Mwanamaji
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 2,906
- 4,532
Nitajihu kesho,ok?
Mkuu umeandika ''nitajihu'', nadhani tu tuelewe kwamba makosa ya kiuandishi ni mambo ya kawaida tu kama ujumbe unaweza ukaeleweka.
Nitajihu kesho,ok?
My kaka, Italy haikuchukua hatua mwanzo..wengi wakawa infected , na sisi tusipochukua hatua ugonjwa ndio ushaingia hivyo ...tusisubiri wale wote walioambukizwa waambukize wengine..maambukizi yakishakua makubwa.ndio tuweke lockdown...hata pamoja na virus kuua wengi , hali ya Italy ime improve baada ya kuweka lockdown,hata Spain nao hali ni hivyo hivyo..yanayotokea duniani lazima yatu guide katika kufanya maamuzi..au ulikua unataka mpaka na sisi tusibiri coronavirus ku 'gain momentum' ??...ndio tuchukue hatua????lockdown haiepukiki..ku accept this is better than living in denial......Again Italy nadhani sababu hawakuchukua hatua mapema, wengi wakawa infected ,I believe hivi vifo tunavyoviona sasa hivivinatokana na hao walioambukizwa KABLA ya lockdown na sio NEW PATIENTS ….(what I believe). baada ya hawa watu walioambukizwa kabla ya lockdown kuisha,then tutaona improvement...kama wataendelea na lockdown though..kuzuia maambukizi mapya...
Halafu hizo 'news' zinatoka kwenye credible sources..lol..CORONA VIRUS being a novel subject..sidhani kuna RESEARCH nyingi..LOL..we do rely on 'news'..nisamehe kama nimekukwaza mahali bro...
True..... Dada umejitahidi kumueleza ukweli..... we don't need to have scientific research au data kujua kama lock down inasaidia kupunguza mambukizi mapya, ni logic tu naona kaka amengangania scientifical proof na data za ugonjwa ku support lock-down..........which is wrong hu ungonjwa inahitaji common sense na little medical knowledge kupambana nao, sio academic papers au research, hamna namna Tz will lock down with in this month no other alternative au tupate the worse
Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu hi ni emergency mda wa scietific research na academic presentations haupo tena, nchi kama Brazil wingereza US wamebadilisha viwanja vya mipila kua emergency medical facilities,........ hapa huwezi kutafuta utafiti wa kisayansi kuhusu effectiveness ya lock-down ndo maana kuna haja ya kua na ginius leaders wenye uwezo wa kufanya maamuzi kwa wakati kama hu, sio wale wa kusikilizia kwanza kuona upepo.Umesema ''we don't need to have scientific research au data kujua kama lockdown inasaidia kupunguza kasi ya maambukizi ya COVID 19 ama la...''
Halafu ukaja kusema ili kupambana na huu ugonjwa uhataji kutumia ''common sense na little medical knowledge kupambana nao, sio academic papers au research''
Mkuu mulwanaka hauoni kama hiyo itakua ni namna dhaifu sana ya kupambana na janga ''serious'' kama la COVID19 ?
What is the solutionsKwanza naomba nikupongeze kwa ''kukomaa nae'' ndugu mtoa mada, umeonyesha kuhimili mjadala na kuwasilisha kile unachokisimamia kwa umahiri mkubwa. Hongera sana dada Rebeca 83
Naomba nianze kuchangia mjadala kwa kunukuu maneno yako haya...
''I believe hivi vifo tunavyoviona sasa hivi vinatokana na hao walioambukizwa KABLA ya lockdown na sio NEW PATIENTS ….(what I believe)''
Uhalisia wa mambo ni kwamba nchini Italia bado kuna maambukizi mapya kila siku.
Imani yako inakinzana na data za kisayansi.
Kwa hoja hii tu (belief), unapoteza uhalali wa kuendelea kujadili mjadala huu ambao umejikita kwenye sayansi zaidi.
Mchango wangu kwenye mada:
Naungana na ndugu MM Togolani kwamba kwa sasa, lockdown haitakua njia muafaka na stahiki ya kukabiliana na mlipuko wa COVID19 pamoja na ''madhara yake'' (sio vifo pekee).
Sababu zangu:
1. Aina ya maisha tunayoishi. (mtoa mada kaeleza vya kutosha)
2. Nature ya ueneaji wa ugonjwa husika dhidi ya ''tabia zetu'' (Mtu mmoja anatoka nje anaweza kuwaletea balaa mliopo ndani).
NB; Unapotatua tatizo moja, hautakiwi kusababisha tatizo jingine kubwa kuliko lile unalolitatua. (Total lockdown kwa sasa, kwa Tanzania, itakiuka hii kanuni).
Ieleweke wazi kwamba tunaopingana na lockdown tunaunga mkono jitihada na njia zingine zinazosaidia kupunguza kasi ya kuenea na madhara ya COVID 19 kama tunavyoshauriwa na wataalamu wa afya.
Nilikuwa nimelewa jana ndio maana nikaomba hivyo na bahati mbaya nikakosea!Kuna typing error na syntax error,i hope umeelewa!Naomba niulize,hivi hangover iking'ang'ania unatumiaga nini kupata nafuu?Mkuu umeandika ''nitajihu'', nadhani tu tuelewe kwamba makosa ya kiuandishi ni mambo ya kawaida tu kama ujumbe unaweza ukaeleweka.
Huwa napata ukakasi tu ninapoona mtu anafanya makosa ya kizembe,yaani nakuwa irritated kabisaa!Tigershark .. Ila rafiki yangu kuna uwezekano mkubwa ukawa na tatizo kubwa la ukosoaji usio na tija au una matatizo (reservations) binafsi na mwandishi. Dunia iko busy inajadili janga la Corona na namna ya kukabiliana nalo, ila kwako cha maana unachokiona (na kuona kinafaa kujadiliwa kwenye huu uzi) ni makosa ya uandishi pekee!!! Seriously!!!. Naona haujadili mada umeng'ang'ana na uandishi.
Naomba niwe nakutumia maandishi yangu unisahihishe kabla sijayaweka hapa maana inaonekana you are a qualified proofreader. Please.
MM Togolani
Mkuu yamepita!Sasa ngoja nitulie kidogo hangover iiishe nitakuja na mchango wangu kwenye hii hoja!Ndugu Tigershark.
Moja, nashukuru sana kwa kunikosoa. Ni kweli nasumbuka sana kuandika Kiswahili fasaha. Lengo la kuandika hapa ni kufikia watu walio wengi na kufikisha ujumbe kuliko usahihi/ufasaha wa lugha. Hivyo nitatumia Kiswahili hivyohivyo ninavyoweza. Hata hivyo nitajitahidi kujifunza na kusahihisha ninapokosea. Uandishi wa kutumia lugha fasaha unahitaji muda mrefu ambao kwa sasa sina kabisa. Unisaheme bure. Sisi tuliosoma namba muda mwingi tuliacha kujifunza Kiswahili tulipofanya mtihani wa mwisho wa kidato cha nne.
Pili, mimi sijawahi kuwa mwandishi wa Rais. Mimi sio Togolani Mavura aliyekua msaidizi wa Mh Kikwete hivyo musimuhusishe na makosa yangu ya uandishi. Mimi ni Mathew Togolani Mndeme. Sijawahi kufanya kazi ya uandishi. Kazi yangu ni kufundisha (ila sio soma la Kiswahili na Kiswahili sio lugha ya kufundishia).
Ubarikiwe.
MM togolani
Huyo genius leader afanye hayo maamuzi basing on what ?Mkuu hi ni emergency mda wa scietific research na academic presentations haupo tena, nchi kama Brazil wingereza US wamebadilisha viwanja vya mipila kua emergency medical facilities,........ hapa huwezi kutafuta utafiti wa kisayansi kuhusu effectiveness ya lock-down ndo maana kuna haja ya kua na ginius leaders wenye uwezo wa kufanya maamuzi kwa wakati kama hu, sio wale wa kusikilizia kwanza kuona upepo.
Sent using Jamii Forums mobile app
What is the solutions
We ulitakaje? Unapesa wewe ya kukas ndani siku tatu? Kama we unayo umewaza kuhusu shangazi zako, wajomba zako, mama zako, dada na kaka zako wakiwa na familia zao.? Je wote kwao wans system za maji safi au wengine wanapanga foleni kwa jirani?Endeleeni kuleta utani kwenye mambo ya msingi hivyo hivyo siku mwanaccm akipata korona ndio mtatia akili.
Sent using Jamii Forums mobile app
Good thinkingMUHTASARI:
Nchi nyingi duniani, hasa za Magharibi, zimetangaza karantini au “lockdown” inayowazuia wananchi kutoka ndani muda wote isipokua kutafuta mahitaji ya lazima tu (dawa na chakula). Hatua hii imechukuliwa na nchi ambazo maambukizi ya Covid-19 yamekua makubwa, sio kwa lengo la kuzuia watu wasipate maambuziki, bali zinalenga kupunguza kasi ya maambukizi kwa wakati mmoja ili mfumo wa utoaji huduma za afya usilemewe na kushindwa kuwahudumia wanaozidiwa. Lockdown haina muda maalum na itaendelea hadi mlipuko wa Covid-19 utakapoonekana umepungua au kwisha. Hivyo watu wengi hapa Tanzania nao wanaishauri serikali kufanya hivyo wakiamini ni hatua ya lazima kwa sasa na wanachukulia kutotangaza karantini mapema ni uzembe au ni kutokujali.
Katika makala hii, nimeeleza kwa nini sio sahihi kwa nchi yetu na nyingi za kiafrika kutangaza Lockdown. Pia nimeshauri kwa kusisitiza serikali isiwaze kabisa kuchukua hatua hii katika hatua hii hasa kwa sababu haitekelezeki kwenye mazingira yetu na hatujui mlipuko utachukua muda gani. Iwapo njia hii itatutumika, madhara yake kwa wananchi yanaweza kuwa makubwa kuliko yatokanayo na Covid-19. Nimeeleza hoja yangu kwa kutumia uzoefu binafsi wa kuwa kwenye karantini. Pia nimefananisha mazingira ya utekelezaji wa amri hii kwenye nchi za Magharibi na nchi zetu ili kuweka hoja yangu katika muktadha.Kwa undani zaidi soma makala nzima hapa chini.
View attachment 1406728
Utangulizi
Nianze ujumbe wangu kwa kutangaza maslahi binafsi. Hapa nilipo, hii ni wiki ya pili tunamaliza tukiwa chini ya “total lockdown”. Nchi nzima tunalazimika kukaa ndani muda na hatujui tutatoka lini. Sina hakika na watu wengine waliowahi kuishi mazingira ya aina hii, ila niseme kwa ujasiri kabisa kwamba mazingira haya ni mabaya, ni magumu, na yanaumiza sana kisaikolojia. Muda mwingi huwezi kufanya lolote la maana kwa kuwa unakua kama umepoteza "network". Mtu asiombe kabisa kukosa uhuru wa kutoka ndani. Ninapingana kwa 100% na kila ambaye anaishawishi, anaishauri, au anailazimisha serikali kutangaza karantine kama nchi nyingine au anailaumu kwa kutokufanya hivyo.
Nini msingi wa hoja yangu?
Labda nieleze kwa kifupi nini maana ya kuwa kwenye karantini katika uhalisia ili kuweka ninachoongea kwenye muktadha:
Unajua kwa nini wanaweza kufanya haya?
- Wazazi, watoto na munaoishi nao munashinda mukiwa mumejifungia ndani: usiku unakuja, asubuhi inafika, munaaendelea na zoezi kama jana. Mbaya zaidi hamujui zoezi hili litakwisha lini. Wakati mwingine munasahau siku au tarehe maana hakuna matukio yanayowakumbusha. Serikali inasema inaweza kuwa hivi hadi miezi 6.
- Haijalishi munakokuita nyumbani au ndani kukoje kwa maana ya ukubwa/udogo, ubaya/uzuri na kuna nini cha kufurahisha au kufanya: munazunguka humohumo mchana na usiku.
- Munatoka ndani mara moja au mbili kwa wiki kwenda kutafuta mahitaji ya lazima. Na mahitaji ya lazima ni chakula na madawa maana maduka ya mahitaji mengine yamefungwa. Munashauriwa kama inawezekana muagize vyakula online.
- Wakati mwingine vitu vya lazima hakuna madukani/supermarkets maana kutokana na hofu, watu wananunua kwa wingi hivyo vinakwisha.
- Ukifika supermarket mupanga foleni ndefu ya kuingia ndani kwa vile munatakiwa muwe umbali wa mita 2 kati ya mtu na mtu na hamutakiwi kuingia wengi kwa wakati mmoja ili musisongamane. Unaweza kufika ndani unakosa unachotaka.
- Kwa anayeweza, munaruhusiwa kutoka nje mara moja kwa siku kufanya zoezi moja (kutembea au kukimbia) na uwe mwenyewe au na mtu wa familia yako maana hakuna kukutana zaidi ya watu wawili.
- Makazi mengi hayana viwanja vya nje kama kwetu Afrika maana nyumba zimejengwa kwa mipango na kubana nafasi. Mara nyingi, nje ya mlango ni bararaba ya mtaa.
- Sheria imepitishwa na bunge kwamba ukikamatwa kwenye mkusanyiko au unazurura unaweza kutozwa faini na polisi ya hadi milioni tatu za Tanzania (zile faini za papo kwa hapo kama za makosa ya barabarani)
Wenzetu wanapochukua hatua hizi za kukaa ndani ni kwa sababu mazingira yao yanaruhusu ya yameandaliwa hivyo. Kwa mfano:
Haya ndio mazingira ya wenzetu yanayowaruhusu kutangaza TOTAL LOCKDOWN au KARANTINI kirahisi kama vile wanatangaza mshahara kupanda. Wanaposema watu wakae ndani wasitoke, wana hakika kwa zaidi ya 95% mazingira ya kila mtu yanamruhusu kukaa ndani na akaishi bila matatizo makubwa. Pia, kwa kuwa wana mifumo inayofanya kazi na makazi yamepangika, kwa sehemu kubwa wanajua kila mtu anayefanya kazi (binafsi au kijiajiri), kipato chake, na anaishi wapi. Hivyo serikali wanaweza kutangaza kutoa ruzuku za kuishi kwa kiwango fulani kwa kila raia au mfanyakazi kipindi hiki cha mlipuko na watu wakazipata bila mizengwe.
- Wao kukaa ndani sio jambo geni. Maisha yao kwa sehemu kubwa ni ya kibinafsi. Watu wanakaa ndani muda mwingi maana yale maisha ya kijamaa/kijamii wameyaacha. Munaweza kuiishi milango imetazamana na jirani zako lakini musisalimiane hata munapogongana mukitoka au kuingia ndani. Unaweza usimjue jirani yako munayetazamana au kutengwa na ukuta kua ni nani, anafanya nini, nk. Huku ndiko tumeiga msemo wa “mind your own business” na “I don’t care what yu think about me” na tunadhani ni maendeleo.
- Nchi za Ulaya zina msimu wa baridi kuanzia mwezi wa 10 na wa 11 hadi mwishoni mwa mwezi wa tatu. Kipindi hiki hali ya hewa inaweza kua mbaya muda mwingi sababu ya upepo mkali, mvua nyingi, baridi ni kali, na kunaweza kuwa na barafu. Giza linakua muda mrefu kuliko mchana. Kuna kipindi linaanza kuingia saa tisa jioni na linaendelea hadi kesho yake saa mbili asubuhi. Hivyo mchana kwa maana ya mwanga unaweza kuwa kama masaa 6 hadi 8 tu. Kwa jumla, mazingira hayaruhusu kukaa nje wala kutembea hivyo kama mtu hana anapolazimika kwenda basi muda mwingi ni kukaa ndani.
- Nyumba za wenzetu hazijengwi kienyeji kama sisi ambapo kila mtu anajijengea atakavyo na atakapo. Nyumba zinajengwa na makampuni au na serikali kwa mipango na viwango maalumu. Kutokana na hali ya hewa ya baridi na majanga kama vimbunga, nyumba zinajengwa zikiwa na uwezo wa kustahimili baridi na upepo mkali. Madirisha yana vioo viwili; ukuta wa nyumba una kuta mbili na katikati unajazwa vitu vya kupunguza hewa ya baridi; paa linadhibitiwa kiasi kwamba mvu akinyesha unaweza usijue iwapo hujatazama nje.
- Kila nyumba ina maji yasiyokatika; ina bomba la gesi linaloingia ndani kama maji; ina umeme wa uhakika usiokatika. Nyumba zisizo na mabomba ya gesi basi umeme ndio unatumika kupikia na kwenye mifumo ya kupasha maji na nyumba joto.
- Kila nyumba inapojengwa, inaingiziwa waya (connection) ya TV, simu ya landline na internet. Huduma hizi ni za uhakika kwa kila nyumba labda uwe tu huwezi kulipia bills. Internet ni rahisi sana hivyo kwa gharama ambayo hapa kwetu mtu anatumia kununua bando la GB kama ya 20, kwao unapata internet ya kutumia vifaa zaidi ya kumi kwa wakati mmoja (simu, computers, smart tv, tablets) usiku na mchana mwezi mzima mukifanya kila munachotaka kwenye internet bila kupimiwa.
- Huduma za maji, umeme, internet, gesi, simu, tv hazikatiki na hazikatwi kienyeji hata ukishindwa kulipa bills. Tarehe ya kulipia ikifika huna pesa kwenye akaunti utafutatiliwa na kukumbushwa kwanza kwa muda ingawa ukichelewa sana utapigwa faini ya kukuumiza.
- Unaweza kuagiza KITU CHOCHOTE online (kwa kupiga simu au internet) na kikaletwa hadi mlangoni iwe dawa, chakula, nguo, viatu, mashuka, vinywaji, nk.
- Ukiiumwa unawasiliana na daktari kituo cha afya uliposajiliwa kabla ya uamuzi wa kwenda iwapo sio matatizo ya dharura. Matatizo yote ya dharura ukipiga simu ndani ya dakika chache ambulance iko mlangoni na ukichelewa kufungua wanaweza kuvunja mlango wakaingia wakidhani umezidiwa.
- Ukipata tatizo kama kupigwa na mke au mume, kuingiliwa na wezi, au mtoto kupigwa na mzazi; ukipiga simu ndani ya dakika chache polisi wako mlangoni.
Sasa linganisha mazingira haya yao nay a kwetu.
Sasa niambie, serikali ikitangaza karantini ya kumtaka kila mtu akae ndani na asichangamane hata na jirani yake tutaishije kwenye mazingira haya? Tutaweza kuishi hivyo hata kwa wiki moja? Na kama tukilazimika kwa kiboko kama kule Kenya, unadhani ni madhara kiasi gani tutapata?
- Sisi wananchi wengi hawana uwezo wa kununua chakula cha kesho. Inamlazimu mtu kutoka ndani kila siku ili angalau aweze kuweka mlo mezani.
- Sisi tumezoea kwenda dukani/sokoni kila siku au mara kadhaa kwa wiki kununua kila kitu kidogokigogo: tubamia, kaunga, tudagaa, tunyanya, tuvitunguu, tumchicha, nk.
- Sisi tuna familia nyingi hazijui umeme ni nini. Hata walionao, hauna uhakika wa kuwaka kila siku. Kwa wenzetu umeme kukatika kwenye nyumba kwa nusu dakika tu ni moja ya miujiza kwa mwaka labda kuwe na majanga kama vimbunga, mafuriko, nk.
- Sisi watu wengi hawana maji ya bomba ndani. Wengi inawalazimu kila siku kwenda kuteka maji mtoni, bombani, kisimani, chemchem, bwawani au hata kuomba kwa jirani mwenye uwezo. Wengi inawalazimu kutembea umbali mrefu kupata maji.
- Makazi yetu hayana anuani za kueleweka hivyo hatuwezi kuwa na huduma za kununua vitu online na kushushiwa nyumbani hata kama tukitaka.
- Wengi wetu tunaishi kwenye nyumba mbovu, mbaya, hazina mvuto, na wengine ni ndogo sana ukilinganisha na ukubwa wa familia. Pia wote nchi nzima tunaishi na mifugo kadhaa ndani ya nyumba. Kama sio mbuzi, kuku, kondoo au ng’ombe, basi tunaishi na mende, panya, viroboto, nzi na mbu.
- Hatuna maduka makubwa (supermarkets) kila mahali karibu na watu ambapo utasema watapata mahitaji ya lazima kwa urahisi wakiwa kwenye karantini. Wengi hutembea au kusafiri mbali kununua chakula madukani au sokoni
- Wananchi wengi wanatumia mkaa, kuni au mafuta ya taa kupikia. Wengine wakitaka kuwasha moto lazima wakaombe kiberiti au kaa la moto kwa jirani.
- Wengi wetu hatuna vyoo vya ndani na vya nje havitamaniki.
Mwisho
Msukumo wa kuishauri serikali kutangaza total lockdown, kama ilivyo kwa misukumo mingine kwenye janga hili, inatoka kwa kundi dogo la watu wenye uwezo (middle class). Duniani kote kundi hili hujisahau na kudhani kila mtu ana maisha kama yao. Lina kiwango kikubwa sana cha ubinafsi na wakati mwingine wanasahau kabisa kwamba hata ndugu zao wa karibu hawana uwezo walionao wao. Lakini ukweli ni kwamba kwa watanzania walio wengi karantini ya kututaka kukaa ndani ni janga kubwa mara nyingi kuliko Covid-19. Wanaoshawishi hatua hii wakumbuke kwanza kijijini kwao walikotoka wao au wazazi wao kukoje kabla hawajashauri total lockdown.
Serikali ichukue kila tahadhari na hatua wanazoshauriwa na wataalamu kuhusu kuzuia au kupunguza maambukizi ya Covid-19. Tusikilize wataalamu ni kwa jinsi gani tunaweza kuwakinga watu ambao wakipata maambukizi watadhuruka zaidi (wazee, wenye magonjwa ya kupua, na wenye chronic diseases). Ila isikubali wala kusikiliza ushawishi wa mtu, watu, taasisi, au nchi yoyote kuilazimisha kutangaza karantini katika hatua ya sasa.
Karantini ya kuwataka watu kukaa nyumbani (tena kwa muda usiojulikana) ni njia isiyofaa kwa wananchi wetu. Itakua na madhara makubwa sana kiafya, kijamii, na kimaisha iwapo itachukuliwa katika hatua hii. ndio tuko mwanzoni kabisa mwa maambukizi na hatuna hata mgonjwa mmoja aliye na hali mbaya. Kutangaza lockdown itakua ni sawa na kumkimbia mbwa kwa kuingia kwenye zoo walipo simba na chui huku ukidhani unatafuta kinga.
Kwa ngazi ya maambukizi tuliyopo sisi (ukilinganisha na nchi zilizoathirika sana na tabia ya mlipuko), bado tunaweza kuwa na maambukizi hadi miezi 5 au 6 kuanzia sasa. Njia ya lockdown naweza kusaidia kama suluhisho la mwisho kabisa wakati maambukizi yamezidi uwezo wa kukabiliana nayo: kwa maana ya kwamba watu wengi walioambukizwa watakua na hali mbaya kiafya (critical conditions). Ikifika hatua hiyo, mlipuko utakua umefika kileleni na kukaribia kushuka hivyo muda wa watu kukaa ndani utakua ni mfupi na madhara yatakua kidogo. Kitu cha kushauri serikali kwa sasa ni namna ya kuandaa mikakati ya nini cha kufanya iwapo tutalazimika kufikia hatua hiyo (worse case scenario). Ukiweka watu ndani sasa wakati hujui utawaweka kwa muda gani na huna uwezo wa kuwahudumia, madhara yake ni makubwa sana.
Pia tukumbuke sio lazima kila nchi ifikie hatua ya kua na vifo vingi kama tunavyoona Italy, Spain na kwingine. Ni makosa kuchukulia kinachotokea kwenye nchi hizo kama kielelezo na sababu ya kujengea hofu na taharuki katika kufanya maamuzi.
MM Togolani ([email protected])
Mwathirika wa "Total Lockdown"
------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
Ziada na hitimisho
Kwenye uzi huu nimefafanua na nimejibu hoja kinzani na maswali ya wachangiaji kadiri nilivyoweza. Kwa kufanya hivyo nimefafanua mambo mengine ambayo sikuyataja kwenye makala yangu. Kwa ujumla ninaweza kuhitimisha hoja namaswali yao kama ifuatavyo:
Nikisoma maoni, matusi, maonyo, hofu na taahadhari ya waotamani serikali itangaze total lockdown, hakuna hata mmoja anayetoa suluhisho au mbinu ya utekelezaje wake. Hakuna anayetoa data yoyote kiuchumi, kijamii, afya, nk. Hawatuambii watanzania wasio na maji, ajira, umeme, nk ambao wataathirika kuanzia siku ya kwanza ni asilimia ngapi na watasidikaje. Hoja yao ni moja tu, HOFU na watu wengi watakufa tusipotangaza Lockdown sasa. Hakuna scientific argument yoyote wanayotoa yenye ushawishi au theory and practices za crisis management or outbreaks control/response.
Kauli zao zinaonesha kifo kinachotisha ni cha Corona pekee. Vifo vitokanavyo na njaa, malaria, kipindupindu, kuhara, na utapiamlo (baadhi ya maradhi ambayo yatakumba wengi kukiwa na lockdown ya muda mrefu) havitishi wala sio tatizo. Tatizo ni Corona tu kwa madai kwamba tutakufa kama Italy na Spain. Wakati hofu hizi ni za msingi ila hazitakiwi kuwa msingi wa maamuzi na kufikiria kwetu.
Watu hawa hawaelevi bado inamaanisha nini hasa kuwa kwenye total lockdown. Hawatazami multiplying effect ya lockdown. Hawaelewi makampuni mengi yatafungwa na wafanyakazi watapoteza kazi. Hakuna mwajiri ataendelea kulipa mshahara watu wasiofanya kazi na yeye hazalishi. Hata makampuni yatakayooperate yatapunguza wafanyakazi kwa sehemu kubwa maana hakuna biashara. Nimeongea na wafanyakazi kadhaa wa sekta ya utalii wako majumbani hawana kazi na hawajui kazi itarejea lini. Waliobahatika kubaki na ajira wengine wameahidiwa wanalipwa nusu ya mshahara kwa miezi 3 au 5 wakati kisha maamuzi mengine yatafuata.
Kinachotokea na kitakachotokea zaidi, uwezo wa serikali kukusanya kodi utakua mdogo maana hakuna biashara; uzalishaji unapungua; PAYE itapungua maana watu wamepoteza kazi. Nchi yetu bado inategemea makusanyo ya kila mwezi kugharamia mahitaji muhim ya nchi kama kulipa wafanyakazi, kununua madawa, ulinzi na usalama, na kazi za utawala wa nchi.
Hivyo unapoishauri serikali kukimbilia total lockdown sasa na kwa muda usiojulikana (maana ndio tuko asubuhi mwa mlipuko), tuiambie pia itaendeshaje nchi. Kama hatuelewi complexity ya lockdown basi tuendelee tu kuisilikiliza kwenye vyombo vya habari kuliko kujiona sisi ni wataalamu wa utekelezahi wa total lockdown. Nirudie tena, huwezi kukimbia kung'atwa na mbwa (Corona) kwa kukimbilia walipo chui na simba (madhara ya total lockdown).
Namishukuruni waliosoma, waliochangia, waliokosoa, waliosahihisha, walioniita mjinga, na hata walionitukana. Wote wametumia uhuru weo kadiri ilivyowapendeza. Bado kuna mambo mengi ya muhim ya kuchambua na kujadili kuhusu Covid-19.
Mubarikiwe.
MM Togolani.
Yaani uumwe corona halafu ufanya kazi ngumu halafu utegemee kupona?Kua na hakika kwamba hatutakufa kama kuku. Hata tukiugua wote, tuna hakika (from existing evidence) wengi watapona.
Pili, huu uzi utabaki hapa labda JF waamua kuushusha. Matokeo yoyote yatakayotokea, hayabadili ukweli kwamba lockdown is an impractical solution in our setting and imposing it at the onset of the outbreak is an irrelevant and illogical decision. Mark may my position on this matter for future references.
MM Togolani
Ajifunze kuandika vizuri!Ushauri wangu kwenye Corona ni huu mara zote kwa watu kama hawa,tuombe Mungu sana Corona isienee nchini maana tutaisha kama kuku!
Bado naona serikali inafanya mchezo na Corona,tunaona watu bado wanakusanyika vituo vya mabasi,tunaona Makonda bado anakusanya watu na kuwahutubia,level seat bado sio suluhisho maana distance kati ya mtu na mtu ni Zero distance nk!
Kwa mazingira kama hayo,ni kuomba muujiza tu ndio utuokoe!
Hao walioamua total lockdown wana sababu zao,huenda wamepiga hesabu wakaona ni heri wachache wafe wengi wapome,kupanga ni kuchagua!
Kenya wako njia moja kwenda total lockdown. Watakapokwenda total lockdown utakuja hapa kufuta bandiko lako?
South Africa na Rwanda wako on total lockdown. Rwanda kaongeza siku 15 baada ya 14 za kwanza kwisha. Je hawa ndiyo wajinga sana na hawajui walitendalo.
Nadhani tatizo ni kushindwa kuelewa nature ya mlipuko kwenye huu ugonjwa. Ukiielewa vyema utatambua ugonjwa ukishaingia only way out for now ni total lockdown (pekee).
Tokea waathirika 200,000 jana, leo waathirika ni zaidi ya 1,000,000. Endeleeni kujidanganya kuwa nyie mna ufumbuzi usio na maumivu.
Wakuu hamna haja ya kuchukiana huo ndiyo ukweli mchungu.
Anasema Angel Merkel na pia Trump, changamoto za corona hazijawahi onekana tangu world war 2. Hali kadhalika kuutokomeza kwake hakuta kosa maumivu kweli kweli.
Ni rahisi zaidi kusalimu amri na kutoweka kwa huu ugonjwa au kupambana na ku survive. Uchaguzi ni wetu kama taifa.
Ina fahamika kwa nini ufumbuzi hauwezi kuwa wa mtu mmoja mmoja.
'Fools die'.
Rudi kwanza ukajifunze kuandika, nyie ndio wahamiaji haramu halafu mkipata bahati ya kupewa kitambulisho cha uraia mnaanza kujifanya wazawa ili mpate uongozi.
Shubaamit
Sent using Jamii Forums mobile app