Serikali isimamishe shughuli za Precision Air haraka

Uzuri ajali ya ndege huwa haiachwi ipite, lazima majibu ya kiuchunguzi yatapatikana...
 
Kuna ka ukweli flani hapa nimewahi kupanda hii kitu kama mara tatu hivi kwa Route za Dar to Mwanza na Dodoma to Kilimanjaro ni kweli hizi ndege za Precision air ni kama zimeanza kuchoka flani hivi.!
Kuna mdau aliwahi kunambia kwamba hizi ndege zilinunuliwa mtumba kutoka UN ila sina uhakika
 
mleta umeongea vitu vyenye madini.

Tusubiri uchunguzi sababu zinaweza kuwa nyingi za kiufundi, Hali ya hewa, Hata uchovu wa rubani na kuadhiri maamuzi yake .
 
mleta umeongea vitu vyenye madini.

Tusubiri uchunguzi sababu zinaweza kuwa nyingi za kiufundi, Hali ya hewa, Hata uchovu wa rubani na kuadhiri maamuzi yake .

Sawa
 
Kwa kosa gani?
 
Waliowahi kutumia ndege za precision wameweka ushahidi wa hitilafu wanazokutana nazo.
Mimi binafsi pia nimekutana na hali zisizo za kawaida sio chini ya mara tatu kuanzia mwaka 2017.

Ndege zichunguzwe pamoja na kua hali ya hewa imechangia kwenye ajali.

Mnaobisha msilete ushabiki wa kudai kua ni wivu dhidi ya precision. Kama umewah kua ndani ya ndege hizi na ukaskia majibu yao pindi inapotokea shida hutotaman kutumia ndege hizi.
 
Mimi nilihairisha kupanda precision siku tulipotoka Arusha tunakuja mwanza tukashindwa kutua kukatangaziwa tunaweza kitua bukoba au Uganda ikashindikana tukarudi Arusha baada ya hapo nikarudi nyumbani usiku nikaondoka na Air Tanzania Kilimanjaro nikatua mwanza safi kabisa.Toka wakati huo mimi ni mteja mwaminifu wa Air Tanzania.Siku hiyo nilitubu zaidi ya mara 20 ,watu walisali sana Sasa safari kama hizi za Nini Sasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…