Kwanza naomba nikupongeze kwa ''kukomaa nae'' ndugu mtoa mada, umeonyesha kuhimili mjadala na kuwasilisha kile unachokisimamia kwa umahiri mkubwa. Hongera sana dada
Rebeca 83
Naomba nianze kuchangia mjadala kwa kunukuu maneno yako haya...
''
I believe hivi vifo tunavyoviona sasa hivi vinatokana na hao walioambukizwa KABLA ya lockdown na sio NEW PATIENTS ….(what I believe)''
Uhalisia wa mambo ni kwamba nchini Italia bado kuna maambukizi mapya kila siku.
Imani yako inakinzana na data za kisayansi.
Kwa hoja hii tu (belief), unapoteza uhalali wa kuendelea kujadili mjadala huu ambao umejikita kwenye sayansi zaidi.
Mchango wangu kwenye mada:
Naungana na ndugu
MM Togolani kwamba kwa sasa, lockdown haitakua njia muafaka na stahiki ya kukabiliana na mlipuko wa COVID19 pamoja na ''madhara yake'' (sio vifo pekee).
Sababu zangu:
1. Aina ya maisha tunayoishi. (mtoa mada kaeleza vya kutosha)
2. Nature ya ueneaji wa ugonjwa husika dhidi ya ''tabia zetu'' (Mtu mmoja anatoka nje anaweza kuwaletea balaa mliopo ndani).
NB; Unapotatua tatizo moja, hautakiwi kusababisha tatizo jingine kubwa kuliko lile unalolitatua. (Total lockdown kwa sasa, kwa Tanzania, itakiuka hii kanuni).
Ieleweke wazi kwamba tunaopingana na lockdown tunaunga mkono jitihada na njia zingine zinazosaidia kupunguza kasi ya kuenea na madhara ya COVID 19 kama tunavyoshauriwa na wataalamu wa afya.