Serikali isipowapiga marufuku 'Mitume na Manabii' wa mchongo, miaka michache ijayo tutakuwa na Taifa la ovyo sana

Wacha Magugu na Ngano vikue pamoja.Mwenye shamba atakuja kuchambua mwenyewe. Ngano aweke ghalani Magugu achome moto. Wewe ni nani hata uhukumu? Hakuna mtu anaweza kuzuia kazi ya Mungu kufanyika. Wewe mwenyewe huo ulionao ni ushetani unakutesa Ndio maana hupendi kazi ya Mungu ifanyike. Tubu Sasa. Wokovu ni Sasa. Yesu anakupenda.
 
Wewe hujui siasa za nchi hii, Samia akipiga marufuku watasema anataka kuifanya Tanzania iwe Islamic state, atajiongezea chuki na maadui wengi zaidi
Magufuli alipoona anazongwa sana na Katoliki na Lutheran kwa udikteta wake kipindi kile, aliwatumia hawa manabii uchwara na kuwaita ikulu au kila kilipokuwa na shughuli ya serikali

Akina Kakobe, Gamanywa, Gwajima, Mzee wa Upako walituniwa sana kisiasa
 
Wacha waliwe pesa zao na muda wao ujinga ni kipaji cha mtu.
DAR hakuna mashamba ya kulima unataka manabii waishi vipi?
 
Matapeli kwa jina la yesu yalitabiriwa haya.Na watu kwa ujinga na uhaba wa iman wanajazana kuwalimbikizia watu utajiri.Wanahubiri c kuwafundisha watu biblia wajengwe ktk imani na mola bali wanahubiriwa majini,utajiri,kazi,kuoa na kuolewa,uchawi yani ujinga mzigo.
 
Manabii ni mbadala wa wizara ya afya wanaisaidia serikali kwenye kutimiza wajibu huo hivyo hawataguswa kamwe
 
Bora manabii feki au bora ukawekeze Qnet, forever living unapigwa mchana kweupe. Ujanja na wewe kuwa mpigaji
 
Hii ndio inawatia umasikini waumini moja kwa moja lakini hawajifunzi na wala huwaambii kitu. Nchi hii imefika mahali pabaya sana.
Naona kama Watu wamekata tamaa.
 
Kuna mambo mengi yanasababisha watu kuingia huko wakitegemea kupata wepesi wa maisha.

Ukiangalia wanawake wengi wanaoingia huko ni wale ambao wametelekezwa, wamenyanyasika katika ndoa, wamezalishwa na kuachwa na wametendwa na wanaume. Hivyo sisi wanaume tuna changia tatizo hili kwa kiasi kikubwa. Wanawake hawa huingia huko ili kupata faraja, kupata matumaini, kutetea ndoa zao n.k.

Pili ni ukosefu wa ajira. Kama watu wangekuwa busy na shughuli zao zinazo waingizia kipata cha kutosha wasingeoata muda wa kwenda huko. Lakini hujikuta wakiingia huko wakidhani kwamba labda mungu atawafungulia wapate kazi, biashara n.k.

Hat hivyo, Mimi nadhani ni upepo tu na unapita. Miongo miwili ijayo sidhani kama watapata mtu wa kumfanyia haya. Watu watajitambua na kuona kuwa wamepotezewa muda bila mafanikio waliyo tarajia.

Cha msingi kila mtu aelimisha watu wake wa karibu ambao wamejiingiza huko.

Mimi dada yangu alikuwa huko..nimeongea naye sana nikajaribu kumwelewesha..ingawa ilichuka muda hatimaye amatoka. Nilimwambia vitu vinne.
1. Ajenge tabia ya kusali na kumuomba mwenyezi mungu akiwa peke yake. Kila mtu anauwezo wa kuomba na kusikilizwa na mungu bila kuhitaji kuombewa. Mungu hana wakala na haitaji wakala. Hivyo kama ni swala la maombi afanye mwenyewe na mungu atamsikiliza.
2. Makanisa ni social gathering. Si jambo baya watu wenye imani inayofanana kuunda umoja kama ilivyo saccoss, vicoba etc. Lakini mwisho wa siku Mungu huangalia imani na matendo ya mmoja mmoja na anambariki kwao. Hivyo haubarikiwi.kwa sababu unasali au uko kwenye kanisa fulani.
3. Hawa wanaojiita mitume ni wapiga kama wapigaji wengine. Nikamwambia, je fedha zote ambazo wanakusanya kwa waumini huwa wanazipeleka wapi? Umewahi kusikia hata wameanzisha kituo cha watoto yatima? umewahi kusikia hata wana support watoto walio kwenye mazingira magumu kusoma? umewahi kusikia hata wameanzisha zahanati. Umewahi kusikia wamefanya jambo lolote kwenye jamii yenu?
4. Pia nikampa assignment afuatilie watu wanasimama pale mbele na kushuhudia. Mimi nilimwambia wale ni wa michongo akawa anabisha. Siku moja akafuatwa na washirika wa mchungaji waka mtengeneza jumapili ijayo atoe ushuhuda. Akaahidiwa kupewa 50,000. Nashukuru mungu siku hiyo ndo ikawa mwisho wa kuamini hao ndugu...na kidogo akapungiza kwenda na hatimaye akaacha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…