Nadhani hapa kuna point ya msingi anayojenga
Sijijui. Ni vyema
MM Togolani na wengine tujadili kwa mtizamo hasi(na sio chanya peke yake). Mfano, pale ambapo tutaendelea kuacha watu wajitafutia riziki halafu hapo hapo waambukizane wengi, hapo serikali itamudu kuwahudumia kwa hali hiyo hiyo uliyoelezea ya mazingira yetu ya kitanzania? Ni dhahiri kuwa kama maambukizi yakiongezeka na kubidi total lockdown, maana yake kutakua na maambukizi mengi yatakayoendelea kwa kiwango kikubwa na kuambatana na vifo kutokana na serikali kushindwa kabisa kumudu kutoa huduma za afya zinazohitajika kwa wagonjwa.
Ni kweli ugonjwa hauna dawa, ila magonjwa yanayoambatana kama kisukari , pressure, n.k yana dawa hata za kupunguza makali tu. Sasa kama tu kwa haliya kawaida dawa zinakua changamoto, je wakati wa total lockdown tunategemea serikali kuweza kuwatibu? Na je mifumo yetu ya afya inaweza kumudu tofauti tu kidogo tu ya idadi kubwa ya wagonjwa itakayoongezeka?
Mimi nafikiri tukiangalia kwa mtazamo chanya ni vyema kuona total lockdown ikizaa matunda. Ila kwa hali yetu ya kitanzania, lockdown iwe ya muda mfupi. Ikionekana kuna kupungua kwa maambukizi unafungua tena halafu unawaweka watu lockdown tena hali ikibadilika mpaka hali itakapokua shwari.
Pia, serikali kuanza kujiandaa na kuimarisha mifumo ya afya. Ifanye taratibu za vyakula kwa kipindi cha hatari. Kama mpango wa TASAF ungekua effective tungeweza kujua priority ilipo. Hata hivyo, ni mahali pa kuanzia kutambua familia duni hasa zilizoko maeneo ya karibu na miji. Pia sio lazima kufanya total lockdown. Kama kijijini rate ya maambukizi ikiwa ndogo then hakuna haja ya lockdwon huko. Ila kwa sehemu kama Dsm na zenye mikusanyiko ni vyema hili likawepo. Hata kama haliko kama wafanyavyo wenzetu basi kuwa na control mfano za social distancing n.k. Kingine tunaweza customize namna tutakavyoita hali hii hatari. Wale wasio na umuhimu wa kwenda nje wabaki majumbani - na hii itawezekana pale tu serikali itakapotamka hali ya hatari. Ila kama haijatamka maana yake hata wale wanaotaka kufanya kazi majumbani hawana justification ya kufanya hivyo na hili ni kwa taasisi za umma zaidi. Kwa private wanaweza kuwa na utaratibu binafsi ila kwa taasisi za umma haziwezi jiwekea utaratibu wa kufanya kazi majumbani wakati serikali haijatangaza hali ya hatari.
Mwisho, mjadala huu bado ni mzuri kwa kuangalia mantiki ya pande zote. Ila namalizia kwa kusema kuna umuhimu wa customized total lockdown kwa baadhi ya sehemu yenye hatari zaidi. Kijijini wanaweza kuendelea kwenda shamba kama kawaida. Ila mjini kama jiji la dsm aisee tunahitaji kufanya kitu zaidi. MM Togolani nakusubiri hapa.