Serikali isikubali kutangaza “total lockdown” au Karantini. Wanaoishawishi ama hawajui wanachokishauri au ni wabinafsi

Acha Acha mambo hayo wafunge tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Naunga mkono hoja.
 
Mtoa mada kakwambia yeye ni muathirika wa total lockdown, hivyo yupo nchi inayofanya hivyo...Wewe unaanza kuleta mambo ya uandishi wake;yana uhusiano gani na content yake?
Ajifunze kuandika vizuri!Ushauri wangu kwenye Corona ni huu mara zote kwa watu kama hawa,tuombe Mungu sana Corona isienee nchini maana tutaisha kama kuku!
Bado naona serikali inafanya mchezo na Corona,tunaona watu bado wanakusanyika vituo vya mabasi,tunaona Makonda bado anakusanya watu na kuwahutubia,level seat bado sio suluhisho maana distance kati ya mtu na mtu ni Zero distance nk!
Kwa mazingira kama hayo,ni kuomba muujiza tu ndio utuokoe!
Hao walioamua total lockdown wana sababu zao,huenda wamepiga hesabu wakaona ni heri wachache wafe wengi wapome,kupanga ni kuchagua!
 
Kwann mmezifunga shule na vyuo? Alafu usifikiri wamelock down kwa kupenda yakifika shingoni Mtalock down wenyewe tu. Haya siyo mambo ya kujisifu.tuombe MUNGU ATUSAIDIE tu
 
Sasa hivi maeneo ya mjini watu ni wachache kuliko kawaida. Watu wameamua kuchukua hadhari kadiri inavyowezekana. Kampeni kubwa iwe ni ya matumizi ya barakoa. Ikibidi kufanya lockdown, basi iwe ni kwa asiye na barakoa: usitoke nje bila barakoa, hata ya kutengeneza kimila.
 
Kawaulize Kenya kwa nini hakuna total lockdown mpaka sasa ilhali cases zimehit 100+ sababu unaongea mambo ya aibu tu

Kenya wako njia moja kwenda total lockdown. Watakapokwenda total lockdown utakuja hapa kufuta bandiko lako?

South Africa na Rwanda wako on total lockdown. Rwanda kaongeza siku 15 baada ya 14 za kwanza kwisha. Je hawa ndiyo wajinga sana na hawajui walitendalo.

Nadhani tatizo ni kushindwa kuelewa nature ya mlipuko kwenye huu ugonjwa. Ukiielewa vyema utatambua ugonjwa ukishaingia only way out for now ni total lockdown (pekee).

Tokea waathirika 200,000 jana, leo waathirika ni zaidi ya 1,000,000. Endeleeni kujidanganya kuwa nyie mna ufumbuzi usio na maumivu.

Wakuu hamna haja ya kuchukiana huo ndiyo ukweli mchungu.

Anasema Angel Merkel na pia Trump, changamoto za corona hazijawahi onekana tangu world war 2. Hali kadhalika kuutokomeza kwake hakuta kosa maumivu kweli kweli.

Ni rahisi zaidi kusalimu amri na kutoweka kwa huu ugonjwa au kupambana na ku survive. Uchaguzi ni wetu kama taifa.

Ina fahamika kwa nini ufumbuzi hauwezi kuwa wa mtu mmoja mmoja.

'Fools die'.
 
Lock down inakuja. Utake usitake. Kwanza tumeshachelewa kuanza na matokeo ya kuchelewa tutaanza kuyaona muda siyo mrefu.
Watanzania Tujiandae kulia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sielewi pointi yako ni nini
 
Nakuunga mkono mkuu. Serikali haijazuia 'personal or family lock down', anayeweza kujifungia ajifungie sisi wengine tuendele na mambo yetu.

Sent using Jamii Forums mobile app

Lockdown ni solution ya nchi haiwezi kuwa ya mtu mmoja mmoja au familia.

Huu siyo ukimwi wakuu.

Ndiyo maana lockdown zinakuwa enforced. Bakora hata risasi zinatembea.

Imeshaelezwa sana hii. Bila shaka utakuwa umewasili tu muda mfupi uliopita tokea sayari nyingine.

Karibu duniani mkuu. Tafadhali ujisikie kama uko Mars.
 
Tena hapo Kahama ikitangazwa Lockdown cha moto mtapata.

Mazingira yake sio tofauti na Dar

Sent using Jamii Forums mobile app
 
when a slave dies he loses nothing but his pain!! ni kweli maskini hana cha kupoteza!! matajiri wasiojua njaa ndio wanaoshinikiza lockdown ili wajaze misosi ndani na kufurahia mateso ya maskini watakaopigwa mabuti na virungu kwa kutapatapa barabarani kutafuta msosi,

Karl Marx anasema economic determinism should be a point of departure yaani mtu anaposhinikiza jambo lake au kuanzisha mgogoro wowote angalia kuna maslahi gani ya kiuchumi atapata, Max Weber anasema uende mbali zaidi kuangalia maslahi mengine kama political gains, power, new social status na mengine! walioshindwa uchaguzi na wapinzani ndio wanataka total lockdown ili kuwe na vurugu wapate agenda!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…