Serikali isitishe kujenga Dodoma kwanza

Stupidity thread
 
Loud and clear
 
Watanzania tuache habari za kumuachia Mungu. Watu waovu kwa watu wanamtanguliza kama kichaka, hata wakoloni walitufanyia hivyohivyo wakati wanakuja kutupora. Binafsi sihudhurii mkutano wa siasa ambao unatanguliza masheikh na wachungaji, ni kupumbaza wananchi. Wabunge kama hawa hawezi kuwepo kwenye katiba, bunge na mahakama kama za Kenya.
 
Kenya
Itatutawala huko mbele ya safari
 
Hapo kwa wabunge 19 umekosea,hata ukiwatoa hao bungeni nafasi zao zotajazwa na wengine fasta na kuendelea kula pesa. Bora waendelee kula haohao mpaka wananchi watakapokuwa serious na katiba mpya
 
Hapo kwa wabunge 19 umekosea,hata ukiwatoa hao bungeni nafasi zao zotajazwa na wengine fasta na kuendelea kula pesa. Bora waendelee kula haohao mpaka wananchi watakapokuwa serious na katiba mpya
Ziliwe na walio Halali, Sasa tangu wako pale izo pesa zinalika kihalali, si wizi tu,
 
Dawa ni kufundishana namna nzuri ya kupiga kura. Kila mtu awe tayari kudai katiba mpya inayolinda kura yake isipotee.

Njia nzuri ya kufikia huko ni machafuko tu.
 
Kama una pesa ya Bando ni wazi huna njaa..

Vijijini bando ni anasa.
Ndo maana tulioko Mjini ndo tunawatunza walioko vijijin, ukitumia bibi au ndugu yako Kijiji 40, tiyari umeongezea mzunguko wa mahali pale , ila vijijin watu pia wameelimika wengine kwao sio anasa kama tulio mjini
 

Wewe fikiri Mtu anamuomba Mtu kunukuu mistari ya Neno la Mungu anaye muamini. Huyo mtu anaye ombwa anafanywa amkufuru Mungu pengine bila yeye kujua. Anaye omba anamdhalilisha Mungu wake bila kujua. Matendo ya Mitume 12:21-23
 
Wewe fikiri Mtu anamuomba Mtu kunukuu mistari ya Neno la Mungu anaye muamini. Huyo mtu anaye ombwa anafanywa amkufuru Mungu pengine bila yeye kujua. Anaye omba anamdhalilisha Mungu wake bila kujua. Matendo ya Mitume 12:21-23
Mtu yeyote anaetaka kukufanya punda wake atakupumbaza kwanza kwa neno la mungu, lakini wao hawaliishi neno la mungu ila wanakutaka wewe umuogope mungu. Kila kulikokuwa na ofisi za wakoloni kulikuwa na wamissionari. Sasa hivi kila waliko wanasiasa wako masheikh, mapadre na wachungaji sawa na walivyofanya wakoloni, copy and paste.
 
Natamani kusikia serikali ikisema kwasasa kutokana na hali mbaya ya uchumi, ukame, COVID-19 na kupanda kwa bidhaa tumesitisha kujenga mji wa serikali Dodoma badala yake tutajikita kwenye miradi ya mkakati kama kupeleka mawasiliano(mkongo) hadi ngazi ya kila wilaya na tarafa, maji, umeme, dawa, mikopo ya elimu hadi hapo hali ya uchumi itakapotengemaa.

Lakini sio kuendelea kujenga majengo ambayo tayari yapo dar es salaam na kwingine kwa kuongeza tozo kwa wananchi. Hebu fikiria serikali imeshakata Kodi (PAYE) kwenye mshahara wa mtumishi, halafu kile kilichobaki kilichopelekwa Benki serikali wanakivizia tena njiani wakati unakotoa Benki na kukikata tena. Ni sawa na mnunuzi wa ng'ombe aliyenunua ng'ombe wako mnadani kisha akatuma wezi wakufuate nyumannyuma wakuibie hizo hela njiani wakati ukielekea nyumbani kwako.
 
Unajua gharama ya kuwarudisha watumishi Dar es salaam??. By the way ujenzi wa Dodoma unachukua percentage ndogo sana ya bajeti ya Serikali. Ungekuwa hata umekuja na facts tu basi huenda ingesaidia kufanya judgement. Pia ujenzi wa Dodoma unaongeza pesa kwenye mzunguko na umetoa ajira kwa watu wengi wasio na elimu na wenye elimu pia
 
Kama lengo ni kuboresha mzunguuko wa fedha na ajira kwa watu tungeweza kuuongeza mzunguuko wa pesa kwenye jamii zaidi kama pesa hiyo ingetumika kuwapa wananchi wengi kazi ya kuchimba na kutandika mkongo kuelekea kwenye kata zao. Kazi hiyo ingekuwa na multiplication effect kwa taifa. Kwani watu wengi wangeweza kuhudumiwa hukohuko kwenye kata zao bila kulazimika kusafiri na kukusanyika makao makuu ya wilaya, mkoa au wizarani. Hata shule za kata zingeweza kufundishwa na walimu walioko dsm.

Tunajua kuwa kwenye miradi hiyo ya dodoma kuna maslahi ya watu. Badala ya kuipeleka serikali kwa wananchi mnatengeneza mradi wa kuikusanya serikali sehemu moja, yaani bomu likipigwa linalipua serikali yote kwa wakati mmoja. Haya ni matope sio ubongo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…