Serikali isipowapiga marufuku 'Mitume na Manabii' wa mchongo, miaka michache ijayo tutakuwa na Taifa la ovyo sana

Wacha Magugu na Ngano vikue pamoja.Mwenye shamba atakuja kuchambua mwenyewe. Ngano aweke ghalani Magugu achome moto. Wewe ni nani hata uhukumu? Hakuna mtu anaweza kuzuia kazi ya Mungu kufanyika. Wewe mwenyewe huo ulionao ni ushetani unakutesa Ndio maana hupendi kazi ya Mungu ifanyike. Tubu Sasa. Wokovu ni Sasa. Yesu anakupenda.
 
Wewe hujui siasa za nchi hii, Samia akipiga marufuku watasema anataka kuifanya Tanzania iwe Islamic state, atajiongezea chuki na maadui wengi zaidi
Magufuli alipoona anazongwa sana na Katoliki na Lutheran kwa udikteta wake kipindi kile, aliwatumia hawa manabii uchwara na kuwaita ikulu au kila kilipokuwa na shughuli ya serikali

Akina Kakobe, Gamanywa, Gwajima, Mzee wa Upako walituniwa sana kisiasa
 
Wacha waliwe pesa zao na muda wao ujinga ni kipaji cha mtu.
DAR hakuna mashamba ya kulima unataka manabii waishi vipi?
 
Naingia kwenye mada moja kwa moja bila kupepesa macho wala kutikisa masikio. Kwa muda mrefu sasa nimekuwa nikifuatilia huduma zinazotolewa na hawa manabii na mitume wanaoibuka kama uyoga hapa nchini.

Nimegundua Serikali isipochukua maamuzi magumu kuwapiga marufuku hawa watu, miaka michache ijayo tutakuwa na taifa na kizazi zembe na ovyo sana. Sisemi maneno matupu bali nina ushahidi kuntu juu ya hili jambo.

View attachment 2411428
Nimezaliwa Kenya lakini kwa bahati nzuri nimekulia jiji la Dar ambako manabii na mitume wengi huibukia na kuanza kazi yao ovu ya kuwarubuni akina mama na watoto wakiwakamua fedha bila huruma.

Mwanzoni aliibuka nabii Tito lakini huyu jamaa Mungu alimpiga kipapai na kumuondoa kwenye ushetani moja kwa moja. Baadaye alikuja Mtume na Nabii Josepahat Mwingira ambaye hadi sasa yupo na anajaribu kujitanua hadi nchi za nje ijapokuwa soko limekuwa gumu baada ya kuibuka manabii wengine. Hajakaa sana akaja mama wa upepo wa kisulisuli kutoka mlima wa moto.

Naye alizipiga sana kabla ya kuitwa na Mungu wa ukweli kwenye nyumba yake ya milele.

View attachment 2411459
Alifuata Nabii Lusekelo (Mzee wa Upako) akawadanganya sana akina mama kwamba atawapa upako wa kununua magari na kuwajaza mali nyingine kedekede. Pia aliwarubuni kuwa atawapa upako wa kuhamia nje ya nchi wakaishi maisha mazuri huko (kumbuka Wasabato masalia waliokusanyika uwanja wa ndege kutaka kwenda Marekani pasipokuwa na pasipoti wala nauli ya kuendea huko). Mzee wa Upako aliwapiga sana hela akina mama kabla ya Mungu wa kweli kumuumbua kwenye ulevi na huo ndio ukawa mwisho wake.

Hatimaye amekuja Nabii Mwamposa (Bulldozer); sasa hivi huyu ndiye yupo kwenye chati. Uzuri ni kwamba baada ya nabii mmoja kuwa maarufu na kuongezeka kiwango cha upigaji, Mungu humshusha ghafla na kumrudisha chini kabisa. Mungu ni mkubwa na wala hajawahi kudhihakiwa.

Huyu Bulldozer sasa hivi amekuwa mwiba kwenye kuwaibia fedha akina mama. Eti anawaambia watoe pesa zote walizonazo wampe kama sadaka (kujimaliza) kisha atawaombea wapate utajiri.

Makubwa! Kama ana uwezo wa kuwabariki wenzake wapate fedha, kwanini asijibariki yeye mwenyewe apate mamilioni ya fedha badala ya kutumia ulaghai kuwauzia wafuasi wake mafuta, maji na udongo wa upako? Hana tofauti na mganga wa jadi anayekuambia umlipe pesa akupe pesa za majini.

Kwanini yeye asitengeneze hizo fedha za majini badala yake anawaomba wateja fedha halali halafu anawaahidi fedha za majini? Nonsense!

Baada ya watu wengi kugundua utume na unabii ni njia ya kutoka kimaisha, kila mtu sasa anataka kukimbilia huko. Eti hadi Masanja Mkandamizaji naye kafungua kijiwe cha kupigia hela, anajiita “Askofu”. Ni askofu gani ambaye anaibuka from no where hajaenda hata bible college akasome theology anakuja hapa kuwadanganya watanzania kwamba yeye ni Askofu? Hivi hawa watu wanatuonaje?

Wanwake wengi wamewaacha waume zao baada ya kupigiwa ramli na manabii zao kwamba waume walio nao kwa sasa sio waume sahihi, hivyo kupelekea ndoa nyingi kuvunnjika na kusababisha maumivu kwa watoto wasiokuwa na hatia na wengi wao wamegeuka kuwa ombamba na watoto wa mitaani. Inauma sana.

Akina mama wapo tayari kugegedwa na manabii au kukubali kushiriki ujinga wowote ilmradi tu waahidiwe mafanikio hewa. Akina mama wasiopata mimba kwa muda mrefu ni rahisi kurubuniwa na manabii wanaojidai kuingiza upako ukeni kupitia uume. Na kwa akili zao finyu, wanawake hawakatai wala kupinga kila masharti wanayopewa na mitume na manabii hawa wa mchongo.

Mh mama Samia, wanawake wenzako na wapigakura wako wanaaangamizwa kwa kukosa maarifa. Wanapotoshwa kwa kiasi kikubwa sana na hawa manabii na mitume wa mchongo. Hakuna fedha/mafanikio yanayopatikana pasipo kufanya kazi

. Kama tukiendelea na tabia hii ya kuishi kwa kutegemea miujiza, baada ya miaka michache ijayo taifa hili litakuwa na watu wa ajabu sana, wasiopenda kufanya kazi lakini wanataka mafanikio ya haraka kupitia miujiza ya kufikirika.

Tazama hata wazungu waliotuletea hizi dini za ajabu tukasahau dini zetu za jadi wao hawashiriki kwenye miujiza hii ya kufikirika. Wachina wajapan, wahindi na makabila mengine huko Ulaya na Asia huwezi kuwaona wakiamninishwa kirahi kama sisi waswahili.

Amkeni kumekucha!
Matapeli kwa jina la yesu yalitabiriwa haya.Na watu kwa ujinga na uhaba wa iman wanajazana kuwalimbikizia watu utajiri.Wanahubiri c kuwafundisha watu biblia wajengwe ktk imani na mola bali wanahubiriwa majini,utajiri,kazi,kuoa na kuolewa,uchawi yani ujinga mzigo.
 
Manabii ni mbadala wa wizara ya afya wanaisaidia serikali kwenye kutimiza wajibu huo hivyo hawataguswa kamwe
 
Bora manabii feki au bora ukawekeze Qnet, forever living unapigwa mchana kweupe. Ujanja na wewe kuwa mpigaji
 
Hii ndio inawatia umasikini waumini moja kwa moja lakini hawajifunzi na wala huwaambii kitu. Nchi hii imefika mahali pabaya sana.
Naona kama Watu wamekata tamaa.
 
Kuna mambo mengi yanasababisha watu kuingia huko wakitegemea kupata wepesi wa maisha.

Ukiangalia wanawake wengi wanaoingia huko ni wale ambao wametelekezwa, wamenyanyasika katika ndoa, wamezalishwa na kuachwa na wametendwa na wanaume. Hivyo sisi wanaume tuna changia tatizo hili kwa kiasi kikubwa. Wanawake hawa huingia huko ili kupata faraja, kupata matumaini, kutetea ndoa zao n.k.

Pili ni ukosefu wa ajira. Kama watu wangekuwa busy na shughuli zao zinazo waingizia kipata cha kutosha wasingeoata muda wa kwenda huko. Lakini hujikuta wakiingia huko wakidhani kwamba labda mungu atawafungulia wapate kazi, biashara n.k.

Hat hivyo, Mimi nadhani ni upepo tu na unapita. Miongo miwili ijayo sidhani kama watapata mtu wa kumfanyia haya. Watu watajitambua na kuona kuwa wamepotezewa muda bila mafanikio waliyo tarajia.

Cha msingi kila mtu aelimisha watu wake wa karibu ambao wamejiingiza huko.

Mimi dada yangu alikuwa huko..nimeongea naye sana nikajaribu kumwelewesha..ingawa ilichuka muda hatimaye amatoka. Nilimwambia vitu vinne.
1. Ajenge tabia ya kusali na kumuomba mwenyezi mungu akiwa peke yake. Kila mtu anauwezo wa kuomba na kusikilizwa na mungu bila kuhitaji kuombewa. Mungu hana wakala na haitaji wakala. Hivyo kama ni swala la maombi afanye mwenyewe na mungu atamsikiliza.
2. Makanisa ni social gathering. Si jambo baya watu wenye imani inayofanana kuunda umoja kama ilivyo saccoss, vicoba etc. Lakini mwisho wa siku Mungu huangalia imani na matendo ya mmoja mmoja na anambariki kwao. Hivyo haubarikiwi.kwa sababu unasali au uko kwenye kanisa fulani.
3. Hawa wanaojiita mitume ni wapiga kama wapigaji wengine. Nikamwambia, je fedha zote ambazo wanakusanya kwa waumini huwa wanazipeleka wapi? Umewahi kusikia hata wameanzisha kituo cha watoto yatima? umewahi kusikia hata wana support watoto walio kwenye mazingira magumu kusoma? umewahi kusikia hata wameanzisha zahanati. Umewahi kusikia wamefanya jambo lolote kwenye jamii yenu?
4. Pia nikampa assignment afuatilie watu wanasimama pale mbele na kushuhudia. Mimi nilimwambia wale ni wa michongo akawa anabisha. Siku moja akafuatwa na washirika wa mchungaji waka mtengeneza jumapili ijayo atoe ushuhuda. Akaahidiwa kupewa 50,000. Nashukuru mungu siku hiyo ndo ikawa mwisho wa kuamini hao ndugu...na kidogo akapungiza kwenda na hatimaye akaacha.
 
Back
Top Bottom