Serikali isikubali kutangaza “total lockdown” au Karantini. Wanaoishawishi ama hawajui wanachokishauri au ni wabinafsi

Soma bandiko lako kisha usome bandiko nililoandika kufuatia lako, utaelewa tu bila shaka.
Sijaelewa hizo aya zako za chini zina uhusiano gani na post yangu... Ila ngoja nikujibu zile zinazohusiana; lockdown inategemea idadi ya maambukizi ya nchi husika pamoja na kasi ya maambukizi ya hiyo nchi...Totally lockdown sio mkumbo,inaenda na uhalisia.. Wewe unapiga kelele sababu upo bongo,hujui yanayoendelea huko nje... Tembelea forum za hizo nchi zilizo ktk total lockdown ulinganishe na hali hiyo ikiwa tz ndo upate uhalisia.., sio kuleta mambo ya trump,sijui hata kaingiaje hapa.
 
Mkuu si nia yangu kupigishana kelele na wewe.

Kaza uzi hapo hapo jiaminishe uko vizuri. Kwani taabu iko wapi?
 
Nakuunga mkono mkuu. Serikali haijazuia 'personal or family lock down', anayeweza kujifungia ajifungie sisi wengine tuendele na mambo yetu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hawana lolote!! Ukiwasikiliza utadhania wana huruma sana na maskini, kumbe wana yao, ili kuja kufaidika na tabu watakazo kuwa wanapata masikini, wakati wa total lock down!!
 
Nimegundua kuwa wimbi la wasiojua kuandika kwa ufasaha JF limeongezeka sana,yaani wamekuja upesi kama dhoruba!Sijui tatizo ni nini?Hasahasa tatizo hili lipo hasa kwa wale wafa na tai shingoni!
Huyu unayesema hajui kuandika alikuwa Mwandishi wa Hotuba wa Rais Kikwete, akiachiwa kazi hiyo na January Makamba...

So fikiri kabla ya kusema, yawezekana aliyoyaandika yanazidi upeo wa akili zako, Pole sana!

Finally, Linganisha muda MM Togolani aliojiunga JF(2010) na muda wako Wewe, Then uweke hoja zako chini tujadili
 
Mkuu si nia yangu kupigishana kelele na wewe.

Kaza uzi hapo hapo jiaminishe uko vizuri. Kwani taabu iko wapi?
Endelea kupingana na uhalisia...Namba zikipanda unafikir haitakuja? Itakuja tu...Na ndo utaona hicho unachokililia kije kana kwamba ni burudani hivi... Siku njema.
 
Uko sawa kabisa.

Ila jiulize maswali. Lengo la Lockdown ni kitu gani? Bila shaka utaniambia ni kuzuia maambukizi watu wengi wasiugue na baadhi yao wakafa (maana tunajua sehemu kubwa ya wanaougua wanapona). Sasa ni asilimia ngapi ya watanzania wanaweza kubaki ndani wakiwa hawana chakula wala maji kwa hata wiki moja wakaishi? Itasidia nini kukimbia m

Nadhani hili ni jukumu la msomaji. What do you think?
Sitetei uwepo wa lockdown... Umenisoma vibaya nadhani.
 
Ajifunze kuandika vizuri!Ushauri wangu kwenye Corona ni huu mara zote kwa watu kama hawa,tuombe Mungu sana Corona isienee nchini maana tutaisha kama kuku!
Bado naona serikali inafanya mchezo na Corona,tunaona watu bado wanakusanyika vituo vya mabasi,tunaona Makonda bado anakusanya watu na kuwahutubia,level seat bado sio suluhisho maana distance kati ya mtu na mtu ni Zero distance nk!
Kwa mazingira kama hayo,ni kuomba muujiza tu ndio utuokoe!
Hao walioamua total lockdown wana sababu zao,huenda wamepiga hesabu wakaona ni heri wachache wafe wengi wapome,kupanga ni kuchagua!

Uko sawa kabisa.

Ila jiulize maswali. Lengo la Lockdown ni kitu gani? Bila shaka utaniambia ni kuzuia maambukizi watu wengi wasiugue na baadhi yao wakafa (maana tunajua sehemu kubwa ya wanaougua wanapona). Sasa ni asilimia ngapi ya watanzania wanaweza kubaki ndani wakiwa hawana chakula wala maji kwa hata wiki moja wakaishi? Itasidia nini kukimbia maambukizi ya Covid-19 halafu watu wakafa na njaa, utapiamlo, na magonjwa mengine kama kipindupindu, malaria na kuhara? Utakua umeokoa nini na kupunguza nini?

Mimi siesemei serikali wala sijasema viongozi wasichukue tahadhari nyingine za kitaalamu wanazopewa. Nimezungumzia jambo moja tu kwamb Lockdown haifai kwa nchi yetu kwa sasa. Inaweza kuwa worse case scenario tutakapoona tumezidiwa na hakuna namna. Wakati huo athari ya kukaa ndani itakua ya muda mfupi na tumejiadhaa nayo. Hata hivyo sio lazima kila nchi ifikie walipo Italy na Spain.

La uandishi nakuachia maana kama ungeona hakuna cha maana usingesoma
 
Kenya wako njia moja kwenda total lockdown. Watakapokwenda total lockdown utakuja hapa kufuta bandiko lako?

South Africa na Rwanda wako on total lockdown. Rwanda kaongeza siku 15 baada ya 14 za kwanza kwisha. Je hawa ndiyo wajinga sana na hawajui walitendalo.

Nadhani tatizo ni kushindwa kuelewa nature ya mlipuko kwenye huu ugonjwa. Ukiielewa vyema utatambua ugonjwa ukishaingia only way out for now ni total lockdown (pekee).

Tokea waathirika 200,000 jana, leo waathirika ni zaidi ya 1,000,000. Endeleeni kujidanganya kuwa nyie mna ufumbuzi usio na maumivu.

Wakuu hamna haja ya kuchukiana huo ndiyo ukweli mchungu.

Anasema Angel Merkel na pia Trump, changamoto za corona hazijawahi onekana tangu world war 2. Hali kadhalika kuutokomeza kwake hakuta kosa maumivu kweli kweli.

Ni rahisi zaidi kusalimu amri na kutoweka kwa huu ugonjwa au kupambana na ku survive. Uchaguzi ni wetu kama taifa.

Ina fahamika kwa nini ufumbuzi hauwezi kuwa wa mtu mmoja mmoja.

'Fools die'.

Uko sawa kwenda dhana ya nature ya ugonjwa. Ila nasita kukubaliana nawe kwamba uwezo wetu wa kufikiri na kufanya maamuzi yanayotufaa unategemea nchi nyingine kama ulizozitaja zimefanya nini.

Ila jiulize maswali. Lengo la Lockdown ni kitu gani? Bila shaka utaniambia ni kuzuia maambukizi watu wengi wasiugue na baadhi yao wakafa (maana tunajua sehemu kubwa ya wanaougua wanapona). Sasa ni asilimia ngapi ya watanzania wanaweza kubaki ndani wakiwa hawana chakula wala maji kwa hata wiki moja wakaishi? Itasidia nini kukimbia maambukizi ya Covid-19 halafu watu wakafa na njaa, utapiamlo, na magonjwa mengine kama kipindupindu, malaria na kuhara? Utakua umeokoa nini na kupunguza nini?

Ok, tuchukulie lockdown ni lazima kwa sasa. Tusaidie kutuambia itachukua muda gani kukaa ndani (maana hatujui kilele cha maambukizi kitafika lini). Tuambie mamilioni ya watanzania wasio na kazi au akiba ya chakula wataishije kwa kukaa ndani. Tuambie wanaotegemea kutembea kms kadhaa wakachote maji, kuni, mkaan nk watayapata wapi.
 
MUHTASARI:
Nchi nyingi duniani, hasa za Magharibi, zimetangaza karantini au “lockdown” inayowazuia wanachi kutoka ndani muda wote isipokua kutafuta mahitaji ya lazima tu (dawa na chakula). Hatua hii imechukuliwa na nchi ambazo maambukizi ya Covid-19 yamekua makubwa, sio kwa lengo la kuzuia watu wasipate maambuziki, bali zinalenga kupunguza kasi ya maambukizi kwa wakti mmoja ili mfumo wa utoaji huduma za afya usilemewe zaidi. Hali hiyo haina muda maalum na itaendelea hadi mlipuko wa Covid-19 utakapoonekana umepungua au kwisha. Hivyo watu wengi hapa kwetu nao wanaishauri serikali kufanya hivyo wakiamini ni hatua ya lazima kwa sasa na wanachukulia kutotangaza karantini mapema ni uzembe au ni kutokujali.

Katika makala hii, nimeeleza kwa nini sio sahihi kwa nchi yetu na nyingi za kiafrika kufanya hivyo. Pia ninashauri kwa kusisitiza serikali isiwaze kabisa kuchukua hatua hii sababu haifai na haitekelezeki kwenye mazingira yetu. Iwapo njia hii itatutumika, madhara yake kwa wananchi yanaweza kuwa makubwa kuliko tatizo linaloepukwa. Nimeeleza hoja yangu kwa kutumia uzoefu binafsi wa kuwa kwenye karantini na kufananisha mazingira ya utekelezaji wa amri hii kwenye nchi za Magharibi unapolinganisha na nchi zetu. Kwa undani zaidi soma makala nzima hapa chini.

View attachment 1406728

Utangulizi
Nianze ujumbe wangu kwa kutangaza maslahi binafsi. Hapa nilipo, hii ni wiki ya pili tunamaliza tukiwa chini ya “total lockdown”. Nchi nzima tunalazimika kukaa ndani tu na hatujui tutatoka lini. Sina hakika na watu wengine waliowahi kuishi mazingira ya aina hii, ila niseme kwa ujasiri kabisa kwamba mazingira haya ni mabaya, ni magumu, na yanaumiza sana kisaikolojia. Muda mwingi huwezi kufanya lolote la maana kwa kuwa unakua kama umepoteza "network". Mtu asiombe kabisa kukosa uhuru wa kutoka ndani.

Kwa nini nashauri hili?
Kwa sababu hizi na kwa hoja nitakazozieleza hapa, ninapingana kwa 100% na kila ambaye anaishawishi, anaishauri, au anailazimisha serikali kutangaza karantine kama nchi nyingine au anailaumu kwa kutokufanya hivyo. Labda nieleze kwa kifupi nini maana ya kuwa kwenye karantini katika uhalisia ili kuweka ninachoongea kwenye muktadha:
  1. Wazazi, watoto na munaoishi nao munashinda mukiwa mumejifungia ndani: usiku unakuja, asubuhi inafika, munaaendelea na zoezi kam ajana. Mbaya zaidi hamujui zoezi hili litakwisha lini. Wakati mwingine munasahau siku au tarehe maana hakuna matukio yanayowakumbusha. Serikali inasema inaweza kuwa hivi hadi miezi 6.

  2. Haijalishi mukakokuita nyumbani au ndani kukoje kwa maana ya ukubwa/udogo, ubaya/uzuri na kuna nini cha kufurahisha au kufanya: munazunguka humohumo mchana na usiku.

  3. Munatoka ndani mara moja au mbili kwa wiki kwenda kutafuta mahitaji ya lazima. Na mahitaji ya lazima ni chakula na mdawa pekee maana maduka mengine yote yasiyo ya chakula na madawa yamefungwa. Munashauriwa kufanya hivyo inapokua ni lazima lakini kama inawezekana muagize online.

  4. Wakati mwingine vitu vya lazima hakuna madukani au supermarkets maana watu wananunua kwa wingi kwa hofu hivyo vinakwisha.

  5. Ukifika supermarket mupanga foleni ndefu ya kuingia ndani kwa vile munatakiwa muwe umbali wa mita 2 kati ya mtu na mtu na hamutakiwi kuingia wengi kwa wakati mmoja ili musisongamane. Na unaweza kufiuka ndani unakosa unachotaka.

  6. Kwa anayeweza, munaruhusiwa kutoka nje mara moja kwa siku kufanya zoezi moja (kutembea au kukimbia) na uwe mwenyewe au na mtu wa familia yako maana hakuna kukutana zaidi ya watu wawili.

  7. Makazi mengi hayana viwanja vya nje kama kwetu Afrika maana nyumba zimejengwa kwa mipango na kubana nafasi. Mara nyingi, nje ya mlango ni bararaba ya mtaa.

  8. Sheria imepitishwa na bunge kwamba ukikamatwa kwenye mkusanyiko au unazurura unaweza kutozwa faini na polisi ya hadi milioni tatu za Tanzania (zile faini za papo kwa hapo kama za makosa ya barabarani)
Unajua kwa nini wanaweza kufanya haya?
Wenzetu wanapochukua hatua hizi za kukaa ndani ni kwa sababu mazingira yao yanaruhusu ya yameandaliwa hivyo. Kwa mfano:
  1. Wao kukaa ndani sio jambo geni. Maisha yao kwa sehemu kubwa ni ya kibinafsi. Watu wanakaa ndani muda mwingi maana yale maisha ya kijamaa/kijamii wameyaacha. Munaweza kuiishi milango imetazamana na jirani zako lakini musisalimiane hata munapogongana mukitoka au kuingia ndani. Unaweza usimjue jirani yako munayetazamana au kutengwa na ukuta ni nani, anafanya nini, nk. Huku ndiko tumeiga msemo wa “mind your own business” na “I don’t care what yu think of me” na tunadhani ni maendeleo.

  2. Nchi za Ulaya zina msimu wa baridi kuanzia mwezi wa 10 na wa 11 hadi mwishoni mwa mwezi wa tatu. Kipindi hiki hali ya hewa inaweza kua mbaya muda mwingi na baridi ni kali sana. Giza linakua muda mrefu kuliko mchana. Kuna kipindi linaanza kuingia saa tisa jioni na linaendelea hadi saa mbili asubuhi Kesho yake. Hivyo mchana kwa maana ya mwanga unaweza kuwa kama masaa 6 hadi 8 tu. Mvua na barafu huweza kuwepo kwa wingi pia. Kwa jumla, mazingira hayaruhusu kukaa nje wala kutembea hivyo kama mtu hana anapolazimika kwenda basi muda mwingi ni kukaa ndani.

  3. Nyumba za wenzetu hazijengwi kienyeji kama sisi ambapo kila mtu anajijengea atakavyo na atakapo. Nyumba zinajengwa na makampuni na serikali kwa mipango na viwango maalumu. Kutokana na hali ya hewa ya baridi na majanga kama vimbunga, zinajengwa zikiwa na uwezo wa kustahimili baridi na upepo mkali. Madirisha yana vioo viwili; ukuta wa nyumba una leya mbuli na katikati unajazwa vitu vya kupunguza hewa ya baridi; paa linadhibitiwa kiasi kwamba mvu akinyesha unaweza usijue kama hujatazama nje.

  4. Kila nyumba ina maji yasiyokatika; ina bomba la gesi linaloingia ndani kama maji isiyokatika; ina umeme wa uhakika usiokatika. Nyumba zisizo na mabomba ya gesi basi umeme ndio unatumika kupikia na kwenye mifumo ya kupasha maji na nyumba joto.

  5. Kila nyumba inaijengwa, inaingiziwa waya (connection) ya TV, simu ya landline na internet. Huduma hizi ni za uhakika kwa kila nyumba labda uwe tu huwezi kulipia bills. Internet ni rahisi sana hivyo kwa gharama ambayo hapa kwetu mtu anatumia kununua bando la GB kama ya 20, kwao unapata internet ya kutumia vifaa zaidi ya kumi kwa wakati mmoja (simu, computers, smart tv, tablets) usiku na mchana mwezi mzima mukifanya kila munachotaka kwenye internet bila kupimiwa.

  6. Huduma za maji, umeme, internet, gesi, simu, tv hazikatiki na hazikatwi kienyeji hata ukishindwa kulipa bills. Tarehe ya kulipia ikifika huna pesa kwenye kwenye akaunti utafutatiliwa na kukumbushwa kwanza kwa muda ingawa ukichelewa sana utapigwa faini ya kukuumiza.

  7. Unaweza kuagiza KITU CHOCHOTE online (kwa kupiga simu au internet) na kikaletwa hadi mlangoni iwe dawa, chakula, nguo, viatu, mashuka, vinywaji, nk.

  8. Ukiiumwa unawasiliana na daktari kituo cha afya uliposajiliwa kabla ya uamuzi wakwenda hospitali kama sio matatizo ya dharura. Matatizo yote ya dharura ukipiga simu ndani ya dakika chache ambulance iko mlangoni na ukichelewa kufungua wanaweza kuvunja mlango wakaingia wakidhani umezidiwa.

  9. Ukipata tatizo kama kupigwa na mwenza, kuingiliwa na wezi, au mtoto kupigwa na mzazi; ukipiga simu ndani ya dakika chache polisi wako mlangoni.
Haya ndio mazingira ya wenzetu yanayowaruhusu kutangaza TOTAL LOCKDOWN au KARANTINI kirahisi kama vile wanatangaza mshahara kupanda. Wanaposema watu wakae ndani wasitoke, wana hakika kwa zaidi ya 95% mazingira ya kila mtu yanamruhusu kukaa ndani na akaishi bila matatizo makubwa. Pia, kwa kuwa wana mifumo inayofanya kazi na makazi yamepangika, kwa sehemu kubwa wanajua kila mtu anayefanya kazi (binafsi au kijiajiri), kipato chake, na anaishi wapi. Hivyo serikali wanaweza kutangaza kutoa ruzuku za kuishi kwa kiwango fulani kwa kila raia au mfanyakazi huu muda wa mlipuko na wakazipata bila mizengwe.

Sasa linganisha mazingira haya yao nay a kwetu.
  1. Sisi wananchi wengi hawana uwezo wa kununua chakula cha kesho. Inamlazimu mtu kutoka ndani kila siku ili angalau aweze kuweka mlo mezani.

  2. Sisi tumezoea kwenda duknai/sokoni kila siku au mara kadhaa kwa wiki kununua kila kitu kidogokigogo. tubamia, kaunga, tudagaa, tunyanya, tuvitunguu, tumchicha, nk.

  3. Sisi tuna familia nyingi hazijui umeme ni nini. Hata walionao, hauna uhakika wa kuwaka kila siku. Kwa wenzetu umeme kukatika kwenye nyumba kwa nusu dakika tu ni moja ya miujiza kwa mwaka labda kuwe na majanga kama vimbunga, mafuriko, nk.

  4. Sisi watu wengi hawana maji ya bomba ndani. Wengi inawalazimu kila siku kwenda kuteka maji mtoni, bombani, kisimani, chemchem, bwawani au hata kuomba kwa jirani mwenye uwezo. Wengi inawalazimu kutembea umbali mrefu kupata maji.

  5. Makazi yetu hayana anuani za kueleweka hivyo hatuwezi kuwa na huduma za kununua vitu online na kushushiwa nyumbani hata kama tukitaka.
  6. Wengi wetu tunaishi kwenye nyumba mbovu, mbaya, hazina mvuto, na wengine ni ndogo sana ukilinganisha na ukubwa wa familia. Pia wote nchi nzima tunaishi na mifugo kadhaa ndani ya nyumba. Kama sio mbuzi, kuku, kondoo au ng’ombe, basi tunaishi na mende, panya, viroboto, nzi na mbu.

  7. Hatuna maduka makubwa (supermarkets) kila mahali karibu na watu ambapo utasema mahitaji ya lazima unapokua kwenye karantini utayapata kwa karibu kirahisi. Wengi hutembea au kusafiri mbali kwenda madukani au sokoni kupata chakula.

  8. Wananchi wengi wanatumia mkaa, kuni au mafuta ya taaa kupikia. Wengine wakitaka kuwasha moto lazima wakaombe kiberiti au kaa la moto kwa jirani.

  9. Wengi wetu hatuna vyoo vya ndani na vya nje havitamaniki.
Sasa niambie, serikali ikitangaza karantini ya kumtaka kila mtu akae ndani na asichangamane hata na jirani yake tutaishije kwenye mazingira haya? Tutaweza kuishi hivyo hata kwa wiki moja? Na kama tukilazimika kwa kiboko kama kule Kenya, unadhani ni madhara kiasi gani tutapata?

Mwisho
Msukumo wa kuishauri serikali kutangaza lock-down, kama ilivyo kwa misukumo mingi, inatoka kwa kundo dogo la watu wenye uwezo (middle class). Duniani kote kundi hili hujisahau na kudhani kila mtu ana maisha kama yao. Lina kiwango kikubwa sana cha ubinafsi na wakati mwingine wanasahau kabisa kwamba hata ndugu zao wa karibu kabisa hawana uwezo walionao wa. Lakini ukweli ni kwamba kwa watanzania walio wengi karantini ya kututaka kukaa ndani ni hata kubwa mara nyingi kuliko Covid-19. Wanashawishi hatua hii wakumbuke kwanza kijijini kwao walikotoka wao au wazazi wao kabla hawajashauri lockdown.

Serikali ichukue kila tahadhari na hatua wanazoshauriwa na wataalamu kuhusu kuzuia au kupunguza maambukizi ya Covid-19. Tusikilize wataalamu ni kwa jinsi gani tunaweza kuwakinga watu ambao wakipata maambukizi watadhuruka zaidi (wazee, wenye magonjwa ya kupua, na wenye chronic diseases). Ila isikubali wala kusikiliza ushawishi wa mtu, watu, taasisi, au nchi yoyote kwamba inalazimika kutangaza karantini katika hatua ya sasa.

Karantini ya kuwataka watu kukaa nyumbani (tena kwa muda usiojulikana) ni njia isiyofaa kwa wananchi wetu. Itakua na madhara makubwa sana kiafya, kijamii, na kimaisha iwapo itachukuliwa katika hatua hii. Kufanya hivyo itakua ni sawa na kukimbia kuumwa na mbwa kwa kuingia kwenye zoo walipo simba na chui huku ukidhani unatafuta kinga.

Kwa ngazi ya maambukizi tuliyopo sisi (ukilinganisha na nchi zilizoathirika sana), bado tunaweza kuwa na maambukizi hadi miezi 5 au 6 kuanzia sasa. Njia hii inaweza kusaidia kama suluhisho la mwisho kabisa wakati maambukizi yamezidi uwezo wa kukabiliana nayo, kwa maana ya kwamba watu wengi walioambukizwa watakua na hali mbaya kiafya (critical conditions). Ikifika hatua hiyo, mlipuko utakua umefika kileleni na kukaribia kushuka hivyo muda wa watu kukaa ndani utakua ni mfupi na madhara yatakua kidogo. Kitu cha kushauri serikali kwa sasa ni namna ya kuandaa mikakati ya nini cha kufanya iwapo tutalazimika kufikia hatua hiyo (worse case scenario). Ukiweka watu ndani sasa wakati hujui utawaweka kwa muda gani, madhara yake ni makubwa sana.

Pia tukumbuke sio lazima kila nchi ifikie hatua ya kua na vifo vingi kama tunavyoona Italy, Spain na kwingine. Ni makosa kuchukulia kinachotokea kwenye nchi hizo kama kielelezo.

MM Togolani ([email protected])
Mwathirika wa "Total Lockdown"
Mkuu naona na wewe umeandika eti? Sawa tusubirie wakati mnalazwa pale kwa mkapa tena chini au kwa magodoro mliyotoka nayo nyumbani ndo akili zitakurudi na kuanzia hapo utaelewa kwamba lockdown ingekuwa na faida zaidi kwako kuliko huu upupu ulio uweka hapa.For your information Mimi na familia yangu tumeshajiweka lockdown wenyewe,hatuna sababu ya kumsubiria Magufuli,but wewe endelea kupiga kazi nikisha maliza kucoronwa utanikopesha hela kwa riba ya asilimia 200
 
Hapa sio inshu ya mwana ccm!! Huo ndio ukweli maisha yetu ya ndege tunduni hatuwezi!! Nyie wachache wenye uwezo ndio mnaona sawa, kwani una uhakika wa kutunza familia hata kwa miezi mitatu, bila kufanya kazi, akiba au mshahara unao!! Na ndio waoga sana, lakini masikini siku zote huwa hana cha kupoteza, na sio muoga.
Mkuu Kama hujawahi onja sumu au kupita mikumi kwa baskeli basi wewe mwoga tu
 
Wengi wenu humu hata hilo neno "lockdown" mmelisikia hivi majuzi tu!

Sasa hivi kila mtu kawa mjuaji.....
oooh "tunataka lockdown"....

Wagonjwa wenyewe ishirini ambao ni sawa sawa na asilimia sifuri nukta sifuri ya wagonjwa wote wa corona dunia!

Jamani, muwaache wabangaizaji watafute maisha. Msiwaongezee mzigo mwingine wa hiyo corona!

Kila mtu achukue tahadhari binafsi. Ukiona haujatosheka unaweza kujifungia kwenye contena ili corona asikupate!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu naona na wewe umeandika eti? Sawa tusubirie wakati mnalazwa pale kwa mkapa tena chini au kwa magodoro mliyotoka nayo nyumbani ndo akili zitakurudi na kuanzia hapo utaelewa kwamba lockdown ingekuwa na faida zaidi kwako kuliko huu upupu ulio uweka hapa.For your information Mimi na familia yangu tumeshajiweka lockdown wenyewe,hatuna sababu ya kumsubiria Magufuli,but wewe subiria mkuu

Ndugu Sijijui Tahadhari binafsi ni jambo la msingi sana. Hongera kwa hatua hii nzuri uliyochukua. Ila mimi nilichoongelea ni zaidi ya mimi binafsi au familia yangu. Nimeongelea Tanzania kama nchi na hali za wananchi wake ambazo zinanihusu sana.
 
Ungekuwa serious ungeishauri serikali wafanye kitu kuliko kuwambia watu wakafe au wakaambukizane kwa wingi eti kisa wanajitafutia riziki while ukijua mfumo wetu wa afya hauwezi ukawahandle Wala kuwatibu pale hali itakapokuwa imekuwa mbaya.Siku zote kwa watu wenye akili kinga ni bora kuliko tiba.sasa ninyi kwa ujinga wenu singizieni umasikini wa mtanzania,sasa wakishaambukizana kwa maelfu ndo umasikini wao utakuwa umeisha mkuu
 
when a slave dies he loses nothing but his pain!! ni kweli maskini hana cha kupoteza!! matajiri wasiojua njaa ndio wanaoshinikiza lockdown ili wajaze misosi ndani na kufurahia mateso ya maskini watakaopigwa mabuti na virungu kwa kutapatapa barabarani kutafuta msosi,

Karl Marx anasema economic determinism should be a point of departure yaani mtu anaposhinikiza jambo lake au kuanzisha mgogoro wowote angalia kuna maslahi gani ya kiuchumi atapata, Max Weber anasema uende mbali zaidi kuangalia maslahi mengine kama political gains, power, new social status na mengine! walioshindwa uchaguzi na wapinzani ndio wanataka total lockdown ili kuwe na vurugu wapate agenda!!!
Utakapokuwa kuwa umelazwa pale taifa bila nesi Wala daktari wa kukuhudumia ndiyo utaelewa lockdown ilikuwa kwa faida yako but for now wanyoshee vidole wengine na aendelea kupiga mzigo kaka? Wewe si mpangaizaji?
 
Sijaelewa hizo aya zako za chini zina uhusiano gani na post yangu... Ila ngoja nikujibu zile zinazohusiana; lockdown inategemea idadi ya maambukizi ya nchi husika pamoja na kasi ya maambukizi ya hiyo nchi...Totally lockdown sio mkumbo,inaenda na uhalisia.. Wewe unapiga kelele sababu upo bongo,hujui yanayoendelea huko nje... Tembelea forum za hizo nchi zilizo ktk total lockdown ulinganishe na hali hiyo ikiwa tz ndo upate uhalisia.., sio kuleta mambo ya trump,sijui hata kaingiaje hapa.
Si kwamba bongo hatuna maambukizi sema mfumo wetu wa afya ni hoe hae,Jana Kuna familia moja imebebwa huko mbezi msakuzi baada ya baba kuugua corona aliyoambukizwa huko Kongo,je safari nzima na roli lake toka tunduma mpaka amewashushia wangapi hilo zigo.Kama Tanzania haina Mungu wa pekee yake just wait you will see
 
Na wenzetu wana supermarket kila mtaa. huku sasa, mmh mie nipo kahama supermarket zipo tano 5, na idadi ya wananchi wa hapa kahama mji ni 1.5+million.
Na katika hizo supermarket yenye akili ni ROYAL Supermarket na royal food tu.
Karibu bidhaa zote zinapatikani masokoni
Ukiacha supermarket umejiuliza hapo kahama mna hospital ngapi na manesi wangapi na zinaweza kuhudumia watu wangapi kwa mpigo? Kama US wanachemsha na wanamlaumu Trump kwa kufanya uzembe sisi tutaisha na hii lugha ya umasikini sijui itatoweka na kila mtu atajiweka mwenyewe kwenye lockdown same way mipaka yetu ilivyojifunga
 
MUHTASARI:
Nchi nyingi duniani, hasa za Magharibi, zimetangaza karantini au “lockdown” inayowazuia wanachi kutoka ndani muda wote isipokua kutafuta mahitaji ya lazima tu (dawa na chakula). Hatua hii imechukuliwa na nchi ambazo maambukizi ya Covid-19 yamekua makubwa, sio kwa lengo la kuzuia watu wasipate maambuziki, bali zinalenga kupunguza kasi ya maambukizi kwa wakti mmoja ili mfumo wa utoaji huduma za afya usilemewe zaidi. Hali hiyo haina muda maalum na itaendelea hadi mlipuko wa Covid-19 utakapoonekana umepungua au kwisha. Hivyo watu wengi hapa kwetu nao wanaishauri serikali kufanya hivyo wakiamini ni hatua ya lazima kwa sasa na wanachukulia kutotangaza karantini mapema ni uzembe au ni kutokujali.

Katika makala hii, nimeeleza kwa nini sio sahihi kwa nchi yetu na nyingi za kiafrika kufanya hivyo. Pia ninashauri kwa kusisitiza serikali isiwaze kabisa kuchukua hatua hii sababu haifai na haitekelezeki kwenye mazingira yetu. Iwapo njia hii itatutumika, madhara yake kwa wananchi yanaweza kuwa makubwa kuliko tatizo linaloepukwa. Nimeeleza hoja yangu kwa kutumia uzoefu binafsi wa kuwa kwenye karantini na kufananisha mazingira ya utekelezaji wa amri hii kwenye nchi za Magharibi unapolinganisha na nchi zetu. Kwa undani zaidi soma makala nzima hapa chini.

View attachment 1406728

Utangulizi
Nianze ujumbe wangu kwa kutangaza maslahi binafsi. Hapa nilipo, hii ni wiki ya pili tunamaliza tukiwa chini ya “total lockdown”. Nchi nzima tunalazimika kukaa ndani tu na hatujui tutatoka lini. Sina hakika na watu wengine waliowahi kuishi mazingira ya aina hii, ila niseme kwa ujasiri kabisa kwamba mazingira haya ni mabaya, ni magumu, na yanaumiza sana kisaikolojia. Muda mwingi huwezi kufanya lolote la maana kwa kuwa unakua kama umepoteza "network". Mtu asiombe kabisa kukosa uhuru wa kutoka ndani.

Kwa nini nashauri hili?
Kwa sababu hizi na kwa hoja nitakazozieleza hapa, ninapingana kwa 100% na kila ambaye anaishawishi, anaishauri, au anailazimisha serikali kutangaza karantine kama nchi nyingine au anailaumu kwa kutokufanya hivyo. Labda nieleze kwa kifupi nini maana ya kuwa kwenye karantini katika uhalisia ili kuweka ninachoongea kwenye muktadha:
  1. Wazazi, watoto na munaoishi nao munashinda mukiwa mumejifungia ndani: usiku unakuja, asubuhi inafika, munaaendelea na zoezi kam ajana. Mbaya zaidi hamujui zoezi hili litakwisha lini. Wakati mwingine munasahau siku au tarehe maana hakuna matukio yanayowakumbusha. Serikali inasema inaweza kuwa hivi hadi miezi 6.

  2. Haijalishi mukakokuita nyumbani au ndani kukoje kwa maana ya ukubwa/udogo, ubaya/uzuri na kuna nini cha kufurahisha au kufanya: munazunguka humohumo mchana na usiku.

  3. Munatoka ndani mara moja au mbili kwa wiki kwenda kutafuta mahitaji ya lazima. Na mahitaji ya lazima ni chakula na mdawa pekee maana maduka mengine yote yasiyo ya chakula na madawa yamefungwa. Munashauriwa kufanya hivyo inapokua ni lazima lakini kama inawezekana muagize online.

  4. Wakati mwingine vitu vya lazima hakuna madukani au supermarkets maana watu wananunua kwa wingi kwa hofu hivyo vinakwisha.

  5. Ukifika supermarket mupanga foleni ndefu ya kuingia ndani kwa vile munatakiwa muwe umbali wa mita 2 kati ya mtu na mtu na hamutakiwi kuingia wengi kwa wakati mmoja ili musisongamane. Na unaweza kufiuka ndani unakosa unachotaka.

  6. Kwa anayeweza, munaruhusiwa kutoka nje mara moja kwa siku kufanya zoezi moja (kutembea au kukimbia) na uwe mwenyewe au na mtu wa familia yako maana hakuna kukutana zaidi ya watu wawili.

  7. Makazi mengi hayana viwanja vya nje kama kwetu Afrika maana nyumba zimejengwa kwa mipango na kubana nafasi. Mara nyingi, nje ya mlango ni bararaba ya mtaa.

  8. Sheria imepitishwa na bunge kwamba ukikamatwa kwenye mkusanyiko au unazurura unaweza kutozwa faini na polisi ya hadi milioni tatu za Tanzania (zile faini za papo kwa hapo kama za makosa ya barabarani)
Unajua kwa nini wanaweza kufanya haya?
Wenzetu wanapochukua hatua hizi za kukaa ndani ni kwa sababu mazingira yao yanaruhusu ya yameandaliwa hivyo. Kwa mfano:
  1. Wao kukaa ndani sio jambo geni. Maisha yao kwa sehemu kubwa ni ya kibinafsi. Watu wanakaa ndani muda mwingi maana yale maisha ya kijamaa/kijamii wameyaacha. Munaweza kuiishi milango imetazamana na jirani zako lakini musisalimiane hata munapogongana mukitoka au kuingia ndani. Unaweza usimjue jirani yako munayetazamana au kutengwa na ukuta ni nani, anafanya nini, nk. Huku ndiko tumeiga msemo wa “mind your own business” na “I don’t care what yu think of me” na tunadhani ni maendeleo.

  2. Nchi za Ulaya zina msimu wa baridi kuanzia mwezi wa 10 na wa 11 hadi mwishoni mwa mwezi wa tatu. Kipindi hiki hali ya hewa inaweza kua mbaya muda mwingi na baridi ni kali sana. Giza linakua muda mrefu kuliko mchana. Kuna kipindi linaanza kuingia saa tisa jioni na linaendelea hadi saa mbili asubuhi Kesho yake. Hivyo mchana kwa maana ya mwanga unaweza kuwa kama masaa 6 hadi 8 tu. Mvua na barafu huweza kuwepo kwa wingi pia. Kwa jumla, mazingira hayaruhusu kukaa nje wala kutembea hivyo kama mtu hana anapolazimika kwenda basi muda mwingi ni kukaa ndani.

  3. Nyumba za wenzetu hazijengwi kienyeji kama sisi ambapo kila mtu anajijengea atakavyo na atakapo. Nyumba zinajengwa na makampuni na serikali kwa mipango na viwango maalumu. Kutokana na hali ya hewa ya baridi na majanga kama vimbunga, zinajengwa zikiwa na uwezo wa kustahimili baridi na upepo mkali. Madirisha yana vioo viwili; ukuta wa nyumba una leya mbuli na katikati unajazwa vitu vya kupunguza hewa ya baridi; paa linadhibitiwa kiasi kwamba mvu akinyesha unaweza usijue kama hujatazama nje.

  4. Kila nyumba ina maji yasiyokatika; ina bomba la gesi linaloingia ndani kama maji isiyokatika; ina umeme wa uhakika usiokatika. Nyumba zisizo na mabomba ya gesi basi umeme ndio unatumika kupikia na kwenye mifumo ya kupasha maji na nyumba joto.

  5. Kila nyumba inaijengwa, inaingiziwa waya (connection) ya TV, simu ya landline na internet. Huduma hizi ni za uhakika kwa kila nyumba labda uwe tu huwezi kulipia bills. Internet ni rahisi sana hivyo kwa gharama ambayo hapa kwetu mtu anatumia kununua bando la GB kama ya 20, kwao unapata internet ya kutumia vifaa zaidi ya kumi kwa wakati mmoja (simu, computers, smart tv, tablets) usiku na mchana mwezi mzima mukifanya kila munachotaka kwenye internet bila kupimiwa.

  6. Huduma za maji, umeme, internet, gesi, simu, tv hazikatiki na hazikatwi kienyeji hata ukishindwa kulipa bills. Tarehe ya kulipia ikifika huna pesa kwenye kwenye akaunti utafutatiliwa na kukumbushwa kwanza kwa muda ingawa ukichelewa sana utapigwa faini ya kukuumiza.

  7. Unaweza kuagiza KITU CHOCHOTE online (kwa kupiga simu au internet) na kikaletwa hadi mlangoni iwe dawa, chakula, nguo, viatu, mashuka, vinywaji, nk.

  8. Ukiiumwa unawasiliana na daktari kituo cha afya uliposajiliwa kabla ya uamuzi wakwenda hospitali kama sio matatizo ya dharura. Matatizo yote ya dharura ukipiga simu ndani ya dakika chache ambulance iko mlangoni na ukichelewa kufungua wanaweza kuvunja mlango wakaingia wakidhani umezidiwa.

  9. Ukipata tatizo kama kupigwa na mwenza, kuingiliwa na wezi, au mtoto kupigwa na mzazi; ukipiga simu ndani ya dakika chache polisi wako mlangoni.
Haya ndio mazingira ya wenzetu yanayowaruhusu kutangaza TOTAL LOCKDOWN au KARANTINI kirahisi kama vile wanatangaza mshahara kupanda. Wanaposema watu wakae ndani wasitoke, wana hakika kwa zaidi ya 95% mazingira ya kila mtu yanamruhusu kukaa ndani na akaishi bila matatizo makubwa. Pia, kwa kuwa wana mifumo inayofanya kazi na makazi yamepangika, kwa sehemu kubwa wanajua kila mtu anayefanya kazi (binafsi au kijiajiri), kipato chake, na anaishi wapi. Hivyo serikali wanaweza kutangaza kutoa ruzuku za kuishi kwa kiwango fulani kwa kila raia au mfanyakazi huu muda wa mlipuko na wakazipata bila mizengwe.

Sasa linganisha mazingira haya yao nay a kwetu.
  1. Sisi wananchi wengi hawana uwezo wa kununua chakula cha kesho. Inamlazimu mtu kutoka ndani kila siku ili angalau aweze kuweka mlo mezani.

  2. Sisi tumezoea kwenda duknai/sokoni kila siku au mara kadhaa kwa wiki kununua kila kitu kidogokigogo. tubamia, kaunga, tudagaa, tunyanya, tuvitunguu, tumchicha, nk.

  3. Sisi tuna familia nyingi hazijui umeme ni nini. Hata walionao, hauna uhakika wa kuwaka kila siku. Kwa wenzetu umeme kukatika kwenye nyumba kwa nusu dakika tu ni moja ya miujiza kwa mwaka labda kuwe na majanga kama vimbunga, mafuriko, nk.

  4. Sisi watu wengi hawana maji ya bomba ndani. Wengi inawalazimu kila siku kwenda kuteka maji mtoni, bombani, kisimani, chemchem, bwawani au hata kuomba kwa jirani mwenye uwezo. Wengi inawalazimu kutembea umbali mrefu kupata maji.

  5. Makazi yetu hayana anuani za kueleweka hivyo hatuwezi kuwa na huduma za kununua vitu online na kushushiwa nyumbani hata kama tukitaka.
  6. Wengi wetu tunaishi kwenye nyumba mbovu, mbaya, hazina mvuto, na wengine ni ndogo sana ukilinganisha na ukubwa wa familia. Pia wote nchi nzima tunaishi na mifugo kadhaa ndani ya nyumba. Kama sio mbuzi, kuku, kondoo au ng’ombe, basi tunaishi na mende, panya, viroboto, nzi na mbu.

  7. Hatuna maduka makubwa (supermarkets) kila mahali karibu na watu ambapo utasema mahitaji ya lazima unapokua kwenye karantini utayapata kwa karibu kirahisi. Wengi hutembea au kusafiri mbali kwenda madukani au sokoni kupata chakula.

  8. Wananchi wengi wanatumia mkaa, kuni au mafuta ya taaa kupikia. Wengine wakitaka kuwasha moto lazima wakaombe kiberiti au kaa la moto kwa jirani.

  9. Wengi wetu hatuna vyoo vya ndani na vya nje havitamaniki.
Sasa niambie, serikali ikitangaza karantini ya kumtaka kila mtu akae ndani na asichangamane hata na jirani yake tutaishije kwenye mazingira haya? Tutaweza kuishi hivyo hata kwa wiki moja? Na kama tukilazimika kwa kiboko kama kule Kenya, unadhani ni madhara kiasi gani tutapata?

Mwisho
Msukumo wa kuishauri serikali kutangaza lock-down, kama ilivyo kwa misukumo mingi, inatoka kwa kundo dogo la watu wenye uwezo (middle class). Duniani kote kundi hili hujisahau na kudhani kila mtu ana maisha kama yao. Lina kiwango kikubwa sana cha ubinafsi na wakati mwingine wanasahau kabisa kwamba hata ndugu zao wa karibu kabisa hawana uwezo walionao wa. Lakini ukweli ni kwamba kwa watanzania walio wengi karantini ya kututaka kukaa ndani ni hata kubwa mara nyingi kuliko Covid-19. Wanashawishi hatua hii wakumbuke kwanza kijijini kwao walikotoka wao au wazazi wao kabla hawajashauri lockdown.

Serikali ichukue kila tahadhari na hatua wanazoshauriwa na wataalamu kuhusu kuzuia au kupunguza maambukizi ya Covid-19. Tusikilize wataalamu ni kwa jinsi gani tunaweza kuwakinga watu ambao wakipata maambukizi watadhuruka zaidi (wazee, wenye magonjwa ya kupua, na wenye chronic diseases). Ila isikubali wala kusikiliza ushawishi wa mtu, watu, taasisi, au nchi yoyote kwamba inalazimika kutangaza karantini katika hatua ya sasa.

Karantini ya kuwataka watu kukaa nyumbani (tena kwa muda usiojulikana) ni njia isiyofaa kwa wananchi wetu. Itakua na madhara makubwa sana kiafya, kijamii, na kimaisha iwapo itachukuliwa katika hatua hii. Kufanya hivyo itakua ni sawa na kukimbia kuumwa na mbwa kwa kuingia kwenye zoo walipo simba na chui huku ukidhani unatafuta kinga.

Kwa ngazi ya maambukizi tuliyopo sisi (ukilinganisha na nchi zilizoathirika sana), bado tunaweza kuwa na maambukizi hadi miezi 5 au 6 kuanzia sasa. Njia hii inaweza kusaidia kama suluhisho la mwisho kabisa wakati maambukizi yamezidi uwezo wa kukabiliana nayo, kwa maana ya kwamba watu wengi walioambukizwa watakua na hali mbaya kiafya (critical conditions). Ikifika hatua hiyo, mlipuko utakua umefika kileleni na kukaribia kushuka hivyo muda wa watu kukaa ndani utakua ni mfupi na madhara yatakua kidogo. Kitu cha kushauri serikali kwa sasa ni namna ya kuandaa mikakati ya nini cha kufanya iwapo tutalazimika kufikia hatua hiyo (worse case scenario). Ukiweka watu ndani sasa wakati hujui utawaweka kwa muda gani, madhara yake ni makubwa sana.

Pia tukumbuke sio lazima kila nchi ifikie hatua ya kua na vifo vingi kama tunavyoona Italy, Spain na kwingine. Ni makosa kuchukulia kinachotokea kwenye nchi hizo kama kielelezo.

MM Togolani ([email protected])
Mwathirika wa "Total Lockdown"
Wewe Togolani una uhuni usio na kipimo na uliopitiliza. Ebu peleka use...ge wako huku

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom