Serikali isimamie Tamko la Maaskofu lisisomwe Kanisani

Hakuna aliyewajibu toka wameanza mitandaoni, wakaja mikutanoni, sasa wameanza makanisani, waingie na barabarani. Wawaambie na taasisi yao ya bakwata iwasaidie kusambaza waraka misikitini.

Watu hatuna muda na ujinga.
Nani ana jeuri ya kuwajibu? Kwani wamenyamaza kwa kwa kupenda?

Mama akienda mahali, intelijensia inasambazwa, mabango hata ya siri yanaibuliwa na kupokwa.

Wanaume hawakutaka kuwapa tabu wana-intel, wakatangaza wazi watasoma waraka na hakuna aliyezuia.

Lingekuwa jambo la wapinzani kwanza wangekutana na virungu vya polisi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tulifikirie hili swala bila jazba kwa sababu ni jambo ambalo linaweza kuhatarisha amani ya nchi. Propaganda hiyo itakayotokea na huo waraka wa TEC kusomwa Kanisani ni jambo ambalo serikali itashindwa kutanzua.

TEC imetoa tamko na serikali imesikia, hiyo inatosha. Serikali iingize mkono Kanisani. That is my robotic advice. Vinginevyo sasa, tutakuwa na serikali ngapi?
Hawana huo uwezo.
 
Hahahahaha.

Slaa, leo kaongea kiheshima, kama wale wa jana. Hakuna kujimwambafai.
 
Tulifikirie hili swala bila jazba kwa sababu ni jambo ambalo linaweza kuhatarisha amani ya nchi. Propaganda hiyo itakayotokea na huo waraka wa TEC kusomwa Kanisani ni jambo ambalo serikali itashindwa kutanzua.

TEC imetoa tamko na serikali imesikia, hiyo inatosha. Serikali iingize mkono Kanisani. That is my robotic advice. Vinginevyo sasa, tutakuwa na serikali ngapi?
Jumuiya ndogondogo ni zaidi ya hapo kanisani unapo paona.
 
HAIWEZEKANI KUWATENGA VIONGOZI WA KANISA NA SIASA ZA NCHI YAO!

Wapendwa Watanzania!
Limekuwa ni jambo la kawaida kwa watawala au watu walio karibu na watawala wa Tanzania wakibanwa na viongozi wa dini hasa maaskofu huanza kutoa maneno ya propaganda dhidi ya viongozi wa dini wakiwaambia 'wasichanganye dini na siasa'. Msemo huu wanautumia kama kichaka cha kujifichia wasiguswe na viongozi wa dini!

Kauli hizo zimeibuka tena kwa kishindo zaidi kuanzia mwezi Juni 2023 baada ya maaskofu kuingilia sakata la Mkataba wa Bandari. Hivi karibuni tuliikemea Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ilipoitisha mkutano wa viongozi wa vyama vya siasa ili kujadili hoja ya viongozi wa dini kuonekana wakiwa na viongozi wa vyama vya siasa.

Tumeona ni wajibu wetu ili kuwaelimisha watu kuhusu suala hili kusudi wasije wakapotoshwa na wanasiasa katika suala zima la kudai haki katika taifa lao. Wanasiasa ni wajanja sana na wanajua nafasi na nguvu ya viongozi wa dini katika jamii ndio maana wanatumia nguvu ili kupotosha ukweli kuhusu nafasi ya viongozi wa dini katika ukombozi wa kifikra katika taifa.

Tunapenda kukiri kuwa hili tunaloliandika ndilo eneo ambalo sisi tuna ubobezi nalo, kwa hiyo hatubahatishi bali tunakiandika tunachokijua, tulichokisomea na kukifundisha katika ngazi za Chuo Kikuu.

Kwa upande wa Wakristo, chimbuko la dini hiyo ni mji wa Yerusalemu, Israeli ya Kale. Lakini, ni vizuri watu wakaelewa kuwa Ukristo una mizizi yake miaka 5000 kabla ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo. Hivyo, msingi mkubwa wa mafundisho ya Ukristo ni Biblia Takatifu yenye sehemu kuu mbili - Agano Jipya na Agano la Kale.

Dini haifanywi kwa wanyama na wala siasa pia haifanywi kwa ndege. Dini ni mfumo mzima wa maisha ambao ndani yake kuna mambo mengi. Tunaposoma au kufundisha kuhusu dini lazima tusome maisha ya jamii nzima ambayo kwanza dini ilifika kwayo. Kwa upande wa Wakristo, sisi tunasoma kuhusu jamii mbalimbali kama Misri, Syria, Ukaldayo (Babeli), Rumi, Wagiriki, Jordan, Waisraeli, Waajemi, Waarabu, Lebanon, nk.

Katika kusoma na kujifunza dini tunafundisha waumini kuishi kwa mifano ya jamii hizo ikiwa ni pamoja na kuiga mema na kuyaacha mabaya na hayo yanawezekana tu kwa kusoma kuhusu maisha yao kupitia viongozi au manabii wao.

Tunaposoma na kujifunza Biblia tunakutana na mambo yafuatayo:
1. Familia (family institutions): familia, ndoa, watoto, wajane, urithi, kifo, maziko, nafasi ya wanawake katika jamii, nk

2. Taasisi za Kiraia (Civili institutions): idadi ya watu, utumwa, taasisi ya kifalme, familia za kifalme, utawala, ajira na uchumi, kilimo, Afya na tiba, sheria na haki, mgawanyo wa muda, vipimo vya uzito, mahakama, nk.

3. Taasisi za Kijeshi (military institutions): majeshi ya Israeli, ngome za kijeshi, mbinu za kivita, siraha za kivita, vita, vita vitakatifu, nk

4. Taasisi za dini (Religious institutions): ibada, madhabahu, nyumba za ibada, uongozi wa taasisi za dini, Ofisi ya Ukuhani, Ofisi ya Walawi, sadaka, imani potofu, uchawi, utaratibu wa ibada, siku za ibada, sherehe na siku za sikukuu, nk.

Watu waliokuwa juu ya yote hayo ni viongozi wa dini na ndio waliopewa majukumu ya kuifundisha na kuionya jamii. Taasisi hizo ziliwekwa kwa ajili ya watu na kilichotofautisha ni ratiba. Wakati wa vita walipigana na wakati wa amani watu hao walifanya sherehe. Wakati wa mambo mazito ikiwemo kujua mustakabari wa nchi walikwenda kutafuta ushauri kwa viongozi wa dini. Alipotokea kiongozi mkorofi au jeuri alikemewa na viongozi wa dini au hata kutangaziwa kuondolewa madarakani na hao viongozi wa dini.

Sisi Askofu Mwamakula tunaitoa kwenu elimu hii ili msiyumbishwe ili muelewe kuwa viongozi wa dini kuingilia kati mtafaruku wa kisiasa au kiutawala ni ishara kuwa jamii yenu iko na afya!
Je, nini kimekushangaza? Je, nini maoni yako?

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki
Dar es Salaam, 20 Agosti 2023; 12:35 jioni.

Sent from my TECNO BC1 using JamiiForums mobile app
 
Hakuna aliyewajibu toka wameanza mitandaoni, wakaja mikutanoni, sasa wameanza makanisani, waingie na barabarani. Wawaambie na taasisi yao ya bakwata iwasaidie kusambaza waraka misikitini.

Watu hatuna muda na ujinga.
Mnamiliki vyombo vya usalama
Tunajua nini maana ya kusema mtatujibu.
 
Mama katowa majibu jana kwa vitendo, mapoyoyo hamkumuelewa.

Kwa mara ya kwanza, toka aisambaratishe bodi ya wakatoliki mwaka 2021, TPA wamepeleka faida serikalini.

Hizo ndo zinaitwa pumba tena mbichi.

Yaani serikali ilikasimu Wakatoliki kuendesha Bodi ya TPA? Nchi hii ina siri nyingi sana😄
 
Leo kanisani kondoo wameimbishwa kwaya mpya ya DP-WORLD.

Unayo habari?
 
Back
Top Bottom