisalimiane hata munapogongana mukitoka au kuingia ndani. Unaweza usimjue jirani yako munayetazamana au kutengwa na ukuta kua ni nani, anafanya nini, nk. Huku ndiko tumeiga msemo wa “mind your own business” na “I don’t care what yu think about me” na tunadhani ni maendeleo.

  2. Nchi za Ulaya zina msimu wa baridi kuanzia mwezi wa 10 na wa 11 hadi mwishoni mwa mwezi wa tatu. Kipindi hiki hali ya hewa inaweza kua mbaya muda mwingi sababu ya upepo mkali, mvua nyingi, baridi ni kali, na kunaweza kuwa na barafu. Giza linakua muda mrefu kuliko mchana. Kuna kipindi linaanza kuingia saa tisa jioni na linaendelea hadi kesho yake saa mbili asubuhi. Hivyo mchana kwa maana ya mwanga unaweza kuwa kama masaa 6 hadi 8 tu. Kwa jumla, mazingira hayaruhusu kukaa nje wala kutembea hivyo kama mtu hana anapolazimika kwenda basi muda mwingi ni kukaa ndani.

  3. Nyumba za wenzetu hazijengwi kienyeji kama sisi ambapo kila mtu anajijengea atakavyo na atakapo. Nyumba zinajengwa na makampuni au na serikali kwa mipango na viwango maalumu. Kutokana na hali ya hewa ya baridi na majanga kama vimbunga, nyumba zinajengwa zikiwa na uwezo wa kustahimili baridi na upepo mkali. Madirisha yana vioo viwili; ukuta wa nyumba una kuta mbili na katikati unajazwa vitu vya kupunguza hewa ya baridi; paa linadhibitiwa kiasi kwamba mvu akinyesha unaweza usijue iwapo hujatazama nje.

  4. Kila nyumba ina maji yasiyokatika; ina bomba la gesi linaloingia ndani kama maji; ina umeme wa uhakika usiokatika. Nyumba zisizo na mabomba ya gesi basi umeme ndio unatumika kupikia na kwenye mifumo ya kupasha maji na nyumba joto.

  5. Kila nyumba inapojengwa, inaingiziwa waya (connection) ya TV, simu ya landline na internet. Huduma hizi ni za uhakika kwa kila nyumba labda uwe tu huwezi kulipia bills. Internet ni rahisi sana hivyo kwa gharama ambayo hapa kwetu mtu anatumia kununua bando la GB kama ya 20, kwao unapata internet ya kutumia vifaa zaidi ya kumi kwa wakati mmoja (simu, computers, smart tv, tablets) usiku na mchana mwezi mzima mukifanya kila munachotaka kwenye internet bila kupimiwa.

  6. Huduma za maji, umeme, internet, gesi, simu, tv hazikatiki na hazikatwi kienyeji hata ukishindwa kulipa bills. Tarehe ya kulipia ikifika huna pesa kwenye akaunti utafutatiliwa na kukumbushwa kwanza kwa muda ingawa ukichelewa sana utapigwa faini ya kukuumiza.

  7. Unaweza kuagiza KITU CHOCHOTE online (kwa kupiga simu au internet) na kikaletwa hadi mlangoni iwe dawa, chakula, nguo, viatu, mashuka, vinywaji, nk.

  8. Ukiiumwa unawasiliana na daktari kituo cha afya uliposajiliwa kabla ya uamuzi wa kwenda iwapo sio matatizo ya dharura. Matatizo yote ya dharura ukipiga simu ndani ya dakika chache ambulance iko mlangoni na ukichelewa kufungua wanaweza kuvunja mlango wakaingia wakidhani umezidiwa.

  9. Ukipata tatizo kama kupigwa na mke au mume, kuingiliwa na wezi, au mtoto kupigwa na mzazi; ukipiga simu ndani ya dakika chache polisi wako mlangoni.
Haya ndio mazingira ya wenzetu yanayowaruhusu kutangaza TOTAL LOCKDOWN au KARANTINI kirahisi kama vile wanatangaza mshahara kupanda. Wanaposema watu wakae ndani wasitoke, wana hakika kwa zaidi ya 95% mazingira ya kila mtu yanamruhusu kukaa ndani na akaishi bila matatizo makubwa. Pia, kwa kuwa wana mifumo inayofanya kazi na makazi yamepangika, kwa sehemu kubwa wanajua kila mtu anayefanya kazi (binafsi au kijiajiri), kipato chake, na anaishi wapi. Hivyo serikali wanaweza kutangaza kutoa ruzuku za kuishi kwa kiwango fulani kwa kila raia au mfanyakazi kipindi hiki cha mlipuko na watu wakazipata bila mizengwe.

Sasa linganisha mazingira haya yao nay a kwetu.
  1. Sisi wananchi wengi hawana uwezo wa kununua chakula cha kesho. Inamlazimu mtu kutoka ndani kila siku ili angalau aweze kuweka mlo mezani.

  2. Sisi tumezoea kwenda dukani/sokoni kila siku au mara kadhaa kwa wiki kununua kila kitu kidogokigogo: tubamia, kaunga, tudagaa, tunyanya, tuvitunguu, tumchicha, nk.

  3. Sisi tuna familia nyingi hazijui umeme ni nini. Hata walionao, hauna uhakika wa kuwaka kila siku. Kwa wenzetu umeme kukatika kwenye nyumba kwa nusu dakika tu ni moja ya miujiza kwa mwaka labda kuwe na majanga kama vimbunga, mafuriko, nk.

  4. Sisi watu wengi hawana maji ya bomba ndani. Wengi inawalazimu kila siku kwenda kuteka maji mtoni, bombani, kisimani, chemchem, bwawani au hata kuomba kwa jirani mwenye uwezo. Wengi inawalazimu kutembea umbali mrefu kupata maji.

  5. Makazi yetu hayana anuani za kueleweka hivyo hatuwezi kuwa na huduma za kununua vitu online na kushushiwa nyumbani hata kama tukitaka.

  6. Wengi wetu tunaishi kwenye nyumba mbovu, mbaya, hazina mvuto, na wengine ni ndogo sana ukilinganisha na ukubwa wa familia. Pia wote nchi nzima tunaishi na mifugo kadhaa ndani ya nyumba. Kama sio mbuzi, kuku, kondoo au ng’ombe, basi tunaishi na mende, panya, viroboto, nzi na mbu.

  7. Hatuna maduka makubwa (supermarkets) kila mahali karibu na watu ambapo utasema watapata mahitaji ya lazima kwa urahisi wakiwa kwenye karantini. Wengi hutembea au kusafiri mbali kununua chakula madukani au sokoni

  8. Wananchi wengi wanatumia mkaa, kuni au mafuta ya taa kupikia. Wengine wakitaka kuwasha moto lazima wakaombe kiberiti au kaa la moto kwa jirani.

  9. Wengi wetu hatuna vyoo vya ndani na vya nje havitamaniki.
Sasa niambie, serikali ikitangaza karantini ya kumtaka kila mtu akae ndani na asichangamane hata na jirani yake tutaishije kwenye mazingira haya? Tutaweza kuishi hivyo hata kwa wiki moja? Na kama tukilazimika kwa kiboko kama kule Kenya, unadhani ni madhara kiasi gani tutapata?

Mwisho
Msukumo wa kuishauri serikali kutangaza total lockdown, kama ilivyo kwa misukumo mingine kwenye janga hili, inatoka kwa kundi dogo la watu wenye uwezo (middle class). Duniani kote kundi hili hujisahau na kudhani kila mtu ana maisha kama yao. Lina kiwango kikubwa sana cha ubinafsi na wakati mwingine wanasahau kabisa kwamba hata ndugu zao wa karibu hawana uwezo walionao wao. Lakini ukweli ni kwamba kwa watanzania walio wengi karantini ya kututaka kukaa ndani ni janga kubwa mara nyingi kuliko Covid-19. Wanaoshawishi hatua hii wakumbuke kwanza kijijini kwao walikotoka wao au wazazi wao kukoje kabla hawajashauri total lockdown.

Serikali ichukue kila tahadhari na hatua wanazoshauriwa na wataalamu kuhusu kuzuia au kupunguza maambukizi ya Covid-19. Tusikilize wataalamu ni kwa jinsi gani tunaweza kuwakinga watu ambao wakipata maambukizi watadhuruka zaidi (wazee, wenye magonjwa ya kupua, na wenye chronic diseases). Ila isikubali wala kusikiliza ushawishi wa mtu, watu, taasisi, au nchi yoyote kuilazimisha kutangaza karantini katika hatua ya sasa.

Karantini ya kuwataka watu kukaa nyumbani (tena kwa muda usiojulikana) ni njia isiyofaa kwa wananchi wetu. Itakua na madhara makubwa sana kiafya, kijamii, na kimaisha iwapo itachukuliwa katika hatua hii. ndio tuko mwanzoni kabisa mwa maambukizi na hatuna hata mgonjwa mmoja aliye na hali mbaya. Kutangaza lockdown itakua ni sawa na kumkimbia mbwa kwa kuingia kwenye zoo walipo simba na chui huku ukidhani unatafuta kinga.

Kwa ngazi ya maambukizi tuliyopo sisi (ukilinganisha na nchi zilizoathirika sana na tabia ya mlipuko), bado tunaweza kuwa na maambukizi hadi miezi 5 au 6 kuanzia sasa. Njia ya lockdown naweza kusaidia kama suluhisho la mwisho kabisa wakati maambukizi yamezidi uwezo wa kukabiliana nayo: kwa maana ya kwamba watu wengi walioambukizwa watakua na hali mbaya kiafya (critical conditions). Ikifika hatua hiyo, mlipuko utakua umefika kileleni na kukaribia kushuka hivyo muda wa watu kukaa ndani utakua ni mfupi na madhara yatakua kidogo. Kitu cha kushauri serikali kwa sasa ni namna ya kuandaa mikakati ya nini cha kufanya iwapo tutalazimika kufikia hatua hiyo (worse case scenario). Ukiweka watu ndani sasa wakati hujui utawaweka kwa muda gani na huna uwezo wa kuwahudumia, madhara yake ni makubwa sana.

Pia tukumbuke sio lazima kila nchi ifikie hatua ya kua na vifo vingi kama tunavyoona Italy, Spain na kwingine. Ni makosa kuchukulia kinachotokea kwenye nchi hizo kama kielelezo na sababu ya kujengea hofu na taharuki katika kufanya maamuzi.

MM Togolani ([email protected])
Mwathirika wa "Total Lockdown"

------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
Ziada na hitimisho
Kwenye uzi huu nimefafanua na nimejibu hoja kinzani na maswali ya wachangiaji kadiri nilivyoweza. Kwa kufanya hivyo nimefafanua mambo mengine ambayo sikuyataja kwenye makala yangu. Kwa ujumla ninaweza kuhitimisha hoja namaswali yao kama ifuatavyo:

Nikisoma maoni, matusi, maonyo, hofu na taahadhari ya waotamani serikali itangaze total lockdown, hakuna hata mmoja anayetoa suluhisho au mbinu ya utekelezaje wake. Hakuna anayetoa data yoyote kiuchumi, kijamii, afya, nk. Hawatuambii watanzania wasio na maji, ajira, umeme, nk ambao wataathirika kuanzia siku ya kwanza ni asilimia ngapi na watasidikaje. Hoja yao ni moja tu, HOFU na watu wengi watakufa tusipotangaza Lockdown sasa. Hakuna scientific argument yoyote wanayotoa yenye ushawishi au theory and practices za crisis management or outbreaks control/response.

Kauli zao zinaonesha kifo kinachotisha ni cha Corona pekee. Vifo vitokanavyo na njaa, malaria, kipindupindu, kuhara, na utapiamlo (baadhi ya maradhi ambayo yatakumba wengi kukiwa na lockdown ya muda mrefu) havitishi wala sio tatizo. Tatizo ni Corona tu kwa madai kwamba tutakufa kama Italy na Spain. Wakati hofu hizi ni za msingi ila hazitakiwi kuwa msingi wa maamuzi na kufikiria kwetu.

Watu hawa hawaelevi bado inamaanisha nini hasa kuwa kwenye total lockdown. Hawatazami multiplying effect ya lockdown. Hawaelewi makampuni mengi yatafungwa na wafanyakazi watapoteza kazi. Hakuna mwajiri ataendelea kulipa mshahara watu wasiofanya kazi na yeye hazalishi. Hata makampuni yatakayooperate yatapunguza wafanyakazi kwa sehemu kubwa maana hakuna biashara. Nimeongea na wafanyakazi kadhaa wa sekta ya utalii wako majumbani hawana kazi na hawajui kazi itarejea lini. Waliobahatika kubaki na ajira wengine wameahidiwa wanalipwa nusu ya mshahara kwa miezi 3 au 5 wakati kisha maamuzi mengine yatafuata.

Kinachotokea na kitakachotokea zaidi, uwezo wa serikali kukusanya kodi utakua mdogo maana hakuna biashara; uzalishaji unapungua; PAYE itapungua maana watu wamepoteza kazi. Nchi yetu bado inategemea makusanyo ya kila mwezi kugharamia mahitaji muhim ya nchi kama kulipa wafanyakazi, kununua madawa, ulinzi na usalama, na kazi za utawala wa nchi.

Hivyo unapoishauri serikali kukimbilia total lockdown sasa na kwa muda usiojulikana (maana ndio tuko asubuhi mwa mlipuko), tuiambie pia itaendeshaje nchi. Kama hatuelewi complexity ya lockdown basi tuendelee tu kuisilikiliza kwenye vyombo vya habari kuliko kujiona sisi ni wataalamu wa utekelezahi wa total lockdown. Nirudie tena, huwezi kukimbia kung'atwa na mbwa (Corona) kwa kukimbilia walipo chui na simba (madhara ya total lockdown).

Namishukuruni waliosoma, waliochangia, waliokosoa, waliosahihisha, walioniita mjinga, na hata walionitukana. Wote wametumia uhuru weo kadiri ilivyowapendeza. Bado kuna mambo mengi ya muhim ya kuchambua na kujadili kuhusu Covid-19.

Mubarikiwe.

MM Togolani.
Tukianza kupukutika kama kuku wenye kideli naomba pandisha huu uzi
 
Kua na hakika kwamba hatutakufa kama kuku. Hata tukiugua wote, tuna hakika (from existing evidence) wengi watapona.

Pili, huu uzi utabaki hapa labda JF waamua kuushusha. Matokeo yoyote yatakayotokea, hayabadili ukweli kwamba lockdown is an impractical solution in our setting and imposing it at the onset of the outbreak is an irrelevant and illogical decision. Mark may my position on this matter for future references.

MM Togolani
 
Tigershark .. Ila rafiki yangu kuna uwezekano mkubwa ukawa na tatizo kubwa la ukosoaji usio na tija au una matatizo (reservations) binafsi na mwandishi. Dunia iko busy inajadili janga la Corona na namna ya kukabiliana nalo, ila kwako cha maana unachokiona (na kuona kinafaa kujadiliwa kwenye huu uzi) ni makosa ya uandishi pekee!!! Seriously!!!. Naona haujadili mada umeng'ang'ana na uandishi.

Naomba niwe nakutumia maandishi yangu unisahihishe kabla sijayaweka hapa maana inaonekana you are a qualified proofreader. Please.

MM Togolani
I am drunk,nitarespond kesho plz
 
Ndugu Tigershark.

Moja, nashukuru sana kwa kunikosoa. Ni kweli nasumbuka sana kuandika Kiswahili fasaha. Lengo la kuandika hapa ni kufikia watu walio wengi na kufikisha ujumbe kuliko usahihi/ufasaha wa lugha. Hivyo nitatumia Kiswahili hivyohivyo ninavyoweza. Hata hivyo nitajitahidi kujifunza na kusahihisha ninapokosea. Uandishi wa kutumia lugha fasaha unahitaji muda mrefu ambao kwa sasa sina kabisa. Unisaheme bure. Sisi tuliosoma namba muda mwingi tuliacha kujifunza Kiswahili tulipofanya mtihani wa mwisho wa kidato cha nne.

Pili, mimi sijawahi kuwa mwandishi wa Rais. Mimi sio Togolani Mavura aliyekua msaidizi wa Mh Kikwete hivyo musimuhusishe na makosa yangu ya uandishi. Mimi ni Mathew Togolani Mndeme. Sijawahi kufanya kazi ya uandishi. Kazi yangu ni kufundisha (ila sio soma la Kiswahili na Kiswahili sio lugha ya kufundishia).

Ubarikiwe.

MM togolani
Nitajihu kesho,ok?
 
Back
Top Bottom