Serikali isimamie Tamko la Maaskofu lisisomwe Kanisani

Hakuna anayecheza na dini naamini kila mtu anauheshimu ukubwa wa taasisi katoliki.

Huu ni uwekezaji wa pili hapo bandarini unaotarajia kufanyika kuanza mwezi wa kumi mwaka huu, kutakuwa na uwekezaji wa tatu hapo hapo bandarini pia kutakuwa na uwekezaji wa bagamoyo port.

Inategemea uwezo wa mtu mmoja wa kutazama hii mipango ya kiserikali imekaa vipi, maana serikali kuu inapokea malalamiko kila siku kutoka kwa mataifa ya jirani kwamba kuna uzembe hapo bandarini na wateja wanaikimbia hiyo bandari kila siku, sidhani kama viongozi wa kanisa wanayatazama yanayotokea katika muktadha huo,kwa kweli sidhani.
 

Unajaribu kueleza kuwa serikali inashindwa kudhibiti uadilifu hapo bandarini?
 
Unajaribu kueleza kuwa serikali inashindwa kudhibiti uadilifu hapo bandarini?
Tatizo letu kitaifa ni pana zaidi ya uadilifu. Kuna masuala ya teknolojia za kisasa kukosekana hapo bandarini. Kuna masuala ya sekta nzima ya usafiri majini kuhitaji kuongezewa uwezo wa kielimu.

Inasikitisha kuona maaskofu wanaingia kirahisi kwenye huu mtego wa 'mwarabu' kutaka kupewa bandari na kuiuza nchi!.
 

Kwa mujibu wa mkataba, unahusisha Bandari ngapi?
Umri wa mkataba?
Na unazungumziaje kuhusu baadhi ya sheria za nchi kubadilishwa kisa huu mkataba?
 
Kwa mujibu wa mkataba, unahusisha Bandari ngapi?
Umri wa mkataba?
Na unazungumziaje kuhusu baadhi ya sheria za nchi kubadilishwa kisa huu mkataba?
TPA tu hapo kurasini, gati namba tatu mpaka namba nane yaani ni asilimia nane ya eneo zima la bandari ya Tanzania.

Umri wa mikataba ya kazi ndio swali sahihi zaidi, inategemea na ukubwa wa biashara zinazokwenda kufanyika, inetegemea na uwekezaji wa mwekezaji na namna anavyorudisha faida yake.

Hana uwezo mwekezaji mmoja wa kubadilisha sheria nyingine za nchi, ni sawa na pale airport kuna Swissport anafanya uwekezaji wa miaka na miaka, hakuna sheria yoyote ya nchi iliyoguswa na ni hivyo kwa suala zima la bandari.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…